baadhi ya wanafunzi waandamizi wa karate mtindo wa goju ryu katika dojo (shule) yao ya zanaki enzi hizo. juu kulia ni japhet kaseba, bingwa wa kick boxing, ambaye wengi walikuwa hawafahamu kwamba mchezo huu aliuanza zamani tena katika shule inayofundisha karate halisi. wadau wa mwanza bila shaka huyo wa juu kushoto mnamkumbuka kwani si mwingine bali senpai mathew kalambo ambaye sasa ana mkanda mweusi na ni mwalimu ya goju ryu hapo mwanza kwenye ukumbi wa ghandi hall
hawa ni baadhi ya makarateka wa dojo la zanaki la goju ryu enzi hizo. wa pili shoto juu ni senpai murudker ambaye ndiye mwanafunzi mkuu katika dojo hilo hadi leo. kushoto kwake ni senpai almasi ambaye ni msaidizi wake. senpai kalambo wa mwanza amekaa wa pili shoto

eh!michuzi !umenikumbusha mbali!
ReplyDeletemaana pale Zanaki katika hekalu la kujilinda,nakumbuka chuo kile kulikuwa na kina SENSEI RUMADHA FUNDI na wenziwe akina MAGOMA wakiwa na mwalimu wa Sensei Nantambo Guru Kamara Bombani,mmerekani mwenye hasili ya kiafrika
eh!michuzi !umenikumbusha mbali!
ReplyDeletemaana pale Zanaki katika hekalu la kujilinda,nakumbuka chuo kile kulikuwa na kina SENSEI RUMADHA FUNDI na wenziwe akina MAGOMA wakiwa na mwalimu wa Sensei Nantambo Guru Kamara Bombani,mmerekani mwenye hasili ya kiafrika
We anony sio HASILI sema ASILI! na sio mmerekani, sema mmarekani
ReplyDeleteSensei Rumadha Fundi na Senpai Magoma, wao waliondoka Zanaki dojo kwenda India,Phillipine, Japan na Singapore 1982.
ReplyDeleteBaadae Sensei Rumadha kwenda Marekani 1988 na kujiunga na Master Sensei Morio Higaonna kule San Diego, Marekani. Senpai Magoma yupo Bongo na wote katika picha hapo waliwahi kufanya mazoezi pamoja na kina Michuzi enzi hizo.
Mdau.
Michuzi umenikumbusha wanakarateka wenzangu pale Zanaki Dojo.Picha ya juu hapo kulia namwona Mbesse (ndio Japhet) Chini wa kwanza kushoto namwona Mzee Almasi.
ReplyDeletePicha ya chini wa Kwanza kushoto waliosimama: ni Sempai Heri Kivuli, Mohamed Murudker (alikuwa na Hotel oposite na Shule ya msingi Mnazi Mmoja, Mzee Almasi, (anayefuata simkumbuki) na mwisho waliosisima kulia ni Sempai Mbezi.
Waliokaa kuanzia kushoto ni:
Sempai Charles, anayefuate simkumbuki, watatu ni Benson (huyo alikuwa anapenda kiingereza, nguzo za mafunzo yeye anataka kusema kwa kiingereza wakati nusu darasa ngeli ilikuwa haipandi. Wa mwisho hapo sikumbuki jina.
Asante sana Michuzi.
Muhidin,
ReplyDeleteWeka basi picha za walechekechea za watoto wa dojo Zanaki wadogo enzi zile kina Rumadha,Farid, Ahmed, Abdallah Atik na Feisal na wale watoto wa Upanga( Bomani Brigade)'78--81 hasa ktk maonyesho ya dojo kuzaliwa.
Kohai
picha chini walioketi namwona sempai charles (rip), na mstari wa kati namuona kariboti wa kwanza kushoto na sempai ndaukile wa kwanza kulia.
ReplyDeletekweli tumetoka mbali
Tarehe February 03, 2009 2:39 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteWewe ulikuwa pale lini? Kumbe Sempai chale hatunaye tena?
Tarehe February 02, 2009 9:08 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteWatoto wengine walikuwepo pale ni kina Seifu, Bibula, Mbesse (Japhet),Hamis (wa ilala),Masala,msofe's watoto mapacha, hao ni baadhininaowakumbuka Mbesse anafanya Kick Boxing siku hizi. Hao wengine sijui wako wapi siku hizi.