HABARI ZINASEMA BASI LA ABIRIA LIENDALO MBEYA LA 'SUMRI'  NAMBA  T134 ASA LIMEPATA AJALI MCHANA HUU KIASI CHA KILOMITA 10 TO MAFINGA MKOANI IRINGA, BAADA YA KUGONGA LORI LA MAFUTA (YA DIZELI) LILILOKUWA LIMEPAKI PEMBENI MWA BARABARA.

 INASEMEKANA   ABIRIA WAWILI WANAHOFIWA KUWA WAMEPOTEZA MAISHA. CHANZO CHA AJALI HAKIJAJULIKANA NA GLOBU YA JAMII INAFUATILIA NA ITALETA HABARI KWA KADRI ZINAVYOPATIKANA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. malori mengi ndo chanzo cha ajali ktk nchi nyingi za africa madereva wa malori wanaendesha long distance bila kupumzika na ni wazembe mno wana park ovyo ovyo tu wakishachoka inabidi wachukuliwe nao hatuakali kwani malori mengi mno yamesababisha vifo va ndugu wengi

    ReplyDelete
  2. Ni bahati mbaya sana. Pole yaowalioumia. Nafikiri kati ya Agosti na Septemba 2008 nilikuta ajali ya gari la SUMRY eneo na Mafinga (Kinyanambo 'A') nikaambiwa kuna waliokufa pia.

    Nadhani ukiachilia mbali uzembe wa madereva, malori yanayoegeshwa ovyo pembeni mwa barabara, kujaribu kulitangulia gari la mbele (overtake), kutofuata ratiba zilizowekwa, abiria kuhimiza dereva kwenda upesi, adhabu ndogo za wanausalama barabarani, kulewa, kuendesha bila mafunzo ya kutosha (lesseni halali), na mengine mengi sana, TATIZO KUBWA SANA LIKO UPANDE WA SERIKALI KUTOTENGENEZA BARABARA KUWA PANA. LICHA YA KUTOKUWA PANA VYA KUTOSHA, ZINA MASHIMO NK. TUNAHITAJI BARABARA ZENYE UPANA UNAORUHUSU KUPISHANA GARI 3 KWA WAKATI MMOJA.

    VINGINEVYO, TUTAENDELEA KUWAPOTEZA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI, NA WATANZANIA WENGI KWA JUMLA.

    Msomaji wako Mwenyekiti,

    MAREKANI.

    ReplyDelete
  3. KWA WANAOYAJUA MABASI YA SUMRI, KUPATA AJALI SI HABARI, HABARI NI MABASI YA SUMRI KUTOPATA AJALI.

    ReplyDelete
  4. Inasikitisha sana jinsi tunavyopaparikia ufumbuzi usioleta utatuzi wakati majawabu rahisi yenye ufanisi mkubwa zaidi yapo. Kuna kipindi tuliparamia ma spidi gavana...sijui ulikuwa mradi wa nani. Hawa madereva wetu leo anajifunza umakanika mwembeni kesho amekuwa dereva wataendelea kupata ajali kila siku. Kwa nini madereva wa Kamata na Relwe enzi hizo hawakuwa wakipata ajali za aina tunazosikia leo hii? Kwa nini madereva wa Uda hawapati ajali za madereva wa daladala?
    Namwomba Mungu awape nguvu walioathirika kwa namna moja ama nyingine na ajali hii katika kipindi hiki kigumu, Amina.

    ReplyDelete
  5. Hayo mabasi ya Sumry, ajali kwao si hoja. Hii sijui ni ya ngapi kwa mkoa wa Iringa tu. RTO analifahamu hilo, kwani abiria tusio wavumilivu tumekuwa tukimpa taarifa za mwendo kasi wa mabasi haya. sioni kama kuna hatua thabiti kudhibiti kampuni hii. Nimekuwa nikijiuliza kuna nini?? Kuna dereva mmoja ni kama kichaa vile anaitwa Babu Ally, nadhani kabobea kwa bangi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...