Mjadala huu nimeufuma kule kwa
mamanamwana.blogspot.com
nikaona ngoja na wadau wa globu ya jamii watie baraka zao...

-------------------------
Na Jiang Alipo
Mtoto huyu mkazi wa Dar es Salaam aliwashangaza wengi katika fukwe ya Coco Beach siku ya X Mas kwa umahiri wake wa kufakamia Safari Laga bila kutikisika. Kwa mujibu wa mama yake mdau huyu huondoka hadi bia mbili na yupo fiti.

Najua kitaalam hii haiko sawa kabisa lakini hii si mara ya kwanza kuona mtoto,tena wengine wadogo kuliko huyu, chini ya mwaka mmoja, akipewa pombe anywe. Wenyewe wanasema 'haina shida anaonja tuu'. Najua hata nyiyni wenzangu mmeshuhudia haya, na labda mnamjua mtoto angalau mmoja anayeonja.

Wazazi wenzangu mnasemaje juu ya tabia hii ya kuwaruhusu watoto kunywa vilevi wangali wadogo, hata kama ni kuonja tuu? na tufanyeje kuwashauri wazazi wenzetu wenye tabia hii waone adhari zake?
Picha na Mroki Mroki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Mi ninachojua kama mtoto ni mchanga halafu analia sana usiku unaweza ukampa wisky kidogo kanalewa halafu kanalala, maana kuna wakati wote mmechoka kumbembeleza. Teh teh teh

    ReplyDelete
  2. ndio maana nchi za Afrika tuna majinias wachache kwa sababu ya Watoto kunywa pombe wakiwa na umri mdogo, ndio maana hata bia za bongo zimewekewa onyo la kutonywewa na watoto chini ya miaka 18.

    kingine kinachodumaza akili za watoto ingawa ni kwa kiwango kidogo ni pamoja na chai, kahawa pamoja cocoa, hii inashauriwa kuanza kunywewa baada ya mtoto kufikisha miaka 4 - 5

    ReplyDelete
  3. Huyu mama ashitakiwe na anyang`anywe mtoto na serikali! ana bahati angekuwa kuwa huku marekani! mh! angeozea jela!

    ReplyDelete
  4. Kaka misupu huu mjadala utakuwa hujautendea haki ikiwa hutaambatanisha na ile picha ya mama yake huyu mtoto anavyofurahia mtoto wake anavyofakamia kilaji

    ReplyDelete
  5. Michuzi,
    Hii ni kali ya mwaka 2009. Du, kaka! Yanki linakula mbuyu ambao hata sisi wazee tunauogopa. Jamani, hiki kizazi cha wabongo kinaelekea wapi?? Nakumbuka Ulaya na Marekani mimi kwa vile nina kisura cha kitoto wakati nimeenda age ya kutosha nilikuwa naambiwa nionyeshe passport ili waniuzie bia tena bia laini. Yaani kule Ulaya na Marekani mpaka ufikie miaka 18 ndio unaruhusiwa kupata ulabu. Huku kwetu sasa, nadhani tuweke sheria sasa jamani. Mh! Haka katoto katafikisha kweli umri wa miaka 20, kama kanaanza mbuyu sasa hivi? Aliyemfundisha huyu mtoto anatakiwa akamatwe na kupelekwa mahakamani kabisa.

    ReplyDelete
  6. kudadadeki kaniacha hoi kweli kweli

    ReplyDelete
  7. Hili ndilo aina ya taifa tunalo lijenga Watz. Kitendo cha mzazi kushabikia mtoto kunywa kiasi hicho ni kutokuwa na mtazamo na wa maendeleo na mwelekeo kwa maisha ya huyo mtoto na taifa kwa jumla. Baadaye huyo mtoto atakapokuwa "chapombe"amebobea kwenye ulevi, ni mzazi huyohuyo ndiye atakayekuwa wa kwanza kulalamka kuwa "watoto wa siku hizi bwana! wameshindkana kabisa". Amesahau kuwa ni yeye mwenyewe alimuachia aonje kidogo tangu akiwa mdogo. Hiyo haishii hapo. Mzazi kama huyo ataendelea kumuachia huyo mtoto ajaribu na vitu vingine pia (utavitaja mwenyewe)ambavyo ukilinganisha havina faida kwa malezi ya huyo mtoto ukilinganisha na hasara za hapo baadae. Ni vema wazazi wakawa na malengo juu ya watoto wao kuliko kuwa na mawazo ya bora liende. usitegemee serikali au shule baadae ikusaidie kumrekebisha huyo mtoto wakati wewe mwenyewe ulishindwa kumpa malezi bora. Wenzetu walioendelea wanapanga tangu mtoto hajazaliwa, kwamba huyo mtoto wanataka aje kuwa nani. Je Sisi tunafanyaje? tunaweza kuiga hili pia? au tunaiga mambo ya hovyohovyo tu na kuacha ya msingi?Huo ni mtazamo wangu, wengine wanaweza kufikiria tofauti.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  8. Kama taifa lenyewe la kesho ndio hili!!!basi tumekwisha wadosi na watish watanyonga tani yao.

