HABARI NJEMA KWA WA TANZANIA WOTE
Jumba la Sinemal itakalotumika kuonyeshewa sinema hiyo:
AMC Theatres
1400 Main Street.
Chama Cha Mapinduzi nchini Marekani kinapenda kuwajulisha watanzania wote kuwa kimekamilisha mipango yake ya kuonyesha sinema zenye lengo la kuitangaza tanzania katika kumbi mbali mabali nchini Marekani. Sinema ya kwanza itaonyeshwa katika kumbi la AMC lililopo katikati ya jiji la Kansas City, Missouri siku ya Alhamisi ya tarehe 23/ 04/2009 kuanzia saa 1:45 usiku.
Kabra ya sinema hiyo video ifuatayo http://www.
Address kamili ya ukumbi huo wa AMC ni:
AMC Theatres
1400 Main Street.
Kansas City, MO 64105
Pia tunapenda kuwafamisha kuwa CCM nchini marekani imefanikisha Tanzania kujiunga na shirika la Ethnic Enrichment Commissiner linalotumika kuzitangaza nchi mbali mbali wanachama katika nyanja za kiuchumi, utamaduni, na mambo yote yanayousiana na nchi mwanachama. Kwa taharifa zaidi kuhusiana na hili shirika tembelea tovuti yao na ukibonyeza pale panaposema Countries utakuta bendera ya Tanzania tayari imeshatundikwa na ukibonyeza kwenye bendera ya nchi yetu basi utakutana na mambo yote yanayohusu tanzania. Tovuti yao ni www.eeckc.org
Kwa taharifa na maelezo zaidi wasiliana na wafuatao hapa chini
Michael Ndejembi--Mwenyekiti CCM makao makuu nchini Marekani 713 384 4567
Miraji Malewa--Katibu mkuu CCM makao makuu nchini Marekani 832 741 4452
Deogratias Rutabana--Mwenyekiti CCM shina la Kansas City, Missouri - Marekani 816 812 5495
Mungu Ibariki Tanzania.
Taarifa hii imeletwa na uongozi wa CCM nchini Marekani


CCM kumbe wako mpaka huku. Dah. mi sikujua. Kadi mnazo? Ninataka kujiunga CCM sasa kwani wanamageuzi bado wanaendealea kugeuka na kugeuzana! Nitumieni kadi ya CCM miye!
ReplyDeletehabari nzuri , tumefurahi kusikia hivyo , tunamatumaini na mengi mazuri yatakuja
ReplyDeleteNamimi naomba card,Inaweza ikanitoa nikirudi Bongo LINE ya kupata UFISADI.
ReplyDeleteCCM OOYEE!!!!
ReplyDeleteKWAKWELI CCM MAREKANI MNASTAHILI PONGEZA KWA JITIHADA ZENU, NYINYI NI WASAFIRI BADO MPO NJIANI, NA NI MATUMAINI YANGU MTAFIKA PALE MNAPOKWENDA.
"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
"SALAMU KUTOKA UNITED KINGDOM (UK)"
Mimi nimegundua kuwa hawa jamaa wa ccm nchi za nje mitizimo yao ni mizuri. Nimependezwa sana na hili tangazo na nawaombea wazidi kuitangaza nchi yetu.
ReplyDeleteMichuzi na wewe kazi yako ni nzuri sana.
Hivi nyinyi wenzetu mliopo nje ya nchi,amna chama kingine mnachoshabikia zaidi ya ccm? maana kila mkitoa maoni yenu ama mnapokutana katika mambo yenu ni ccm tu ndio inayozungumzwa, mnakatazwa kujiunga ama kushabikia vyama vingine? mbona mnatupa hofu.
ReplyDeleteWatanzania wenzetu mliopo nje ya nchi wote mkifanya mambo kama haya Tanzania yetu itafika mbali sana.
