Liverpool manager Rafael Benitez has rejected the Anfield club's latest contract offer, BBC Sport understands.
Benitez, 48, says he will only accept the deal if he gains more control over football matters instead of having to answer to chief executive Rick Parry. "The owners feel (my) decisions need to be subject to the chief executive," Benitez told the Liverpool Echo.
"But I know that I am subject to results and to our fans and they are the best judges I will ever have."
Benitez, who has agreed the financial terms and length of the proposed contract, has informed the club's American owners Tom Hicks and George Gillett of his stand.
The Spaniard insists he has a strong relationship with the co-owners but says that the deal on offer would not allow him to manage football matters at Liverpool to the best of his abilities.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. ndio manake.Rick Parry hana la maana analolifanya ktk suala la usajili.amekuwa akikunja sana kununua wachezaji wenye akili timamu.Rick Parry amekuwa kikwazo tangu enzi za Gerrard Houllier.
    Goma Benitez Gomaaaaaaaa.

    "LFC 4 LIFE"

    ReplyDelete
  2. Misupu unapata tabu bure hata kama ni wewe kila kitu kipo wazi huyu jamaa lazima atafute kisingizio kwani moto wa ManU ameshauona na ameshajuwa kuwa kuropoka kwake juu ya Sir Guffer hakujamsaidia kitu ....kifupi anatafuta tundu la kutokea teh... teh.. teh.. thijui itakuwavipi kama ni wewe ungefanya vipi thithemi sana.

    ReplyDelete
  3. Premier League Uingereza Jumamosi:

    -Chelsea wanawakaribisha Stoke City.
    -Hull itakipinga nyumbani na Arsenal.
    -Bolton nyumbani kwao watajaribu kupunguza kasi ya ManUtd.

    Liverpool jumamosi hawana mechi hivyo masikio na macho yao yatakuwa kusikiliza wengine wanaendeleaje ktk Ligi.

    ManUtd ikiweza kushinda kesho ugenini Bolton watafikisha pointi 47 na kushika uongozi toka kwa Liverpool yenye pointi 46.

    Chelsea wakiweza kuwashinda Stoke City watafikisha pointi 45. Felipe Scolari amekanusha uvumi wa magezeti kuwa mambo siyo shwari kutokana na Drogba kutoonekana ktk mechi na Southend United, nakuuita uvumi huo kuwa ni upuuzi.

    ReplyDelete
  4. figo then hii? na bado

    ReplyDelete
  5. mkataba ndio unamchanganya jamaa ndio maana anaanza kuchachawa na kumuongelea SAF na David Gill. Kajaza A4 uzushi mtupu, hata point hana. Soma uchambuzu kamili HAPA.

    Timu nyingine kufundisha/kuspport ni kujipa presha tu; we muulize Houlier!!

    ReplyDelete
  6. HATA UKIPEWA KIBARUA CHA KUPALILIA MIKOROSHO HUWEZI KUMPA MSHARTI MWENYE SHAMBA NI YEYE NDO ATAKUPA MASHARITI NILIMIE MIKOROSHO YANGU KUANZIA UPANDE HUU KUELEKEA KULE HUWEZI KUANZA OO NO NATAKA NIANZIE PALE.

