ukumbi wa hoteli ya lamada ulifurika waigizaji na wadau wa filamu katika sherehe aliyoandaa steve kanumba juzi usiku kumshukuru na kumuaga director wa filamu toka nigeria, femi oyedegbe, baada ya kumaliza kumtengenezea filamu mpya
director femi (aliyekaa shoto) akiwa na muigizaji princess sheila toka uganda (nyekundu aliekaa) steve kanumba na igwe mtitu wakiwa na waigizaji walioshiriki kwenye filamu hiyo mpya ya kanumba
steve kanumba akipozi na mama yake mzazi (shoto) na dotnata
nyota kibao wa filamu na luninga walitoa nasaha zao kwa zamu. hapo ni biko akisema yake. wengine toka shoto ni steve kanumba, janet mwenda-talawa, jb na h baba
ali choki ambaye alitumbuiza na bendi yake ya tot plus akitoa zawadi maalumu kwa director femi oyedegbe toka nigeria
bosi mkuu wa kampuni ya filamu inayoongoza nchini ya game first, igwe mtitu, akisema machache huku ali choki na princess leila toka uganda wakimsikiliza
igwe mtitu akiwatambulisha mama mzazi wa kanumba na masanja mkandamikzaji kwenye hafla hiyo iliyofana vilivyo
mdau mkubwa wa filamu na muziki pedejee chief kiumbe akisema yake machache. hapa ameahidi kuanza kusaidia fani ya filamu baada ya kusaidia sana fani ya muziki
h baba alitoa shoo kali katika hafla hiyo
bingwa wa kula vichwa papaa bitebo akitoa nasaha kwa wadau wa filamu
supa bokelo wa tot plus alipanda wadau katika kuonesha manjonjo yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hongera zako Kanumba kwa kupiga hatua mbili mbele! Salam zake da Wema kwa kurudi hatua kumi nyuma!

    ReplyDelete
  2. Sasa wewe Supa Bokelo (picha ya chini kabisa) ndio uchezaji gani huo wa kukanyaga kanyaga wageni waalikwa?

    Tena hao unaowakanyaga ni kina mama watu wazima sawa na mama yako.

    ReplyDelete
  3. Sasa mbona wote walipewa maji ni kwa nini??

    ReplyDelete
  4. Mibange hii jamani Mh!!!

    ReplyDelete
  5. Mibange hii!!!!!!!! @ picha ya tatu!!!!

    ReplyDelete
  6. Jamani watu wengine wakishalewa na kuvuta bangi zao msiwaruhusu kupanga jukwaani. Ona sasa picha ya tatu kijana huyo alivyokosa adabu na kwenda kuwaparamia akina mama wa watu. Mwe!! ADABU MBAYA SANA. Mwenye bendi hiyo ampige chini fasta fasta. Kuna siku ataenda kumparamia WAZIRI ama RAIS! Ashikishwe adabu.

    ReplyDelete
  7. We bokole acha tabia ya kukanyaga kanyaga mama za watu utapigwa

    ReplyDelete
  8. Aaah sherehe gani hii full maji hamna hata coke jamaa anajua kubana matumizi hata hao wapopo wake wamemshangaa pati bila beer na kula pia aaah sio kweli jamaaa kama huyawezi unaacha tu sio kualika watu unawapa majiii mpaka matumbo yajaea ahahaha

    ReplyDelete
  9. Nakuunga mkono anon wa 6:51 AM, sijui hata aliwaandaa kisaikolijia kuwa atawarukia hivyo! Some manjonjos bwana......Wangemkwepa akaishia uso je?

    ReplyDelete
  10. Huyo sijui mnaemuita bokole hana lolote anataka hela ya kutunzwa tu, si mnakumbuka wale wacheza shoo wanaojivika makalio makuuuubwa kisha wanachezacheza kwenye matafrija, sana kwenye shoo za maharusi wakiona hakuna mtu anawearushia angakau jero, hufuata mtu mmoja mmoja akamtingishia kwa karaha, hadi utatoa tu hela kuepuka ile adha ya kudhalilika pale wakati anakutingishia, basi ndo zao hao, sasa hapo angewakanyaja hao kinamama vibaya je si angewaumiza muone aunt doti alivyolemewa na hilo limguu, inaboa bwana acheni hizo.