ReplyDeleteNamna hii CCM mtatawala daima. Viongozi na wanachama nawapongeza sana kwa mambo mnayofanya sio tu kufanya sherehe kulewa pombe. Nawaomba msikate tamaa maana hata wenzetu wa nchi zingine ndio wanavyofanya wawapo ugenini.
Mtandao wetu wa jamii kila siku unazidi kutuabarisha. Kazi njema!!!!!Mkuuuuu
vyama vingine bado wako ktk mageuzi jaman,hawana uhakika wa uanachama mguu pande,,,tobo,,,
ReplyDeleteila mmh!!ccm nje za nchi
Hatuna chama cha mapinduzi hapa Amerika ila kuna wapuuzi kadhaa wanaojipendekeza,marekani tunajumuia za watanzania.Huyo mwenyekiti alichaguliwa wapi na nani marekani tuna majimbo zaidi ya 50 Kansas City haiwezi kutuwakilisha watanzania wote Mwenyekiti nakuona kama hujaliangalia hilo kwa upana.
ReplyDeletenawasilisha.
Mtanzania/Mzalendo.
binafsi nawapongeza sana hawa jamaa
ReplyDeletekwani kazi wanazozifanya ni kwa maendeleo ya tanzania tofauti baadhi ya watu wanavyodhani. nilitaka kumshauri huyu mwenyekiti bwana michael ndejembi kwamba ongea pia na viongozi kule nyumbani ili tuwe na siku yetu hapa marekani, kama vile uhuru day
nadhani we mzalendo ndio mpuuzi kama hata uwepo wa ccm hapa marekani huujui unawezaje kujua viongozi wake wamepetikana vipi, tatizo wajinga wajinga kama wewe mko wengi sana. acha uwendawazimu wako kama huna cha kuandika kaangalie porno.
ReplyDeletejamii ya kitanzania inatakiwa kuwa na tabia ya kutambua mchango wa watu kama hawa badala ya kuanza kuwakashfu kama baadhi yetu tunavyofanya. sio tatizo kwa kina ndejembi kusimama na kuwaletea nafasi nzuri kama hii ambayo naamini hata ubalozi wetu haujawahi kufanya, si hivyo tu ni vigumu sana kwa sisi watanzania kuwa na mawazo kama haya ya kuisaidia nchi yetu kama tunapokuwa nje ya nchi. Nadhani ni vizuri kuwapongeza CCM Marekani kwa kazi nzuri ili pia kuwapa moyo wengine wenye mawazo kama haya.
ReplyDeletemwana harakati
CCM hii ya Marekani haiongozwi na wapuuzi wala mafisadi ila ni watu wenye kujua nini wanafanya na kwa faida ya nani, wanaelewa watumie njia gani kufanikisha malengo yao. kama kunajumuia za kutanzania zinafanya nini zaidi ya majungu wakikutana. tujifunze kuheshimu, kutambua na kuzienzi kazi zetu.
ReplyDeleteSafi sana ccm US hii ni zaidi ya kila kitu. jamani niko marekani kwa zaidi ya miaka kumi na tatu sasa sijaona mtu mwenye mawazo mazuri na endelevu kama dogo ndejembi. kuwa na wazo then ukaliweka kuwa kitu halisi kama hivi si kitu kidogo jamani na hasa ukizingatia kuwa mawazo yetu huwa ni wapi nikabebe mabox nilipwe dola nyingi nikamchukue demu wa fulani, sasa ktk kipindi kama hiki watu kibao hawana kazi si rahisi ukawa na mawazo mazuri kama haya. bwana ndejembi we endelea mimi niko pamoja nawe hata ma wife wangu anakusifu sana kwa mambo yako mazuri.
ReplyDeleteCCM ndio yenyewe na hasa ikiwa na watu kama kina michael mambo huwa mswano sana, sisi tutakuwepo kujionea sinema hiyo mapema kabisa.
