YES KAKA MICHUZI,
NI MARA ANGU YA KWANZA KUJA KWENYE POSTING YAKO ILA NAOMBA UNISAIDIE KITU KIMOJA HAPA.
KAKA MICHUZI NAOMBA WADAU LEO HII TUUSIKE KWENYE KUCHANGIA HII MADA HIVI MICHUZI MAJENEZA YALIYO PALE NNJE YA HOSPITALI YA MUHIMBILI JE NI HALALI KUWEPO SEHEMU KAMA HILE?
NA JE KAMA MGONJWA KAZIDIWA AKIYAONA YALE ANAJISIKIAJE?
NAOMBA MSAADA WAKO WEWE PAMOJA NA WADAU WA BLOGU YA JAMII
MDAU ABDALLAH NGATUNGA
TEMEKE
DAR ES SALAAM.


Maisha ya Mwanadamu hapa Duniani mara zote yameambatana na ukweli juu ya Kifo. kwa mwanadamu Yeyote mwenye umri wa uelewa anajua kuhusu ukweli wa kifo. Zamani katika makabira mbalimbali ilikuwa hata ni mwiko kuandaa kaburi kabla ya mtu kufa. Lakini jambo hilo sasa ni lakawaida.
ReplyDeleteUwepo wa Majeneza Katika Hospitari kwakweli ni jambo la msaada kwani ni ukweli kila siku kuna ndugu zetu wanao kufa katika Hospitari hiyo. Ni urahisi na msaada kuhifadhi na kufanya mipango ya mazishi kwa urahisi. naelewa ilivyokuwa vigumu, hapo awali kuandaa Jeneza mara Msiba unapotokea. Kuna purukushani za kutosha katikamaandalizi hayo. Hivyo mimi sioni athari yoyote ya uwepo wa majeneza kwani ni ukweli usiopingika kwamba vifo vipo na mahitaji ya majeneza yapo.
Kama unakubali kuwa lazima siku moja utakufa hakuna tatizo lolote kuona majeneza maana ndio matayarisho ya kifo, watu wengine wananunua nafasi za kuzikwa kwa kutambua kuwa lazima watakufa. Kuna watu wasiokubali hata kuandika mirathi kwa woga wa kifo nadhani haya yamepitwa na wakati. Namna nyingine ya kuwaza hili ni je ukipata msiba na jeneza unalipata jirani si unapunguza kazi na gharama?
ReplyDeletewewe vipi, je ni halali kuweka vyakula nje nje pale sokoni? je mwenye njaa akipitapita hujisikiaje? masuali mengine bwana!
ReplyDeleteusiogope mzee kufa ni sehemu ya maisha na hata uogope utakufa tu!!!!mbona tunapoenda kuzika tunayabeba jkabisa na tena wengine wanabeba maiti bila jeneza!!na kama sisi tukiogopa je nchi kama kongo DRC zenye vita na ambako watu wanakufa tena sio kwa kuumwa wengine kuchinjwa wasemeje?mie naona ni poa tu kuwepo majeneza pale mhimbili!!!!nakushukuru mtoa mada maana na mimi napenda sana kujua mitazamo ya watu juu ya kitu hiki!!!
ReplyDeletemajeneza kuwepo pale ni sawa kabisa kwani ndo sokoni mwake na nahisi mgonjwa akiyaone yale anapata nafuu bila kupenda kwani akifikiri du ile ndo itakuwa ghetto yangu nikiachia ngazi moja kwa moja anatinga ktk mjengo huo lazima apate ahueni ni vigumu sana kukubali na pia ni biashara ngumu kidogo lakini hakuna jinsi kwa maoni yangu mimi ni powa tu na pia inakuwa rahisi kwa wafiwa wasihangaike kwenda mbali kupata mahitaji ya jeneza hayo ni maoni yangu nionavo mdau stellenbosch
ReplyDeletekweli hospitali sio sehemu ya kuwa majeneza. Na siku hizi majeneza yamekuwa dili kweli kama wanaombea watu wafe bwana. ila watafute sehemu zakuuza majeneza sio mbele ya ikulu. Kwengine na mie naomba kuuliza.
