Heshima yako mkuu wa Wilaya ya nanihii.
Wiki iliyopita (Ijumaa-Machi 27,2009) Chuo Kikuu cha DODOMA (Udom) kulikuwa na Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi (UDOSO).
Mchuano mkali ulikuwa ni kwa wagombea wa nafasi ya Rais wa College of Social Sciences and Humanities, nd.Ambrose Maratho na nd.Terri Gilead.
Matokeo kamili ya uchaguzi huo yalikuwa kama ifuatavyo:-Nafasi ya Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu kizima cha Dodoma (UDOSO),Raymond Magambo alishinda kwa kupata kura 2675 huku mpinzani wake David Nyangaka akiambulia kura 1076.
Ngazi ya makamu wa Rais wa UDOSO ilinyakuliwa na nd.Milton Isaya kwa kupata kura 1894 huku mpinzani wake Nd.Eliphace akipata kura 1768.Ngazi ya College,matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:- College of Social Sciences and Humanities,aliyeshinda nafasi ya Rais ni nd.Ambrose Maratho aliyepata kura 1257 huku mpinzani wake Nd.Terri Gilead akiambulia kura 790.
Nafasi ya Naibu Rais ilichukuliwa na kijana kutoka Zanzibar,Nd.Bakari Ali Khamis kwa jumla ya kura 1282 huku mpinzani wake Bi.Ngungi Rhoda (mwenye asili ya Kenya) akipata kura 759.
College of Education,nafasi ya Urais ilinyakuliwa na Nd.Sabhuni Joel kwa kupata kura 905 huku wapinzani wake Nd.Johannes Paul akipata kura 325 na aliyefuatia ni Dunia Salutwe aliyepata kura 200.
Nafasi ya Makamu ilinyakuliwa na Bi.Ndelwa Uria na kumshinda vikali mpinzani wake Nd.Msilanga Miyango.College of Informatics (wazee wa Computer) hakukuwa na upinzani,kwani kila nafasi ilikuwa na mgombea mmoja mmoja tu.
Nafasi ya Rais ni Nd.Honorious Amon na Makamu wake ni James Chambo.


SELEMANI TAMBWE
BA.PSPA 2nd Year
Habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hiki Chuo kimetoa wapi walimu? Haya si mauzauza tu?

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa kwanini mtoa habari alifika mahali akasema anayetoka zanzibar, na anayetoka Kenya, wakati wajina karibu sita yote ya mwanzo hakutaja wanatoka wapi. Je kuna kaitikadi ka ukabila hapa?
    Nadhani wote ni wanchuo kwa hiyo wanasifa.

    ReplyDelete
  3. Again I have to admit first lady is goergous ...yaani mpaka anavutia kumtazama
    mdau Houston

    ReplyDelete
  4. Terri was supposed to be the President. Siasa chafu za upinzani ndio zilitawala. Ngoja tuone waliochaguliwa watafanya nini.

    ReplyDelete
  5. hapa pana harufu ya udini kwani wakristu watupu wamejipanga.kwani UDOM imekuwa nyegezi st augustine?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...