Home
Unlabelled
dogo wa uswazi leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Dear Wasomaji
ReplyDeletehicho kibali cha kuruhusu mtu kufuga simba katika maeneo ya makazi ya watu kilitolewa na nani?
Je kulifanyika hali ya kuangalia adhari endapo huyo simba ataruka ukuta?
Je wizara ya maliasili na utalii na wanyama pori wanampango gani
Je huyu aliyeadhirika kwa kugongwa na bajaji aliposikia simba na kukatwa mguu atalipwa na insuarance gani?
Kuna aliyejiuzulu kuhusu sakata hili?
Wasomaji, msiokuwa mnafahamu hii siyo issue ya simba na yanga, ni kuwa kuna mtu alikuwa anafuga simba huko tegeta!
Tanzani kazi ipo
Hivi mkuu wa wilaya ya nanihii...ina maana katuni za kipanya ndo umezipiga buti? Tuambizane mwanakwetu!
ReplyDeletesawa MK ubigwa wenu safari hii, ila Barca watawatoa.
ReplyDeleteSisi wakazi wa tegeta tumeshagundua kuwa habari za simba katoroka Zoo ni za uzushi mtupu.
ReplyDeleteInaonekana huyu mzushi ana tofauti zake binafsi na wamiliki wa hiyo Zoo.
Huyo mzushi ndiye wa kutafuta na alaaniwe kwa sababu ametoa taarifa za uongo za kutisha watu.
Mimi jana nimetembelea pale Zoo na familia yangu hao Simba wapo, Twiga , Zebra, Nyumbu, Makobe makubwa, mamba nk
Ni bahati tumepata Zoo sehemu ya karibu kwenda kutembea na Familia zetu kuliko mfumo dume wa akina Baba kushinda Baa.
Nashauri hawa wazushi wa simba katoroka waende kiungwana kwa mmiliki wa Zoo wamuulize yeye alifanyaje akafanikiwa ili wapate mwanga ili nao waanzishe ili ziwepo Zoo nyingi hapa DAR kama ilivyo nchi za wenzetu.
hahaaaha kweli sasa vipi walimuona au kakimbilia Bagamoyo
ReplyDeleteMimi pia nilikuwa nina hamu ya kujuwa kulikoni mbona kp hatumuoni? This doesnt mean kwamba dogo wa uswazi hayuko ft, no yuko bomba mbaya. Could this be true kwamba ni issue ya terms nini maana kp naye at times ujasiriamali anauzidishaga sana. Its my opinion anyway.
ReplyDeleteHee! uzushi mwingine hauna mana kabisa. Hivi huyu jamaa aliyeanzisha uzushi eti Simba katoroka Zoo ya Tegeta naamini lengo lilikuwa kumwaribia biashara mtanzania mwenzetu masikini. Leo nilipofika pale Zoo na mke wangu na tukakuta Simba wote 2 wapo tulishindwa kuvumilia tukacheka sana maana duh, huyu mzushi ana roho mbaya sana ana nia ya kutushawishi wakazi wa tegeta tuichukie Zoo. Atafute sababu nyingine hiyo ya uongo imefeli.
ReplyDeleteMisupu....si vibaya ukitolea majibu suala la kutoonekana kipanya kama baadhi ya wadau walivyokuuliza. Acha kuweka pamba masikioni!
ReplyDeletetatizo la Mithupu huwa anaignore sana watu. Akiamua kujibu kuh Kipanya atajibu lakini anaweza akanyamaza hata watu wakianza kumtukana atawalia ngumu. Huyu ndiyo balozi wa Tegeta bwana.
ReplyDeleteYaelekea mwenye hii zoo anajaribu kujitetea kwa njia nyingine ukweli unabaki pale pale,Hii si zoo labda niite holdling ground ya export.imezungukwa na makazi ya watu,na kibaya zaidi yaelekea hawa wanyama hawalishwi ipasavyo,ukweli haifai kuwa hapa,mimi nimkazi wa hapa Tegeta.hawa wanyama hawapo kwenye hali nzuri,huwezi kueleza habari ya uzushi wakati hali halisi inaonekana,sasa lazima tujue hata Mbagala watu walilalamika hivyo hivyo zamani jamani hii kambi ipo jirani na makazi watawala wakala jiwe,sasa subirini hapa malipuko ya magonjwa.ninavyojua mimi wanyama na ndege wana magonjwa mengi ya ajabu kama mafua nk.hapa sioni huyu jamaa antetea nini?? huwezi kulinganisha hii zoo na za ulaya kama anvyodai.wenzetu wameendelea wapo dunia ya kwanza sisi umasikini mtupu na rushwa za kupewa vibali vya kufungua zoo kwenye mazingira yaliyojaa utata hata environments zenyewe hazipo kwenye standard ni hatari kwa afya za watu.
