MICHUZI,
Kama kuna timu ya mpira wa miguu iliyowahi kunivutia ni Pamba ya Mwanza wana TP Lindanda.
Kama kuna timu ya mpira wa miguu iliyowahi kunivutia ni Pamba ya Mwanza wana TP Lindanda.
Je wewe na wadau wako wanaweza kuniambia ni wapi walipo baadhi ya wachezaji wa timu hiyo mwanzoni mwa miaka ile ya tisini?
Paul Rwechungura, George Masatu, Hussein Masha, Nteze John, Fumo Felician, Abdallah Bori, Khalfan Ngassa, Mao Mkami, Edibily Lunyamila, Bea Simba, Abdallah Kaburu, Kitwana Suleiman na wengineo?
NAWAKILISHA MKUU
Mdau Dar.
Lunyamila hakuwahi kuchezea Pamba, alikuwa RTC Shinyanga baada ya hapo akachukuliwa Yanga (au kuna timu nyingine alichezea lakini sio TP Lindanda)
ReplyDeletedeo mkuki na alphonce modest Dan mhoja John makelele Hamza mponda Beya simba jamaa walifunika enzi yao
ReplyDeleteMdau fanya utafiti kwanza kabla ya kuanza kuandika maana unataka kuwachokoza waosha vinywa. E.Lunyamila hakuwahi kuchezea Pamba pumbavu we!!!!
ReplyDeletelunyamila hajawahi chezea pamba.
ReplyDeleteMimi sio mfatiliaje wa mpira, lakini nakumbuka Fumo Felician nilimsikia miaka hiyo. Alikuwa kinara wa Pamba. Ukisema Pamba ya Mwanza unamuongelea Fumo Felician!
ReplyDeleteMdau kwa jinsi inavyoonekana wewe ni shabiki gazeti na redio, pia vikao redio za mbao vya kabla ya mechi na baada ni vyako sana , maana hii lizi ina hadi Edibily, Kaburu? Huyu si alikuwa Pilsner kama sijasahau..we haya we!
ReplyDeleteYaani amekosea tu mchezaji mmoja ndio kumtukana?? Anachosema tu ni kwamba TP Lindanda ilivyokuwa na wachezaji moto na hilo halina ubishi kuna wengine nadhani kama Bitebo na mwingine namba kumi wao alikuwa jina kama Hiza au Hija.
ReplyDeleteHalafu pia kulikuwa na timu nyingine zilizokuwa moto mfano RTC Kagera ya akina Kichochi Lemba. Na pia RTC Kigoma ya akina Mwangata.
hivi yule rajabu musoma hakukipiga na hao washikaji wengine dogo alikuwa tishio sana
ReplyDeletepoa tu issa isghu za soka mpira zetu za muziki-nyimbo za zamani unabana haina noma bwana si unapendelea kwakuwa wewe ni mkuu wa wilaya
ReplyDeleteAlfonce Modest hivi aliwahi kuichezea Pamba ya mwanza?mimi ninakumbuka alikua Reli ya morogoro na simba.
ReplyDeletelunyamila hakuwahi kuwa mchezaji wa pamba hapo umechemsha mdau
ReplyDeletetimu ilikuwa ileeeeee Reli Morogoro - Kibogo ya Vigogo.wachezaji wake hawakuwa na majina ya kutisha lkn nakumbuka ilikuwa kizaazaa sana wakiwa uwanjani.nakumbuka majina machache kama kina Sahau Kambi,Hamisi Fujo,Juma Limonga,Adam Selemani,Dancun Butinini,David Mihambo,Abdallah Mkali,Masenga,Mbuyi Yondani,na wengine kadhaa.Majimaji Songea nao walikuwa wamo somehow.ila kwa saaana nalikuwa napenda sana ule utani wa jadi baina ya African Sports na Coast Union ya miaka ileeee.
ReplyDeleteyani soka ya kipindi ile kama ingekuwa na aksesi ya pesa kama sasa hivi labda tungekuwa na wachezaji kadhaa Yuropu.
ebwana umenivunja mbavu kweli kwani jamaa umemtukana sana muombe msamaha lakini,lakini pia awe ana fikilia kuandika kitu kwani kuna watu wana kumbu kumbu kuliko yeye.kuna akina ali bushiri,hamza mponda,juma mhina kipa.na wengine wengi tu.na hata kama anataka kufaham walipo aulize watu watampatia informasion UKEREWE HAPA.