    ReplyDelete
  9. Jamani mmesahau billboard kubwa miaka ile "eti Urithi wetu ni Seregenti" lilihusu bia ya Serengeti, nilikuwa nashindwa kulielewa yaani tunarithi ulevi. Mweeh!! Huyo mama ni mmoja tu, wako wengi wanaowapa watoto kilevi, na pia ili mtoto mdogo asukwe rasta basi baadhi ya salon huwapa dozi ndogo ya Valium. msishangae watoto wa kike wakiwa na addiction ya madawa baadae. kisa urembo, ili iweje?? Kina Mama mpo? Huu si uzushi kama mlikuwa hamjui.

    ReplyDelete
  10. Jamani haya ni matunda ya tabia ambayo pia wazazi wanakuwa nayo. Nilimwona mama yake na huyo mtoto mwenye mapepe wa kutupa. Kinywaji alichokuwa amefakamia mama mtu hata mwanaume huwezi kukibeba. Sasa mama wa aina ile unategemea nini hata kwa watoto. Na hasa watoto kama hawa utakuta baba zao hata hawajulikani. Hivyo mama anakuwa na full power ya kufanya lolote kwa mtoto. Mimi nimewahi kushuhudia mama mmoja anamfanyia mpango binti wake wa miaka 13 kwa mwanaume ili akipewa pesa naye aambulie. Sasa kwa hali ya mama kama yule, definitely kumpa bia ya safari mtoto wa miaka 5 kama huyo dogo ni kawaida. Maana yawezekana alizoea kumpa ili asinzie halafu mama aendelee na starehe zake pasipo usumbufu. Hapo hakuna cha kushangaa.
    Mkuu wa wilaya ya ninihiiiii nawasilisha.
    Mdau

    ReplyDelete
  11. Tatizo ni kukosa kuzingatia sheria.Mtoto chini ya miaka 18 haruhusiwi kuingia baa pia.Nchi nyingine ukienda baa na mtoto chini ya miaka 18 wanakufukuza sababu ukibanwa utakoma baa inafungwa na mwenye kuuza vinywaji unaenda jela.

    Tanzania mijitu mizima tena imesoma utakuta inaingia na watoto wao baa bila haya na wenye baa wanawatazama tu.

    Maofisa ustawi wa jamii na polisi tembeleeni kwenye baa kamateni wavunja sheria na kuwaburuza mahakamani na kuwafunga na kuwafungia baa zao.

    Huyo mhudumu aliyempa pombe huyo mtoto naye inabidi atiwe mbaroni na kushtakiwa.

    Pia jamii haina huruma ilibidi imkemee huyo mama na kumnyang`anya hiyo chupa huyo mtoto na kumkaripia asirudie tena.Mchango wa jamii uko wapi? Mtoto wa mwenzio ni mwanao na ukiona anapotoka msaidie hata kama si mwanao wa kuzaa.

