JK akimpongeza Mzee Kawawa baada ya kuzindua kitabu chake Ikulu leo. Kitabu hicho, kinachoelezea maisha ya Mzee huyu ambaye wengi wanamwita Simba wa Vita, kimeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu chini ya usimamizi wa Profesa John Magoti, Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere cha Kivukoni. Sherehe za usinduzi wa kitabu hicho unaendelea nyumbani kwa Mzee Kawawa huko Madale jioni hii
JK na rais mstaafu Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mzee Kawawa


Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mh. Pius Msekwa kwenye uzinduzi huo
Mama Maria Nyerere akiongea na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho leo Ikulu






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Tegeta tunaomba utupatie namna ya kupata hicho kitabu tafadhali, tuweze kumsoma "Simba wa Vita"
    Mzawa

    ReplyDelete
  2. Raisi mstaafu maisha ni mazuri kwa kweli

    ReplyDelete
  3. picha No1:JK-mzee hongera sana unatu inspire vijana wako
    Kawawa-nashukuru mwanangu namcheki Beni kwa mbali anakusubiri kwa hamu angalia jamaa atakulostisha!
    picha No2:Beni - kakitabu kangu kakitoka msomaji akisoma page kumi za kwanza kama hana moyo mgumu lazima azimie maana humo ni tunaongelea pesa nangai na mapapaa wote wa mujini tehe tehe tehe
    JK-tehe tehe hili jamaa fala nini halijui kuwa nalivutia pumzi
    picha no3:Mzee mwinyi-mi changu peji 100 za kwanza ni mambo ya jogging na kutroti page 500 zilizobaki ni kila kitu ruksaaa!
    Msekwa - mi changu sijui kingekuwa na issues gani?
    picha ya mwisho:ben-mama natumaini kila kitu kipo sawa maana kama kuna tatizo tafadhali nifahamishe hapa ndo chama kubwa napumua dollars
    mama nyerere-nakuombea umrudie mungu mwanangu!

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa kitabu hicho. Tunaomba watu mashuhuri ktk siasa na academia bongo mzindue vitabu vya maisha yenu ili muwape inspireshen vijana.

    ReplyDelete
  5. Haya ndio mambo tunataka kusikia. Big up Michuzi, inabidi wakubwa wawe mifano, wakiandika sisi vijana tutasoma.
    I love this...

    ReplyDelete
  6. Mzee ruksa nakumbuka kipindi chako cha utawala watuwalikuwa na hela. Msomi na asiye msomi wotw walikuwa na hela.

    ReplyDelete
  7. mkuuu wa wilaya tunakufagilia kwa kutobagua wadau!
    this is freedom of speech bwana!
    udumu mkuu wa wilaya letu kubwa!!!!

    ReplyDelete
  8. HAKI YA NANI VILE,,,izi pichaz?

    ReplyDelete
  9. ...mmmmmmm, naona mstaafu wetu ananona tu!

    ReplyDelete
  10. Je kile kitabu anachoandika Mkapa juu ya alivyouza mali za umma kinatoka lini?

    ReplyDelete
  11. U wazi ni lazima uwepo. hata kwa madhambi yaliyotokea. Wote tu binadamu tu!

    Historia yetu iandikwe bila kupotoshwa au kufichwa fichwa!

    Kuna wengi wanayajua ya Tanganyika sana. Muda utakuja na watayaandika, penda wasipende wenye kukataa kuyatangaza!

    ReplyDelete
  12. MKAPA NAONEKANA MORE PROFESSIONAL SI WA KUCHEKACHEKA KINAFIKI KAMA NANIHII MPENDA MASIFA NA NCHI IMEMSHINDA,na critict wa ccm Msolopogazi USA.

    ReplyDelete
  13. MKAPA ANONEKANA MORE PROFESSIONAL KULIKO WENGINE UKWELI UNABAKI PALEPALE.

    ReplyDelete
  14. Election matters . mnapochagua raisi uzuri, sIjui boys to men haya nyinyi ndio mnaopata shida bills ngumu. kodi yetu ndio hiyo inatumika kama kicheche .
    Yamewakuta marekani sasa . Huku shida zimeshaanza wenye nchi ndio hao Republican pesa wameshaweka kwingine DOWJONES ndio hiyo speculator kukichwa negative eti ooh haimpendi Obama . Watu wanampenda lakini wale wenye pesa wasipompenda cha moto tunakiona sasa . kazi hamna, wezi kila mahala na OBAMA TUNAMPENDA LAKINI Cha moto tutakiona ,COST YA HUO URAISI WAKE TUTAKOMA . REPUBLICAN HAWAMSUPPORT KABISAAAAAAAAA NA TUTAKOMA

    ReplyDelete
  15. sisi wadau wa hapa The Huge tutakipata vipi hicho kitabu tupo katika kazi pevu ya kukamilisha mandalizi ya mwisho ....??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...