Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Masoko na Biashara, Bi. Joyce Mapunjo akifungua  Semina kwa wenye Viwanda na Wafanyabiashara wa Tanzania. Semina hiyo ilifanyika katika Viwanja vya SabaSaba, ni sehemu ya  matokeo ya Utafiti uliofanyika nchini Uingereza, katika kulenga Masoko ya Nje na kujipanua Kibiashara.
David Potts wa Bradford University, Uingereza, akitoa maelezo ya Utafiti wa biashara katika kulenga Masoko ya Nje kwenye Warsha hiyo.  
Dk. Herbert Robinson na Dk.  Hildebrand Shayo wa South Bank University, London, wakiwa kwenye vikundi vilivyogawanywa kwenye Warsha hiyo kwa ajili ya kutoa maelekezo kwa wafanyabiashara hao 

Kituo cha Biashara cha Tanzania kilichoko London, Uingereza kwa kushirikiana na Bodi ya Biashara ya nje (BET), kiliratibu warsha ya uwasilishi wa matokeo ya tafiti za masoko ya nje kwa bidhaa za Tanzania. 

Warsha hii ya siku mbili ilifadhiliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko ilifanyika katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Saba Saba, tarehe 15 na 16 April 2009 na kuhudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 50 waliowakilisha sekta mbali mbali. 

Mgeni rasmi katika warsha hiyo alikuwa Katibu Mkuu, Bi Joyce Mapunjo ambaye alielezea umuhimu wa taarifa za masoko na kuwataka wafanyabiashara kuzitumia vizuri fursa zilizoonyeshwa na ripoti za tafiti hizo kwa manufaa yao na ya Taifa. 

Alimpongeza Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara (TTC – London) Bwana Yusuf Kashangwa kwa kusimamia vizuri zoezi na kukamilisha tafiti hizo na kwamba Serikali kupitia Wizara wataangalia jinsi ya kuimarisha shughuli za vituo vyetu vya Biashara vilivyoko nje ili kuboresha shughuli zake. 

Bi Mapunjo, aliwaasa wanawarsha na wataalam waliowasilisha ripoti hizo kutoa mapendekezo yatakayofanyiwa kazi na Wizara ili Taifa liweze kuongeza mauzo ya bidhaa zake nje ya nchi. 

Tafiti za masoko zilizowasilishwa zilihusika na bidhaa za mboga mboga na matunda, nta na asali, sanaa na ubunifu wa mikono, na vyakula vilivyosindikwa na vinywaji; tafiti ambazo zilifanywa na wataalam wa London South Bank University. 

Kabla ya uwasilishi wa matokeo ya Tafiti hizi Dr. David Pott wa Chuo Kikuu cha Bradford cha Uingereza aliwasilisha matokeo ya utafiti wake juu ya hali ya biashara ya nje nchini Tanzania tangu tupate uhuru na changamoto zote tulizopitia. 

Washiriki walifurahishwa na matokeo ya tafiti hizi na kwamba zimewafumbua macho na pia kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizo katika uwezo wao kwa nia ya kuboresha bidhaa zao ili ziweze kukubalika katika masoko ya kimataifa. 

Mwishowe, mikakati ilijadiliwa na mapendekezo yalitolewa ya jinsi ya kuboresha mauzo ya bidhaa za Tanzania nchi za nje. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. PETER NALITOLELAApril 23, 2009

    WW DAKTARI SHAYO, MBONA HAUKUMWALIKA MWENZIO YOHANNA MASHAKA WA ECONOMIC CRISIS YA MEREKANI KUKUSAIDIA KWA MAANA HUYO NDO SWAHIBA WAKO. NADHANI NYINYI HAMUJASOMA MUZUMBE VINGINEVYO MUNGESHIRIKIANA KATIKA SHUGULI ZENU KAMA HIZI ILI MUWASHINDE MASENENE WOTE. HONGERA SHAYO NAONA MIWANI IMETULIA KWELI KWELI NA TAI KALI

    ReplyDelete
  2. Jamani tubandikieni basi hiyo ripoti ya huo utafiti tusome tuelimike.
    Mzawa

    ReplyDelete
  3. Hivi hii taasisi TCCIA (wafanya biashara wakulima na viwanda) ipo bado? Tangu aondoke Musiba sisikii sana siku hizi.

    ReplyDelete
  4. Hiyo Report bandikeni hapa ili pia na sisi tutoe maoni. Tupe link yake tafadhali.Hatua nzuri.Nafikiri pesa ya mlipa kodi wa TZ or UK imetumika kufanya utafiti hivyo wana haki ya kuiona. Hata kama mmejitolea bure kufanya huu utafiti, basi ni vizuri sana kutujumuisha kuisoma.Hongereni Shayo, Kashangwa na Bradford University.

    ReplyDelete
  5. hizi ndio picha za kutuwekea na si zile za fulani katembelea london.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...