wamkumbuka mtoto samwel nkya ambaye uso wake uliharibika kutokana na madhara ya madawa alipokuwa mdogo. basi hivyo ndivyo anavyoonekana sam leo, baada ya kufanyiwa plastic surgery huko india na sasa anadunda kama kawa.
mtoto sam na wazazi wake wanatoa shukrani za dhati kwa wasamaria wema wote mliotoa michango ya hali na mali hadi kufanikisha zoezi hili ambalo vinginevyo uso wake wote ungemeguka. wanasema hawana cha kutoa ili kuwashukuru zaidi ya asante pamoja na dua kwamba Mola awajaalie maisha mazuri na afya njema
kwa picha na habari yake ya awali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mungu awabariki nyote!Huu ndiyo moyo wa Kitanzania.Cha kufanya kwa sasa,wazazi endeleeni kumpa malezi mazuri pamoja na lishe bora mwanenu.Pindi atakapo ongezeka mwili na kuwa mkubwa haebu jaribuni kutafuta ushauri wa kitaalamu kuanzi sasa,afikiapo umri pengine anaweza kufanyiwa plastic surgery nyingine ndogo na sura yake ikarejea kabisa katika hali yake ya kawaida.Lakini muhimu kwa sasa aepukane na mavyakula ya nje yenye lots of chemicals and artificial nutrients!Hakuna lisilo wezekana katika sayansi!God Bless You Samwel Nkya,you will be somebody one day!

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu atampa uzima wake. Bora ungeweka na picha ya alivyokuwa zamani ili wadau waone mabadiliko na ustadi wa hao madaktari...

    ReplyDelete
  3. Ooooooouph thanks LORD.kwanza kabisa namshukuru mungu juu ya huyu mtoto.pili waganga na wauguzi wote waliowajibika juu ya huyu mtoto tatu watanzania wenzangu wote mlioguswa na kufanikisha matibabu ya Samm MUNGU zidi kumpigania MWISHO wazazi nawashauri mumpeleke kwenye maombi ili azidi kupata uponyaji zaid BWANA ANATENDA BWANA ANAFANYA

    ReplyDelete
  4. NAIPONGEZA BLOG NA MICHUZI KWA LIBENEKE KWA KUFANIKISHA OPARATION YA SAMWELI NKYA

    ReplyDelete
  5. kwani huyo mtoto alipelekwa wapi kufanyiwa huo upasuwaji, india nini? kwani bado hakuna tofauti kubwa, nina uhakika kama angepelekwa viwanja vya maana kwani msingeweza kumtambua kwa kumlinganisha na picha yake ya zamani

    Mbega mweupe

    ReplyDelete
  6. we mbega ni kuku wewe

    ReplyDelete
  7. aleluja,,,
    ila bado iyo operesheni sura haijakaa sawa-sawa,inawezekana kabisa.
    michuzi blogu juuuu,ubarikiwe sana bro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...