msanii anayekuja juu kwa kasi ya ajabu coster siboka "mfalme" akionesha albamu yake mpya iitwayo 'niwe wange' yenye vibao motomoto 10 katika mahadhi ya ukerewe, wajita, wahaya na kisukuma. anapatikana costasiboka@hotmail.com ama simu namba +255 787 499 961
coster siboka akiwa na wanenguaji wake wakijiandaa kwa ziara maalumu ya mikoa ya kanda ya ziwa, wakianzia kigoma wakati huu wa pasaka, kisha watashukia mwanza, musoma, mara na bukoba chini ya udhamini wa kilaji cha balimi. hiyo pozi isikustue wkani coster pia ni mtunisha misuli bingwa na anashikilia taji la mr guiness mwaka wa tatu mfululizo. hivyo yuko fiti na habari toka kigoma zinasema 'mfalme' anasubiriwa kwa hamu na maelfu wa wapenzi wa muziki wake ambao unakubalika kanda ya ziwa kwa sana.  muone na msikilize mfalme siboka hapo chini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...