
Bwana Michuzi,
kwanza napenda kukupongeza kwa blog yako maana tunapata habari nyingi na kwa haraka na zenye maana, tena bila kubagua mada ambapo kila mtu katika jamii anapata kitu kidogo. Pili napenda kukutumia picha ya panzi mwenye rangi sawasawa na bendera yetu ya taifa. Panzi huyu nimekutana nae maeneo ya kisarawe, si vibaya kama utaona vema kumweka kwenye blog yetu ya jamii na wengine wamwone.
Kila la kheri
Mdau Frank John
Kila la kheri
Mdau Frank John
,
He!!!
ReplyDeleteBadala ya Twiga mi naona huyu ndo angefaa kuwa nembo ya Taifa
Du huyu ni senene anawakilisha masenene wake mungu wa bariki wadudu hawa
ReplyDeleteHapa Michuzi mweleze mdau Frank John kacheza ile mbaya!Huyu Panzi ndiyo haswa Saizi yetu Wadanganyika,au mnasemaje wandugu?Nembo hii ya Panzi itawakilisha vilivyo kwa uhalisia wake Akili zetu za Panzi zilivyo!Kenya wanatujua!Uganda usiseme!Rwanda na Burundi ndio kabisaaa!Ukipata Chuma Chakavu umekosa soko wewe wabwagie Wadanganyika tu!Lipakepake rangi ksiha waeleze jipya,uuuuh umeukata!Waziri atalipigia debe weeeeee,hadi kamati za bunge ndani katika kuhubiri,jamani huyu mnae muona ni Tembo sio Fisi jamani!Hawa wanao waambia eti huyu Fisi wakati ni Tembo,mafisadi hao,msiwaamini!Mimi Waziri wenu nimesema!Basi hata huyo mbunge wenu kijana machachari hamumwamini pia?Sasa itakuwaje?Mbona lile Kanya Bonya bunge lili idhinisha?Iweje hili chuma chakavu jamani,kuna mkono wa mtu nini?Tutaonana bungeni.Si mtaleta vijimuswada vyenu visivyo kichwa wala mkia,tutaona sasa!Hauziwi mtu hapa Mbuzi ndani ya Gunia!Alaaah,unajua nilishatoka off point wazee!Hapa tunazungumzia Panzi,si ndio!Akili za Panzi kwelikweli,ulishasahau mara hii?Panzi kwelikweli!Huyo Panzi kanivutia acheni masihara,kwa hizo rangi za Taifa?acha kabisa...
ReplyDeletewote hapo juu inawezekana mkawa vipofu, hana rangi za bendera ya taifa japo anamvuto. kumbuka rangi nne, nyeusi kijani ,blue, na njano. hapo mnaona rangi ya kijani, labda angemfukuzia katika majani halafu ndo ampige picha, hata hivyo nakubali anarangi zenye mvuto.
ReplyDeleteHa ha ha mdau hiyo ni bendera ya Taifa gani?? Labda Taifa la PEMBA!
ReplyDeleteHongera mdau kwa juhudi uliyofanya kumbaka ili uweze kumpiga picha na kuwakilisha. Anapendeza lakini rangi hazijatimia.
ReplyDeleteSAFI SANA AMA KWELI MUNGU MKUBWA
ReplyDeleteMPILI
HUYU ANGELIFAA KTK KUTANGAZA BAADHI YA BIASHARA NA MAMBO KADHAA YA BONGO PIA KUNA SAMAKI MWENYE RANGI HIZO ZA TAIFA,HEBU WAVUVI TUAOMBA MUTUBANDIKIE PIA PICHA YAKE
ReplyDeletebalanguru huyu (kwa lugha ya kitoto zaidi unaweza kumuita balale), siyo panzi.
ReplyDelete