Shkamoo kaka Michuzi na wanablogu wako kutoka pande zote za dunia.
Mi hua nimezoe kupita 2 kwa mbali ila leo nimeamua kugonga hodi na natumaini ntakaribishwa. Wabongo wana tabia yakuitana wakabila mtu anapojivunia anapotokea...mi sioni kama ni sawa that's why nikaamua kuandika kuhusu hiii mada!

Usiporinga utaishia KURINGIWA!
Siku zote mtu akisifia asili yake haswa kabila sometimes anaitwa MKABILA au MBINAFSI.Jiulize kama mtu hajaupathamani ukabila wake na kujivunia atafikia wapi kujivunia utaifa wake??Kama we huwezi kusema mimi ni MMASSAI,MJALUO au hata MMAKONDE kwa majivuno utafika sehemuuseme wewe ni MTANZANIA kwa majivuno???
Nikiwa bongomtu akiniuliza ''we mtu wa wapi?'' ntamjibu ''uchaggani'' bilakujali sifa mbaya tunazobambikiwa wachagga kwasababu napenda asili yangu.Nikiwa nje ya nchi ntajitambulisha kamaMtanzania even though tunaweza kujulikana kwa sifa ambazosio nzuri sana.Ukikaa na kufikiria sana tena kwa makini utagundua kwamba kila kitu kina faults,ziwe za kweli au la,watu wanazitilia maanani.
Utasikia....WAZUNGU ni wabaya(roho),wachoyo,wabinafsi...WAAFRIKA au watu weusi ni wezi,wakorofi,wajinga n.k.Sasa wewe utakataa sio mwafrikka kwasababu wanaitwa wezi???Labda unaweza ila hutakiwi kufanya hivyo,unatakiwa ujivune na una nafasi yakuonyesha kwamba wasemavyo SIVYO.
Mtanzania akiwa nje anajiskia raha sana kuongelea anapotokea(asili yake)...Tanzania this..Tanzania that!!Unaowaelezea wanakuita mtaifa au mbinafsi???I don't think so!Actually watakuona kama mzalendo anaependa, anaejali na kujivunia asili yake.Mtu wa maana ni yule anaeitambua thamani yake,anapotokea na kile alichonacho.
So the next time someone is proud of being from a certain tribe and ain't afraid of saying so,don't go around hating nakumwita mkabila.Kwanza kama hamjui,the fact kwamba Tanzania ina makabila mengi yenye mila na desturi ,lugha na sifa tofauti inafanya nchi yetu iwe na mvuto zaidi.Kama wote tungekua WAMASSAI nani angemu-admire mwenzake?.Nani angemtania mwenzake??Think about it.
Mimi ni MCHAGGA and I'm more than proud. Hata mkisema wachagga wezi na wanawake wanaua waume zao I don't care. I'm CHAGGA for life.
''YOU CAN ONLY ACHIEVE WHAT YOU GIVE YOURSELF CREDIT FOR''
Mwisho wa yote nakushukuru kaka Michuzi kwakupost mada yangu na wote walitumia muda wao wa thamani kusoma nilichokiandika.Kama kuna nilimuudha kwa namna yoyote ile, iwe kwakuchanganya lugha au kutetea ukabila naomba anisamehe sana.
By Lillian

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Da' Lillian ametoa onyo kabisa kwamba hasiti kumtoa roho mumewe ikibidi tehee hee.
    Niache utani kidogo. Naomba Lillian au mdau mwingine anifafanulie. Mtu anavyoambiwa aringie kuwa Mwafrika au Mdigo ni kwa sababu zipi ajivunie hilo? Unakuwa umefanya kazi gani hata kuwa Mngindo mwenye rangi ya majiyakunde? Umefanya kazi gani iliyokufanya uwe mfupi kama Andunje au mrefu kama Hasheem Thabeet? Mtu aliyezaliwa na rangi nyeupe kama inayopatikana kwa wingi kwa ndugu zetu Warangi ana haki sawa ya kujivunia weupe wake na mtu aliyepata weupe kwa kupiga mkorogo? Mimi nadhani aliyepiga mkorogo ana sababu zaidi za kujivunia. Mpiga mkorogo atatafuta Jiki na vikorombwezo vingine vyote vya kujipaka, atavumilia maumivu makali hata kufikia malengo ya kuwa mweupe. Ni tofauti na mtu aliyezaliwa akiwa mweupe. Aoge, asioge, apake mafuta, asipake ndio rangi yake hiyo. Badala ya kupoteza muda kuringia rangi yake na kuwa proud na rangi yake, ni bora achape kazi kwa bidii ili aweze kujivunia matunda ya kazi yake.
    Kwa wapenda michezo, mtu unaweza kabisa kujivunia kuwa mshabiki wa Miembeni au KMKM kwa sababu umeamua mwenyewe kushabikia timu ya ushindi. Lakini huwezi kujivunia kuzaliwa Unguja wala Australia. Hukufanya uamuzi wowote katika hilo.

