Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakimpa pole mot0to albino,Mtoba Malosa ambaye alinusurika kukatwa mkono wa kulia na watu ambao hawajafahamika nyumbani kwa wazazi wake njia nne, Kashishi, wilayani Urambo hivi karibuni. Mtoto huyo kalazwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora ya Kitete. shoto ni mama wa motto huyo Kulwa Malosa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika mkutano aliouitisha wa kujadili mikakati ya kukomesha mauaji ya albino na vikongwe akiwa na mototo Stella wakati alipozungumza na viongozi wa serikali, vyama vya siasa , dini na maalbino kwenye ukumbi wa Vijana katika mji Mdogo wa Chato
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Luambow baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Januari 20,2009, kwa ajili ya kuongoza mkutano wa kujadili mikakati ya kukomesha mauaji ya albino na vikongwe. Kushoto kwake ni mkewe Tunu


Msanii wa kikundi cha sanaa cha Bujora cha Mwanza, Yassin Anrthony akicheza ngoma ya nyoka wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ili kuongoza kikao cha kujadili mikakati wa kukomesha mauaji ya albino na vikongwe kwenye ukumbi wa vijana katika mji mdogo wa Chato


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na madiwani wa jiji la Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Januari 20,2008 kuongoza kikao cha kujadili mikakati ya kukomesha mauaji ya albino





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Inaonekana kuwa kazi ya udiwani haiwezi kufanyika bila ya kuwa na majoho na makofia ya ajabu ajabu.
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. Mwaka juzi wataalam walitoa ripoti kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya albino kuliko nchi zingine za Afrika. Tangu wakati huo naona kama ukatili dhidi yao umeongezeka. Nadhani watu kutoka nchi zingine wanalipa watu wenye uchu wa pesa huko Bongo kuwafanyia albino wetu ukatili huo.

    Mbona miaka ya nyuma tulikuwa hatusikii ukatili hivyo? Wengi tumesoma na kukaa na albino bila shida.

    ReplyDelete
  3. MAUAJI YA ALBINO NI UBAGUZI WA RANGI (RACISM) KAMA ULIOKUWEPO AFRIKA KUSINI NA NCHI ZINGINE ZA MAGHARIBI.

    NAWASILISHA

    MDAU

    ReplyDelete
  4. jamani nani aliwashauri hao madiwani wavae hivyo. hizo kofia sijui niseme ni kama wawindaji wa zamani au ma DC wa enzi za ukoloni. hizo joho zao ni za kuchekesha pia. sijui ni nguo za dini au vipi. naomba hao madiwani wamtafute designer mwingine awa designie uniform nyingine. good luck.

    ReplyDelete
  5. hongera sana Bwana Pinda na familia yako, wewe ni ROLE MODEL, umeonyesha kuguswa kwako kwa vitendo na mawaziri wako wanatakiwa wafuate nyayo zako, kila mmoja na kwa vitendo aonyeshe yuko na imani kiasi gani katika vita dhidi ya majangili wa maaalbino. jee Waheshimiwa Mawaziri wa TZ nanyi mutachukua mtoto mmoja ili muonyeshe ujasiri wenu na kuchukizwa? very numberr counts!!!
    Mdau, zenjibaar

    ReplyDelete
  6. Jamani Juzi nilivyoangalia taarifa ya habari kuhusu huyu mtoto kweli nililia hivi binadamu tumefikia hatua hiyo? mtoto mdogo hajui hata kosa lake wala hata kujua kama yeye ni albino. Na hata wanyama hawana roho hiyo. Kweli hatuna tofauti na watu wanaopigana vita na kuua watu wasio na hatia tofauti yetu ni kwamba ni jamii fulani tu wanaotafutwa. Mungu tunusuru.

    ReplyDelete
  7. Kwanini viongozi wetu kila wanapokwenda sehemu kikazi wanapokelewa kwa ngoma vigelegele wakati wanakuwa wamekwenda kikazi na sio kisherehe, na inaelekea hizi tabia wanazifurahia sana, huku Ulaya hata aje nani huwezi kuona upuuzi huo, sasa ongalia ngoma za utamaduni wanalipwa si ajabu hao tena pesa nyingi kama sikosei kwa sababu ya kwenda kumpokea mtu aliyekuja kufanya kazi yake.

    ReplyDelete
  8. Kwa maoni yangu serekali yetu imeshindwa kuwalinda hao albino. Inasikitisha kwamba mpaka sasa hivi wameshindwa kumkamata mtu hata mmoja anayehusika na unyama huo. Kwa nini kila albino asipewe ulinzi wa masaa 24. Tuna jeshi la polisi na jeshi la kulinda taifa nk... Hawana kazi wanalipwa bure maana hata nauli za daladala hawalipi --- Kwa nini wasilinde hao albino? Kwa sasa hivi usalama wa albino mtanzania uko hatarini kupita hata wa mawaziri na Raisi ... kwa nini wasipewe walinzi? Nauhakika idadi ya Albino Tanzania haifiki hata robo ya jeshi la polisi--- Wapeni ulinzi tafadhali.

    Cha kusikitisha zaidi sisi watanzania hatufikirii jinsi ya kutatua tatizo hili tunasubiri Mzungu aje na mawazo yake na kufungua NGO basi utashangaaa mauaji yanapungua ghafla!!! Bila ka NGO na ulaji fulani nduguzangu Albino kimbieni nchi!!

    ReplyDelete
  9. Che mponda nadhani Albino wanauliwa na wabongo wenyewe,ikumbukwe Tanzania ni mingoni mwa nchi watu wake ni wakatili.

    Wazee vikongwe wanaendelea kuuwawa kila siku kwa imani za kichawi,na hamna chochote cha maana kinachofanyika.Walbino inabidi kuomba hifadhi katika nchi zingine na mabalozi ya nchi za nje,maana hali inatisha.Mkija huku nchi za Ulaya mtapata hifadhi tu ndugu zangu maana hii hali ya hatari inajulikana dunia nzima.Najisikia fedhea na aibu kuwa MTanzania.

    Bra gjort Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...