JK akiwa katika picha pamoja na wadau mbalimbali wa los angeles baada ya kuongea nao jijini humo leo akiwa katika ziara ya kikazi ya wiki moja nchini marekani.
Jengeni na kuendeleza kwetu –
JK awaambia Watanzania Marekani

Na Mwandishi Maalum, Los Angeles, Marekani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa wajibu mkubwa wa Watanzania wanaoishi nchi za nje ni kufanya jitihada za kujenga na kuendeleza kwao, ili kuthibitisha ubora wa kuishi kwao nje.

Rais amesema kuwa na wala Watanzania hao wasihangaike na kutafuta jinsi ya kusaidia kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa sababu shughuli hiyo ni wajibu wa Serikali na wanaweza wasiwe na uwezo wa kushiriki katika kuendeleza miradi hiyo mikubwa ya maendeleo.

“Mkiweza kupata mwekezaji mzuri, leteni tu. Mkipata mtu mwenye fedha za kusaidia ujenzi wa miradi mikubwa kama mabarabara na shule leteni, lakini ushauri wangu mkubwa kwenu ni huu…jengeni na endelezeni kwenu kwanza, ili mthibitishe kwa nini ni bora kuishi nje,” Rais Kikwete amewaambia Watanzania wanaoishi katika eneo la Kusini mwa Jimbo la California.

Akizungumza na Watanzania hao leo, Jumanne, Mei 19, 2009, kwenye Hoteli ya Beverly Hills Hilton mjini Los Angeles, Rais Kikwete amesema:
“Ujumbe wangu kwenu ni kwamba msisahau kwenu. Wathibitishie mliowaacha nyumbani kuwa ni bora zaidi kuishi huku mliko kuliko nyumbani. Jengeni kwenu, endelezeni kwenu. Msije kufikia mahali mnarudi nyumbani mkakosa hata mahali pa kufikia,” amewaambia Watanzania hao wanachama wa Chama cha Watanzania Wanaoishi Kusini mwa California.

Rais amewasisitizia Watanzania hao wakati akijibu maswali yao: “Tengenezeni kwenu. Haya makubwa ya ujenzi wa mabarabara, tuachie sisi wa Serikali, ndio maana tupo. Hatutaki kuwasumbua kwa masuala ya ujenzi wa barabara na shule. Hii ndiyo kazi na wajibu wetu. Nyie jengeni kwenu, ili ndugu zenu wajue kuwa kuishi kwenu nje kuna maana.”

Rais Kikwete ambaye amekutana na kuzungumza na Watanzania hao baada ya kuwa amewasili mjini Los Angeles akitokea mjini San Francisco ambako alianzia ziara yake ya Marekani pia ametumia muda mwingi kuelezea mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali yake ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule 2,700 za sekondari katika miaka mitatu iliyopita.

Rais amezungumzia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta za elimu, afya, ujenzi wa barabara, akisisitiza kuwa, kwa mfano, kiwango cha malaria nchini kimepungua kwa kiasi cha asilimia 38 katika miaka mitatu kutokana na maamuzi ya Serikali tokea iingie madarakani.

“Ni kweli kuwa malaria inabakia ugonjwa unaoua watu wengi zaidi nchini, lakini hatua tulizozichukua katika miaka mitatu, minne iliyopita, zimepunguza kiwango cha malaria kwa asilimia 38. Katika Zanzibar ni kama tumemaliza ungonjwa huo kabisa.”

Rais pia amewaeleza Watanzania hao kuhusu mpango mkubwa wa Serikali kujenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata nchini akiongeza:

“Hata kwa yale magonjwa ambayo tumekuwa tunalazimika kuwapeleka watu nje, tunachukua hatua. Kwa mfano, Wachina wamekubali kutujengea hospitali kubwa ya kutibu magonjwa ya moyo.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2009

    RAISI WETU KASEMA TUNAWEZA KUENDELEA KUBEBA MA BOX SASA MNAOPIGA KELELE TURUDI BONGO WAKATI YEYE MWENYEWE ANAELEWA MAISHA KOKOTE KULE. RAISI KIKWETE JUU. MFAGIA BARABARA TEXAS.

