Kituo cha Biashara cha Tanzania kilichoko London, Uingereza kwa kushirikiana na Bodi ya Biashara ya nje (BET), kiliratibu warsha ya uwasilishi wa matokeo ya tafiti za masoko ya nje kwa bidhaa za Tanzania.
Warsha hii ya siku mbili ilifadhiliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko ilifanyika katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Saba Saba, tarehe 15 na 16 April 2009 na kuhudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 50 waliowakilisha sekta mbali mbali.
Mgeni rasmi katika warsha hiyo alikuwa Katibu Mkuu, Bi Joyce Mapunjo ambaye alielezea umuhimu wa taarifa za masoko na kuwataka wafanyabiashara kuzitumia vizuri fursa zilizoonyeshwa na ripoti za tafiti hizo kwa manufaa yao na ya Taifa.
Alimpongeza Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara (TTC – London) Bwana Yusuf Kashangwa kwa kusimamia vizuri zoezi na kukamilisha tafiti hizo na kwamba Serikali kupitia Wizara wataangalia jinsi ya kuimarisha shughuli za vituo vyetu vya Biashara vilivyoko nje ili kuboresha shughuli zake.
Bi Mapunjo, aliwaasa wanawarsha na wataalam waliowasilisha ripoti hizo kutoa mapendekezo yatakayofanyiwa kazi na Wizara ili Taifa liweze kuongeza mauzo ya bidhaa zake nje ya nchi.
Tafiti za masoko zilizowasilishwa zilihusika na bidhaa za mboga mboga na matunda, nta na asali, sanaa na ubunifu wa mikono, na vyakula vilivyosindikwa na vinywaji; tafiti ambazo zilifanywa na wataalam wa London South Bank University.
Kabla ya uwasilishi wa matokeo ya Tafiti hizi Dr. David Pott wa Chuo Kikuu cha Bradford cha Uingereza aliwasilisha matokeo ya utafiti wake juu ya hali ya biashara ya nje nchini Tanzania tangu tupate uhuru na changamoto zote tulizopitia.
Washiriki walifurahishwa na matokeo ya tafiti hizi na kwamba zimewafumbua macho na pia kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizo katika uwezo wao kwa nia ya kuboresha bidhaa zao ili ziweze kukubalika katika masoko ya kimataifa.
Mwishowe, mikakati ilijadiliwa na mapendekezo yalitolewa ya jinsi ya kuboresha mauzo ya bidhaa za Tanzania nchi za nje.


WW DAKTARI SHAYO, MBONA HAUKUMWALIKA MWENZIO YOHANNA MASHAKA WA ECONOMIC CRISIS YA MEREKANI KUKUSAIDIA KWA MAANA HUYO NDO SWAHIBA WAKO. NADHANI NYINYI HAMUJASOMA MUZUMBE VINGINEVYO MUNGESHIRIKIANA KATIKA SHUGULI ZENU KAMA HIZI ILI MUWASHINDE MASENENE WOTE. HONGERA SHAYO NAONA MIWANI IMETULIA KWELI KWELI NA TAI KALI
ReplyDeleteJamani tubandikieni basi hiyo ripoti ya huo utafiti tusome tuelimike.
ReplyDeleteMzawa
Hivi hii taasisi TCCIA (wafanya biashara wakulima na viwanda) ipo bado? Tangu aondoke Musiba sisikii sana siku hizi.
ReplyDeleteHiyo Report bandikeni hapa ili pia na sisi tutoe maoni. Tupe link yake tafadhali.Hatua nzuri.Nafikiri pesa ya mlipa kodi wa TZ or UK imetumika kufanya utafiti hivyo wana haki ya kuiona. Hata kama mmejitolea bure kufanya huu utafiti, basi ni vizuri sana kutujumuisha kuisoma.Hongereni Shayo, Kashangwa na Bradford University.
ReplyDeletehizi ndio picha za kutuwekea na si zile za fulani katembelea london.
ReplyDelete