MICHUZI,
Kama kuna timu ya mpira wa miguu iliyowahi kunivutia ni Pamba ya Mwanza wana TP Lindanda.
Je wewe na wadau wako wanaweza kuniambia ni wapi walipo baadhi ya wachezaji wa timu hiyo mwanzoni mwa miaka ile ya tisini?

Paul Rwechungura, George Masatu, Hussein Masha, Nteze John, Fumo Felician, Abdallah Bori, Khalfan Ngassa, Mao Mkami, Edibily Lunyamila, Bea Simba, Abdallah Kaburu, Kitwana Suleiman na wengineo?
NAWAKILISHA MKUU
Mdau Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. Lunyamila hakuwahi kuchezea Pamba, alikuwa RTC Shinyanga baada ya hapo akachukuliwa Yanga (au kuna timu nyingine alichezea lakini sio TP Lindanda)

    ReplyDelete
  2. deo mkuki na alphonce modest Dan mhoja John makelele Hamza mponda Beya simba jamaa walifunika enzi yao

    ReplyDelete
  3. Mdau fanya utafiti kwanza kabla ya kuanza kuandika maana unataka kuwachokoza waosha vinywa. E.Lunyamila hakuwahi kuchezea Pamba pumbavu we!!!!

    ReplyDelete
  4. lunyamila hajawahi chezea pamba.

    ReplyDelete
  5. Mimi sio mfatiliaje wa mpira, lakini nakumbuka Fumo Felician nilimsikia miaka hiyo. Alikuwa kinara wa Pamba. Ukisema Pamba ya Mwanza unamuongelea Fumo Felician!

    ReplyDelete
  6. Mdau kwa jinsi inavyoonekana wewe ni shabiki gazeti na redio, pia vikao redio za mbao vya kabla ya mechi na baada ni vyako sana , maana hii lizi ina hadi Edibily, Kaburu? Huyu si alikuwa Pilsner kama sijasahau..we haya we!

    ReplyDelete
  7. Yaani amekosea tu mchezaji mmoja ndio kumtukana?? Anachosema tu ni kwamba TP Lindanda ilivyokuwa na wachezaji moto na hilo halina ubishi kuna wengine nadhani kama Bitebo na mwingine namba kumi wao alikuwa jina kama Hiza au Hija.

    Halafu pia kulikuwa na timu nyingine zilizokuwa moto mfano RTC Kagera ya akina Kichochi Lemba. Na pia RTC Kigoma ya akina Mwangata.

    ReplyDelete
  8. hivi yule rajabu musoma hakukipiga na hao washikaji wengine dogo alikuwa tishio sana

    ReplyDelete
  9. poa tu issa isghu za soka mpira zetu za muziki-nyimbo za zamani unabana haina noma bwana si unapendelea kwakuwa wewe ni mkuu wa wilaya

    ReplyDelete
  10. Alfonce Modest hivi aliwahi kuichezea Pamba ya mwanza?mimi ninakumbuka alikua Reli ya morogoro na simba.

    ReplyDelete
  11. lunyamila hakuwahi kuwa mchezaji wa pamba hapo umechemsha mdau

    ReplyDelete
  12. timu ilikuwa ileeeeee Reli Morogoro - Kibogo ya Vigogo.wachezaji wake hawakuwa na majina ya kutisha lkn nakumbuka ilikuwa kizaazaa sana wakiwa uwanjani.nakumbuka majina machache kama kina Sahau Kambi,Hamisi Fujo,Juma Limonga,Adam Selemani,Dancun Butinini,David Mihambo,Abdallah Mkali,Masenga,Mbuyi Yondani,na wengine kadhaa.Majimaji Songea nao walikuwa wamo somehow.ila kwa saaana nalikuwa napenda sana ule utani wa jadi baina ya African Sports na Coast Union ya miaka ileeee.
    yani soka ya kipindi ile kama ingekuwa na aksesi ya pesa kama sasa hivi labda tungekuwa na wachezaji kadhaa Yuropu.

    ReplyDelete
  13. ebwana umenivunja mbavu kweli kwani jamaa umemtukana sana muombe msamaha lakini,lakini pia awe ana fikilia kuandika kitu kwani kuna watu wana kumbu kumbu kuliko yeye.kuna akina ali bushiri,hamza mponda,juma mhina kipa.na wengine wengi tu.na hata kama anataka kufaham walipo aulize watu watampatia informasion UKEREWE HAPA.