    ReplyDelete
  2. SurvivorDMay 20, 2009

    Hii nimeipenda! Unajua Kikwete ni G! Anaelewa situation. He has been there, done that. Ameeleza ukweli. Kazi kwetu wadau wa ughaibuni. Tusife moyo jamani!!

    PS. Ningemshauri tu Mh. Rais awawajibishe watu wa TRA na bandari wanaojaza ubadhirifu, rushwa, na ukiritimba mpaka watu tulio g'ambo tunashindwa hata kuingiza magari tuliyonunua huku nchini kwetu wenyewe.

    Ni bora kuchukua vitu huku kama Magari, friji nk. kwani viko authentic, lakini tukifika home tunanyanyaswa sana ilhali vitu tunavyoingiza ni vyetu mali yetu na jasho letu wenyewe!! This is not fair Mr President, tutajengaje nchi namna hii kama tunanyanyasana wenyewe kwa wenyewe??? :(

    Survivor.
    Mdau UK (representing Rock City).

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2009

    MTALII WETU JUU. MA-BOX TUTABEBA HASWAA NA BARABARA TUTAFAGIA ILI MRADI TUNAPATA HELA YA KULA. CHOCHOTE KINAKUJIA USONI UNAFANYA TU. HII BOMBA KWELI KWELI. MAMBO YEE, MAMBO WAA. PIGENI MZIGO WANA NCHI. KIAMA CHAO MAFISADI TUTABEBA MA-BOX KUWEKEZA BoT WANAZIBEBA WATAKIONA CHA MOTO. NA LITAWACHWEA HASWA...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2009

    Mdau wa ROCK City umeongea Point ila inategemea hivyo Vitu unaingiza kwa Uraia wa Wapi? KIKWETE anaongea Point.

    Rock City msubiri Kikwete akitokea mitaa yenu Muulize pengine utajibiwa vizuri, ila kukujibu tu atakujibu vizuri ila ukifika kwa wahusika watakuzungusha. xxxx. Jamani Kikwete njooni huku mikoani ya kati mtujengee Viwanda tufanye kazi. au mmesahau kuna Mikoa mengine?.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2009

    Nashukuru kikwete amezungumzia ujenzi wa shule 2,700 lakini cha ajabu hajagusia hizo shule zina madawati ya kutosha au laa, pia hakusema kwa kipindi hicho ni waalimu wangapi walihitimu na shule na kuajiriwa ktk hizo shule. Kazi kweli kweli.

    Walio nje jengeni kwenu manake nini? si ni kufanya miradi ya aina zote kama wana uwezo, walio nje wana uwezo wa kujenga shule na pi amiradi mingine mikubwa, Raisi alitakuwa awahimize kuthink big kwa hao walioko nje wana nafasi kubwa ya kufanya vitu vikubwa iwapo juhudi zao watazielekeza kwenye kufanya vitu vikubwa na bila kussau vidogo

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2009

    Mafanikio katika elimu? Labda anazungumzia "bora elimu" ni elimu bora manake idadi ya shule na wanafunzi imeongezeka lakini ubora wa elimu umeendelea kuporomoka. Haishangazi wanafunzi 'mlimani' kusoma wakiwa wamesimama nje ya madarasa kwa kukosa viti!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2009

    Kwani wewe kubeba mabox Ulaya na kuwa mmchinga Tz kuna tofauti gani? Fagia, safisha vyoo jenga nyumbani, wako waTz kibao hawana ajira ni wamachinga tu, uwezo wa kujenga hawana,mapato yako ya siku moja kwao ni mapato ya mwezi, Tusidanganyane akili mu kichwa Rais keshasema -BOX UGHAIBUNI - JENGA KWENU, finali uzeeni.

