kaka Michuzi,
Hivi karibuni nilikuwa mjini Antwerp, nikakutana na vijana wa kitanzania waliokuwa wakiwania kupata nondoz za pili huko Ubeligiji, nikawauliza kama kuna wabongo wengi kule, wakaniambia wapo na wakamtaja Manara, nikagundua hawakuwa wanafahamu wasifu wake kamili.

nikawafahamisha mimi nilikuwa mshabiki wake mkubwa wakati anacheza soka bongo i.e. Pan African SC. Wakafanya mawasiliano tukaenda kumtembelea nyumbani kwake.

Tulikuta ''hapatoshi'' wabongo warundi wakenya wakiwa wanapiga stori.

Jamaa yuko fiti kama unavyomuona kushoto (mie nipo shoto kwake), na anafanya kazi kama kawaida ila wengi hawajui kwamba huko bongo ni bonge la staa wa enzi hizo.

Nimeona nikutumie hii picha ili wadau wamwone mtu wao, ameishi ubeligiji zaidi ya miaka 25, na alikuwa hajawahi kufika Bongo mpaka mwaka jana kwa miaka zaidi ya miaka 23
Mdau Geoff

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. wakina manara wengi walikuwa wanacheza soka. Huyu ni nani? Jina lake la kwanza.

    ReplyDelete
  2. WE MDAU HAPO UJUU HEBU SOMA KWANZA KABLA YA KUULIZA.JINA LAKE NI KASSIM MANARA.INAONYESHA ULIKUWA HUJAZALIWA WAKATI HUU.
    MDAU

    ReplyDelete
  3. mdau ulieleta hii message unatuchanganya,kushoto kwako halafu tena na weye ni wa kushoto vipi hapo.nionavyo picha, Kassim yupo Kulia na weye kushoto au???Uandishi wa habari sio rahisi kihivyo.
    Na habari ndo hiyo........

    ReplyDelete
  4. sorry naweza kuwa out of topic..Mimi nategemea kwenda Ghent University September mwaka huu..naweza kupata contact ya mtz yeyote nikifika? Nasubiri message via king_sam02@hotmail.com
    SAM-ISTANBUL TURKEY

    ReplyDelete
  5. Habari zilizozagaa hapa Bongo ni kwamba Kassim alifariki siku nyingi nchini Austria. Hebu wadau wenzangu nipeni ukweli wa habari hii.

    ReplyDelete
  6. Miaka 23 bila kurudi nyumbani? Alikua na murder case au tatizo ni ilikuwa nauli?

    ReplyDelete
  7. SIO LAZIMA UCHANGIE ANON WA28/02/09 10:37 UMESHAAMBIWA KASIM,INAONENAKANA HAO KINA MANARA WENGINE HATA UWAJUI,WAKO WENGI LAKINI AWAFANANI KISURA INGEKUWA PICHA YA BAPO,MOHAMED AU COMPUTER UNGEJUA HUYO NANI,ASANTE MDAU KWA PICHA NZURI STRIKER TUNAKUMISI BONGO TAMBARARE MUULIZE ABDALAH JOHN AKA KAIZER.

    ReplyDelete
  8. kukaa miaka 25 ubalgiji sio kweli kama ana muda mrefu basi miaka minne.

    ReplyDelete
  9. Kama ni Kasim Manara namkumbuka kwani alisoma shule na dada yangu pale Karume Magomeni mikumi, baada ya shule waliyokuwa wakisoma DA pale upanga kufutwa ili kupisha ambapo sasa ni makao makuu ya Jeshi la ulinzi..katika kundi la wanafunzi hao pia alikuwapo Juma Pondamali...hizo ni kumbukumbu kutoka kwa sista...baadae akaja kucheza mpira, Yanga(toto) Pan, sikumbuki kama alicheza Taifa Stars...

    ReplyDelete
  10. MICHUZI MBONA UNAKUWA MBAGUZI KATIKA KUPOST MAONI.KWANIN KUTAKI UKWELI WA WANAOISHI NJE YA NCHI UJULIKANE,UNAFIKIRI KWA NINI NDUGU ZETU WANALOEA NJE YA NCHI NA HAWARUDI.KWANINI WANAOMBA MICHANGO YA KUSAFIRISHA MAITI, NA WANASEMA HUKU KUNA NEEMA. UNAIUA NCHI KWA KUTOPOST MAONI YANAYOTOA UKWELI.