    ReplyDelete
  14. EDIBILLY LUNYAMILA NI MWENYEJI WA KIGOMA NA ALIONEKANA KUWA NI MTU WA MPIRA KWA MARA YA KWANZA ALIPOCHEZEATIMU YA UMISETA YA KIGOMA, UMISETA NI MASHINDANO YA TIMU ZA SEKONDARI ZIKU HIZO ZA MIKOA

    ReplyDelete
  15. H.Makene,S.WAZIRI,M.Mwameja(goalies)Dougals muhani,Muhando mdeve,Hilaly hemed(dogodogo)razak yusuf(careca)Husein Mwakuruzo(luga)Elisha john,Raphael john,Victor kepha Mnkanwa,Abdallah Burhan,Kasa Mussa,Kassim Mwajeki,Ali Maumba,Mohamed Kampira,Idrisa Ngulungu,Said Kolongo,Joseph lazaro,Abbas Mchemba,Mchunga Bakari,wadau wa tanga nisaidieni kumalizi majina yao nimewachanganya coastal union na wana kimanumanu african sports...TANGA OYEEEEEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  16. Yeah hiyo ilikuwa inaitwa TP-Lindanda wana kawekamo hapo mjini Kirumba ilikuwa tatizo..PAMBA VS YANGA , PAMBA VS SIMBA , PAMBA VS MAJIMAJI....Jukwaani kakaa Charles Hillary bwana wee pembeni kakaa Beya Simba katikati Kitwana SELEMANI pembeni Hamza Mponda ,huku mpishi mwenyewe Hussein Masha ,last man mzee mzima George Masatu ,halafu ball dance Mao Mkami,Sheikh Amir Mafutaha nyie acheni hao walikuwa wacheza mpira siyo mambo ya siku hizi wapiga hewa wanaitwa wachezaji.... jamani tukubali lakini Tanzania football ya mpaka 90-es haitakaa ikarudi tena hasikudanganye mtu even social atmosphere was really different with situation nowdays ingawaje financially enzi hizi mpira ulikuwa haulipi ndiyo maana wachezaji wote wa miaka hiyo wanasukuma maisha, second the football of the 90-es hakuonyesha mafanikio internationally but for local standard was great moment in the society
    Nakumbuka mechi Simba vs Pamba -Dar
    with 10 minute John Makelele aliisha funga bao 3 dhidi ya Pamba ...Charles Hillary ana-comment ...John Makelele ZIGZAG anawanyanyasa wenzake hapa bao la tatu we hacha tu ,baada ya mechi hiyo gari la simba zilisukumwa mpaka msimbazi wanawake walitandika kanga barabarani basi inapita juu... hiyo ilikuwa issue siyo mambo ya siku hizi Simba vs Yanga mjini watu wamejaa miaka hiyo bwana mechi kama hiyo huoni mtu mjini kuanzia saa tisa watu wote Taifa...
    Mwanza ndiyo usiseme siku ya mechi ni sherehe mji mzima ilikuwa kama meeting point "CCM KIRUMBA' nakumbuka Lake siku hiyo hata kama kuna self-relience Magadura alikuwa anaachia watu tu.......
    yeah it was nice memory for our generation....
    TP LINDANDA...
    Mdau
    Wa kamachumu

    ReplyDelete
  17. Doh! Kuna mtu amenikumbusha tim ya RTC Kigoma,ilikua kiboko,maana enzi hizo kulikua na akina Patrick Mwangata,Omar Mavumbi,Yusuph Mfaume,Juma Haruna,Hamza Maneno,Dadi Fares,Cheche Kagile,Makumbi Juma,Ali Katolila,Wastara Baribari,Sanif Lazaro,Abdala Buruhani,Amri Ibrahim,Idd Makeresa,Willy Kamugisha,Na wengine wengi nimewasahau,hapo Lake Tanganyika Stadium ilikua inakua balaa.Mdau wa mwanga KGM UK.

    ReplyDelete
  18. NAKUBALIANA NA WADAU MPIRA WA ENZI HIZO ULIKUWA MPIRA TIMUZA DARAJA LA KWANZA ZOTE ZILIKUWA TISHIO NA LIGI ILIKUWA NA MVUTANO SIYO MAMBO YENU YA SASA...MIE NIMECHEZA MPIRA BONGO NA BAADHI YA WACHEZAJI AMBAO BAADAYE WALIKUJA KUWA MAARUFU..WAKINA MBUI JORDAN ALIKUWA CAPTAIN WETU TIMU YA UWANJA WA CCM KIRUMBA..HALAFU WENGI WAO WAMETOKA LAKE SECONDARY WAKINA NTEZE JOHN, JONH MWANZA ,WILLY ,, WENGINE WENGI TU TUMEKUTANA UMISETA KANDA YA ZIWA , JKT...N.K LAKINI JAMANI HATA DARAJA LA NNE ILIKUWA KAZI KUPANDA LA TATU MPIRA ULIKUWA NI MGUMU SIYO LELEMAMA KAMA SASA HIVI.. KILA MTU ANACHEZA...
    MDAU
    WA KAMACHUMU..