ReplyDeleteEDIBILLY LUNYAMILA NI MWENYEJI WA KIGOMA NA ALIONEKANA KUWA NI MTU WA MPIRA KWA MARA YA KWANZA ALIPOCHEZEATIMU YA UMISETA YA KIGOMA, UMISETA NI MASHINDANO YA TIMU ZA SEKONDARI ZIKU HIZO ZA MIKOA
ReplyDeleteH.Makene,S.WAZIRI,M.Mwameja(goalies)Dougals muhani,Muhando mdeve,Hilaly hemed(dogodogo)razak yusuf(careca)Husein Mwakuruzo(luga)Elisha john,Raphael john,Victor kepha Mnkanwa,Abdallah Burhan,Kasa Mussa,Kassim Mwajeki,Ali Maumba,Mohamed Kampira,Idrisa Ngulungu,Said Kolongo,Joseph lazaro,Abbas Mchemba,Mchunga Bakari,wadau wa tanga nisaidieni kumalizi majina yao nimewachanganya coastal union na wana kimanumanu african sports...TANGA OYEEEEEEEEEEEEEE.
ReplyDeleteYeah hiyo ilikuwa inaitwa TP-Lindanda wana kawekamo hapo mjini Kirumba ilikuwa tatizo..PAMBA VS YANGA , PAMBA VS SIMBA , PAMBA VS MAJIMAJI....Jukwaani kakaa Charles Hillary bwana wee pembeni kakaa Beya Simba katikati Kitwana SELEMANI pembeni Hamza Mponda ,huku mpishi mwenyewe Hussein Masha ,last man mzee mzima George Masatu ,halafu ball dance Mao Mkami,Sheikh Amir Mafutaha nyie acheni hao walikuwa wacheza mpira siyo mambo ya siku hizi wapiga hewa wanaitwa wachezaji.... jamani tukubali lakini Tanzania football ya mpaka 90-es haitakaa ikarudi tena hasikudanganye mtu even social atmosphere was really different with situation nowdays ingawaje financially enzi hizi mpira ulikuwa haulipi ndiyo maana wachezaji wote wa miaka hiyo wanasukuma maisha, second the football of the 90-es hakuonyesha mafanikio internationally but for local standard was great moment in the society
ReplyDeleteNakumbuka mechi Simba vs Pamba -Dar
with 10 minute John Makelele aliisha funga bao 3 dhidi ya Pamba ...Charles Hillary ana-comment ...John Makelele ZIGZAG anawanyanyasa wenzake hapa bao la tatu we hacha tu ,baada ya mechi hiyo gari la simba zilisukumwa mpaka msimbazi wanawake walitandika kanga barabarani basi inapita juu... hiyo ilikuwa issue siyo mambo ya siku hizi Simba vs Yanga mjini watu wamejaa miaka hiyo bwana mechi kama hiyo huoni mtu mjini kuanzia saa tisa watu wote Taifa...
Mwanza ndiyo usiseme siku ya mechi ni sherehe mji mzima ilikuwa kama meeting point "CCM KIRUMBA' nakumbuka Lake siku hiyo hata kama kuna self-relience Magadura alikuwa anaachia watu tu.......
yeah it was nice memory for our generation....
TP LINDANDA...
Mdau
Wa kamachumu
Doh! Kuna mtu amenikumbusha tim ya RTC Kigoma,ilikua kiboko,maana enzi hizo kulikua na akina Patrick Mwangata,Omar Mavumbi,Yusuph Mfaume,Juma Haruna,Hamza Maneno,Dadi Fares,Cheche Kagile,Makumbi Juma,Ali Katolila,Wastara Baribari,Sanif Lazaro,Abdala Buruhani,Amri Ibrahim,Idd Makeresa,Willy Kamugisha,Na wengine wengi nimewasahau,hapo Lake Tanganyika Stadium ilikua inakua balaa.Mdau wa mwanga KGM UK.