    ReplyDelete
  8. maisha popote wadau ubebe box uwe machinga alimradi upae kula na kusonga mbele

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2009

    wewe sister hapo kushoto kwa JK nimekufananisha na sister mmoja nilisoma nae miaka ya 1998-2000 kulee kwa maremu mzee mjale. kwa jina edwardina,na class kwetu alikuwa msichana pekeyake.sasa kama niwewe naomba tafadhali ujibu hapa kama utaiona hii.
    iwould be greatful.

    xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2009

    Nyie wadau mnashabikia kukua ulaya kisa kikwete kasema mnachekesha san.Tatizo letu wabongo hatuna ambition sasa mtu utabeba maboksi ukiwa na miaka 60.Wether ulaya au Bongo mtu inabidi uangalie future mtu ukiwa na carrier hata ukiwa US una uwezo wa kuzeeka na peace of mind.
    kazi zenyewe za maboksi hazina uhakika leo unayo kesho una sasa mtu kwa mpango huo utaweza ku build retirement fund,kusomesha watoto and save for your funeral kweli????
    Jamani wandugu tuangalie future na maslahi mimi sifagilii bongo wala America nafagilia confortable life na saving for future.wengi wanaoshabikia maboksi inaonekean bado ni vijana wadongo hawajaanza maisha na kuishi pay check to pay check si tatizo
    Misupuu ni hayo tu
    Happy vacation

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2009

    ni kweli watu tunahitaji kujenga kwetu lakini wasimamizi hakuna wizi mtupu

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2009

    ni kweli ndugu rais umesema kweli , ni wengi tunatamani sana kujenga kwetu lakini kinachotukwamisha ni usimamizi wa hao ndugu zetu au jamaa zetu tunaowaamini lakini ndio hivyo Wizi mtupu.mwisho wa yote wanakupigia picha ya nyumba ya jirani na kukuambia nyumba yako imefikia hivi, au ni hii hapa imekwisha. ukijafanikiwa kwenda home unakwenda kuta hamna cha nyumba yako wala hela.inakuwaje sasa muheshimiwa!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2009

    Mh ama kweli wabeba box, wasafisha vyoo, waosha wazee, na huyo mtalii mwenzenu lenu moja. yani walewaleee!!! kila kukicha hamna jipya!!!
    haya sie yetu macho. nae akimaliza muda wake atakuja kuwaunga mkono kuendeleza libeneke hukohuko.
    Asifiwe, TZ

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2009

    he!! makubwa haya. kwa mara nyingine nashuhudia usanii wa mtalii wetu. eti anasema na ninamnukuu

    ''wala Watanzania hao wasihangaike na kutafuta jinsi ya kusaidia kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa sababu shughuli hiyo ni wajibu wa Serikali na wanaweza wasiwe na uwezo wa kushiriki katika kuendeleza miradi hiyo mikubwa ya maendeleo''.
    Mh hiyo serikali yake imeshashindwa kuleta maendeleo. ni ufisadi tu kwa kwenda mbele!!!
    duh! ama kweli!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2009

    Shule 2700, walimu wangapi? shule sio majengo! "wachina wamekubali kutujengea hospitali kubwa!" Open your eyes, nani anakujengea kitu for free! Barabara zilizojengwa ni chachena hafifu sana hazitamaliza miaka mitano. Guys, mtapata papers lini mkatembee Bongo msidanganywe. And, do we need a president kuja kuinitiate promotion ya utalii/biashara? Kudadedeki!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 21, 2009

    Hii IMETULIA......sasa waheshimiwa wabeba maboksi si mmeona mlivyosisitiziwa kujenga home?...na si mnaelewa midhali KARATASI haziko basi hamtaweza kutoka.....sasa kwa hili lisiwasumbue sana...NYIE KUFENI NA HAYO MABOKSI ILA PESA TULETEENI TUWASAIDIE KUJENGA ....(Mtajuuuta kutufahamu)

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 21, 2009

    Politics as usual... Next time karibu Texas.
    Mchumi wa Texas

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2009

    Na sisi tulioko bongo tunaoishi mijini, tusisahau kujenga madongo kuinama kwetu tujijengee heshima.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 21, 2009

    Serikali iachiwe miradi mikubwa itafanya yenyewe?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 21, 2009

    Wabongo mlio Mbele kweli mnapendeza. Si bure viongozi wetu wanazimia company yenu kuliko ya wachovu tuliyobaki TZ.

    Ni rahisi zaidi kwa bank cashier mswahili aliye LA kupiga story na viongozi wetu kuliko Daktari mswahili aliye Ocean Road Hospital kupata fursa kama hiyo.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 21, 2009

    mie sina shida na wanaofanya kazi nje hata kama ni ya kuzibua vyoo.
    Mie tatizo ni rais wetu kutokuwa na muda wa kusikiliza kero za wananchi wake kwani yeye ni safari za nje tu. Nchi inakwenda kombo, kikubwa zaidi ni kutokuwa na maamuzi kama raisi.


