maandalizi ya kili marathon 2009 ambapo wakimbiaji 4,000 toka kila pembe ya dunia wapo

Mashindano ya kimataifa ya marathoni yajulikanayo kama ‘Kilimanjaro International Marathon’ yanatarajiwa kufanyika Jumapili hii tarehe Mosi Machi 2009 mjini Moshi, na kwa mwaka wa pili mfululizo mtandao unaoongoza nchini Tanzania – Vodacom inadhamini mashindano yajulikanayo kama ‘Vodacom 5KM Fun Run’.


Kulingana na matayarisho yaliyokwisha andaliwa, Vodacom Tanzania inaamini kuwa mahudhurio ya mwaka huu yatakuwa makubwa zaidi ya mwaka jana na kufanya mashindano hayo kuendelea kuwa na hadhi bora zaidi ya kimataifa, na inawahakikishia wakimbiaji wote kuwa watafurahia zaidi mashindano ya mwaka huu.
Njia mpya ya Vodacom 5KM Fun Run:
Tofauti na mwaka jana, mwaka huu mashindano ya Vodacom 5KM Fun Run yataanzia Moshi Golf Club na kumalizia MUCCOBS.
Mashindano yatapita barabara ya Sekou Toure, kupitia Arusha roundabout, na kisha itapita barabara ya Boma mpaka Clock Tower Vodashop, na wakati wa kurudi itapita barabara ya

Uru (Keys Hotel) mpaka MUCCOBS.


Ratiba:

Kuanza: Corporate relay Saa 1:15 asubuhi

Kuanza: Vodacom 5KM Fun Run Saa 1:30 asubuhi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Mi napenda kutoa dukuduku langu linalonikera sana na jinsi Watani wa Jadi(Kenya) wanavyojitangaza na MLIMA KILIMANJARO licha ya kwamba hawana haki ya kufanya hivyo.

    Siwezi kuwalaumu Wakenya wakati Wizara ya Utalii nchini inashindwa kuutangaza Mlima Kilimanjaro na kuonekana kama upo ndani ya Tanzania.

    Nasema hivyo kwa sababu kuna taarifa karibu mwezi mzima sasa imekuwa ikitolewa na vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni na hasa Uingereza kwamba kuna watu mashuhuri wanaenda kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watoto masikini(RED NOSE).

    Moja kati ya taraifa hiyo imeandikwa kwenye mtandao wa YAHOO ikisema STARS SET OFF FOR KILIMANJARO CLIMB; Tena bila kuataja mlima huo kama upo Tanzania!

    Kati ya nyota hao yup mke wa beki wa kushoto wa CHELSEA na ENGLAND ASHLEY COLE, CHERYL COLE na mwanabendi mwenzake KIMBERLY WALSH na mwanamuziki nyota wa TAKE THAT, GARY BARLOW.

    Nyota hao waliondoka UK kwa ndege maalum ya shirika la ndege la KENYA(Kenya AIRWAYS)na ikiwa imepakwa rangi nyekundu kwenye pua yake kuambatana na sherehe hizo za kuchangisha fedha za kusaidia masikini. Watatua Nairobi kabla ya kwenda kupanda mlima Kilimanjaro Arusha Tanzania.

    SWALI LANGU NI HAYA:-

    Hivi serikali yetu haikuwa na taarifa za ujio wa nyota hao wakashindwa kuandaa utaratibu ambao ungesaidia kuitangaza nchi kwa kupitia mlima Kilimanjaro?

    Je hakuna ndege itakayo Uk-Amsterdam-na kutua Kilimanjaro (KLM) ambako safari yao ingekuwa fupi zaidi badala ya kupitia nchi jirani ya Kenya?

    Mbona Uganda ambayo ipo karibu na Tanzania, haitumii ujanja kama watumiao Wakenya wa kuitangaza nchi kwa kutumia Mlima Kilimanjaro?

    Yapo maswali mengi kuhusu Kenya kuitangaza nchi yao kwa kutumia jina la Kilimanjaro kama vile upo ndani ya Kenya wakati hawana chembe ya ardhi zaidi ya kuuona kwa mbali tena mpakani?

    Viongozi gani wasiojua hata haki miliki ya mali za nchi yao. Hivi Wakenya wangefurahi kusikia Tanzania inajitangaza kwa kupitia moja ya rasilimali zao?

    Ubalozi wa Tanzania UK kwa kushirikiana na Mali Asili walitumia zaidi ya £50,000 kutangaza biahsara ya utalii ya Tanzania kwenye mabasi, taxi na vituo vya mabasi UK. Je matangazao hayo hayakusaidia kuwafungua wageni na kujua Kilimanjaro ipo Tanzania?

    Kama KILIMANJARO haupo Tanzania, bora serikali ikatangaza rasmi na kuweka jambo hili wazi badala ya kuwaachia watu wasio na haki miliki ya kitu fulani, kutumia jina la kitu au nchi fulani kujipatia fedha isivyo halali.

    Wote tunafahamu maana ya haki miliki. COKE hawawezi kutengeza soda yao kwa kutumia INGREDIENTS za PEPSI kwani kwa kufanya hivyo wanajua kitim kitim chake. Vipi Wakenya wajitangaze kwa kutumia mali ya nchi jirani bila kushutumiwa?

    Mengi ninayo naweza kujaza BLOG yako kuhusu Wakenya na MLIMA KILIMANJARO. Nina imani wapo watakaounga mkono na kuwaamsha viongozi wenye BONGOLALA.

    MDAU, MACAU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...