ReplyDeleteKweli kuna watu hamtumii akili kidogo kufikiria Annony 11.11 am 17 may.Hapa swala ni kwa nini Zoo(what ever holding export)iweke jirani na makazi ya watu. Leo unashekelea kwenda na familia kuona wanyama unasahau kesho wanaweza kutoroka au kuvunja makazi ukizingatia wanamtu wakuwa hudumia kwa liche, Siku akifanya uzembe wakamtoka wakija kwenye makazi yenu Utaendelea kucheka. Na kama ndio mfumo dume wa kukaa baa kwa mumeo huko Zoo anashinda siku nzima au anaenda kila siku. Kwanini wanyama wakali wakee Serengeti;Mikumi ,Manyara n,k sehemu yao na watu tusiende kujenga kule. Think twice wacha kusupport ujinga huu. kama nikuona wanyama unafunga safari family mnaenda sio iwe hatari kwa mwengine. Unataka tukuchangie michango isiyoyalazima kwa maafa ya kuaribiwa na simba wakati tunaweza yaepuka. Mpaka siku aje kuwa wa watu ndio unagundua hapakustaili pale kuwa zoo. Jingeni mazingira ya kuepuka hatari kabla ya kutokea. bye
ReplyDeletehuyu jamaa mzushi ana roho mbaya na ni wivu tu ndio unaomsumbua. inaonesha ana tofauti zake binafsi na wamiliki wa Zoo. Mimi sintasahau uzushi wake uliotikisa karibu nchi nzima eti simba wametoroka zoo ya Tegeta ikabidi niwazuie wanangu wasiende shule Alhamisi na Ijumaa kumbe ni upuuzi mtupu.
ReplyDeleteNilipothibitisha kuwa ni uongo nimeshangaa sana na nikawaombea wenye Zoo Mungu azidi kuwapa. huyu mwenye roho mbaya aangalie sana mwenyezi Mungu atampa fundisho kwani wakazi wote wa Tegeta, boko, bunju, Salasala, mbezi nk tumepata ukweli kuwa ni habari za uongo.
Nina uhakika bahati na mibaraka yako Mwenyezi Mungu atakunyanganya atawapa wenye Zoo kwa vile unatumia uzushi na uongo kuwapiga vita .
Mzushi jaribu kuzusha jingine kwa hili umenasa watu wanakucheka mitaani kwani umemtangazia kwa gharama ya bure mmiliki wa Zoo biashara yake sasa kila mtu anajua kumbe Zoo iko Tegeta.The impact is positive kwa wenye Zoo!!!
Hivi swala la Simba wametoroka Zoo limeisha vipi. Wamiliki inabidi walipwe fidia na mzushi kusema habari za uongo.
ReplyDeletePili, inabidi na sisi wakazi wa Tegeta nk huyu mzushi atulipe fidia katuweka roho juu siku 3 bila amani. Hii ni aibu.
Inabidi huyu mzushi alipe Fidia Mashule kwani masomo yalikatishwa kwa taarifa zake za uongo za kuogopesha watu.
EH! sasa wivu wa namna hii ni uchawi. Mbona wasafirishaji wa NYOKA, ndege, mijusi na vinyonga holding grounds zao tena hazifai na ni chafu kabisa zimetapakaa Dar kote na hazina usalama kama hiyo zoo ya Tegeta?
ReplyDeleteTena inaonesha na wewe mzushi unafanya biashara hiyo, hivyo unampiga vita mfanya biashara mwenzako! Ungeaanza kusakama hao wenzako mnaofuga mitaani nyoka hatari Black mamba na Green mamba tugekuelewa.
Hoja yako iko weak na bahati mbaya umeanza na uongo wa kuogopesha watu kuwa simba katoroka ZOO kumbe si kweli.
Makelele yako hayo ya kiwivuwivu yatasababisha nyote mlazimishwe mtafute maeneo makubwa kama Zoo ya Tegeta ya kufugia hao nyoka na ndege wenu mhame,Buguruni,kinondoni
Mwenge,vingunguti,kurasini,tandale nk ili mwache kufugia uani. tena wengine mnafugia nyumba za kupanga na ni usumbufu kwa wapangaji wenzenu lakini watu wanavumilia.
Acha wivu na ubabaishaji ila kamwone mmiliki wa Zoo ya tegeta akupe SIRI ya mafanikio yake hadi akajenga ZOO yenye usalama.
La sivyo utaendelea kuona wivu hadi lini maana Zoo ya Tegeta ndiyo pekee iliyo na uzio imara na usalama hivyo nina imani Serikali itaendelea kushawishika kumpa kila msaada. Wewe endelea kupiga wivu, mwenzako ataendelea kupaa na kuboresha zaidi.
Watu wengine bwana!!!!!Uongo wako simba katoroka umemtangazia biashara bure mmiliki wa Zoo sasa kila mkazi wa DAR anajua kumbe kuna ZOO Tegeta!!!!!
lakini kweli mbona hayo maholding Grounds ya ndege,vinyonga na nyoka yametapakaa dar nzima tena vichochoroni kwenye makazi ya msongamano ya watu zenyewe hazitaleta mafua ya ndenge ila mzushi anaisema zoo ya Tegeta tu!!
ReplyDeleteHuyu mzushi si angeanza kupiga vita hizo holding grounds tungemwelewa kuliko kupiga vita zoo ya tegeta iliyo na uzio imara na majengo mazuri ya kufugia wanyama. ROHO MBAYA NI TATIZO KWA MAENDELEO !!!