    Mangi wa K'Koo

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 21, 2009

    RAIS HONGERA , SHULE 2700 KWA MIAKA MITATU. JE VITENDEA KAZI VIMEPATIKANA, AU NI MAJENGO TU YA KURUNDIKA WANAFUNZI "BORA ELIMU". JE KUNA WALIMU WA KUTOSHA KWENYE HIZO SHULE ZILIZOJENGWA? MADAWATI? VIFAA VYA KUFUNDISHIA? N.K
    SI AJABU NDIO MAANA TUNA SHULE KAMA NJIRO ARUSHA...FORM FREE HAWAJUI "KUSOMA WALA KUANDIKA".
    ITS REALLY FUNNY TUNAPOJIVUNIA MAJENGO YA SHULE..WAKATI NI ELIMU HAKUNA...KAZI IPO?

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 21, 2009

    TK AU CPWAA UMEAMUA KUJIWEKA MBELEMBELE MAANA HADI KWENYE TV (ITV) NIMEONA WEWE NDO MSTARI WA MBELE UKIPIGA MAKOFI....CHEKO LAKO DADAAAAAAAAAA HALOOOOOOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 21, 2009

    Nawaonea huruma. Nimekaa sana huko nikabeba boksi nikatuma hela za maendeleo hamna kilichofanyika. Nilipoamua kupiga shule na kumaliza na kurudi huku mambo ni mswano sana. Carrrer path naiona, life ya choice, mikopo nje nje (nishajenga nyumba mbili, naishi moja napangisha moja)etc and all that only in two years na sio mtoto wa fisadi. Huyo anawadanganya mbaki huko ili waliopo huku competition ipunguwe. Jitahidini mmalize kilichowapeleka huko mrudi tuendeleze taifa pamoja. Kama ulikuwa hujui kujiendeleza mwenyewe ni njia bora tu ya kuendeleza taifa kwani in the process unawasaidia wengine wengi tu. Ukijenga unatoa ajira kwa mafundi, ukinunua gari utatoa ajira kwa waoshaji nk. Karibuni nyumbani tufaidi wote matunda ya uhuru.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 21, 2009

    Siku zote Rais wetu anakauli nzuri na ahadi nzuri kusikia masikioni kwa jamani(mfano;Maisha bora kwa kila mtanzania)Ila ukiangalia maisha ni magumu sana;mafuta yameshuka bei lakini vyakula bado vipo juu wkt gharama za kisafirisha toka mashambani vimepungua. Pili Ufisadi ulikuwepo siku nyingi isipokuwa leo hii ndio watu tunaona wanakwenda mahakamani. Isiwe kisingizio Ufisadi ndio maana mambo mengine ya maendeleo na maisha magumu yasiboreshe. Tutamuongeza mitano nachopenda kuona Nini atatufanya na kutuashia km kumbukumbu ya utawala wake. Mkapa pamoja na yote yaliyomkumba Pesa ilikuwa na thamani. Uwanja mpya katuachia; barabara zimejenga na madaraja yamejengwa. Tunasubiri ya JK kwa vitendo sio Slogan tu and Nice words. Njooni na mabox mfungue viwanda msaidie ajira kwa wamchinga, thanks

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 21, 2009

    jenga kwenu ukiwepo
    izi za kutuma?utakuta patupu na unawatia wezio majaribu

    me nala kabisaaa

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 21, 2009

    kazi ipo izi pichaz

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 21, 2009

    maboxxxxxxx

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 21, 2009

    “Hata kwa yale magonjwa ambayo tumekuwa tunalazimika kuwapeleka watu nje, tunachukua hatua. Kwa mfano, Wachina wamekubali kutujengea hospitali kubwa ya kutibu magonjwa ya moyo.”

    sasa kwnini msiwaombe waendeshe TRA na wizara zingine kwasababu jamaa wamefanikiwa sana mainfarstructure, wapeni miaka 10 muone mafanikio