ReplyDeleteNAKUBALIANA NA WADAU MPIRA WA ENZI HIZO ULIKUWA MPIRA TIMUZA DARAJA LA KWANZA ZOTE ZILIKUWA TISHIO NA LIGI ILIKUWA NA MVUTANO SIYO MAMBO YENU YA SASA...MIE NIMECHEZA MPIRA BONGO NA BAADHI YA WACHEZAJI AMBAO BAADAYE WALIKUJA KUWA MAARUFU..WAKINA MBUI JORDAN ALIKUWA CAPTAIN WETU TIMU YA UWANJA WA CCM KIRUMBA..HALAFU WENGI WAO WAMETOKA LAKE SECONDARY WAKINA NTEZE JOHN, JONH MWANZA ,WILLY ,, WENGINE WENGI TU TUMEKUTANA UMISETA KANDA YA ZIWA , JKT...N.K LAKINI JAMANI HATA DARAJA LA NNE ILIKUWA KAZI KUPANDA LA TATU MPIRA ULIKUWA NI MGUMU SIYO LELEMAMA KAMA SASA HIVI.. KILA MTU ANACHEZA...
ReplyDeleteMDAU
WA KAMACHUMU..
Hivi jamani siku hizi ni kwamba hakuna wachezaji weney talent kama zamani au basi tu sifuatilii, manake zamani likitajwa list la Yanga, Simba au Pamba. Kila position ina mchezaji mwenye jina na aliyebobea.Alafu wachezaji wa siku hizi afya ndogo. Mambo ya chips vumbi hayo , badala ya kuchapa ugali wa muhogo na Makande kama zamani.
ReplyDeleteNilipoona jina TP Lindanda wana kawekamo.
ReplyDeleteNamkumbuka sana mtangazaji marehemu DOMINIC CHILIMBO(RIP).
Namkumbuka pia jamaa mmoja alikuwa shabiki mkubwa wa pamba alikuwa na baiskeli yake ambayo alikuwa anaitumia kufanyia manjonjo ya kushangilia..
Bado nakumbuka majina kama George Magere Masatu,Alfan Ngasa,Fumo Felician,Madata Lugudisa..
Nakumbuka enzi hizo sina kiingilia inabidi niende kwanza mlimani kitangiri(gola) kucheki gemu live kutoka milimani..aaa aaaa
Ukiona dakika za lala salama tunaanza kujivuta ili kuingia "fungulia mbwa"..aaaa aa
Nawakumbuka sana wadau wa Nyamagana,Nyanza,Nyakahoja,Kirumba etc siku zilikuwa mwake..
TP LINDANDA WANA KAWEKAMO!!! Walikuwa wanatandaza boli la kibrazili. Ushirika Moshi je, wadau mnaikumbuka? Nao walikuwa mpira chini. Pasi za uhakika zinagongwa kama nini.
ReplyDelete1.Paul Rwechungura
ReplyDelete2.David Mwakalebela
3.Beya Simba
4. ?
5. George Masatu
6. Hussein Masha
7.Beya Simba
8.Khalfan Ngassa
9. John Makelele
10. Juma Amir
11.?
Du! wewe mdau ingawa mimi sio mshabiki wa kabumbu lakini mwenzangu umezidi kwa kuchapia. yaani hata Edibili naye alichezea Pamba? Mimi nakumbuka huyo alikuwa pale Shinyanga baadae Marehemu Gulamali akamtoa huko akaja kumrostisha Dar kwa kumleta Yanga. Baada ya kuwika wika kidogo, kuna wakati alienda kujaribu mprira nadhani Ujerumani kama sijakosea, akashindwa, na huo ndio ukawa mwisho wake.
ReplyDeleteMdau
Cardiff
Paul Rwechungura yuko ndani Philadelphia,Fumo Yuko mwanza wengine sijui
ReplyDeleteMdau.
Mdau wa 2:42
ReplyDeleteNamba nne uliyemwacha ni Abdalla Bori
na 11 ni Fumo Felician
Kuhusu Bori ni mchezaji pekee alipenda kunywa sana gongo kabla ya mechi. alisifika sana kwa hilo
Mbona mmemsahau libero/mkoba wa hiyo kikosi ya Pamba, Rajab Msoma, Kichochi Lemba, Alli Bushiri, Madata Lubigisa...Arusha napo Ndovu walikuwa mstarini...James Kisaka,Saidi Mrisho (Ziko wa Kilosa), Dunia Adonis, Juma Mkulila, Simon Kishoka, Muhudini Cheupe, Hamis Gaga, Lila Shomari, Rashid Iddi Chama, Mohamed Bob Chopa, Frank Kasanga Bwalya, Mohamed Mateneke,etc. Simba na Yanga wakijitahidi ni droo tu..!
