MBUNIFU wa mavazi wa muda mrefu Fatma Amour (pichani) anatarajia kufanya onyesho la mavazi litakalojulikana kwa jina la Kakakuona 2009. Onyesho hilo linakuja mahsusi katika kusherehekea siku kuu ya Wanawake duniani.

Onyesho hilo limepangwa kufanyika tarehe 7 Machi, 2009 katika ukumbi wa Dar alive zamani Malaika karibu na Cine club jijini Dar es salaam.. Onyesho litakalofanyika by the sea side na lina kuja na ujumbe “Unavyovaa ndivyo ulivyo”

Balozi wa Redds 2007 Victoria Martin, Miss Tanania 2008 Nasreen Karim, na Jamila Nyangasa Miss Internaional 2008, ni miongoni mwa wanamitindo watakaopita jukwani pamoja na wanamitindo wengine mahiri kutoka kampuni ya Dollywood Tz.
Kusindikiza shoo atakuwepo mwanamuziki anayekuja juu kwa sasa Angeris, pamoja na Ngoma za asili pia zitakuwepo kutoka kwa kundi maarufu la Simba Arts. Tiketi za onyesho zipo taryari mtaa kwa shilingi 20000/- tu (Piga namba 07137363610 ama 0713 689689 utaletewa ulipo).


Usiku huo wa aina yake utaweka kumbukumbu ya aina yake katika medani ya mitindo nchini kwa kuwa mavazi yatakayoonyeshwa ni yale ya kiasili, yaliyonakshiwa kwa vito vya kiafrika yanayojali rangi za kitaifa na muonekanao wa kupendeza.

Onyesho hilo linakuja juu ya udhamini makini wa Jarida la Exel, Dollywood Tanzania Ltd, DTP, Vayle Spring, British Council, JD Entertainment, Aqua Drill, Easy Finance, Sofia Productions, CxC Tours na Raque.com.
Fatma Amour ni mmoja wa wabunifu waliobobea nchini. Ni mbunifu wa mataji ya Redds Ambassador na mshindi wa shindano la ubunifu wa mavazi la Rafda kwa miaka miwili mfululizo.
Kwa wapenzi wa mitindo hii si ya kukosa.
Kwa mawasiliano Zaidi Simu
hizi hapa:
0784 700866
/ 0713 689 689

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...