WAZIRI MKUU ASEMA KUFUTA LESENI ZA WAGANGA WA JADI NI HATUA YA MPITO
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kufutwa kwa leseni za waganga wa jadi ni hatua yampito inayojaribu kutafuta njia madhubuti ya kuwabaini waganga wa tiba asilia waliohalali na wasio halali.
Ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakatialipokutana na ujumbe wa Chama cha Waganga wa Tiba Asilia Tanzania (CHAWATIATA)ambapo alitumia fursa hiyo kuwaeleza ni kwa nini Serikali imefikia uamuzi wa kufutaleseni zote za waganga wa jadi kuanzia Januari 23, mwaka huu.
Waziri Mkuu alisema uamuzi huo ulitokana na mapendekezo yaliyotolewa na wagangawengi kwenye mikutano aliyoifanya wakati wa ziara yake katika mikoa ya Kagera,Mwanza, Tabora na Shinyanga kuhamasisha jitihada za Serikali za kupambana na vitendovya mauaji ya Albino na Vikongwe kwa imani za ushirikina.
Alisema mapendekezo yao yamefuatia kutotumika ipasavyo kwa Sheria ya Tiba Asili naTiba Mbadala Na. 23 ya mwaka 2002 (The Traditional and Alterntive Medicine Act,2002) ambayo kanuni za utekelezaji wake zilikuwa hazijatengenezwa.
Alisema kukosekana kwa kanuni hizi kumesababisha waganga wa jadi wasajiliwe kwakutumia taratibu za kiutendaji na si kisheria yaani kupitia Halmashauri za Miji,Manispaa na Halmashauri za Wilaya jambo ambalo pia limepenyeza mianya ya rushwa kwa watoa vibali vya waganga.
“Serikali haikusimamia vizuri suala hili tangu sheria ilipotungwa na matokeo yake kukawa hakuna mfumo halisi wa kuwatambua na kuwasajili waganga wa jadi, wenginewakatumia rushwa kupata vibali kwani baadhi ya Halmashauri ziligeuza usajili huu kuwa kama chanzo kimojawapo cha mapato… Halmashauri zilijali idadi ya watuwanaosajiliwa bila kuangalia kama ni waganga halali au matapeli,” alisema.
“Nilipomaliza ziara hiyo, tarehe 28 Januari nilimwandikia barua Waziri wa Afya naUstawi wa Jamii ili kujua hatua gani wamefikia kuhusu hizi kanuni kwani ni muda sasa umepita… leo hii (jana) amenijibu kuwa kanuni ziko tayari ila tulimshauri piaazingatie maoni tuliyopewa wakati wa ziara yangu hivi majuzi,” alifafanua.
Akifafanua, Waziri Mkuu alisema baadhi ya masuala yaliyotolewa maoni ni kuhakikisifa za mganga kwa kuangalia kama chanzo chake ni katika familia au la. Piawalishauri kwamba waganga watakaosajiliwa upya wawe wameidhinishwa na uongozi wakijiji, mtaa na kata wanazoishi na kutolea huduma zao.
“Ushauri mwingine tuliopewa ni kuhakikisha kwamba waganga wanaohamia sehemu nyinginewanakuwa na barua za utambulisho kutoka katika Halmashauri zao kwenda Halmashauriwanazohamia na pia wawe na vituo maalum vya kutolea huduma zao,” alisema.
Aidha, ilikubaliwa kwamba waganga watakaosajiliwa upya wasiwe na huduma za mikoba(outreach services) katika tiba asili kwani wengine huharibu sehemu moja nakukimbilia sehemu nyingine kwa kigezo cha kuhamisha huduma.
Waziri Mkuu alisema viongozi wa mikoa aliokutana nao wameagizwa kuanzia leo Februari mosi wasimamie zoezi la utoaji elimu kwa wananchi ili kuwahamasisha wawe tayari kushiriki kura ya maoni ya siri ambayo Rais Jakaya Kikwete alisema itafanyika nchinzima.
Katika hotuba yake ya mwaka mpya, Rais Kikwete alisema itaanzishwa kura hiyo ya siri ili wananchi wawataje waganga na wapiga ramli wanaoendeleza mauaji ya Albino naVikongwe, ili hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi yao.
Vilevile, Waziri Mkuu alisema mwezi Machi litaendeshwa zoezi la kupiga kura hizoambalo linatarajiwa kuendeshwa kwa kanda na liwe limekamilika ifikapo Machi 31,mwaka huu.
“Tukimaliza zoezi hilo, madodoso yatachambuliwa na taarifa zake zitasadiakubaini nani ni mganga halisi na nani si halali,” alisema.