    ReplyDelete
  2. WHO CARES??????!!!!!!!!PELEKA MAMBO HAYO KENYA AU UGANDA,JARIBU KUFIKIRIA UTAISAIDIA VIPI NCHI YAKO KUONDOKANA NA UMASKINI,MARADHI,NA MATATIZO MENGINE.WAAFRIKA TUNA SAFARI NDEFU SANA YA MAENDELEO,YAANI MTU ANAKAA NA KUANDIKA MASUALA HAYA KATIKA KARNE HII?NA MIMI SIJACHUKIA BALI I FEEL SORRY 4 U NA TAIFA LANGU LA TANZANIA KUWA NA WATU KAMA WEWE KATIKA JAMII.

    ReplyDelete
  3. Lilian,

    Ukabila huwa unakuja pale unapoangalia wa kwenu tu katika kila kitu.

    Mfano kuna nafasi ya kusoma, kazi, kupata mkopo, etc... na kinachokuja kichwani kwako ni Wachagga.

    Yaani kabila kwanza then qualification baadae.

    Sikatai unaweza kupata watu wenye qualifications ndani ya kabila lako, lakini kutokana na ufahari ulionao kwa kabila lako imekuzuia kufikiria kwamba kabila sio qualification.

    Angalia mifano kama pale IPP Media kwa media karibia staff wote ni Wachaga... au viti maalum CHADEMA... karibia wabunge wote ni Wachaga.

    Ndio maana wabongo wanachelea kuchagua mchaga awe raisi maana serikali nzima itajaa wachaga.

    Ukitaka kuwa mjanja don't be so proud. Inabidi ujifunze kuwa kwa Tanzania kuona ufahari wa kabila lako sio kitu kinachokubalika. Jivunie MAFANIKIO yako kama vile elimu, uzoefu wa kikazi/kibiashara, nguvu za mwili, n.k.

    Kama ni kujivunia ulikotoka basi jivunie Mkoa au wilaya yako. Hizo ndizo units za kiutawala na kijiografia zinazokubalika. Sio kabila.

    ReplyDelete
  4. Lili ungetoa kabisa na picha yako watu waone unachoringia.

    ReplyDelete
  5. We Lily

    Hebu toa ukabila wako hapa.

    Kama unaona kujivunia kabila ni deal tafadhali nenda Kenya, Uganda au Nigeria... hapa Tanzania hapakufai.

    Huwezi kulinganisha TANZANIA (ambayo ni nchi) na KABILA (ambao ni mkusanyiko wa kidamu zaidi).

    Leo hii mtu yeyote anaweza kuwa Mtanzania, mradi atimize masharti ya uhamiaji... Je mtu akitaka kuwa Mchaga masharti yakoje?

    ReplyDelete
  6. Sasa umefundisha nini Jamii,kwamba you proud of your kabila?Who cares?
    Stori kama hizo peleka Kenya na Uganda,huna nidhamu kabisa.Peleka uchaga wako huko kibosho.

    ReplyDelete
  7. Jamani msihangaike na mtu kama lily,kwani hapo kashatuonysha kama ni limbukeni na alitaka naye aonena kama kawahi kutoka kwa bro michu...
    ndo mana ukaambiwa
    WACHAGA KWA.......

    ReplyDelete
  8. mdau wa kwanza nimekukubali kuna vitu vya kujivunia bwana, sikatai ukijisiakia comfortable kwamba ww ni mchaga lkn usijivunie sana mbele za watu kwa kitu ambacho hujakitolea jasho kuwa mchaga hujaamua uwe mchaga umezaliwa ukajikuta wewe ni mchaga na ukishajiona kuwa mchaga ni kitu bora kabisa cha kujivunia hata mbele za watu basi ni dhahiri utatanguliza upendeleo katika kila jambo kwa uchaga wako.BINAFSI NIMEJUTA KWA KUPOTEZA MUDA WANGU KUKISOMA ULICHOKIANDIKA HADI MWISHO KWAVILE WAKATI UNAANZA KUANDIKA NILIDHANI MWISHONI UNGEKUWA NA HOJA YA MAANA KUMBE MASHAUZI MATUPU KWA KITU USICHOKITOLEA JASHO UNAONYESHA NI KWA KIASI GANI ULIVYOPUNGUKIWA NA VITU VYA KUJIVUNIA KAMA ELIMU,TABIA,MAENDELEO YA KIMAISHA NK.POLE SANA DADA WA KICHAGA I HOPE NA MENO YAKO PIA YAMEOZA MANAAKE HICHO NDIO KAMA KITAMBULISHO VILE