ReplyDelete1)PAUL RWECHUNGURA
ReplyDelete2)DAVID MWAKALEBELA
3)BEYA SIMBA,
4)MKAMI MAO
5)MASATU
6)HUSSEIN MASHA
7)KITWANA SELEIMANI
8)KHALFAN NGASSA
9)JOHN MAKELELE
10)JUMA AMIR
11)BEYA SIMBA
ILA JAMANI TIMU ZA MWANZA SIO MCHEZO~~~EXPRESS,OAU,NA TIMU MOJA YA MABATINI DUH!!!???
Huyo jamaa amekosea kidogo tu kuhusiana na Edibili, lakini ukweli bado unabaki pale pale tu kwamba TP-Lindanda ilikuwa ni miongoni mwa timu zilizotisha wakati ule wa miaka ya 90. Ukiacha Simba na Yanga, basi Pamba (TP-Lindanda)na Coastal Union (wagosi wa kaya) walikuwa wakifuatia. Wacha leo niwakumbushe line-ups za timu hizi mbili:
ReplyDeletePamba:
1. Paul Rwechungura
2. David Mwakalebela
3. Abdallah Bori/Deo Mkuki
4. James Washokera/ Khalfan Ngasa
5. George Masatu
6. Mao Mkami/Juma Limonga
7. Beya Simba
8. Hussein Masha
9. Hamza Mponda/Juma Amiri Maftah
10.Kitwana Selemani/Danny Muhoja
11.Fumo Felician
Coastal Union:
1. Hamisi Makene/Mohamed Mwameja
2. Said Kolongo
3. Joseph Lazaro
4. Douglas Muhani
5. Idrisa Ngulungu
6. Ally Maumba
7. Ally Jangalu
8. Kassa Mussa
9. Juma Mgunda
10. Hussein Mwakuluzo
11. Razak Yusuf kaleka
I think you have now got a good memory of who were in line ups of those two teams. Thanks and stop accusing the initiator of this good topic on TP-Lindanda.
Maji maji:
ReplyDelete1. Steven Nemes
2. Abdul Ntila
3. Samri Ayubu (Beki mstaarabu)
4. Peter Mhina
5. Mhando Mdeve
6. Octavian Mrope
7. Ahmed Kampira
8. Mohamedi Mkandinga
9. Peter Tino
10. Madaraka Selemani
11. Selestine Sikinde Mbunga
1)PAUL RWECHUNGURA
ReplyDelete2)DEO MKUKI
3)BEYA SIMBA,
4)MKAMI MAO
5)MASATU
6)HUSSEIN MASHA
7)KITWANA SELEIMANI
8)KHALFAN NGASSA
9)FUMO FELICIAN
10)JUMA AMIR
11)NTEZE JOHN
hiyo list balikuwa banalokota kunyavu mpaka banachoka, kocha alikuwa mzaire. ukiingia ccm kirumba kuna bubu mlangoni anapenda rushwa huyo... sweet moments man! ikitokea penati masha anarudi nyuma one step kipa analala huku mpira unaingia huku
Paul rwechungula yupo unyamwezini sijui state gani, masha nilisikia alikuwa UK, others dont know
Ushirika Moshi(Wasomi)
ReplyDelete1.Fanuel Singano/Bahatisha Nduluti
2.Kaunda Mwakitobe/Kusianga Kiata
3.Willy Martin
4.David Rodger/Juma/Mahimbo
5.Said John
6.Michael John/Jaffar kiango
7.Ereneo Mponzi/Said Ngobe
8.Julius Kalambo/Poisont Moyo
9.Omary Abbas/Venance Mwakaluko
10.Abdallah Kaburu/Willy Kiango
11.Waziri Ally/Ghalib Abeid
Je Wadau mnakumbuka hichi kikosi kilivyokuwa kinawasumbua simba na yanga?John Makelele Alitokea hapa na kwenda Simba na Kalambo alikwenda Pan yeye na David Rodger.Hawa walikuwa wanaitwa watandazaji wa chini kama alivyokuwa akisema Mtaalamu Charles Hillary.Mpira enzi hizo siku hizi upuuzi mtupu.
nashukuru sana kwa kunikuna maana mmenikumbusha mbali sana ila mnakosea kiduchu tu kwenye line up yetu ya TP lindanda..BEYA SIMBA HAKUWA BEKI.
