Wadau msiwe na mashaka na kujiuliza wapi wapo INAFRIKA BAND?
Inafrika wametua ulaya kwa kishindo na kuanza kutingisha na kukamua vibaya vibaya!bendi hiyo ya mziki wa dansi inafanya tour ya ulaya kwa udhamini wa "Mama Afrika"bendi hiyo maarufu kutoka jijini Dar, imeshafanikiwa kutingisha katika majukwaa makubwa mbali mbali nchini Ujerumani,Uswiss,Austria na inaendelea kupeperusha bendera ya bongo kwa mlingoti wa mziki.
Inafrika band pia inawajulisha washabiki na wadau wote wa nyumbani Tanzania wasiwe na wasi wasi mara watakapo rudi bongo wanakuja na ALBUM MPYA ambayo ina mziki moto moto.
Inafrika jana walikuwa mjini Oldenburg,Ujerumani na walilakiwa na kiongozi wa bendi ya "The ngoma Africa" mwanamziki mashuhuri Ras Makunja aka bwana kichwa ngumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. POZI HILI LA HAO WAWILI WALIOCHUCHUMAA NI LA HARUSI? MBONA LINATIA MASHAKA.

    ReplyDelete
  2. MBONA HII HABARI HAILEWEKI LENGO LAKE. UNASEMA WAPO MAJUU THEN UNAANZA KULETA HISTORIA YA ZAMANI KUWA WALISHAWAHI KUTIKISA SEHEMU MBALIMBALI. PEOPLE ARE NOT INTERESTED WITH THOSE OLD STORIES.. WAPE WATU HABARI KAMILI KUWA JAMAA WAPO WAPI NA WANATARAJIA KUTUMBUIZA WAPI NA WAPI ILI IKIWEZEKANA WATU WAJIPANGE. AU NDIO YALE YALE YA KUTUMBUIZA KWENYE BIRTHDAY ZA WATU..??? HIZI HABARI NYINGINE ZA KUUZISHA WATU SURA NAFIKIRI ZINAJAZA TU NAFASI BRO MICHU.

    ReplyDelete
  3. Nawapenda sana hii bendi, je wanarudi lini bongo ama wanakuja lini hapa netherlands, plz bro michuzi nijulishe maana nategemea kwenda bongo soon ila kama wanakuja netherlands itakuwa bomba sana.

    Mdau Ned

    ReplyDelete
  4. Duuu walialikwa na Ras Makunja, yule kichwa kichaa kumbe mkarimu hivyo

    ReplyDelete
  5. Inafrika si vibaya kuweka angalau nyimbo mbili ktk mtandao wa Youtube ile watu pande zote za ulimwengu waitambue Inafrika Band na Tanzania. Pia inaweza kupelekea kupata mialiko lukuki ndani ya Afrika na mabara mengine baadaya promoters kuona vitu vyenu ktk Youtube.

    Kilimanjaro Connection, Kilimanjaro Band(njenje), Msondo Ngoma Band, Vumbi Dekula Kahanga, tayari wanaanza kuonekana duniani kwa Youtube bureee.

    ReplyDelete
  6. Brother Michu
    thanks for showing me my neighbours kumbe bado wanaendelea na band,huyo kaka anaitwa ROY (uncle wake dj RICCO) he is very nice guy nakumbuka when I was 2 yrs old nilijikata kidole alinipeleka hospital fast walikuwa na pick up ya blue sisi hata wheel barrow tulikuwa hatuna,enzi za MGANDA STREET

    ReplyDelete
  7. he!Bwana !kaka misupu!asante sana kwa hizi habari!ina maana kiongozi wa mzimu wa dansi ras makunja aka bwana kichwa jiwe!aliacha mambo yake yote na usupa staa wake na kukubali kuwakalimu nduguze!ama kweli mtu kwao!

    ReplyDelete
  8. hi!te! kama walilakiwa na ras makunja !bwana kichwa ngumu!wa kurusha madongo na mawe!inamaana watakuwa wamepewa siri yote ya mafanikio ya mziki barani ulaya?
    kwa sababu huyo ras makunja mwenyewe anajulikana kuwa akikupa dira ya mwelekeo basi hakuna wa kukushinda? aingii hakilini kuwa anaweza kuacha yake yote na kuwa
    pamoja ??????

    ReplyDelete
  9. unajua ras makunja bwana kichwa ngumu,ni mtu mwema sana akiwa nje ya jukwaa,lakini umaruuni wake awapo jukwaani na wale watoto nunda wenziwe mungu wangu!!!!!!

    ReplyDelete
  10. InAfrika mbarikiwe!kumbe mmekutana na ras makunja mwenye kukomaa kichwa,mwambieni kuwa baba wa kambo aliyemwimba anamtafuta na bakora...huku uswahili asijitokeze kabisa

    ReplyDelete
  11. heti tunasikia ras akikushika mkono basi mambo yako ni mazuri!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...