    ReplyDelete
  9. KIRU! KWELI BABA ANGU!!!! NITAMPELEKESHA MTU HAPA!!!. MIMI NI MANGI HARISI SINA MCHEZO! USILETE UTANI HAPA!!!

    ReplyDelete
  10. KWELI NYOKA NI NYOKA TU HATA UMNG'OE MENO YATAOTA TU!NA NYANI NI NYANI TU HATA UMVISHE SUTI!ATABAKI KUA NYANI YANI HUYU LILY INAONESHA NI JINSI GANI ASIVYO NA ELIMU WATU WANAUPINGA UKABILA DUNIANI

    WATU WANAUPINGA UKABILA DUNIANI YEYE ANAUPIGIA DEBE!!INAONESHA NIJINSI GANI ASIVYOJIAMINI MAANA WAMEZOEA KUBEBWA NA ITIKADI ZAO ZA UKABILA!!ILI WAWEZE KUFIKIA MALENGO YAO
    DUNIA NZIMA WATU WANAUPINGA UKABILA MAANA UNANEGATIVE EFFECT NYINGI KULIKO FAIDA NA HII TULIPANDIKIZIWA NA WAZUNGU ILI TUSIPATE MAAENDELEO DAIMA ETI UNAJIVUNIA UKABILA HIVI UMESIKIA LINI MZUNGU ANAJIVUNIA UKABILA HATA SIKUMOJA HUTOSKIA ILA UTASKIA ANAJIVUNIA UTAIFA NA NDIOAMAANA WANAMENDELEO

    SISI TUTABAKIA KUCHINJANA TU KWA KUENDEKEZA UPRIMITIVU NA NDIOMAANA HATUNA MAENDELEO LEO HII MCHAGA AKIPATA MADARAKA WIZI MTUPU ATAKWIBA WEEEEE MPAKA BASI ATALETA WACHAGA WENZIE WAIBE MPAKA BASI

    YA1NI WIZI MTUPU NA CHUKI ZA KIKABILA TU!!HII SIO KARNE YA KUJIVUNIA UKABILA BALI UTAIFA!!

    MSITULETEE ITIKADI ZA RWANDA NA BURUNDI TUKAJUTA MAISHA YENTU YOTE PELEKA MBELE ITIKADI ZAKO!!NASIKITIKA MICHUZI KUWEKA MADA ITAKAYOTUBOMOA NASIO KUTUJENGA
    USINIBINYIE BITOZI WA ZAMANI
    HUU NI WAKT WA UKWELI NA UWAZI IFECT ZA WACHAGA NI MATOKEO YA UKOLONI KWA MSOMI YEYOTE ANALIJUA HILI

    ReplyDelete
  11. POLE LILY KWA MCHANGO WAKO UNAOLETA MKANGANYIKO KWA WALIO WENGI.
    HUENDA NI HIYO SABABU YA "EXPOSURE"NDOGO ULIYOPATA AMA SHULE NDOGO ULIYONAYO,LABDA PIA UKO "NJE" NA UNAJISIKIA KUJISIFU-ANGALIA USIJISAHAU SANA,INAWEZEKANA UMRI NA UFAHAMU WAKO NI MDOGO HATA HUJUI MSINGI YA TANZANIA KUWA KAMA ILIVYO,KUNA JITIHADA NZITO ZA WENYE MAWAZO MEMA ZILIZOFANYIKA!!-JIFUNZE UPATE KUJUA USIKURUPUKE KUANDIKA ETI KWAVILE UNA ACCESS YA INTERNET TAFADHALI.

    WEWE UJIVUNIE UCHAKA;MIMI UKWERE;YULE USUKUMA-ILI IWEJE,YAPO MAMBO YA KUJIVUNIA NA SIYO KIJIBABILA CHAKO;HUENDA WEWE SIYO MTANZANIA ILA UNAPIMA..HAPA USIPIME...TUTAKUMWAGA SISI,EBO!