    Nashauri mtoto huyo atafutwe na polisi na watu wa ustawi wa jamii wawape ushauri nasaha huyo mzazi na mwanawe au wawafungulie mashtaka wote wawili mtoto na mzazi ili vitendo kama hivyo vikome.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  12. Mimi ni mmoja ya watu wanaokunywa sana pombe, sijisifu lakini napenda ze lager! kutokana na kunywa kwangu pombe muda mrefu nimeona madhara yake kwamba usinywe pombe ukiwa na stress, usinywe pombe ukiwa hujala,usinywe pombe ukiwa kazini, usinywe pombe ukiwa na mdogo, usinywe pombe kama huwezi matokeo yake...mtoto mdogo huwa anaelekezwa mambo mengi sana kwa sababu tunajua akili yake haijakomaa...sasa kumpa kilevi mtoto ni kosa kubwa sana kwa sababu ulevi utamharibia akili mtoto

    ReplyDelete
  13. MAMA WA MAOVU

    Mara nyingi tukikataa vilaji, ngono wazi, kamari na dawa za ulevi (narcotics) huambiwa eti unaleta UDINI. Hubandikwa majina kuwa ni Siasa kali au walokole.

    Huu mkojo wa firauni eti ni usraarabu wa watu wa leo, watu wanaokwenda na wakati au liberal. Wako watu wanaofanya suala la ulevi ni la kidini kuwa lina ambatana na dini moja au dhehebu moja na kutopendelea kilaji ni ukereketwa wa dini fulani.

    Pia kuna kushabikia kilevi cha bia kuwa ni ustaarabu unaokubalika na vile vilevi kama changaa au gongo ndio haramu kwa ile hivi vya kisasa vinachangia uchumi wa taifa kama chanzo kikubwa cha kodi.

    Vyombo vyetu vya uenezi wa habari vimerubuniwa na wauzaji wa pombe kwa kuwalipa fedha nyingi kupitia matangazo ya Serengeti, Safari Kilimanjaro, Stout, Gueness, Stella, nk. Pia hudhamini ligi za mpira, mashindano ya ma Miss na mengine kushinikiza akili, bongo nk ziwe zimeridhia kuwa ulevi ni uji au togwa.

    Baadhi ya kampeni za krusedi za Amerika zimejaribu kuvunja nguvu za dini kwa kuweka baa karibu na nyumba za ibada na sehemu wanazoishi watu wa dini zinazopinga ulevi iwe ni njia ya kutenza nguvu ya watu ambao hawataki ulevi na imani yao.

    Katika mikakati ya ku-ifisidi jamii, mkakati uliopitishwa na vyombo vya krusedi ni kueneza utamduni wa ulevi, kamari, dawa za kulevya, na biashara za ukahaba. Vitu hivi vitatu huenda pamoja na kila mlaji kilabu, huenda nje ya ndoa,kuendeleza kuvunja uaminifu, kukuikuza biashara ya changu doa, kueneza magonjwa ya zinaa, nk. kwa sababu Ulabu ni mama wa maovu.

    Nitahimili kuitwa mlokole au siasa kali kwa ushamba wangu wa kukataa kusheherekea tabia ya vinywaji kwa sababu mtoto 'umleavyo ndio akuavyo' ukimlea kwa ulabu atakuwa chakari 24/7

    ReplyDelete
  14. Mama mwenye kumjali mwanae hawezi kumruhusu mwanae mdogo hivyo anywe ulevi, achilia mbali kufurahia mwanae anavyogida chupa.Mzazi mwenye kujali anatakiwa tangu mwanzo azingatie mwanae anakula nini. Sio kula tu bali pia tabia ya mtoto kwa ujumla.Haitoshangaza baada ya miaka kadhaa kitoto hicho kikawa alcoholic- addicted. Wa kulaumiwa nafikiri ni wazazi wake, kwani mtoto hajui jema au baya bali hujifunza kidogo kidogo kutoka kwa wazazi wake na wanaomzunguka. Kama mama anaona sifa kwa mwanae kugida ulevi, inaonyesha ni mzazi wa aina gani, kwani kwenye picha nyingine ya mroki-mroki anaonekana mwenyewe kabeba mbili, basi...well( like mom like son)..alaumiwe mzazi.
    Shime malezi mema wadau, ni vigumu lakini tukijitahidi tutafanikiwa.
    Mama prince.
    (Yeah, he is the prince of my life)

    ReplyDelete
  15. Someni madhara:
    http://dailynews.habarileo.co.tz/home/index.php?id=9331

    ReplyDelete
  16. babu kidevu alikuwa nayo hiyo picha siku nyingi kweli inabidi aiadvirtise blog yake

    ReplyDelete
  17. Na mimi nimegombana na ndugu zangu huko Bongo kuhusu kuwapa watoto wadogo pombe. Yaani wanaona 'fahari' kuwa wanaweza kumpa mtoto bia badala ya soda! Nauliza huyo mtoto aliyelewa akienda barabarani na kugongwa na gari na kufa utajisikiaje?

