mabingwa wapya wa netiboli kwa wanawake kwa nchi za afrika mashariki na kati JKT Dar na makombe yao.
Mabingwa wa netiboli kwa wanaume kwa nchi za afrika mashariki na kati Polisi Zanzibar na kombe lao leo katika uwanja wa Gymkhana

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Mh Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi bahodha wa Poisi Zanzibar kombe la ubingwa la netiboli kwa wanaume kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati iliyonyakuwa leo katika uwanja wa Gymkhana Zenji.
JKT ya Dar ilinyakua ubingwa kwa wanawake kuibugiza Bima ya Uganda kwa mabao 36-35 na kuwavua ubingwa. Polisi Zanzibar waliifunga Msambweni bao 37-22 na kutwaa ubingw wa wanaume.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hii ya Wazenji madume kushinda netiboli imekaaje wajameni?

    ReplyDelete
  2. Kwani Arsenal Ladies wanavyoongoza ligi ya futiboli ya wanawake au Uchina na Marekani zinavyowika kwenye soka la kike imekaaje? Dunia hii patasote hii.

    ReplyDelete
  3. Anon wa kwanza, hiyo haijatulia hata kidogo.

    ReplyDelete
  4. Hakika ninahitaji kuelemishwa.. hii ya wazenji kushinda "NETBOLI" wanaume ikoje haswa!!!.. Kwa uelewa wangu kwamba mpira wa pete ni wa akina mama sasa hii pete ya akina baba ilianza lini??? Ama hii ni staili ya Zenjibari tuu!!??? ...(dRU)

    ReplyDelete
  5. Tatizo naona sport ni kitu gigeni kwa wengi wetu bongo, netiboli ni mchezo wa kawaida kuchezwa na wanaume kama michezo mingine yeyote Dunia nzima hapo hakuna cha kushangaza.

    ReplyDelete
  6. wacheni ushamba ndomana tunakuwa nyuma vitu vingi sana. Uganda Kenya wote wameshiriki na TAnzania bara. Mie mtu wa Bara ila Comment kama hii ilitolewa UK,england wakawa wanasema Basketball na Netball is a Women Sports sababu American Man walishinda Netball hivyohivyo. UK wakaambiwa mbona wanaume wengi hawachezi netball na Basketball wakawa wanasema wanaona kama Women Sports ila Sports ni Sports kuna utengano tu ubavu mmoja watacheza wanawake mmoja wanaume. John.

    ReplyDelete
  7. University of Queensland, Australia.

    This article provides a textual analysis of selected media representations of men's netballers in New Zealand, an analysis of interviews with members of the Otago men's netball team, and a brief description of the author's participant-observation research in this area. The article discusses and challenges stereotypical representations of men who play netball — a sport originally designed specifically for women, and historically dominated by women — as either effeminate or gay cross-dressers. While the idea that men's netballers are perverse `gender-benders' remains widespread, the increasing popularity of social mixed-gender netball, combined with the determined efforts of established men's netballers, is beginning to challenge popular preconceptions. Men's netball provides recreational opportunities for both men who subscribe to hegemonic definitions of masculinity and for men who espouse more marginalized masculinities. Some evidence even suggests that despite altercations between homophobic Otago players and `queer' players from other teams during the 1990s, men's netball has actually provided opportunities for some players to challenge homophobia.

    Key Words: gender • masculinities • media • netball • New Zealand.

    Sipendi kuona wanaume kucheza netball ila wakiona sawa waacheni ni sports kila mtu na uhuru wake. from Hashim.

    ReplyDelete
  8. semeni mtakavyo ila kumbukeni kwa taarifa yenu tu na tanzania bara pia walitia timu yao ya wanaume katika mashindano ya netiboli. na kama alivyosema mtoaji mmoja hapo juu, duniani kuna timu za football za wanawake na sasa wanaume wameamua kuanzisha netiboli za wanaume, ingawa sijui kama wanavaa viskatin na kuruka kama akina dada ha ha ha haha

    ReplyDelete
  9. ok ok washkaji, nimependa namna baadhi ya wadau walivyochangia mada hii. mimi sijawahi kuona wanaume wakicheza netball hadi naondoka tanzania, kwa hiyo suali langu linakuja namna hii, kweli wanawake wanacheza football, rugby, basket ball na hata nimeona american football katika tv. lakini katika michezo yote hiyo wanafata sheria zote za michezo ikiwa pamoja na vivazi kuanzia viatu hadi fulana, jee wanaume wanapocheza netiboli huvaa vile viskati vifupi na vipande vya nguo vyenye nambari kwenye fulana zao? sishangai kuwa wametokea wanaume kucheza netball ila i have to say they are very very brave men. ni sawa na mwanamme kuvaa sketi eti tu kwa sababu wanawake wanavaa suruali.

    ReplyDelete
  10. Huyu mtoa mada wa 17 Feb saa 3:18pm ni mwanabusara hasa.
    Kwani hata mimi nijuavyo, si kila mwanaume yu tayari kuiga yafanywayo na wanawake.
    wala sidhani kama ni hoja ya busara kudai kuwa kwa kuwa wanawake wanafanya hili linalofanywa na wanaume, basi na wanaume watafute linalofanywa na wanawake waliige.
    sidhani kama hiyo ni natural.
    Ila dunia hii ni ya hiari, na sasa imekuwa ulimwengu ni mdogo mno, tamaduni zimechanganyika baina ya jamii mbali mbali.
    Maana sasa hatushangai tena kusikia kuna BWANA mmoja ameolewa kanisani na watu wengi wamehudhuria. Inabidi tukubali tu yaishe, japokuwa ukweli ni kwamba akili inashtuka!
    Haya wenzetu, wanaume endeleeni tu kuiga yanayofanywa na kinadada. Wao si wanaiga mnayoyafanya?
    Ulimwengu wa mwisho huu wazee wanatwambia!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...