profesa lipumba akipongezwa na mh. hamad, kiongozi wa upinzani bungeni, baada ya kuibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa chama cha wananchi CUF katika uchaguzi mkuu uliohitimisha mkutano mkuu wa 4 wa chama hicho katika ukumbi wa diamond jubilee hall jijini dar muda mfupi uliopita. profesa lipumba alipata kura 600 kati ya kura 669 zilizopigwa na kuwashinda wagombea wengine wawili kwa asilimia 98.6. Wagombea wengine koplo stephen masanja alipata kura 10 (asilimia 1.5) na profesa abdalah safari aliyepata kura 6 (asilimia 0.9). maalim seif naye aliweza kutetea vyema kiti chake cha katibu mkuu baada ya kuzoa kura 657 (asilimia 99.5) ambapo nne zilisema hapana na mbili ziliharibika. maalim seif alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kama alivyokuwa makamu wa mwenyekiti aliyepata kura 653 (asilimia 98.6) ambapo 5 ziliharibika na 4 zilisema hapana
profesa ibrahim lipumba akiwa kashikana mikono na mgombea profesa safari baada ya matokeo. mgombea mwingine koplo stephen masanja amesimama kushoto
profesa lipumba akifurahia mara tu baada ya matokeo kutangazwa
wagombea profesa safari na koplo stephen masanja dakika chache kabla ya matokeo kutangazwa
wagombea wakisubiri matokeo
maalim seif akipongezwa baada ya kuibuka mshindi katika kugombea kiti cha katibu mkuu wa CUF ambapo alijitokeza peke yake na kunyakua kura 657 katika kura 669 zilizopiga, wakati mbili ziliharibika na nne zilimkataa
profesa lipumba akipongezwa. nyuma yake ni katibu mkuu wa CUF maalim seif

wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo wakijiandaa kutanganza matokeo
meza kuu
msanii aliyetumbuiza kwa nyimbo ya injili ya 'nibebe' akipongezwa baada ya kutumbuiza










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Viongozi wa kudumu. Zidumu fikra za Mwenyekiti.

    ReplyDelete
  2. Kwanini wasiwatangaze ni viongozi wa maisha?. Itawasaidia pia kupunguza gharama za uchaguzi.

    ReplyDelete
  3. Kwa kifupi, this is boring!! Tumewachoka na hawana jipya wanadumaza upinzani TZ!!

    ReplyDelete
  4. TATIZO NI HAWA WALIOCHAGULIWA AMA WALIOWACHAGUA? KURA ZINAPOHESABIWA NI YULE ALIYEPATA KURA NYINGI NDIYE MSHINDI, MBONA CCM INAWABUNGE AMBAO WAMEKUWA BUNGENI TANGU MIAKA YA SITINI NA MAJIMBO YAO SASA HIVI YAMEKUWA HOI ZAIDI HATULALAMIKI KUWA WAEW WABUNGE WA MAISHA! HAWA WALISHINDA KWENYE UCHAGUZI HAWAKUJIWEKA MADARAKANI. CCM IMEKUWA MADARAKANI KA MIAKA MINGI HALI YA NCHI IKIZIDI KUZOROTA KIAFYA, SASA HIVI NA YENYEWE INAJIDAI KUTUINGIZA KWENYE SABABU ZA KUPOROMOKA HALI YA FEDHA DUNIANI LAKINI HATA HALI ILIPOKUWA NZURI TUMEKUWA TUKIPOROMOKA TU. SISI WENYEWE NDIO TUNAOICHAGUA BILA KUJALI FAIDA TUTAKAYOIPATA BAADAE.

    ReplyDelete
  5. kwa mpango huu CCM itatawala milele, hao watu hawana faida yoyote kwa watanzania.waje wapinzani wapya.

    ReplyDelete
  6. WHEN YU LOOK TO THIS CHAIRPERSON OF THS CHAMA LIKE A CROCODILE SMILE,HA HA HA HA KWAKWELI MWENYEKITI TU AKIGOMBEA U KIKWETE TAYARI YATOSHA KUONA CCM MILELE HATAMU.
    HUYU MNYAMWEZI ANA KITABASAMU CHA KENGE REALLY.LABDA NAE KAANDIKIWA KUONGOZA CHAMA DAIMA KAMA KIKWETE KUONGOZA NCHI DAIMA.
    MDAU K WA UK BANANA

    ReplyDelete
  7. ndo nini sasa!!! izi per diems izi?