    ReplyDelete
  30. Tatizo sisi watu wa nje tunachokosea Ukituma budget ya ujenzi ni lazima yule ndugu yako anayesimamia umlipe pesa yake ya usimamizi sababu na yeye ameacha shughuli zake kufanya kazi zako kwahiyo ukituma 1m na yeye mpe atlest laki kazi zitakwenda tuu .
    living cost dar iko juu sana uki compare na miji mingine dunia ,kwahiyo hilo tulifahamu pia.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 21, 2009

    mimi nashindwa kuwaelewa watu ambao shughuli yao ni kufuatilia tu maisha ya watu wengine na kupiga kelele ooh huyu anapiga box,ooh huyu hataki kurudi nyumbani sijui kujenga nchi,wewe kinakuhusu nini?maana kila mtu ilimradi sio mtoto mdogo wa kuambiwa cha kufanya, na wala hakutegemei kwa chochote kile, basi anahaki ya kuishi popote pale ilimradi tu yeye karidhika kuwa anachokifanya kinampa kuishi na nihalali.kama kudhalilika anadhalilika mwenyewe,kama future basi niyake mwenyewe ilimradi hajatelekeza watoto wake na mkewe na kwa africa pia wazazi.
    mambo ya sijui undugu ndiyo yanayo kwamisha maendeleo ya watu wengine nyakati zingine,utakuta mtu kajisulubu akifanikiwa tu basi kilamtu anajifanya ndugu na anataka msaada! mara huyu aseme mimi ni binamu yake yule binamu wa shangazi yako si unanikumbuka?mara ooh mimi ni mdogo wake yule mume wa shangazi wa mjomba wa babu yako!! ilimradi fujo tu!
    ktk mataifa yaliyoendelea hata ndugu yako tumbo moja hamfuatiliani ktk mambo yenu,kazaliwa kivyake na wewe kivyako fight kivyakovyako!kama ni urithi wa mali za wazazi labda hapo kila mtu anahaki sawa kama wazazi wameamua hivyo.
    sasa mambo ya undugu yanaingia hadi ktk national level ndiyomaana utasikia watu wanapigia wengine kelele eee wa ughaibuni rudini,njooni mjenge nchi! si ujenge wewe basi kwani nani kakushika mikono?
    HII INANIKUMBUSHA MWALIMU MMOJA ALIOWA AKAPANGA UZAZI AKAZAA WATOTO 2,kisha kaka yake ambaye ameaowa wake wawili ana watoto 11 akaibuka na watoto wawili eti kamletea yule MWALIMU akidai eti "WEWE UNA WATOTO 2 TU naomba uchukue na hawa 2 uwasaidie"
    yule teacher akamjibu vizuri sana"UNADHANI MIMI SINAUWEZO WA KUZAA ZAIDI YA WAWILI"? wewe una enjoy stereo mwenyewe kisha watoto nitunze mimi sio?anza mbele fasta na majukumu yako bro kivyako!!!
    sasa hii ndiyo jamii yetu ya waafrica,kufuatiliana ilimradi tu unaona mwenzio anajitahidi kuishi wewe unataka umshike miguu na majukumu yako. pigeni kimya nyie mnao lalamika acha watu waishi maisha yao,ukitaka nawewe nenda ukapige box,kama huwezi basi nenda kalime huko mbwinde kwenu watanzania wasife na njaa basi kama unataka kujenga nchi!
    hata JK anajuwa life ndio maana analinganisha kisha anakaa kimya kuhusu kupiga mabox huko ughaibuni na kukaa kusota bila kazi wala biashara zinazoeleweka bongo,maana hata yeye akimaliza muda wake anamajukumu yake ya kifamilia ambayo hakuna atakaye kwenda kumsaidia kama mzazi na mumue wa mtu!! au warudisheni basi wapiga mabox wa kibongo[wamachinga] muwaambie wakajenge vijijini kwao si wako kariakoo wamejaa na mitaa mingine! kazi kuosha vinywa tu rudini rudini!jenga nchi n.k anayeona aliko box halilipi anarudi mwenyewe wala hahitaji kuambiwa na mtu!anayeona linalipa pia anaendelea na miango yake ya kimaisha kivyake wala huhitaji kumwambia cha kufanya,maana hata jinsi alivyofika huko aliko wewe hujui hata hiyo nauli alitoa wapi! sasa iweje leo uko mstari wa mbele kuchonga na kuelekeza anachostahili kufanya! watu wengine bwana mnakuwa nywele tu lakini hamshirikishi ubongo kwanza kabla ya kusema unachotaka kukisema.

