maofisa wa kamisheni ya ushindani wa haki (fair competition commission) wakis=choma moto bidhaa feki zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 25 kwenye dampo la pugu kinyamwezi nje ya jiji la dar. msemaji wa kamisheni hiyo amesema bidhaa hizo zilizoteketezwa zinafanya hesabu ya bidjhaa feki zilizochomwa moto kati ya mei 2007 na sasa kufikia thamani ya shilingi 1.625 bilioni. amesema karibu bidhaa zote, ikiwa ni pamoja na balbu, spe za magazi, vifaa vya umeme, feni, waya na kadhalika, zinatoka china

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Inamaana sisi hatujuia kwakufanya hivyo tunaaharibu mazingira,tume ya mazingira inafanya nini jamani?
    Ahsanteni!

    ReplyDelete
  2. Hata mimi inanishangaza sana maana hapo kuna kemikali nyingi tu na gas za sumu ambazo zimesambaa kutokana na kuchoma hizo bidhaa.

    1.Je kuna mtu alifanya tafakuri ya athari kama hizo za makemikali hayo na kujua athari kwa afya za viumbe, mimea, mazingira???!!
    2. Je kabla ya kuchoma walipata kibali cha tume ya mazingira?? Wizara ya Afya?? n.k.
    3. Yatakapotokea madhara aidha watu kuugua au wanyama je nani atafidia??
    4. Je tafakuri imefanyika kuhakikisha hizo kemikali na vitu vingine vilivyokuwemo vyenye athari vimeteketea kabisa hapo eneo na hakutakuwa na madhara??!!

    Mimi naamini watu wanaoishi katika eneo hili wanayohaki ya kuwasiliana na Tume ya haki za binadamu au waende mahakama kuu kuiomba iamrishe uchunguzi ufanyike ili hili jambo lichunguzwe na kuhakikisha hali yao ya maisha haitadhurika kutokana na jambo hili.

    Mzawa

    ReplyDelete
  3. Hata mimi inanishangaza sana maana hapo kuna kemikali nyingi tu na gas za sumu ambazo zimesambaa kutokana na kuchoma hizo bidhaa.

    1.Je kuna mtu alifanya tafakuri ya athari kama hizo za makemikali hayo na kujua athari kwa afya za viumbe, mimea, mazingira???!!
    2. Je kabla ya kuchoma walipata kibali cha tume ya mazingira?? Wizara ya Afya?? n.k.
    3. Yatakapotokea madhara aidha watu kuugua au wanyama je nani atafidia??
    4. Je tafakuri imefanyika kuhakikisha hizo kemikali na vitu vingine vilivyokuwemo vyenye athari vimeteketea kabisa hapo eneo na hakutakuwa na madhara??!!

    Mimi naamini watu wanaoishi katika eneo hili wanayohaki ya kuwasiliana na Tume ya haki za binadamu au waende mahakama kuu kuiomba iamrishe uchunguzi ufanyike ili hili jambo lichunguzwe na kuhakikisha hali yao ya maisha haitadhurika kutokana na jambo hili.

    Mzawa

    ReplyDelete
  4. Hayo madude mengine yanapoungua hutoa hewa na moshi ambao si mzuri kwa afya ya binadamu. Hawa wasimamizi wasichangamkie tenda ya kuchoma tu. Waombe vifaa/ mask za kujikinga. Au wawasiliane na watu wa zimamoto watawapa ushauri.

    Ni hatari kwa afya zao kama wataendelea kufanya uchomaji huo bila kujikinga.

    ReplyDelete
  5. Ama kweli bongo tambarare! Huu uchomaji wa kienyeji namana hii ni wazi kuwa una madhara kwa mazingira na viumbe hai waliopo karibu na eneo hilo achilia mbali hao pilisi wanaokenua na mitutu yao hapo. And I can bet- nusu ya hivi vinavyotakiwa kuchomwa moto vimeshauzwa na hao hao wanaojifanya wanajua kuviteketeza! Ipo mitambo ya kisasa ya kuchomea takataka kama hizi, serekali si inunue kwa vile vijisenti vyetu vya EPA vinavyorudishwa kimyakimya?

    ReplyDelete
  6. Ingefaa hizi bidhaa feki ziwekwe kwenye container na kurudishwa huko huko china zilikotoka. Na je, are the people responsible taken to jail for this?

    ReplyDelete
  7. Hivi mnaposema bidhaa feki mna maana gani? Bulb ya watts 100/60 inapowaka kama nyingine unaitambuaje kama ni feki? Siamimi kuwa mali zote za China ni feki, isije tukawa tunaburuzwa tu na wataalamu wa Marekani:) Haya bwana kazi kwenu!

    ReplyDelete
  8. Na mimi najiuliza hizo bidhaa feki ninini? Low quality au ni feki kwa aina gani...????? isije ikawa ni knock out Gucci handbag mnaichoma....kuwafanya matajiri na wafanya biashara kutoka USA waneemeke......

    ReplyDelete
  9. hizi bithaa zimeingiaje nchini? na ni nani kaziingiza? na ni hatua gani anachukuliwa au wanachukuliwa wausika? vitu kama ivi ni vizuri kivizuia kuingia toka bandarini. ngoja nijaribu kuwaelewesha watanzania wenzangu
    1. hivi vitu vimepitaje bandarini? ina maana serikali imechukua kodi batili mpaka vikaingia nchini au ni wahusika wa viwango hawako makini na kazi yao au ni rushwa imetolewa
    2. si sahihi kuonesha tu bithaa zikichomwa bila kutuonesha wahusika wamechukuliwa hatua gani?
    3.serikali iweke sheria na wataalamu zaidi katika bandari yetu ili vitu kama ivi visiingie tena maana bila kufanya ivyo utakuwa ni mchezo wa kila siku kuchoma nchi yetu itakuwa kama jalala la bithaa feki
    3.wale watanzania ambao wamenunua hizi bithaa tayari ambazo hazina viwango katika maduka yaliyosajiliwa na serikali watasaidiwaje?
    4.serikali ifanye msako katika maduka yote yanayouza vifaa bandia na maduka hayo yanyang'anywe leseni na wamiliki washtakiwe

    nchi yetu haiwezi kuendelea kamwe kama hatutafuata sheria na kuacha kutoa au kupokea rushwa. Watanzania tuamke kwa kweli tumelala

    mdau U.S.A

    ReplyDelete
  10. Kwa maoni yangu ni kuwa wananchi wote walionunua vitu feki kama hizo zilizochomwa wanatakiwa kuzirudisha dukani na kupewa pesa zao au kubadilishiwa(recall).
    Hiyo bandari ya Dar ni ujinga na tamaa tu vimejaa hapo hakuna ufanisi wa kazi hapo,maana inachukua mda mwingi sana kupitisha mizigo kuliko bandari yoyote ktk Africa na duniani.Kwani bandari nyingi inachukua masaa tu kutoa mizigo na hakuna mlolongo wa vikampuni vya wajanja kama hapo Dar.
    Mnapoteza mapato ya taifa kwa manufaa yenu nyie viongozi wazembe na wenye tamaa.
    Mheshimiwa JK hebu litazame hili suala.

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana na mdau wa March 01, 12:03 AM. Ingekuwa Kanali Mnali angewacharaza bakora hao waagizaji wa hizo bidhaa feki.

    Mnali for President 2010.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...