Baada ya waalimu kucharazwa bakora, sasa ratiba ni kama ifuatavyo:

March---------------------Madaktari
April---------------------Wahandisi
May-----------------------Wachumi
June----------------------Wanasheria
July----------------------Wahasibu
August----------Wanafunzi vyuo vikuu
September-----------------Masekretari
October-------------------IT/paparazzi
November------------------Wainjilisti
December----Maaskofu/Wachungaji/Paroko/Mashehe


Wanafunzi nje ya nchi wasiliana na balozi nchi unayosoma.

Mwendo ndio huo mpaka heshima irudi. Mnali karejeshwa wizarani kuratibu utaratibu huu.

N.B: Usipoona kundi lako wasiliana haraka na DC aliye karibu na kituo chako cha kazi!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Mbona umewasahau mawaziri, wabunge ne wana siasa????????!!!!!!! Hawa ndio wanahitaji bakora za nguvu kweli kweli.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli michuzi Mstaafu wa jeshi ndugu mnali tupo naye hapa wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kama mratibu wa mafunzo kwa watumishi wote wa serikali-cheo kimepanda.....ila sijajua kama ataratibu zozi zima la ucharazaji wa bakora kwa kada tajwa hapo juu....labda niwasiliane na waziri wa TAMISEMI kujua hilo...nitakupigia simu kwa namba hii 0715 33 22 12.

    ReplyDelete
  3. acha nicheke tu,lakini zamu ya wanasheria moto utawaka!

    ReplyDelete
  4. sijakuelewa fafanua vizuri please

    ReplyDelete
  5. Michu umekosea tarehe,August ni zamu ya Baraza la mawaziri na mwenyekiti wao kula HAMSA WA ISHIRINI na tukio litaonyeshwa live katika TV

    ReplyDelete
  6. Wewe mwenyewe zamu yako lini ya kuchapwa viboko mbona hujaweka tarehe yako tukafahamu?

    ReplyDelete
  7. WANASIASA WAJANJA SANA

    Nadhani unaona mwenyewe jinsi walivyoandaa ratina ya hadaa, wao hawakujiweka. Mamblogger wanaipinga wanataka ianze na wasiasa. Wiki hii mawaziri, maRC, MaDC, Watendaji wa kata na vijiji na wengineo.

    ReplyDelete
  8. Tukimaliza na hao, tumchape Rais!

    ReplyDelete
  9. Oya Michuzi, hiyo mimi naiunga mkono. Lakini kama alivyosema mshkaji hapo juu mbona umewasahau wana-siasa (hasa wabunge)? Hawa mabwana wanatembelea mashangingi wakati hospitali hazina hata bajaji za kubeba wagonjwa? Pili, mabalozi wawakilishi nchi za nje je? Kuna mabalozi wanastahili hamsa hamsini kama mshkaji mwenza hapo juu alivyo-propose. Mfano, balozi majaa na mafisadi wenzie hapa UK wanastahili hilo. Wanasema wanatangaza TZ lakini hamna lolote. Tangazo pale victoria halikukaa hata wiki moja, mamilioni ya wadanganyika yakamezwa. All in all, naunga mkono hoja hii na jaribu kumshauri Mnali awajumuishe wana siasa pia na mabalozi. Thanks!

    ReplyDelete


  10. PENDEKEZO..

    MHESHIMIWA BALOZI WA ZAIN PELEKA SALAMU KWA MKUU WA NCHI AMTEUE MNALI KUWA WAZIRI MKUU ILI APATE FURSA YA KUTEMBEZA BAKORA KWA BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI NZIMA.

    ASANTE.

    ReplyDelete
  11. Aiesee umewasahau Wachoma nyama hasa wa kiti moto wanauwa sana ndugu zetu kwa pressure hapo Bongo.

    ReplyDelete
  12. Watu wanaweza kudhani kuwa it's a joke. Lakini mimi nafikiri hii nchi inahitaji mtu mmoja dizaini hiyo ambaye akili yake inafanyakazi kuliko ya kichaa, ambaye ataipeleka hii nchi mputamputa kwa walau kama term moja tu hivi. Yeye kazi yake itakuwa ni kunyoosha watu wawe na discipline ya kufanyakazi na kufuata sheria na haki akianzia na mawaziri (kama akina Ma**** na wengine wasiofuata utawala bora)na kushuka chini katika ngazi zote za serikali mpaka serikali za mitaa (kwenye vijimungu watu). Baada ya hapo ndipo aachie ngazi ampatie mwingine tuanze kurekebisha misingi ya kiuchumi.Tunahitaji watu kama Idd Amini (RIP)au Lyatonga Mrema (Kwa ajili ya kunyoosha watu tu) kwenye hii Inji.Vinginevyo hii nchi itafika mahali haitatawalika. Tutaendelea kulipa kodi watu watazichukua na kuwajengea mahawala zao mahekalu, tutaletewa misahada toka nje watu watapeleka kwenye akaunti zao visiwani, na wengine wa huku chini tutaendelea kuchinjana kimywa kimywa na wengine kufa kibudu kwenye vibanda vyetu vya kuku (kwa kukosa madaya ya kupunguza makali ya UKIMWI na malaria)na wake zetu wakiendelea kufia Hospitali ya mwananyamala kwa kukosa huduma salama ya kijifungua mpaka dakika za mwisho; huku tukiendelea kujidai kuwa kuna amani ya kudumu Tanzania (Heaven of peace-mwe!!).Kila mtu atakuwa anajifanyia vitu jinsi akili yake inavyomtuma na hakutakuwa na mtu wa kumnyooshea kidole.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  13. Ha ha ha ha ha kwakweli anco mithupu sasa unatuvunja mbavu...ila aliyesema wanasheria moto utawaka sikubaliani naye kwani wao kina nani bakora bakora tu tena za makalio na makoti yao!!!!!!!!!!!ha ha ha ha! tucheke tuongeze siku za kuishi...Big Up Mithupu