    ReplyDelete
  19. Hivi jamani siku hizi ni kwamba hakuna wachezaji weney talent kama zamani au basi tu sifuatilii, manake zamani likitajwa list la Yanga, Simba au Pamba. Kila position ina mchezaji mwenye jina na aliyebobea.Alafu wachezaji wa siku hizi afya ndogo. Mambo ya chips vumbi hayo , badala ya kuchapa ugali wa muhogo na Makande kama zamani.

    ReplyDelete
  20. Nilipoona jina TP Lindanda wana kawekamo.


    Namkumbuka sana mtangazaji marehemu DOMINIC CHILIMBO(RIP).

    Namkumbuka pia jamaa mmoja alikuwa shabiki mkubwa wa pamba alikuwa na baiskeli yake ambayo alikuwa anaitumia kufanyia manjonjo ya kushangilia..


    Bado nakumbuka majina kama George Magere Masatu,Alfan Ngasa,Fumo Felician,Madata Lugudisa..


    Nakumbuka enzi hizo sina kiingilia inabidi niende kwanza mlimani kitangiri(gola) kucheki gemu live kutoka milimani..aaa aaaa

    Ukiona dakika za lala salama tunaanza kujivuta ili kuingia "fungulia mbwa"..aaaa aa


    Nawakumbuka sana wadau wa Nyamagana,Nyanza,Nyakahoja,Kirumba etc siku zilikuwa mwake..

    ReplyDelete
  21. TP LINDANDA WANA KAWEKAMO!!! Walikuwa wanatandaza boli la kibrazili. Ushirika Moshi je, wadau mnaikumbuka? Nao walikuwa mpira chini. Pasi za uhakika zinagongwa kama nini.

    ReplyDelete
  22. 1.Paul Rwechungura
    2.David Mwakalebela
    3.Beya Simba
    4. ?
    5. George Masatu
    6. Hussein Masha
    7.Beya Simba
    8.Khalfan Ngassa
    9. John Makelele
    10. Juma Amir
    11.?

    ReplyDelete
  23. Du! wewe mdau ingawa mimi sio mshabiki wa kabumbu lakini mwenzangu umezidi kwa kuchapia. yaani hata Edibili naye alichezea Pamba? Mimi nakumbuka huyo alikuwa pale Shinyanga baadae Marehemu Gulamali akamtoa huko akaja kumrostisha Dar kwa kumleta Yanga. Baada ya kuwika wika kidogo, kuna wakati alienda kujaribu mprira nadhani Ujerumani kama sijakosea, akashindwa, na huo ndio ukawa mwisho wake.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  24. Paul Rwechungura yuko ndani Philadelphia,Fumo Yuko mwanza wengine sijui

    Mdau.

    ReplyDelete
  25. Mdau wa 2:42

    Namba nne uliyemwacha ni Abdalla Bori

    na 11 ni Fumo Felician

    Kuhusu Bori ni mchezaji pekee alipenda kunywa sana gongo kabla ya mechi. alisifika sana kwa hilo

    ReplyDelete
  26. Mbona mmemsahau libero/mkoba wa hiyo kikosi ya Pamba, Rajab Msoma, Kichochi Lemba, Alli Bushiri, Madata Lubigisa...Arusha napo Ndovu walikuwa mstarini...James Kisaka,Saidi Mrisho (Ziko wa Kilosa), Dunia Adonis, Juma Mkulila, Simon Kishoka, Muhudini Cheupe, Hamis Gaga, Lila Shomari, Rashid Iddi Chama, Mohamed Bob Chopa, Frank Kasanga Bwalya, Mohamed Mateneke,etc. Simba na Yanga wakijitahidi ni droo tu..!