    ReplyDelete
  11. Leo naponda waziwazi wala sijali tena, nimevumilia nimeshidwa.
    Dada alievaa Red, ndio aliekuwa ameshika ile bastola, niliona picha kwa Dada Chemi, nilicheka mbavu sina. Eti nao hao ni actors na Directors, msinichekeshe.
    Hakuna actor hata mmoja hapo, vichekesho tuu. Wabongo wanajua kuridhika ridhika tu, hawataki kuweka juhudi. Siku hizi wanacolaborate eti na Wanigeria kwa hio wanadhani ndio kupiga hatua, hao Wanaija wenewe wachovu, sinema zao kelele tu hata hawaeleweki, vurugu tupu!
    Kibira alivokuja Bongo wakaanza maringo hata kujifunza hawakutaka, kwa minuso hawajambo, waambie waact, aibu tupu!!!!!
    Waangalieni wenzenu South Africa(BTW ni waafrica pia)movie zao zinavokuwa kali, zinaeleweka kuanzia casting director, actor wako convincing na theme zimepangwa vizuri, nasema tena sijaona bado actor wa maana bongo, Ukiachia filamu za Kibira. Bora hata actors wa zamani kama kina Bishanga, Waridi etc kuliko hawa wa sasa hivi, zero kabisa!!

    ReplyDelete
  12. Kanumba unajitahidi kwa kiasi kwa kweli, lakini ushauri wangu ni kukuasa kutoiga sana filamu za kinegeria, ingawa wao ni watamaduni sana lakini filamu zao kwa sasa naona nyingi wanatoa vipande kutoka kwenye sinema za kizungu. pia wewe unaweza kufanya hivyo am sure hukuenda hollywood bure. alafu kuhusiana na swala zima la wacheza filamu unaohusiana nao wengi ni commoners, am sorry kwa kutumia lugha hii lakini huo ndio ukweli jaribu kutafuta wasomi wazuri, mabenka, wanasheria, waimbaji wenye chati kama jd. hawa watasaidia sana kuhamasisha muonekana tofauti wa sekta ya filamu Tanzania na sio kama ilivyo sasa, kwa mtizamo wangu inapendelewa zaidi na watu wamatabaka ya chini zaidi na sio watu wa tabaka la kati na matabaka ya juu. jaribuni sana kuwalenga watu wote. alafu lugha pia dunia tunayoishi leo ni ya utandawazi hivyo filamu zinawakilisha kila mahalai isipoonekana classic basi ndio pale inapotupa picha fulani taifa zima.
    Kingine ni script, synopsis, na content yenyewe iliyopo ndani iwe ni yenye uzito zaidi.

    Hongera Kanumba unachance kubwa ya kuonekana kwa hiyo unaweza kufanyia kazi mawazo haya naomba yasikukere.

    ReplyDelete
  13. Wanaigeria sioni kama ni watu wa maana kabisa na movie zao zimejaa uchawi na maujai tu mabastola kibao. Sidhani kama Kanumba umeukata. Unapotoshwa tu na hao watu. Mie nisingejiidolize nao. Find your own identity.

    ReplyDelete
  14. Hilo lijibaba linalocheza juu!!! ya hao wakina mama alina hata aibu dume zima mpaka limenichosha!!!!! na misuli yote iliyomjaa kuwasimamia hao wakina mama nini!!!! ndio wakuone mjuzi, unawaumiza wenzako.

    ReplyDelete
  15. mnh hizi mbwembwe nyengine bwanaa...??

    cha kunivunja ugoko???

    walahi mie ningemshusha!!!

    kigulu nyembe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...