    ReplyDelete
  11. sasa mwenzetu mtoa maoni namba moja!swali lako linashangaza!ukiuliza wakina manara wapo wengi waliokuwa wanacheza Kandanda! jina umeshambiwa kuwa KASSIM MANARA,sasa jina gani tena unalo uliza!!!
    labda mwenzetu ujui historia kamili ya Kandanda jijini Dar.
    Ndio kusema kwamba wakati Kassim na kaka zake akina sunday na Kitwana wanatamba katika soka wewe ulikuwa bado huko mbali na Dar,yaani ujakuja Dar au ujazaliwa kabisa:POLE SANA

    ReplyDelete
  12. comments za kukera michuzi ndio huwa hazibanii. mfano ni huo aneuliza kwa nini kakaa nje miaka 23 kwani kuna kosa au time limit ya kukaa nje ya nchi? halafu kuna mwengine eti anabisha kuwa eti hakuwa nje miaka 23 ni miaka minne tu! huu ni mtindo ambao michuzi ungelikuwa unauzuia kuingia hapa. mleta habari ameenda kumuona na bila shaka katika kuzunumza ndio ikaja hiyo issue ya kuwa nje muda wote sasa mijitu inatoka na kuruka na vi-comments za kijinga. Michuzi stop these inatuharibia raha za kuja hapa.

    ReplyDelete
  13. Nashangazwa na wanaoshambulia watu ambao walikuwa hawajazaliwa wakati Kitwana Manara anasakata kabumbu. Kuna ujanja gani kuwa ulizaliwa? Mbona hata hao wanaojiona wajanja walikuwa hawajazaliwa wakati Mirambo alipokuwa mtemi wa Wanyamwezi? Halafu badala ya kufurahia kumwona Mtanzania mwenzetu aliye ughaibuni ametulia na marafiki zake kutoka Afrika Mashariki na kati tunaanza kuhoji mipango yake ya maisha na kwa nini hajarudi Tanzania kwa miaka ishirini. Inatuhusu nini kwa nini hajarudi? Tufurahie kwamba anaishi vizuri na Waafrika wenzie huko ughaibuni, kama ilivyo utamaduni wetu Watanzania.

    ReplyDelete
  14. Allan Quaterman,

    Umsolopagazi alibonga: "..Tazama tarishi alikuja toka Natal akalia Makhumazani amekufa na nchi haitamuona tena.. Leo hii namuona mwinda tembo mwerevu, mbwa mwitu.. Nywele zake za kijivu lakini meno yake makali kama zamani.. Je wakumbuka jinsi ulivopeleka risasi kwenye jicho la nyati alikuwa anakuja kutushambulia?.."

    Kassimu upo? Mara ya mwisho nilikuona Uwanja wa taifa kwenye jezi ya Taifa ya manjano na kashata ya bluu kifuani. Wakati namba 1: Juma Pondamalai Mensah, 2: Daudi salum, 3: Maohamedi Kajole machela, 4: Jaffari Abdulrahman, 5, Jella Mtwaga. Utu uzima umenikinga wengine sikumbuki kama ilikuwa heka heka ya safari ya Lagos, Ndola au Khartoum?

    Watabiri wa Kibongo noma.. Uzushi, uzushi, uzushi Kassimu is no more: Kassimu is gone, is gone somewhere in Italy, Kassimu is gone for good.

    Kassimu scored the best goal in Austria!
    kassimu got money from the best gola and bought an expensive boat.
    Kassimu came back home with Mercedes Benz. Those were the the last good things we heard of Kassimu.

    Kassimu smokes, Kassimu sniffs, Kassimu indulges whatsoever harmful. Kassimu is no more. Those were the last sad things we heard of Kassimu Manara.

    Yah man, those were the bullshits the bullshiters bullshitted but mdau wa globu ya jamii counter bullshit those bullshits and left some of us agap!

    God bless you.

    ReplyDelete
  15. Manara tumemona... sasa mimi nimekutana na yule aliyekuwa Tanzania one Paul Rwechungura..yeye yuko maeneo ya Pennsylvania anapiga mzigo kama kawaida (kufuta kinyesi) nae alikuwa staa wa enzi hizo bongo.. picha ntatuma ka michuzi

    ReplyDelete
  16. kushoto-shoto????semeni kavaa t-shirt gani apo basi,,aaggh!!

    rwechungura anafuta kinyesi?wee annon 7.34am hahahahaaaaa yan umenfanya nife mbavu zangu!!!
    watu mna hasira na watu?nyie waacheni km wabeba mavi,wazibua mitaro nk ilmradi wala,wavaa waishi na watoto zao,,HAYATUHUSU thts kind of life they chose..

    ReplyDelete
  17. Hebu muacheni kaka Kasim.Alikuwa Ausria, Italy na sasa yuko Belgem, ana maisha mazuri tu huwa anakuja sana Paris pia anatembelea Holland kwa washakaji zake kaka Bachala na Kabila, na hiyo kusema hajarudi nyumbani ni uamuzi wa mtu, kila mtu ana malengo yake katika maisha.SALMA PARIS

    ReplyDelete
  18. ndugu kassim nimefurahi kukuona hapa, you look good brother! mimi ni nduguyo hussein msomali barabara ya saba dom, unakumbuka kinshasa united, anyway maybe we'll cross path in bongo one day. only thing i remember is you were always good in everything you did back then, i still remember how good you looked when you carried the baton at Tapa primary, you were always more entertaining than jumanne msandawe!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...