    ReplyDelete
  14. Braza Michuzi, tehe tehe tehe teh tehe tehe, acha nicheke kiuchungu'.
    Braza hapa umeone mbali sana.
    Taifa litajengwa tofali kwa tofali
    Mdau

    ReplyDelete
  15. Duh...hii imenivunja mbavu jamani..nyumbani kuna vituko...lol

    ReplyDelete
  16. Chapa kila mmoja mwenye kulipwa mshahara na umma kulingana na mshahara wa mfanyakazi!

    ReplyDelete
  17. Braza Michuzi mbona sijaona siku ya Makonda wa daladala na madereva wao? Hawa wangafaa waanze kabla ya other professionals maana akili zao siku zote ni nyingi sana. Mpe salaam JK na mwambie twamuunga mkono kumrudisha kamanda MNALI wizarani. Tena mambo yekeshatulia huyu kamanda anafaa kuwa Waziri mkubwa na makamu wake awe Mrema. Nawakilisha hoja mheshimiwa balozi!!.

    ReplyDelete
  18. mimi naomba mnipe ajira ya kuwacharaza manesi. hawa watu ni wauaji....hivi mnajua unesi ni wito kwa hiyo acheni kujishebedua eti malipo ni kiduchu

    ReplyDelete
  19. HA HA HA HA MICHUZIIIIIIII NAJUTA KUKUFAHAMU BIG UP SANA MICHUZI KWA POSTING HII.MI NAFIKIRI TUNGEANZA NA NA MANESI THEN MUHESHIMIWA MNALI JIFANYE CHIZI INGIA HADI IKULU KWA YULE JKM.CHAPA BAKORA WOTEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE IKULU.
    MDAU NGATUNGAAA.

    ReplyDelete
  20. wahandisi wasicharazwe, hawana kosa. kwakua wao kila kitu wanatumia hakili.

    ReplyDelete
  21. Michuzi katika ratiba yako naona kila mwezi kuwe na interval ya siku tano za mwanzo ziwe allocated kwa ajili ya kuwachapa MAFISADI. Hivyo basi, kila mwezi siku tano za mwanzo ni maalum kwa ajili ya MAFISADI eidha wawe wameshahukumiwa au bado kesi ziko mahakamani... yaaniii chapa chapa chapaa mpaka displin irudi nchi nzima

    ReplyDelete
  22. kwetu hakuna ubalozi wa bongo wala ofisi ndogo sasa tuende wapi jamaniiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  23. kifimbo cheza kije hapa DC ubalozini...kichape chape wote tu

    ReplyDelete
  24. Nionavyo mimi hakuna haja ya Tanzania kuwa na mabalozi kwani wamekuja huku nje kutalii tu na hawana msaada kwa wananchi wanapoenda kuwaomba msaada.Mfano nilikuwa na shida hapa Ubalozi UK nikaambiwa muhisika hayupo ila kuna anayemshikia nafasi yake.Nipomuuliza utaratibu wa kupata Tanzania Police criminal record letter akaniambia hajui mpaka muhusika mwenye ofisi arudi baada ya mwezi mmoja!!!Sasa kuna maana gani kumuachia kazi mtu hajuia hata namna ya kutatua shida hii ndogo.Na huu ni mfano mdogo tu,yapo mengi.

    ReplyDelete
  25. January - Mawaziri na Wabunge,
    February - Mapolisi na Trafiki na wanaachia mabasi yanatumaliza barabarani kila siku.

    ReplyDelete
  26. DU KAKA MICHU MI NAMFAGILIA SANA MNALI KWA STYLE YAKE YA BAKORA KWANI UPUUZI UMEZIDI TANZAINIA. MI NAPENDEKEZA PIA TIMU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU (TAIFA STARS) IWE YA KWANZA KTK RATIBA YA KUCHARAZWA BAKORA MIA SITA ZA MGONGO. HAMNA MSAMAHA SAFARI HII

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...