    ReplyDelete
  32. wewe mtoa maoni wa mwisho hacha pointless zako kipi yeye kwake ni kipya kwake kwasababu kila kitu amekukuta kuanzia Epa.Richmonduli,Buzwagi,Kiwira,pamoja Na nyinginezo sas kwanini usipe mda wa kufanya mabadiliko hata wewe ukiwa Rais uwezi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja na kwa muda mfupi hivi jamani tuwe wakweli kwa hili na makini kwa serikali yetu achani lawama.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 21, 2009

    Kama kawaida yenu wajinga ndio waliwao....Mtalii huwa zake ni kupiga picha na kutabasamu basi...hakuna kipya hapo..........

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 21, 2009

    duh!!
    mboni mmeng'ang'aniana ivo ktk picha na JK?

    ona yule na msuli sijui mabegani,na uyo anachat na simu

    hahahaaaa

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 21, 2009

    Mtalii wetu inabidi utulie huko nyumbani ili usikilize vilio vya wananchi. Utasikiliza lini matakwa ya wananchi na vilio vyao vya kila siku. Naomba uje NORTH CAROLINA kama MKAPA alivyofanya. Tunataka kukuona na sisi tutoe vilio vyetu kwa watanzania Tz na Nje ya Nchi.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 22, 2009

    Box tutapiga saana, wanaoumia na waumie. We kama kurudi rudi mwenyewe usijidai kuhamasisha watu.

    Kila mtu na ukoo wao.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 22, 2009

    anony wa 2:03 yani huna pointi kabisa umekalia kulalamika tu!! we ulienda nje kwa kuzamia meli nini??!!!
    wewe ndio unatakiwa kushirikisha obongo wako kabla ya kuongea. ungeshirikisha ubongo usingeongea hayo. kuna yule mtanzania aliyewa kusema akiwa NY kuwa ni bora kuwa mbwa marekani kuliko kuwa binadamu bongo. mimi nashawishika kuhisi ni wewe ndo uliyetamka haya.
    halafu nadhani pia wewe hujasoma kabisa ni box mwanzo mwisho bora wenzako hao wamefika huko wakala buku kwanza wana magamba yao sasa ndo wanapiga box ili wakirudi huku tuwakome vizuri blingbling sana, mambo ya hammer nini!! you know you know nyingi halafu baada ya miaka 2 wanapigika kisha wanatamani kurudi states lakini wanashindwa sababu walioverstay na umri umewapiga chini.
    lakini wewe najua hurudi bongo ng'o sababu hushirikishi ubongo wako kabla ya kuongea. you just burst!!! haya tukutakie kila heli na ukimbizi wako huko.
    Asante
    Asifiwe, DSM, BONGOLANDMWAMBAMOTO

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 22, 2009

    big up wakimbizi woote huko!!! niwatakie tu box njema bila kusahau nyetooooozi!!!! mambo ya povuuuuuuzi!!!
    kuleni maisha wanangu kufa kwaja