    ReplyDelete
  27. 1)PAUL RWECHUNGURA
    2)DAVID MWAKALEBELA
    3)BEYA SIMBA,
    4)MKAMI MAO
    5)MASATU
    6)HUSSEIN MASHA
    7)KITWANA SELEIMANI
    8)KHALFAN NGASSA
    9)JOHN MAKELELE
    10)JUMA AMIR
    11)BEYA SIMBA

    ILA JAMANI TIMU ZA MWANZA SIO MCHEZO~~~EXPRESS,OAU,NA TIMU MOJA YA MABATINI DUH!!!???

    ReplyDelete
  28. Huyo jamaa amekosea kidogo tu kuhusiana na Edibili, lakini ukweli bado unabaki pale pale tu kwamba TP-Lindanda ilikuwa ni miongoni mwa timu zilizotisha wakati ule wa miaka ya 90. Ukiacha Simba na Yanga, basi Pamba (TP-Lindanda)na Coastal Union (wagosi wa kaya) walikuwa wakifuatia. Wacha leo niwakumbushe line-ups za timu hizi mbili:
    Pamba:
    1. Paul Rwechungura
    2. David Mwakalebela
    3. Abdallah Bori/Deo Mkuki
    4. James Washokera/ Khalfan Ngasa
    5. George Masatu
    6. Mao Mkami/Juma Limonga
    7. Beya Simba
    8. Hussein Masha
    9. Hamza Mponda/Juma Amiri Maftah
    10.Kitwana Selemani/Danny Muhoja
    11.Fumo Felician

    Coastal Union:
    1. Hamisi Makene/Mohamed Mwameja
    2. Said Kolongo
    3. Joseph Lazaro
    4. Douglas Muhani
    5. Idrisa Ngulungu
    6. Ally Maumba
    7. Ally Jangalu
    8. Kassa Mussa
    9. Juma Mgunda
    10. Hussein Mwakuluzo
    11. Razak Yusuf kaleka

    I think you have now got a good memory of who were in line ups of those two teams. Thanks and stop accusing the initiator of this good topic on TP-Lindanda.

    ReplyDelete
  29. Maji maji:
    1. Steven Nemes
    2. Abdul Ntila
    3. Samri Ayubu (Beki mstaarabu)
    4. Peter Mhina
    5. Mhando Mdeve
    6. Octavian Mrope
    7. Ahmed Kampira
    8. Mohamedi Mkandinga
    9. Peter Tino
    10. Madaraka Selemani
    11. Selestine Sikinde Mbunga

    ReplyDelete
  30. 1)PAUL RWECHUNGURA
    2)DEO MKUKI
    3)BEYA SIMBA,
    4)MKAMI MAO
    5)MASATU
    6)HUSSEIN MASHA
    7)KITWANA SELEIMANI
    8)KHALFAN NGASSA
    9)FUMO FELICIAN
    10)JUMA AMIR
    11)NTEZE JOHN

    hiyo list balikuwa banalokota kunyavu mpaka banachoka, kocha alikuwa mzaire. ukiingia ccm kirumba kuna bubu mlangoni anapenda rushwa huyo... sweet moments man! ikitokea penati masha anarudi nyuma one step kipa analala huku mpira unaingia huku
    Paul rwechungula yupo unyamwezini sijui state gani, masha nilisikia alikuwa UK, others dont know

    ReplyDelete
  31. Ushirika Moshi(Wasomi)
    1.Fanuel Singano/Bahatisha Nduluti
    2.Kaunda Mwakitobe/Kusianga Kiata
    3.Willy Martin
    4.David Rodger/Juma/Mahimbo
    5.Said John
    6.Michael John/Jaffar kiango
    7.Ereneo Mponzi/Said Ngobe
    8.Julius Kalambo/Poisont Moyo
    9.Omary Abbas/Venance Mwakaluko
    10.Abdallah Kaburu/Willy Kiango
    11.Waziri Ally/Ghalib Abeid
    Je Wadau mnakumbuka hichi kikosi kilivyokuwa kinawasumbua simba na yanga?John Makelele Alitokea hapa na kwenda Simba na Kalambo alikwenda Pan yeye na David Rodger.Hawa walikuwa wanaitwa watandazaji wa chini kama alivyokuwa akisema Mtaalamu Charles Hillary.Mpira enzi hizo siku hizi upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  32. nashukuru sana kwa kunikuna maana mmenikumbusha mbali sana ila mnakosea kiduchu tu kwenye line up yetu ya TP lindanda..BEYA SIMBA HAKUWA BEKI.
    1.PAUL RWECHUNGURA/JUMA MHINA/MADATA LUBIGISA
    2.DAVID MWAKALEBELA/ABDALLAH BORI
    3.DEO MKUKI/ALPHONCE MODEST,JOSEPH LUBISHA
    4.RAHID ABDALLAH 'MAGONGO'
    5.MIMI MWENYEWE 'KING'ANG'ANIZI'
    6.MAO MKAMI 'BALL DANCER'
    7.BEYA SIMBA
    8.HUSSEIN AMAN MARSHA
    9.HAMZA MPONDA
    10.NTEZE JOHN 'LUNGU'
    11.JUMA AMIR MAFTAH