ReplyDelete1.PAUL RWECHUNGURA/JUMA MHINA/MADATA LUBIGISA
2.DAVID MWAKALEBELA/ABDALLAH BORI
3.DEO MKUKI/ALPHONCE MODEST,JOSEPH LUBISHA
4.RAHID ABDALLAH 'MAGONGO'
5.MIMI MWENYEWE 'KING'ANG'ANIZI'
6.MAO MKAMI 'BALL DANCER'
7.BEYA SIMBA
8.HUSSEIN AMAN MARSHA
9.HAMZA MPONDA
10.NTEZE JOHN 'LUNGU'
11.JUMA AMIR MAFTAH
To Magere
ReplyDeleteKama kweli ni wewe basi poa kishenzi maana uchezaji wako ulikuwa ni mzuri sana. lakini mbona hukuwataja wachezaji muhimu kama Fumo, Kitwana, Ngasa, Mhoja na wengineo au hawa walikuwa wanatokea bench?
wADAU WA JUU WALIOJARIBU KUPANGA TIMU WAMECHANGANYA SANA GENERATION MBILI TOFAUTI..KUNA LIST ILIYOPANDISHA DARAJA PAMBA ...BAADAYE WAKAJA VIJANA WAPYA.
ReplyDeleteMFANO : Abdallah bori hajacheza na Deo Mkuki , Rashidi Abdallah umemchanganya na Ibra Magongo.. Danny Muhoja hajacheza na Kitwana Selemani..James Washokera na Juma Limonga hawajawahi kuchezea Pamba mie pamba damu siyo mshabiki tu.....PAMBA ONE ILIKUWA NA WATU WAFUATAO:- JUMA MHINA/MADATA LUBIGISA JORAMU MWAKATIKA , ISSA MELOO ,RAJAB RISASI ,RAPHAEL PAUL ,DANNY MUHOJA, IBRA MAGONGO ,RASHID ABDALLAH ,KHALIFAN NGASSA, KHALID BITEBO (MZUZU),EDWARD HIZA WAGINE WAMENITOKA NISAIDIE WADAU....>>> ALAFU NDIYO IKAJA HIYO PAMBA 2 YA VIJANA WOTE HAO ...WENGI WAO TOKA TOTO AFRICAN NA TIMU NYINGINE ZA HAPO MZA , VILE VILE TIMU ZA KANDA YA ZIWA NA UMISETA....
WADAU JAZIE BASI MAONI YENU MENGINE KUHUSU TP LINDANDA
Mdau wa KAMACHUMU..
kwani george gole, jemin kihiza na dad faris hawakuchezea pamba mbona hawatajwi?mpiga debe wao alikuwa marehemu dominic chilambo
ReplyDeleteKweli mnikumbusha mbali sana,nakumbuka Mechi ya Simba/Pamba kwenye Uwanja wa shamba la bibi,jinsi mchezaji huyu Fumo Felician alivyoonyesha unazi wake wa Simba,na kuzomewa sana na wanazi wa Yanga.Lakini balaa liliwakuta siku walipocheza Yanga/Pamba,Fumo alionyesha kiwango cha juu sana,kiasi kwamba nasikia mhindi mmoja mnazi wa Yanga alifariki kwa ugonjwa wa moyo (Pb) hapohapo U/Taifa.
ReplyDeleteHakika wadau wa Mwanza jitahidini kurudisha heshima ya timu hii- wana TP Lindanda-kawekamo.
Kweli mnikumbusha mbali sana,nakumbuka Mechi ya Simba/Pamba kwenye Uwanja wa shamba la bibi,jinsi mchezaji huyu Fumo Felician alivyoonyesha unazi wake wa Simba,na kuzomewa sana na wanazi wa Yanga.Lakini balaa liliwakuta siku walipocheza Yanga/Pamba,Fumo alionyesha kiwango cha juu sana,kiasi kwamba nasikia mhindi mmoja mnazi wa Yanga alifariki kwa ugonjwa wa moyo (Pb) hapohapo U/Taifa.
ReplyDeleteHakika wadau wa Mwanza jitahidini kurudisha heshima ya timu hii- wana TP Lindanda-kawekamo.
acheni hizo timu ilikuwa African Sports bwana..,Hebu mwenye list atuletee
ReplyDeleteAfrican sports
ReplyDeleteDuncan mwambammakonde
francis mandoza
bakari tutu
hassan banda
muhando mdeve
steven kinduru
abass mchemba
twaha omar
victor mkanwa
bkari mchunga
juma burhan