    Pia, hapa Massachusetts umri wa kununua na kunywa pombe ni 21. Ukienda kwenye party za waBongo wakati mwingine unaona watoto wanapewa pombe. Kuna siku ilibidi nimfuate host wa party na kumwonya kuwa polisi wakija yeye atakamatwa na kushitakiwa ingawa siye aliyewapa watoto pombe. Hakuelewa. Nikamwambia watasema kuwa walipewa wakiwa nyumbani kwako. Wala hawajali kama mtu mwingine kawapa hiyo pombe. Wote mtashitakiwa. Na hata wakiwa wanaenda nyumbani na wakapata accident watauliza pombe walikunywa wapi? Utakoma! Kuna sheria kali za pombe hapa USA na ni kwa ajili ya kulinda maisha ya watu.

    ReplyDelete
  18. Dah! Enzi za Mwalimu ...

    ReplyDelete
  19. Mwenye kosa nani:
    a) Mtoto?
    b) Mzazi?
    c) Muuza kilevi?
    d) Watu waliomzunguka?
    e) Serikali i.e sheria?
    f) Wasimamia sheria?

    >>It begins with you!

    ReplyDelete
  20. Kwa tanzania siyo kosa, muongezee nyingine. Nyie mnafikiri kule vijijini tumeanza kuzinywa tuna miaka minga? hata kamera hakuna.

    ReplyDelete
  21. Mimi kwa upande wangu na kwa vile nimeshaona hii naweza nikatetea na pia kujudge hii tabia.

    a) Bongo wanaamini kuwa mtoto akiwa mdogo akiwa anaona watu wanakunywa pombe anazania ni kitu kizuri sana na anamiss so much. Hivyo akililia mpe tena ile kali akionja tu hatataka tena. Mfano nephew wangu hagusi pombe mpaka sasa hivi.

    b) Huku tuliko wanakataza pombe mpaka uwe na miaka 21 lakini ukweli ni kuwa watoto wa huku wako wasted kishenzi kuliko wa kwetu. Wanazinywa kwa siri sana na wengine wanakunywa kwa ule mtindo unaitwa binge drinking. Na hiyo inawauwa kila siku. Na wengine wakifikisha huo umri wanakunywa siku ya sherehe yao wanakunywa 21 shots on their 21 yrs old b'days. Wengi wanakufa na sumu ya pombe.

    Mimi naona ukimwambia mtu usifanye hivi, usifanye vile ndio maana wanakua na hamu ya kujaribu.

    Ila ukiona mtoto anakunywa hiyo pombe na kuimaliza ujue mama yake alikunywa pombe pia wakati akiwa na mimba. Mtoto anazaliwa na pombe kwenye damu hata siku ya kwanza tu duniani huyo mtoto angeweza kumaliza hiyo chupa.

    Ni kuelimishana tu...tutafika. Na pia kuna pombe na pombe. Pombe zingine kama mbenge zile poa hata kwa afya yako lakini nyingine ndio mwanzo wa kuua mapafu. Huyo anayesema unampa mtoto wiski umenimaliza mbavu. Ungekua huku sasa hivi ungeshaishia jela na tungeshakusahau kabisa manake hiyo miaka ya jela wangekupa sio michache.

    ReplyDelete
  22. baada ya kupitia maoni ya waliopo ughaibuni, nimegundua kwamba kinachowatisha ni sheria na sio maadili juu ya malezi na makuzi ya mtoto kuhusiana na vileo.

    ReplyDelete
  23. MDAU BWENI NACHANGIA.

    UJINGA HUU WAKATI WA SERIKALI YA BABA WA TAIFA USINGEKUEKO. NDIO MAANA ALITUDUMAZA KWA MALENGO KAMA HAYA. NAZANI HATA URAYA HAMNA MAMBO HAYA!! JAMII IMEANGAMIA. WAKATI WADOSI WANAPELEKA MITOTO YAO SHULE NA KUJIFUNZA BIASHARA KWENYE MADUKA YAO SISI WAZAWA TUNAJISIFIA MITOTO YETU KUNYWA MIPOMBE. WAKITUZIDI TUNAWAITA MAGABACHOLI.