    ReplyDelete
  12. Mimi nadhani mtu unatakiwa kujivunia maendeleo na si kabila. Kwani mchaga ana damu ya njano na mngoni ana damu ya kijivu? Sisi sote ni binadmu tu hata hao wazungu ni binadamu kama sisi. Tofauti ni rangi ya mwili tu na tukijikata wote twatoka damu nyekundu. Watanzania/waafrika tujikwamue ktk elimu na mengineyo ili na sie tuje tujivune kwamba tumejikwamua kutoka dunia ya tatu. Ukabila sio ishu kabisa.

    c3

    ReplyDelete
  13. KUNA MAKABILA MENGINE HAYAONI HATA HAYA NA NDIOMAANA WANASIFIKA KWAKUA NASIFA CHAFU

    UBINAFSI WIZI ROHO MBAYA UTAPELI KUPENDA MALUMBANO
    ME NAONA HAYA HATA KUJIIITA MCHAGA KWA TABIA ZETU CHAFU

    HIVI TUKIANZA KUJIVUNIA UKABILA KILA KABILA LIKIANZA MIMI FULANI HIVI TUTAJENGA TAIFA LA WATU WANAOJIVUNIA
    NAKUJIITA WAZALENDO KWELI?HII NI AIBU KWA WATU KUTOKUA WAZALENDO WA NCHI NA KUA WAZALENDO WA UKABILA

    SISHANGAI KWA SISI WACHAGA UKINIPA NCHI NAWEZA NIKAIUZA KWA MASLAHI YANGU BINAFSI AMA KWA KABILA LANGU MAANA SINA UZALENDO WA UTAIFA BALI UKABILA TU
    NANDIOMAANA TUNAONGOZA KWA UFISADI SERIKALI NA KWENYE MAKAMPUNI

    ReplyDelete
  14. KUNA MAKABILA MENGINE HAYAONI HATA HAYA NA NDIOMAANA WANASIFIKA KWAKUA NASIFA CHAFU

    UBINAFSI WIZI ROHO MBAYA UTAPELI KUPENDA MALUMBANO
    ME NAONA HAYA HATA KUJIIITA MCHAGA KWA TABIA ZETU CHAFU

    HIVI TUKIANZA KUJIVUNIA UKABILA KILA KABILA LIKIANZA MIMI FULANI HIVI TUTAJENGA TAIFA LA WATU WANAOJIVUNIA
    NAKUJIITA WAZALENDO KWELI?HII NI AIBU KWA WATU KUTOKUA WAZALENDO WA NCHI NA KUA WAZALENDO WA UKABILA

    SISHANGAI KWA SISI WACHAGA UKINIPA NCHI NAWEZA NIKAIUZA KWA MASLAHI YANGU BINAFSI AMA KWA KABILA LANGU MAANA SINA UZALENDO WA UTAIFA BALI UKABILA TU
    NANDIOMAANA TUNAONGOZA KWA UFISADI SERIKALI NA KWENYE MAKAMPUNI

    ReplyDelete
  15. KUNA MAKABILA MENGINE HAYAONI HATA HAYA NA NDIOMAANA WANASIFIKA KWAKUA NASIFA CHAFU

    UBINAFSI WIZI ROHO MBAYA UTAPELI KUPENDA MALUMBANO
    ME NAONA HAYA HATA KUJIIITA MCHAGA KWA TABIA ZETU CHAFU

    HIVI TUKIANZA KUJIVUNIA UKABILA KILA KABILA LIKIANZA MIMI FULANI HIVI TUTAJENGA TAIFA LA WATU WANAOJIVUNIA
    NAKUJIITA WAZALENDO KWELI?HII NI AIBU KWA WATU KUTOKUA WAZALENDO WA NCHI NA KUA WAZALENDO WA UKABILA

    SISHANGAI KWA SISI WACHAGA UKINIPA NCHI NAWEZA NIKAIUZA KWA MASLAHI YANGU BINAFSI AMA KWA KABILA LANGU MAANA SINA UZALENDO WA UTAIFA BALI UKABILA TU
    NANDIOMAANA TUNAONGOZA KWA UFISADI SERIKALI NA KWENYE MAKAMPUNI