Kwa upande wao, viongozi wa CHAWATIATA walimweleza Waziri Mkuu kwamba wanamuunga mkono kwa hatua yake ya kufuta leseni kwani wanaamini hatua hiyo itasadia kuharakisha utekelezaji wa sheria ya Tiba Asilia ambayo ilikuwa haijaanza kazi.
“Kuanza upya kwa usajili wa waganga wa jadi ni jambo ambalo tumekuwa tukiliomba kwamuda mrefu… tunafurahi kwa sababu litawezesha kuwa na mfumo mzuri wa usajili wawaganga na kuondoa waganga matapeli waliokuwa wamevamia fani hii,” alisema Katibu Mkuu wa Chama hicho, Bw. Mithan Magombeka ambaye alifuatana na Bi. Fatma Machangu ambaye ni Katibu Mwenezi wa CHAWATIATA.
waganga walio halali na wasio halali? are you joking guys? kwanza nadhani neno halali hapo limetumika vibaya. hata hivyo ningelipenda kujua ni vipi serikali wataweza kujua kama mganga huyu ni feki au si feki? wanakusudia kuwapa mitihani au test kabla ya kuwapa leseni? nangoja nione watakavyosimamia suali hili. Pia nashangazwa sana kuwa serikali inaamini kuwa kuna waganga wa kienyeji wa kweli. Je serikali inaweza ku-prove kwetu kuwa wako waganga wa kienyeji hao?
ReplyDeleteTHIS LIKE A POLICE STATE, HAISAIDII NA WALA HAITAONDOWA MA-ALUBINO KUULIWA, JUST POLITIKING.
ReplyDeleteAnony 3:25
ReplyDeleteKwanza naomba nikusahihishe kidogo. Serikali inatambua waganga wa jadi na siyo waganga kwa kienyeji kama ulivyosema wewe. Waganga wa Jadi ni wale ambao wanatumia dawa asilia ambazo wamerithi kutoka kwa mababu zetu kabla ya hizi hospitali na sawa za kisasa kuanza. Kwa mfano uchunguzi wa kisayansi umegundua kuwa mti wa mwarobaini una uwezo wa kupambana na magonjwa zaidi ya arobani kwenye mwili wa mwanadamu lakini huwezi kwenda hospitali wakakuambia katumie mwarobani, waganga wa jadi wana elimu hiyo. Kuna miti mingi ambayo inaweza ikapona magonjwa mbalimbali. Pia katika sehemu ambazo hazina hospitali watu wanaenda kwa waganga wa jadi, unaweza ukaenda kwa mganga wa jadi ukamuambia kwamba unaumwa kichwa mara kwa mara naye akakuambia inabidi unywe maji kwa wingi, matunda na mboga za majani au pengine akakupa miti shamba ambayo itakusaidia. Ukimuuliza sababu za kisayansi anaweza asiwe na jibu kwa kuwa yeye ni mganga wa jadi tu anakupa dawa kutokana na jadi. Ila ukienda kwa mganga halafu akakuambia nilitee kucha za jogoo na machozi ya bibi yako sasa hau ndiyo waganga ambao serikali inawatafuta.
Katika sekta ya Waganga wa Kienyeji kuna makundi matatu yanayo shabihiana sana:wapo Waganga wa Jadi,ambao kweli ndio wanaotibu kikwelikweli kwa kutumia mizizi na kiti shamba hata kwa maradhi mengine ambayo hospitali za kisasa pengine zilishindwa kutibu kikamilifu.Pili,wapo waganga wa kienyeji,ambao sio waganga kwelikweli bali ni wale waliovamia fani tu ili kutafuta pesa kwa njia za udanganyifu na kitapeli na wakati mwingine kwa kuzichonganisha familia mbalimbali huko vijiji.Tatu,wapo wanaojulikana kama Wachawi,ambao hufanya ni zaidi ya waganga wa jadi lakini watu wabaya na hatari sana katika jamii na huyafanya mambo yao kwa kificho na usiri mkubwa.Makundi yote hayo matatu yana ushirikiano mkubwa wa karibu.Wakati waganga wa jadi mara nyingi wamekuwa wakifanya uganga wao kwa uwazi zaidi na kwa kukata leseni kwa shughuli hizo,hayo makundi mengine mawili hufanya shughuli zao kwa kificho na hawakati leseni kwa shughuli hizo.Kwa hiyo, kufuatia kauli ya Pinda kwamba kuanzia sasa serikali itazifuta leseni zote za waganga wa jadi ili usajili uanze upya kwa lengo la kudhibiti waganga matapeli,je, kwa hayo makundi mengine mawili ambayo toka awali hayakuhitaji leseni kufanya shughuli zao, uamuzi huo wa serikali utakuwa na umuhimu gani kwao katika kuwazuia wasiendelee na shughuli zao?Ni Tatizo.Biashara hii ya Uganga wa Jadi inaendelea kushamiri hapa nchini