washiriki wa miss tz uk 2008 wakiwa kwenye foto shuti huko london  tayari kwa mtanange wao Juni 14, ya mwaka huo katika  ukumbi wa silverspoon, wembley

Kinyang`anyiro cha kumtafuta mrembo wa Tanzania Ulaya mwaka huu,”Miss Tanzania Europe 2009` kinatarajiwa kufanyika Juni 27 kwenye ukumbi wa Silverspoon ulipo pembeni ya uwanja maarufu wa Wembley,uliopo kaskazini mwa jiji la London.

Akizungumza Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shindano hilo, Juma Mabakila alisema kuwa wamepata baraka zote kutoka kwenye kamati ya Miss Tanzania kwa kupewa idhini ya kuandaa shindano hilo la Ulaya.

Awali miaka miwili mfululizo onyesho hilo lililikuwa mahsusi kwa ajili ya warembo wa London pekee, lakini kamati ya Miss Tanzania mwaka huu imetoa kibali cha kuandaa mashindano ya Ulaya kutokana na kufanikiwa katika shindano la Miss London.

“Kweli tulifanikiwa katika mashindano yetu tuliyofanya miaka miwili iliyopita, tulipeleka washindi wetu kushiriki katika mashndano ya Miss Tanzania na wote walifanikiwa kuingia katika kumi bora, mwaka huu tumejiandaa va kutoksha, “ alisema Mabakila..

Mabakila alisema kama ilivyo katika mashindano yaliyopita, pamoja na kutangaza utamaduni wa Tanzania, kubwa zaidi ni kutumia sanaa ya urembo kutangaza vivutio vya utalii..

Awali mwaka jana Big Brother Afrika wa mwaka juzi Richard Bezuidenhout ambae ni Mtanzania alikuwa mmoja wa majaji wa shindano hilo, huku akisaidiwa na mwenyekiti wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na Jacqueliney Mafuru.
Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza katika onesho hilo ni Banana Zoro na Hafsa Kizinje(pichani ),wasanii wa Kiganda wenye makazi yao hapa London na kujijengea jumaarufu mkubwa, Da Twinz..

Taji la Miss Tanzania UK mwaka 2008, Tusekile Mwakibinga wakati mwaka 2007 mshindi alikuwa, Gladness Katega.Warembo wawili wa Miss Europe 2009 wanakwenda moja kwa moja kushiriki shindano la Miss Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. E BWANA WATOTO WATAMU HAWA,UKILA KWA PILIPILI,CHAPATI AU CHAI YA RANGI,WANAONEKANA SAAAFI TU,TENA HAUHITAJI PILIPILI MANGA
    MDAU-ESKIŞEHIR
    TURKEY

    ReplyDelete
  2. Mr TZUK vipi jamani? Semeni watu tuingie kambini!

    ReplyDelete
  3. hivi inabidi pia kuwa mzuri wa sura? au ni bodies tu?

    ReplyDelete
  4. Acha ulafi wewe anony one. Angalia msije kutafunwa nyie wenyewe.

    ReplyDelete
  5. Hawa wasichana wasituharibia jina zuri la nchi yetu. Vifua vyao waende kumonesha chief Mswati.

    Huu si utamaduni wa kitanzania wa mtu kuonekana nusu uchi. Nawashauri wabadilishe title ya mashindano haya, badala la miss TZ Europe iwe miss Europe au Miss Swaziland.

    Hatupendi kuiaibisha Tanzania kwa mambo ya kuiga tamaduni za kigeni.

    ReplyDelete
  6. Siyo utamaduni yetu hiyo -- wasichana wetu kuenda kuonyesha miili yao namna hii kwa madai na visingizio vya maendeleo!