    NI UZEMBE WA JAMII KWA UJUMLA HUSUSANI SERIKALI.

    ReplyDelete
  24. UKISIKIA LAANA NDIO HII...MFANO HALISI NDIO HUO KWENYE PICHA.

    ReplyDelete
  25. Nyie mnashangaa nini hapo? Mie nikiwa mdogo miaka 3, mwaka 1984, mama angu anakili wazi kwamba alikua ananinywesha ULANZI ili nisilie kwa ajili ya NJAA ili yeye apige jembe si mnajua life la kijijini kwa wale tuliokulia huko…nikakua hivyo ikafika wakati nikawa nikitoka SHULE kula nondoz nikawa naenda zangu kugida ULANZI shambani kwa babu mmoja halafu akawa ananiona bonge la shujaa na mtiifu wa utamaduni kwani watoto wake walikua hawataki kunywa wakati baba yao ndio mgemaji. Nikaendelea kunywa mpaka nilipofika miaka 24 nikaamua kuacha mwenyewe bila shinikizo kwa raha zangu sasa nakunya vinywaji laini tu alcohol 0%.

    Sasa wanafamilia mnaoshangaa nyie mlianza kunywa pombe mkiwa na miaka 18 kweli au ndo mambo ya sema usikike? maana kila mchangiaji anasema Marekani na Ulaya tu, mbona hamtoi personal experience (uzoefu binafsi)? Au kwakua ni safari ndo mwaiona pombe? Kuna madogo Wanakunywa pingu, mbege, ulanzi, kangala n.k na yako safi tu… msinishangae wanajamii mie ni mzaliwa wa Iringa so pombe hasa ULANZI na KIHAMBULE ni sehemu ya maisha la kila siku…lol

    Mdau ughaibuni….

    ReplyDelete
  26. Anonymous wa juu hapo umenibariki Wamarekani wenyewe wanasema kukataza kunywa pombe kunawafanya watoto watamani kunywa zaidi, hii ni sawa na watoto wanaolelewa kigeti kali huko Bongo kila wakipata upenyo hasa wakienda boarding schookls wanafanya mambo ya ajabu hata hayasimuliki

    ReplyDelete
  27. huyu mtoto hana makosa yeyote wenye makosa ni wazazi wake. huyo mama alitakiwa kuzomewa na watu wote waliomwona akifurahia kumwona mtoto wake mwenye umri mdogo kama huo akinywa pombe. pengine mungu alitaka kumuangaza ndio maana jambo kama hilo likatokea hadharani. huyo mama ni wa kulaaniwa. hafai kulea watoto. tafadhali serikali mchukulieni sheria. anaiabisha tanzania yetu. nyie wwnye magazeti onyesheni picha ya huyo mama kwenye ukurasa wa mbele wa magazeti yenu.

    ReplyDelete
  28. Mimi ni mama, baada ya kuona picha hiyo nimejisikia uchungu sana! Naomba wazazi wa huyo kijana wamzuie kunywa pombe

    ReplyDelete
  29. Jamani ewe mzazi!
    Wagenga walisema mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo!

    Wazazi wengine hawashauliki!! Ukimuuliza kwanini unampa mtoto kilevi anakujibu wako! wakoo!!! inakuhusu nini!

    Lakini ewe mama jaribu kumpa mwanao malezi mazuri, kama ungemzoeza kunywa maziwa, juice sidhani kama angetamani bia!
    na mwisho akikosa bia atakula mibangi, unga, mwisho hee teja! kibaka then atavishwa tairi, petrol na kiberiti chwaaaa!!!!!!!

    ReplyDelete
  30. mi nilikaa karibu ya huyo mtoto siku hiyo nikawa nasikia harufu ya nyama ya kuchoma kumbe mtoto maini yalikuwa yanaungua ,nampa pole sana

    ReplyDelete
  31. Naunga mkono wapeni picha hii watu wa magazeti bure.Aliyepiga picha hii aweza pata tuzo ya picha bora 2008.

    picha imebeba ujumbe mzito kwa jamii.