kwasababu ina Soko.Lisingekuwepo Soko,biashara ya uganga isingedumu muda mrefu hata kidogo.Chimbuko la imani za kishirikina ni UJINGA NA UMASKINI.Maadui hao wawili ni Mapacha.Kufuta leseni tu peke yake kwa waganga wa jadi kwa maoni yangu mimi siyo suluhisho la kutosha kukabiliana kikamilifu na haya mauaji ya Albino na Vikongwe.Hata ukifuta leseni za waganga,wachawi bado wataendelea na mambo yao madhali Ujinga na Umaskini umekithiri vijijini!Idadi kubwa ya watanzania hivi sasa ni vijana wenye umri chini ya miaka 35.Wengi wao hawana ajira za uhakika.Hawana elimu ya kutosha wala ujuzi wowote wa kazi.Hata hicho Kilimo chenyewe ni kile cha Ujima cha kutumia jembe la mkono na kusubiri mvua zinyeshe.Kwa hiyo wanakabiliwa na umaskini mkubwa wa kipato.Katika kukabiliana na tatizo hili la mauaji ya Albino na Vikongwe, jitihada za ziada zitahitajika katika kuwabaini hawa waganga wa jadi na wakatambulika rasmi katika maeneo yao.Elimu ya kutosha itolewe kwa wanavijiji ili watambue kwamba hapatazuka mganga mwingine yeyote katika vitongoji vyao iwapo hapajafanyika Utambulisho wowote kwao uliofanywa na viongozi wa kijiji.Na akibainika yeyote atakaye fanya kazi ya Uganga wa Jadi bila ya kufuata utaratibu uliowekwa moja kwa moja atambulike kwamba mtu huyo ni Muuuaji na sheria ichukue mkondo wake.Taasisi za kidini zihusishwe kikamilifu katika zoezi hilo.Wanasosholojia(sociologists)pia wahusishwe kikamilifu katika zoezi hilo.Waalimu wa shule za msingi na sekondari waliopo katika maeneo hayo wapewe heshima yao kwa kuwafanya wao ndio wawe viongozi wa kamati mbalimbali zitakazo simamia na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi hayo katika kutokomeza kabisa mauaji ya Albino na Vikongwe vijijini.Vitabu vya Mungu vitumike katika kuwatoa watu katika Giza la Ushirikina kwa kumwogopa Mungu.---tony----
ReplyDeleteni JEHOVAH tu awezaye,,,
ReplyDeletemmh!!waziri huyu mboni simwelewi kwa kusahihisha matamshi yake ya awali?ina mana ana tungo tata anapokua aongea pao kwa hapo?kila siku ooooh sikumaanisha ivo vile,tumueleweje?hauna msimamo?
mi nahisi hizo dawa wanazotumia zingekuwa zinachunguzwa na wanafarmacia katika laboratory zinazohusika,ili kikajulikana kinachofanywa halafu zikafanywa procedure na test kwa wanyama kwanza kama zilivovumbuliwa dawa za hospitali nyengine na kuregistiwa,halafu dozi zikajulikana na kuuzwa kihalali,siyo karithi kwa babu mara kakupa dozi si saizi yake toxic n.k.
ReplyDeleteotherwise waganga wanaotumia mashetani na ramli hao ndo wa kufungiwa na kuwekwa mikakati kwa kila diwani wa eneo lake kufatili,a hilo manake tumechoka na huu ushirikina
Waziri mkuu amekosea kuwafutia leseni waganga kwani uamuzi wake haukuangalia uwiano wa waganga waliotuhumiwa katika mauaji ya albino na je kwa kufuta leseni hizo atawapatia wateja wa waganga hao tiba mbadala?
ReplyDeleteNi wazi tiba za kisasa za kikemikali hazina uwezo wa kuponya magonjwa sugu kama mitishmba yetu ndio maana mataifa kama uchina,india na wenzetu wa magharibi wanajitahidi sana kurudi kwenye mitishamba.Sasa ni ajabu badala ya kupambana na kiini cha tatizo ambacho ni kuelimishana tu kwamba albino ni hali na wala si viumbe ambao unaweza kuwaua ili kupata utajiri au vinginevyo.
waganga na hotspot za mauaji hayo hasa kanda ya ziwa serikali inaweza kuwekeza katika kuwaelimisha wahusika ili kutokana na imani potofu.
vilevile hakuna sababu ya wafamasia kuzipima dawa za kienyeji ukihitaji san avipimo inabidi uende kwenye modern medicine.
Bwana pinda angeangalia vilevile je wizara ya afya na hospitali zetu zinawafikia walengwa walioko vijiji vya mbali kabisa?kama jibu ni hapana je ametumia jazba za kisiasa na abuse of power kutoa uamuzi huo?
napenda kuwasilisha
NZEHE