ReplyDeleteMa Hospitali mengi ya Serikali yana Ambulance pungufu ila Magari Ya madaktari ni ma Prado yamezidi kibao kila Daktari ana ma prado ma 3. Ambulance pungufu jamani pesa za msaada za madawa na usaidizi wa wagonjwa msiyanunulie magari makubwa hata gari Rahisi utafika hospital nunuweni Ambulance. James Wa Arusha.
Mgonjwa ataona akifa nduguzake awata angaika kutafuta jeneza atakapokufa.
ReplyDeleteHakika si vibaya ni sawa na maduka ya dawa yaliyopo jirani na Muhimbili, Kanisa usaliwe au Msikiti uswaliwe na pia maana halisi ya Muhimbili= Muhimu njia mbili kufa au kupona kifupi cha muhimbili mgonjwa akiona kama wa kufa atastuka atakufa haraka!! na kama wa kupona akiyaona atastuka atajikaza na uzima utamjia
ReplyDeleteMoody
"HILI SWALI LINATIA FORA KATIKA LIST YA MASWALI YA KIZUSHI"
ReplyDeleteWe uliyeuliza ulishawahi kuona kaburi? Unajisikia vipi ukijua kuwa ipo siku utafukiwa ardhini? Waombe watu wa wizara ya adrhi waifiche basi isikustue roho.
ReplyDeleteKibinadamu Majeneza kwenye entrance ya hospitali sio sahihi, maana unaweza kumwathiri mgonjwa kisaikolojia. (kama amezidiwa sana hatayaona anyway) Kwa mgonjwa ambaye hajazidiwa sana
ReplyDeletekuwepo kwayo kunaweza kumfanya mgojwa awe co operative kwa kujua kuwa akikataa kumeza dawa.. kula.. carrying media haipatikani mbali...
Tatizo ni kuwa kuna vitu vingi sana ambayo wahusika hawawajibiki, mimi nadhani majeneza muhimbili ni tatizo dogo zaidi kuliko Bar, groceries, miziki kwa sauti kubwa.. etc etc etc kwenye makazi ya watu... by laws zipo ila hazifuatwi.
Si halali!! mimi ninaona ni ulimbukeni ambay ni kansa inayotutafuna wabongo katika nyanja tofauti. kila mtu mzima anajua kuwa siku yake ya kufa itafika na sio lazima kukumbushwa kwa kuanika majeneza nje. pili, kwa kuyaweka muhimbili ni kutaka kutueleza kuwa kila anayelazwa hospitali mwisho wake ni kuaga dunia! ingefurahisha kupaacha muhimbili pakajulikana kama sehemu ya furaha ya kuponyesha waganjwa.
ReplyDeleteWafanyabiashara ya majeneza wangefungua maduka sehemu nyingine na kuyahifadhi ndani ya jengo, ili mwenye kutafuta aingie humo na kuchagua kama yalivyo maduka ya vifaa vingine. Asiyekuwa na jengo maalumu asipewe leseni ya kufanya biashara hiyo. ebu tuache ulimbukeni!!!!!!
That what we call "markert force" which is driven by demand and supply
ReplyDeleteMajeneza yanaweza kumkumbusha mgonjwa kuandika wosia kama alisahau ili asiwachie wenzie matatizo pindi aitwapo na mola
ReplyDeletemimi kama mgonjwa hapa hospitali nimeshtukia kuwa ni biashala za madaktali make wanasababisha hata vifo ili wa huze hayo majeneza make ni juzi nilikua na kooa nikaomba msaada nimuone doctor chumbani jibu lilikua subili mpaka kesho naalikua anatia story na mshikaji wake make alijua kufika kesho ntakua nsha kufa jeneza litauzwa naOMBA KAMA SERIKALI YETU INA WEZA KUWA HAMISHA HAO WATU HAPO KUPUNGUZA VIFO VYA KIZEMBE HAPO HOSPITALI
ReplyDeletepalliative care itawasaidia wafe vizuri
ReplyDeleteWewe muuliza swali hebu wacha kuuliza maswali ya kitoto / kipuuzi.
ReplyDeleteKifo ni kama kivuli chako kila siku unatembea nacho eh.
Kwa hiyo bora uanze kukizoea tu, ndio maana baadhi ya wanamuziki huwa wanaimba "nitakufaje" ilhali ni wazima wa afya.