    ReplyDelete
  8. Hakuna demokrasia katika baadhi ya vyama vya siasa hapa tanzania. hasa iki cha CUF na TLP. kila siku viongozi ni haohao. ni bora kama alivyosema ndugu yangu hapo juu, Lipumba na seif na hata mlema kule TLP wakatangazwa kuwa ni viongozi wa maisha. hakuna haja ya kupoteza fedha nyingi wakati wa uchaguzi wa vyama. fedha hizo zingeweza kusaidia mambo mengine.
    Ni hatari sana kwa viongozi wa namna hii kuongoza nchi, maana wanaweza kuvunja katiba ili watawale nchi milele.

    ReplyDelete
  9. Anon wa 26 2009 5:10 PM

    Hii ndiyo Democrasy, kama watu wengine bado wanaimani nao basi wewe cha kufanya ni kukubaliana nao.

    Mbona CCM toka uhuru inashinda chaguzi zote kuu hulalamiki?, ndiyo democracy hiyo. Yaani wengi wape. Kama hutaji panda juu kaji...

    ReplyDelete
  10. HUYU MSANII ANAJITAFUTIA TABU, YATAMPATA YALIYOMPATA MZEE REMMY ALIPOIMBA KWENYE JUKWAA LA MREMA. MAMA ANGALIA UTANYANG'ANYWA URAIA KAMUULIZE ULIMWENGU.

    ReplyDelete
  11. Hata sijui ni kwa nini wanapoteza pesa na wakati kufanya uchaguzi wakati kila mtu anajua matokeo. Hii ni kama zama zile za muundo wa chama kimoja tanzania.

    ReplyDelete
  12. HIVI KWELI DEMOKRASIA GANI MTU ANACHAGULIWA KWA 100% BILA KUPINGWA???BONGO NOMA HATA NCHI ZILIZOENDELEA HAKUNA KITU KAMA HICHO HAO VIONGOZI NI WANG`ANG`ANIZI HATARIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  13. Wanachama ndiyo wanahaki ya kumchagua yule wanayedhani ni kwa maslahi yao. Ninyi wote mnaolalamika ni wapambe wa vyama ambavyo mnamuogopa Lipumba na Maalim Seif, mlitaka wachague viongozi weak ili mpate ubwete.

    Kama ni suala la kutokuwa na uchaguzi wawatangaze kuwa viongozi wa maisha bali ushauri huo pia una apply kwenye uchaguzi mkuu. Ni nani asiyejua kuwa CCM hata iweje watashinda uchaguzi? na je kwa nini CCM hao hao wenye serikali wanahaha kuandaa uchaguzi mkuu kila baada ya miaka 5. Jibu ni simple, katiba ndiyo inasema hivyo.

    Kwa style hiyo hata CUF nao katiba yao inawataka wafanye uchaguzi wa viongozi wao. Tuache kuwalaumu Seif na Lipumba, tuwalaumu wanacha wa CUF kwa kuwachagua. Na kwa CCM tusiwalaumu wao tuwalaumu wananchi ambao wanachagua kila uchaguzi. Hiyo ndiyo Demokrasia jamani, demokrasia si kubadili watu au vyama ni kwa watu kuwa na uhuru wa kufanya wayatakayo yakiwamo ya kuweka viongozi na kuwaondoa kwa kura.

    ReplyDelete
  14. Ama kweli nyani haoni nini vilee. Sisisemu ipo miaka nenda rudi madarakani,hatusemi ni `hiyohiyo kila siku...
    M3

    ReplyDelete
  15. Wimbo wa Nibebe ni wa Rose Muhando Je Huyu msanii ni Rose Mhando? Kama sio yeye amewasiliana na Rose kuimba wimbo huu hapo? 3. Je kwanini aimbe wimbo wa YESU wakti watu hapo wanaimani tofauti na yeye alivyovyaa inaashiria dini nyingi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...