ReplyDeletewatu wengine bwana eti ccm iko hata marekani, we ulitaka iwe mpaka wapi? ikisikia usenge ndio huu kama huipendi kaa pembeni endelea kutongoza wake za watu tuachie ccm yetu tujifanyie mambo usituchanganye mjinga wewe.
ReplyDeletee bwana michuzi niulizie kwa hao viongozi wa ccm ni lini wataonyesha huku DC msije mkatusahau.
ReplyDeleteMungu wabariki watu wote wenyemitizamo ya kulisaidia taifa letu. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini kama wenzetu wanavyofanya nawapongeza siangalii wana tumia nini.
ReplyDeleteKwa wale wenye rohoo za kwanini kwa taifa letu basi mungu waangamizie mbali.
Hawa watu washenzi watupu, kama mmeshindwa kufanya kazi za heshima maofisini hapa US , si mrudi tu TZ mkaendelee na chama. Nyie wawili bado mnafanya kazi za home health kwa vichaa , halafu na shue zenu mmeshindwa kutafuta kazi za ofsi mnataka kila mtu ajiunge na CCM , nyinyi kiwa kama wakubwa wao.
ReplyDeletewatu wako busy na kazi bwana hapa Kansas city za proffesional bwana , nyie kazaneni na utumbo wenu wa chama.Najua mtafaidi kugombea ubunge kwa mtindo huo lakini msitake umaarufu kupitia migongo ya wengine hapa.
kweli mambo ni mazuri sana,unajua watu wengine wanapenda majina yao yasikike ila jinsi ya kujitoa hawajui wafanye nini ili atambulike wanaishia majungu na chuki mtu ukibuni kitu chake anaona siyo kitu ila cha kwake ndiyo kitu bwana wewe kama hauna bahati kaa chini utulie fanya kazi yako siyo unajifanya msomi kumbe bure kabisa unapo anza kuzungumzia uelekeo jiangalie wewe mwenyewe upo wApi siyo kulopoka tu na kujiingiza katika mambo ya watu ili upate usawa ukiona hakuna kitu kelele wewe unadhani wao walianza vipi unajitokeza mbele ya watu kumbe wanakudharau tu kazi kukaa kuwadanganya watu tz nina nyumba usa kuna mtz ana nyumba hapa wazaa wenyewe wanahesabika iwe wewe wa kuja jenga nyumbani
ReplyDeleteHONGERA NDEJAMBI
Kazi nzuri vijana!!!!!. Nawapongeza kwa juhudi zenu. Naomba endelea kuitangaza nchi yetu. Nchi yetu inaitaji watu wenye moyo huu, naomba mtu hasiwakatishe tamaa hata kido, tutafika.
ReplyDeleteNimependa sana hili tangazo lenu vijana wa CCM mungu awazidishie.
Kweli hii imenigusa. Ninashangaa sana watanzania wanaokwenda nchi za nje na kuiona tanzania kama si nyumbani kwao kama huyu mwenzetu hapo juu anayedai yeye amesoma na anafanya kazi nzuri. Mimi naamini mtu aliyesoma anakuwa na mawazo ya kusaidia ndugu zake kama hawa wenzetu wa CCM wanavyojitolea kulitangaza taifa letu.
ReplyDeleteSizani maoni yote yanatolewa na watanzania wenye akili timamu. Naamini wengine sio ndugu zetu bali ni wale wanaosikia uchungu wasikiapo Tanzania inaendelea
Mungu ibariki nchi yetu
Iwe ccm,chadema au chama chochote cha siasa/kidinikama mlengho wake ni kusaidi nchi yetu mimi nitajiunga.
ReplyDeleteMawazo yenu ni mazuri ndugu zetu. Sina uakika kama mnapata picha za kisa zaidi. Nitapenda kushirikiana nanyi katika kulitangaza taifa letu
Pia msisaau kuwaeleza wamarekani kuwa nchi yetu inavivutio vingi ikiwa ni pamoja na utulivu.
ReplyDelete