Na wewe hebu anza kuimagine utakufaje ili uwe comfortable na ishu ya kifo, maana kipo around the corner... any time kinaweza kukutembelea.
Kuwepo kwa majeneza nje hasa katika muonekano wa public inaonesha tatizo kubwa la mipango miji tulilonalo hapa nchini kwetu.
ReplyDeleteHuhitaji kuanika jeneza barabarani, nafikiri halmashauri ya manispaa inapaswa ku-address hii issue.
Kwenye somo la marketing hiyo ndio inaitwa POSITIONING!!!
ReplyDeleteSomeni hapa kuhususiana na suala la kifo kwa ujumla.
ReplyDeletehttp://matondo.blogspot.com/2009/01/tuzungumzie-kifo_28.html
ANO FEB 25 9.09PM HUKUELEWA KIPINDI ULIPOKUWA DARASANI KWA SOMO LA MARKETING HAIITWI POSITIONING, HIYO NI LOCATIONING DERIVED FROM DISTRIBUTIONING.
ReplyDeletePOSITIONING IS BASED ON THE AMOUNT %WISE MARKET SHARE YOU OWN IN THE INDUSTRY VS RIVALS.
IF YOU OWN LARGEST MARKET SHARE THAN YOUR RIVALS/COMPETITORS THEN YOU ARE AT POLE(FIRST) POSITION.
Am confused again, Jamani lazima tutazame na cultural context(jinsi watu wanavoishi)hasa mataifa ya ulimwengu wa tatu. Maadili na taratibu yamebakia kuwa misamiati tu!Je nami nikuulize wewe waongea kuhusu majeneza lakini si watu wote wanazikwa na majeneza kwa hiyo ina maana hata kama sizikwi na majeneza itanifanya niogope. Mtu haogopi jeneza anaogopa KIFO.
ReplyDeleteMwisho nataka kukueleza mbona mgonjwa analala wodini na Sanda(Shuka nyeupe). Je vipi alale mtupu ama hospitali waondoe mashuka ili isimletee mawazo ya Kifo Ha ha ha haaaa.. Am remaining here.
Dr Confusion
tuchomane mioto maiti,,,tunajaza sana ardhi na mbanano adi twazikiana juu.
ReplyDeleteiyo ni biashara km zingine mtu apate kipato chake na uraisi wa kununua karibu
habari ndo iyo
Siku zote tuna tabia ya kuchanganya mada.muuliza swali hakuwa na maana kuwa ajui kufa ama anaogopa kufa.
ReplyDeletePamoja na kuwa akuwa wazi sana alichotaka ni hathari ya biashara kama hiyo mahali kama hospitalini. Nashukuru maoni ya wengi yanatoa majibu ya hoja hii.mimi nafikili kungeandaliwa sehemu maalum hata kama ni hapo muhimbili lakini sehemu ya pembeni kabisa, ambapo macho ya wagonjwa hayatafika. hapa nina maana sehemu iliyofichika. kuna hathari kubwa sana kwa mgonjwa na hasa aliyezidiwa kusimuliwa habari ya msiba ama kuona jeneza likichongwa mbele yake.kisakolojia jambo hili linaweza kusababisha kuharakisha kifo cha mgonjwa ama kukata tamaa na kusababisha kifo chake. wala aisaidii mgonjwa eti kumeza dawa.
Mgonjwa atajisikia chochote, ila hakuna jinsi, yanahitajika na kuyatafuta mkiwa mna msiba mkononi ni shughuli nzito, bora yawekwe pale. mimi binafsi siyapendi kabisa mwanzo nilikuwa naangalia upande wa pili nikifika hapo, na machozi yananitoka nikiona yale ya watoto, lakini sasa nimezoea (ya watoto bado sijazoea). Ila ni muhimu, kama mchimba kaburi, unataka afanyeje? awe tu yoyote au kuwe na wataalamu?
ReplyDeleteJe ukiwa mzima huogopi majeneza? unadhani uko mbali kidogo na kifo?
Ukweli kifo ki ndani yetu, jeneza au bila jeneza, lazima tujue, na tuwaze mara kwa mara(realisticaly) plight yetu baada ya kufa, je kuna chochote kitu? And do something abt it.