    ReplyDelete
  7. She love to party, have a good time
    She looks so hearty, feeling fine
    She loves to smoke, sometime shifting coke
    She'll be laughing when there ain't no joke

    A pimpers paradise, tha's all she was now
    A pimpers paradise, that's all she was
    A pimpers paradise, that's all she was
    Every need got an ego to feed
    Every need got an ego to feed

    She loves to model, up in the latest fashion
    She's in the scramble and she moves with passion
    She's getting high, trying to fly the sky
    Now she is bluesing when there ain't no blues
    A pimpers paradise, that's all she was now
    A pimpers paradise, that's all she was
    A pimpers paradise, that's all she was
    Every need got an ego to feed
    Every need got an ego to feed

    A pimpers paradise, that's all she was now
    A pimpers paradise, that's all she was
    A pimpers paradise, I'm sorry for the victim now
    A pimpers paradise, soon their heads, soon their
    Soon their very heads will bow
    Pimpers paradise, don't loose track
    Don't loose track of yourself oh no!
    Pimpers paradise, don't be just a stock, a stock on the shelf
    Stock on the shelf, Pimpers paradise that's all she was

    ReplyDelete
  8. Nyie mnao lalamika kwamba sio tamaduni zetu kueni na mabadiliko,kwani UFISADI ni utamaduni wetu? Umeingia Tanzania na sasa tunaongoza.

    ReplyDelete
  9. Hahahaa..hamna kitu hapo!Sura hazijakaakaa..we could do better.

    ReplyDelete
  10. Wewe Anon wa 7:12

    Kwa hiyo kama tukikubali shari moja, na lingine pia likubalike siyo??

    ReplyDelete
  11. Kama mwanakijiji alivyosema vitumbua vya nyumbani vitamu. Mwanakijiji mbona umepotea na mashairi yako?

    ReplyDelete
  12. HIVI NYIE MNAODAI HUU SIO UTAMADUNI WETU, EMBU NITAJIENIE UTAMADUNI WETU TU UPI MNITAJIE JAMA.

    KAMA UNAKUMBUKA MAMA ZETU WALIKUWA WANASOMA SHULE WANAVAA VIMINI VYA KUFA MTU LEO HII HAO HAO WANADAI SIO UTAMADUNI WETU WAACHI UJINGA .

    MAENDELEO YA KILA KITU NI LAZIMA UIGE HATA WAMASAI WANAVAA SURUALI NA PIA HAWATOBOI MASIKIO SIKU HIZI ,WAMAKONDE HAWACHANJI PIA SIKU HIZI, WATU WA IRINGA HAWALI MBWA KAMA ZAMANI HUONI UTAMADUNI UNAACHWA SABABU YA MAENDELEO SASA HILI LA KUKAA VIFUA WAZI TATIZO LIKO WAPI KWANI WAMETEMBEA BARABARANI HIVYO , WAO WAKO KNY MASHONDANO YANALOWALAZIMU KUSHIRIKI WAKIWA NA KIVAZI CHA HIVYO NA VINGINE , SASA WEWE KAMA KINAKUKWAZA HUNA HAJA YA KUPIGA MAPELELE WEWE JUA NI HALI UA MAENDELEO YA KIULIMWENGU.
    -KIRIMOTO BACK IN STAGE-

    SWALI LA KIZUSHU AU JIBU LA KUMALIZA RUSHWA?

    HIVI RAIS ANAWEZA KUMALIZA RUSHWA NCHINI??

    JIBU NI- UKITAKA KUMALIZA RUSHWA NI KWANZA KWA WEWE KUACHWA KUTOA NA KUPOKEA RUSHWA KWA HIVYO RAIS HATA AIMBE NYIMBO ZOTE STUDIE HAWEZI KUMALIZA RUSHWA. HII RUSHWA IMEKUWA NI PERSONAL 2 PERSONAL ISSUE NA KUIMALIZA LAZIMA IWE HIVYO HIVYO,

    KAMA UNAJIBU TOFAUTI TUELIMISHANE WAUNGWANA.

    ReplyDelete
  13. anonymous wa 4:40 acha ushamba

    ReplyDelete
  14. Ina maana Miss Tz yuropu kila mwaka wana washiriki wale wale. mwaka juzi hawa waliopo ktk hii picha ndio walishiriki sasa na mwaka huu ni hawa hawa au??

    ReplyDelete
  15. mtoto wa 3 toka mbele MTAMU SAAAANA dah!!!

    hii kazi tutapona kweli???

    ReplyDelete
  16. wabovuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...