    ReplyDelete
  16. WEWE LILIAN;HEBU ISHIA HUKO MGOMBANI UKARINGIE "VIPATA" VYA MBEGE NA KULA MAGIMBI "SOWO" YANAYOWASHA KWA KUJIFANYA UNAJIVUNIA UCHAGA WAKO! WEE KALAGABAHO NA UBOZI WAKO-YAANI BADO HUJATOA VUMBI HADI SASA..!KAAZI KWELI KWELI-
    WASALIMIE "MNDENYI" KAMA KWELI UNAPAJUA LA KAMA UPO MITAANI AMA HUKO MBALI,USIJISIKIE SANA KUJIFANYA MJANJA-UTAPOTEZA MWELEKEO WAKO NA SIYO WA JAMII MAANA WENGI KATIKA JAMII TUNAJUA UMUHIMU WA MSHIKAMANO KIZALENDO-"RIA MBEGE KAMA UNAIJUA"
    MDAU-EU

    ReplyDelete
  17. yaani lil umechemka vilivyo,naimani hiyo ndio akili ya wachaga 80%inasikitisha kujivunia huozo wa ukabila ambao ulipelekea mauaji burundi na rwanda.

    ReplyDelete
  18. Hii mada safi, hongera kuileta barazani.

    Mbora wenu ni yule ni mbora mbele ya mungu.
    Ubora wa mtu ni kwa matendo yake njema na sio kwa maringo yake. Ubora wa mtu ni utu wa kutambua kuwa watu wote ni sawa, wanastahiki heshima, haki na msaada.

    Tunaingia kwenye ufisadi tunapojikuza na kujinadi au kutamba kuwa mimi ni bora kuliko wengine aidha kwa kipato, kabila, dini, mkoa, jimbo, jinsia au hata huo utaifa. na kufikia kurimbikiza mali, kujipachika ulafi na ulevi

    Mungu anasema ameumba makabila ili mujuwane sio mujipangie daraja nani zaidi na pia hataki mutembee hapa ardhini kwa kiburi na vishindo.

    Ubora wa kabila moja dhidi ya lingine ndio ulifanya wazungu wawaweke wenzao katika utumwa halafu baadae wakaza kuwavamia wa Afrika kuwachukuwa utumwani.

    Wazungu pia walijiona bora na kutamani kusafisha damu zingine wakainza na Wayahudi. Mauji ya kimbari yalieenea dhidi ya wayahudi ulaya yote. Hapa kwetu wa Hutu na Watusi hawana utani bali ni uadui wa kweli.

    tulipigania kuondoa dhulam ya Wa Boers (Waafrikana) kuwadhalilisha watu wa makabila mengine na hata kuleta apartheid.

    Huko kaskazini mwa Bongo mapigano kati ya Wanchari na Walenchoka si utani au umesikia Wairegi wamepigwa Risasi na kufa papo hapo na Wanyabasi ukadhani ni risasi za majimaji.

    Siku Wapemba wakifanya maandamano dhidi ya Waunguja juu ya utaona Janajweed wanavyotimka ukadhani ya Darfur hayawezi kufika hapa Bongo.

    Mwaka jana tulishuhudia maelfu watu kadhaa wakiuliwa, mali na nyumba zi kiharibiwa huku wakikimbilia nchi za jirani, sababu kubwa ni Wakikuyu kwa kujifanya bora na kuringa kwa uda mrefu hawakutaka Mjaluo awe raisi.

    basi tafadhali sana acha kuringa. maringo si mazuri. Kupenda nchi ni tabia sio ya uzalendo sio kuvaa jezi ya bluu au kuendesha gari ya bendera ya taifa maana mafisadi wakubwa hutembea na mabango kuwa mimi ni mtanzania nambari wani eheee, nambari wani ehe...

    alsmsiki
    (mimi ni mswahili tu nina jali na kuudhika kuitwa chasaka ninapotembelea Moshi vijijini)

    ReplyDelete
  19. KWELI KABISA LINGA NA ULINGIE MAMBO MAZURI NA SIO UCHAFU

    HATA UKIJARIBU KUJISAFISHA KWA PROPAGANDA SIKU ZOTE UTABAKI KUA MCHAFU

    SASA SISI HATUONI MCHAGA ATARINGIA KWA MAZURI GANI ZAIDI YA UCHAFU NA NDIO MAANA KAULETA UCHAFU WAKE HADHARANI!!

    MAANA KAKAANAO HUKO NA KUJIFICHA KAONA ATAA YEYEKAZOELEKA KUSIFIKA KWA MACHAFU NA NDIOMAANA KAULETA UKABILA WAKE HAPA BILA KUJUA KUA HIYO NI SIFA MBAYA

    SASA UTASIFIKA KWA LIPI ZURI ZAIDI YA MABAYA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...