    ReplyDelete
  33. To Magere

    Kama kweli ni wewe basi poa kishenzi maana uchezaji wako ulikuwa ni mzuri sana. lakini mbona hukuwataja wachezaji muhimu kama Fumo, Kitwana, Ngasa, Mhoja na wengineo au hawa walikuwa wanatokea bench?

    ReplyDelete
  34. wADAU WA JUU WALIOJARIBU KUPANGA TIMU WAMECHANGANYA SANA GENERATION MBILI TOFAUTI..KUNA LIST ILIYOPANDISHA DARAJA PAMBA ...BAADAYE WAKAJA VIJANA WAPYA.
    MFANO : Abdallah bori hajacheza na Deo Mkuki , Rashidi Abdallah umemchanganya na Ibra Magongo.. Danny Muhoja hajacheza na Kitwana Selemani..James Washokera na Juma Limonga hawajawahi kuchezea Pamba mie pamba damu siyo mshabiki tu.....PAMBA ONE ILIKUWA NA WATU WAFUATAO:- JUMA MHINA/MADATA LUBIGISA JORAMU MWAKATIKA , ISSA MELOO ,RAJAB RISASI ,RAPHAEL PAUL ,DANNY MUHOJA, IBRA MAGONGO ,RASHID ABDALLAH ,KHALIFAN NGASSA, KHALID BITEBO (MZUZU),EDWARD HIZA WAGINE WAMENITOKA NISAIDIE WADAU....>>> ALAFU NDIYO IKAJA HIYO PAMBA 2 YA VIJANA WOTE HAO ...WENGI WAO TOKA TOTO AFRICAN NA TIMU NYINGINE ZA HAPO MZA , VILE VILE TIMU ZA KANDA YA ZIWA NA UMISETA....
    WADAU JAZIE BASI MAONI YENU MENGINE KUHUSU TP LINDANDA
    Mdau wa KAMACHUMU..

    ReplyDelete
  35. kwani george gole, jemin kihiza na dad faris hawakuchezea pamba mbona hawatajwi?mpiga debe wao alikuwa marehemu dominic chilambo

    ReplyDelete
  36. Kweli mnikumbusha mbali sana,nakumbuka Mechi ya Simba/Pamba kwenye Uwanja wa shamba la bibi,jinsi mchezaji huyu Fumo Felician alivyoonyesha unazi wake wa Simba,na kuzomewa sana na wanazi wa Yanga.Lakini balaa liliwakuta siku walipocheza Yanga/Pamba,Fumo alionyesha kiwango cha juu sana,kiasi kwamba nasikia mhindi mmoja mnazi wa Yanga alifariki kwa ugonjwa wa moyo (Pb) hapohapo U/Taifa.
    Hakika wadau wa Mwanza jitahidini kurudisha heshima ya timu hii- wana TP Lindanda-kawekamo.

    ReplyDelete
  37. Kweli mnikumbusha mbali sana,nakumbuka Mechi ya Simba/Pamba kwenye Uwanja wa shamba la bibi,jinsi mchezaji huyu Fumo Felician alivyoonyesha unazi wake wa Simba,na kuzomewa sana na wanazi wa Yanga.Lakini balaa liliwakuta siku walipocheza Yanga/Pamba,Fumo alionyesha kiwango cha juu sana,kiasi kwamba nasikia mhindi mmoja mnazi wa Yanga alifariki kwa ugonjwa wa moyo (Pb) hapohapo U/Taifa.
    Hakika wadau wa Mwanza jitahidini kurudisha heshima ya timu hii- wana TP Lindanda-kawekamo.

    ReplyDelete
  38. acheni hizo timu ilikuwa African Sports bwana..,Hebu mwenye list atuletee

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 10, 2010

    African sports
    Duncan mwambammakonde
    francis mandoza
    bakari tutu
    hassan banda
    muhando mdeve
    steven kinduru
    abass mchemba
    twaha omar
    victor mkanwa
    bkari mchunga
    juma burhan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...