    ReplyDelete
  32. kwani pale coco beach walipokuwepo hamna askari wakuweza kudadisi dadisi, lakini unaweza ukakuta na askari mwenyewe yupo hapo anacheka tuuuuuuuuuuuu kama lofa.

    ReplyDelete
  33. siyo mtoto huyo, huyo ni mtu mzima ila amedumaa tuu. Namjua huyu mjomba anayeuchapa mtungi, anaitwa Seti, tulisoma naye bagamoyo sekondari. Tangu shule alikuwa anapenda sana kunywa huyu jamaa lakini mambo ya ngono siyo yake.

    ReplyDelete
  34. NDIO ZETU KUWAKILISHA..........SANA TU.
    HIVI NDIO VIPAJI VYETU WABONGO....MNAJIVUNGA NINI NYIE MNAOLALAMIKA....HIYO INA TBS ANGEKUNYWA GONGO JE....??? ALAH.

    By SON'S FATHER.

    ReplyDelete
  35. MIE NIKIMWANGALIA VIZURI HUYO MNAYEMWITA MTOTO NAONA SIYO MTOTO,BALI NI UMBO LAKE TU, KIJEBA HICHO,KIMEKOMAA SANA HAKIPUNGUI MIAKA 18,ONA KAISHIKILIA CHUPA KISAWASAWA KWA MKONO MMOJA BILA SHIDA YOYOTE,ANGEKUWA MTOTO ANGEISHIKA KWA MIKONO MIWILI!

    ReplyDelete
  36. Mama au Baba wa mtoto huyu ana kila dalili za kuwa mtu mjinga katika jamii.Si tu kwamba ujinga wake unajionyesha katika tagbia ya mtoto wake ili kila mtu aone ,lakini pia najitengenezea ZEZETA ambalo atalilisha kulisomesha na hatimaye kushindwa maisha.Pombe kama vilevi vingine vyovyote huathiri ubongo, kwa mtoto anayekua mwenye ubongo ambao haujafikia kukamilika kukua ndio zaidi.
    Si rahisi kumlaumu mtoto lakini jamii imlaumu mzazi wa huyo mtoto.

    ReplyDelete
  37. Pombe kwa watoto inawadumaza akili,mtoto hata akikua vipi akili yake inakuwa bado nyuma sana na wengi wanakuwa kama mazezeta, na some of the autism patients inasemekana ni matokeo ya pombe ila haina uhakika wa kutosha,all in all pombe inaharibu na kudumaza uwezo wa mtoto

    ReplyDelete
  38. INALLILAHI WAINAILLAHI RAJIUN...UKIONA KITU CHOCHOTE KINACHO ASHIRIA MSIBA MKALI KAMA HUU INABIDI TUSEME HIVI...HII INAONYESHA KWAMBA BAADAE TUTAKUA NA TAIFA LA WALEVI WATUPU..JE KUTAKUA NA MAENDELEO KWELI.. WATU WATAFANYA KAZI KWELI..WANAUME MNAO TIA WATU MIMBA NA KUWAACHIA WALEE WATOTO WENYEWE MNAONA MADHARA YAKE...MUNGU HAWEZI KUKATAZA KITU AMBACHO HAKINA MADHARA KWETU..MAADILIYETU YAKO WAPI..SHERIA ZIPO LAKINI TUMEZITUNZA KWENYE MAFAILI TUUU..

    ReplyDelete
  39. Hili suala liangaliwe kitamaduni (cultural) zaidi, ili jamii iweze kubadilika.

    Kuna masuala ya kitamaduni kama:
    -ukeketaji wa kinamama
    -kuchagulaga
    -pombe hata kwa watoto
    -kuolewa watoto wadogo
    -kugoa meno ya mbele uji upite
    -kutoboa masikio
    -kuchanja chale za utambulisho
    -n.k,n.k
    Hivyo serikali na jamii ichague yanayofaa na yasiyofaa ktk tamaduni zetu na kuendesha kampeni ili mabadiliko yapatikane.

    ReplyDelete
  40. Oh my Goodness,angekua ulaya,marekani or any other developed country wazazi wa huyu mtoto wangekua wanaongea na police na social workers period.
    Hivi ni kwa nini jamani,halafu ukute mzazi pembeni anamuona anaona kama sifa.
    Something is seriously wrong.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...