    ReplyDelete
  7. Wabongo bwana,domo jingi akili hakuna.Hii habari ni rahisi sana kuelewa kwa mtu anayefuatilia mpira na mwenye mwanga wa ligi ya england.Benitez ana haki kabisa ktka madai yake.Yeye ka meneja wa timu anastahili kuwa namba moja katika maamuzi yanayohusiana na usajili, na uendeshaji wa timu.Hao kina Hicks,Gillet pamoja na Parry wanachotakiwa ni kushughulikia mambo mengine ya Club kwa ujumla na kumwachia Benitez a-run team.Tatizo la wabongo wengi mnafuatilia "highlights" za ligi nani kashinda,nani kafungwa,nani anaongoza ligi mambo mengine hamyajui halafu mnaanza kupiga domo. Alex Ferguson hakupata success kwa kuwa meneja mzuri tu,bali kwa kupewa uhuru wa kuendesha timu yake anavyotaka yeye sio mabosi wake wanavyotaka aendeshe.Mfano mwingine ni Wenger,jamaa ana uhuru wa kumwaga kama Fergie.Angalieni yaliyotokea kwa MOURINHO.MRUSI alitaka awe remote control Mourinho akagoma mwisho wake mnaujua.Ligi za wenzetu haziendeshwi kibongo bongo.Hawa wamarekani wamwachie Benitez uhuru wa kuendesha timu,kisha waje kum-judge baadaye.
    **ARSENAL FOREVER.

    ReplyDelete
  8. Soka premier League Half-time:

    ManUTD 0 Bolton 0
    Chelsea 0 Stoke City 0
    Man City 0 Wigan 0
    Blackburn 0 Newcastle 0
    Sunderaland 1 Villa 0
    Arsenal Vs Hull mechi itaanza baadaye yaani saa 20:00 EAT.

    Kuhusu Liverpool wao wana wikiendi ndefu mpaka jumatatu watakapo kwaana na Everton.

    ReplyDelete
  9. Full-time premier league results:

    Timu kubwa mbili za soka Uingereza leo wameponea tundu la sindano baada ya kufanikiwa kupata ushindi ktk dakika za majeruhi.

    ManUtd 1 Bolton O. Bao la ManU lilitiwa kimiani dakika ya 90 mfungaji akiwa Babertov, hivyo ManU inaongoza ligi ikiwa na pointi 47.

    Chelsea 2 Stoke City 1. Stoke waliwanyamazisha washabiki wa Chelsea baada ya kuongoz a kwa bao 1 lililofungwa na mtaalamu wa kurusha mipira Uingereza Rory Delup wa Stoke City.

    Chelsea wakicheza nyumbani walifanikiwa kurudisha ktk dakika ya 88 kupitia kwa Baleti. Frank Lampard aliwainua mashabiki ktk dakika ya 90 alipofunga bao na kuiwezesha Chelsea kukumba pointi zote 3 nyumbani London. Chelsea sasa inashika nafasi ya tatu ktk msimamo wa ligi ikiwa na pointi 45.

    Aston Villa waliishinda Sunderland bao 2 kwa 1 na hivyo Aston villa inashikilia nafasi ya 4 ktk ligi.

    Arsenal inaigia uwanjani leo jioni sana hapa Uingereza ktk uwanja wa nyumbani wa Hull city wa KC stadium mjini Hull.

    Liverpool wataremka uwanjani siku ya jumatatu kupambana na Everton. Kutokana na ushindi wa ManUTD leo, Liverpool sasa inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 46.

    Man City 1 Wigan 0
    Blackburn 3 Newcastle 0
    West brom Albion 3 Middlesborough 0

    ReplyDelete
  10. huyo jamaa amekua frustrated maana anajua hawezi kushinda itu msimu huu,safari hiyoooooooooo.wamuachie mtalaaaaaaaaam fergie tu

    ReplyDelete
  11. Mechi ya Arsenal na Hull City ilikuwa ya vuta nikuvute kwani mpaka dakika ya 81, timu hizo zilikuwa nguvu sawa 1-1.Bao la Arsenal lilifungwa na Adebayor na la Hull City lifungwa na Cousin.

    Arsenal walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Nasri baada ya pande la Van Parsie.

    Arsenal iliongeza bao la tatu kupitia mtaalamu wa kupachika mabao ya Arsenal ktk dakika za machewo kupitia kwa Bertner dakika ya 85.

    Hivyo mwisho wa mechi Arsenal 3 Hull City. Arsenal inaedelea kushika nafasi ya tano nyuma ya Asto Villa ktk msimamo wa ligi,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...