Tumezindua leo, ni promo ya Zanzibar. BabKubwa Extra bado inaendelea toka shoto Karokola – Business Development Manager, June Warioba – PR, na Events & Sponsorship ManagerWilliam Mpinga – Trade Marketing Manager wakizindua promo ya bab kubwa mtelezo
Kampuni ya huduma ya simu za mkononi ya Zantel, imezindua promosheni mpya inayojulikana kama BabKubwa Mtelezo ambayo ni mwendelezo wa zile za awali, BabKubwa na BabKubwa Extra, itakayowawezesha watumiaji wa huduma za kampuni hiyo kupata muda bure wa maongezi kwa simu za mtandao wa Zantel kwenda Zantel na pia kuweza kutuma ujumbe mfupi wa bure kwenda mtandao mwingine.
Meneja Biashara wa Zantel, Brian Karokola aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mteja atatakiwa kutumia shilingi 2,000 ili aweze kujipatia shilingi 1,000 za bure ambazo ataweza kutumia kupiga simu kwenye mtandao huo na pia kuweza kutuma ujumbe mfupi mara kumi kwenda mtandao wowote kwa kipindi cha masaa 48.
“Zantel leo inafurahia kuzindua promosheni mpya ya kujipatia pesa zaidi inayojulikana kama BabKubwa Mtelezo, ili kuwawezesha wateja wetu kutumia pesa kidogo na kuendelea kupiga simu bure, na kuweza kuwasiliana kwa urahisi na ndugu, jamaa na marafiki pamoja na washirika wao kibiashara,” alisema Karokola.
“Katika kipindi hiki cha kuporomoka kwa uchumi duniani, Zantel tunaamini kuwa mawasiliano ni muhimu sana katika maisha ya kila siku na ndio maana tunatoa ofa hii ili kupunguza makali ya kifedha kwa wateja wetu” aliongeza.
Karokola alisema promosheni hiyo iliyoanza kupatikana jana ni maalum kwa wateja wa malipo ya kabla wa Zanzibar.
“Tunakusudia kuwawezesha wateja wetu kupata faida kila siku na tunawahakikishia wataendelea kunufaika kupitia promosheni yetu hii ya BabKubwa Mtelezo” aliongeza Karokola.
Meneja huyo alisema wateja wanahitaji kujisajili mara moja ili aweze kuandikishwa kwenye promosheni. Kwa mujibu wa meneja huyo, mteja atatakiwa kupiga namba *127#.
“Tumeanzisha huduma hii ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu na ni mategemeo yetu kwamba wateja wetu watafaidika katika mawasiliano yao ya kila siku na maisha kwa ujumla kwani mawasiliano ni muhimu katika chachu ya maendeleo” alisema.
Katika promosheni ya awali, BabKubwa Extra, mteja alitakiwa kujisajili kwa shilingi 500 na kuzungumza masaa 3 na zaidi ya hapo anapata ujumbe mfupi mara 5 kwenda mitandao yote ya simu.
“Tumeanzisha promosheni hii ili kikidhi mahitaji ya wateja wetu wa Zanzibar na tunatumai watafidika sana katika mawasiliano yao ya kila siku” alisema Karokola.
Akizungumza pia katika mkutano huo na waandishi wa habari, Meneja Masoko wa Zantel, William Mpinga alisema Zantel imedhamiria kuboresha maisha ya wateja wake, na hii pia ni namna nyingine ya kuwashukuru wateja wao kwa kuendelea kuwa nao.
“Tumeamua kuwawezesha wateja wetu kuongea kwa muda mrefu hii ikiwa ni jitihada yetu kuendelea kuijenga familia kubwa ya Zantel na kuwaonyesha kuwa tuko pamoja” alisema.
Mpinga alisema pia wateja wa Zantel wategemee mengi zaidi kutoka kwao kwa sababu nia yao kubwa ni kuhakikisha wateja wanaendelea kuongea.


Brother Michu, usiyabanie haya maoni, plse
ReplyDeletehii promotion ni kama utani kwa maoni yangu, kukuongezea shs 1000 baada ya kutumia 2000!!!!!, bora hata ile ya awali ambayo kwa mia tano mtu anaweza kutumia simu kwa muda wa saa kadhaa, pia ni bora ile promition ya Dar ya 1500/- kwa siku nzima.
kwa promosheni hii, mutaongeza makali ya maisha kwa watumiaji watakotaka kupata ofa hii, na sio kama munavyosema. (tumia zaidi ili unufaike). Kwa nini promotion hii ni znz tu? Najua munahofia Bongo watawajia juu sana kama promoition hii mutaipeleka huko, munajua znz ni mdebwedo tu, no complains
pili, mtandao huu nadhani unazidiwa sana na wateja, ama kuna tatizo la teknolojia duni ama utaalam na ubunifu mdogo, njia za simu hazipatikani mara nyingi wakati wa ofa ama promosheni kama hii. Zantel mumejiandaa vipi na tatizo hili?
huduma kwa wateja nayo ni duni mno, mtu anaweza kuweka on hold kwa zaidi ya nusu saa
Mimi ni mteja wa zantel kwa miaka zaidi ya kumi sasa na kwa usumbufu uliopo, kama si usumbufu wa kubadilisha namba/ laini ya simu ningekuwa nimeshahama.
Ushauri: Zanatel toeni ofa ya kweli sio ubababishaji huu (kwa mawazo yangu), wateja wenu wengi wa Zanzibar ni wanyonge, ukiweka kima kwa saa 48 mtu awe ametumia Tshs 2000, munawalazimisha wateja kutumia Tshs 30,000 kwa mwezi ili waweze kunufaika na shs 15,000/-. Nasubiri kuona matokeo ya promosheni hii ina nina imani haitodumu maana results (profit) itakuwa ndogo, to me this is a poor strategy
Mteja wenu, znz
Sawa sawa mtoto wa Dr. Dhas, Brian naona unafanya mambo!! Kula kichwa mwana naona Kotler inalipa, ha ha
ReplyDeleteKila la Kheri pia huyo anayeponda hiyo promotion naye anachekesha, value ya hiyo offer ni sawa na 50% ya original value, hiyo ni strategy nzuri kwao kwa sasa na recession yenu hii mmejichokea so mnapewa credit za bure unacomplain!! Bongo bongo kweli!
Hii promotion ni tamu halafu inanoga...sasa hao watu wa ZNZ wao siku zote wana complain,i think they want something free...bcoz umeshaambiwa na continuation ya Babkubwa extra na Babkubwa... sasa umepewa wide scope uchague unachokitaka...ZANTEL MUPO JUU WAZEE KAMUENI HIVYO HIVYO...!!!
ReplyDelete