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 22, 2009

    duh!wewe asifiwe wa dar mwambamoto unanipiga madongo et ninawaambia watu washirikishe ubongo kabla ya kuongea na kusema sina point!huenda ukosahihi sinapoint, lakini nahisi huenda ukawa ni miongoni mwa wale watu tegemezi wa ndugu,sasa unaona kime ku-touch wewe. kuhusu kupiga shule umekosea,maana shule yangu ni yanguvu,na nimeipata ktk vyuo vikubwa na kazi yangu pia kwasasa ni ya maana na nimeipata kwa uzito wa shule yangu! ila kabla ya hapa nilisota sana na box ndilo lililonifikisha hapa nilipo sasa,bila box hapa nisinge fika wala!lakini wewe sijui shule yako ila kwa hapo ulipo nadhani kuifikia shule yangu itakuwa muda!hahaha! anyway nami pia najuwa life,tena najuwa nachokifanya,nikikanyaga huko mimi sio mwenzio tena,labda uwe ktk caliber ya watu wazito wenye makampuni au mafisadi wafuja mali za walalahoi.
    kwahivyo ukiona nazungumza hapa kama mwehu usidhani mimi ni kijana wa mtaani kwa sasa,ila life la mtaani nalijuwa A-Z. wewe sidhani kama unajuwa life la mtaani linakuwaje! ila kama unataka njoo na wewe utie mkono kwanza usikie,ukiona linakushikisha ukuta kimbia,lakini ukiwa kidume kama mimi,future utaitia mkononi!hahaha isije ikawa naonge na mtu wa miaka 45 bado eti uko on the way to the future!hapo is too late.
    haya bwana mie na uhakika wa kumlipia mwanangu fee ktk private nursery school ya maana hadi university ya maana pia,je wewe? nashukuru sana box maana lilinipa a way to this future in which iam now! bongo nitarudi lakini narudi kwa heshima sio kama nilivyoondoka.
    wapiga box piga sana,waache waosha vinywa waoshe maana hiyo ni jadi ya akina asifiwe wa dar mwambamoto,lakini ukilala njaa hata maji ya kunywa hakupi atakuita kibaka tu na kukuchoma moto akikuita mwizi! haya bwana asifiwe usifiwe kwenda mbele mkubwa!

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 22, 2009

    bwana anony wa 8:10. natumai hujambo. tuongelee mengine lakini kwa nondoz itakuwa vigumu siwezi jua inawezekana unanizidi hapo sina uhakika. lakini ninachoamini tu ni kwamba kwa kiwango ulichonacho cha basi either tunalingana au ninakuzidi sababu mimi nimeshamaliza hatua zote. kwa hiyo ili tulingane basi nawe pia unatakiwa kuwa umemaliza hatua zote. shule yangu iko hivi. high school T.boys, BA economics UDSM, MSc Economics London School of Economics (LSE)UK, nikafanya masters nyingine tena MSc Econometrics University of Amsterdam (netherlands), baadada ya hapo nikapata fulbright scholarship nikafanya PhD ya Econometrics, UC Berkeley (University. of Carfornia Berkeley).
    nikafanya kama senior research officer, IMF DC kwa miaka 2. kabla ya kuamua kurudi home. kwa sasa niko 37 years old.
    kwa sasa naelekea geneva nilikopata ajira kama senior energy policy officer.
    kama una PhD na wewe basi tunalingana ngoma droo, ila kama umeishia masters basi rudi kidogo class ili tulingane.
    kuhusu ukubwa wa shule nadhani hata mimi shule nilizopita na hata courses nilizosoma ziko juu sana. unaijua econometrics wewe au unaisikia tu? unaijua LSE wewe, unaijua UC bekerley wewe??
    haya mtaalamu box jema. pia hongera kwa kulitumia box vizuri kulipa ada. mimi namshukuru mungu shule zangu zoote za nje nimesoma kwa scholarships nadhani suala la bahati.
    kuhusu maisha siwezi sema kama ninayo mazuri sana ila ninachojua ni kwamba shule imenisaidia napata pesa kwakweli. na nina uwezo wa kufanya na shirika lolote kubwa kwa vyeti nilivyonavyo. US sikupiga box sana sababu nilikuwa nikifanya kazi kama teaching assistant pale UC bekerley nilikuwa nikilipwa vizuri hata nikaweza kujenga nyumbani.
    Ahsante.
    sorry kwa comment yangu naona ilikuuzi sana.
    stay blessed
    cheers, bye!
    Asifiwe, DSM BONGOLANDMWAMBAMOTO

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 23, 2009

    hongera sana dokta asifiwe kama uliyosema niyakweli na sio IMAGINARY PhD ya hapa ktk blog. nakupongeza kwa kuwa wewe ni mtaalam mwenzangu ila field tofauti,mimi kuachilia PhD katika field yangu ambayo ni nyeti pia duniani,nina na MSc-economics,Mphilosophy,na fellowship ktk organisation tofauti zinazo husiana na field yangu. scholarship nilizipata nilipo anza kufanya masters na kuendelea,lakini sitasahau kuwa mwanzo ulikiwa mgumu na box ndilo lilinipa njia ya ku-hoock up hadi matunda ya shule yalipo anza kuzaliwa na kufungua milango ya schollarships zilizo nipeleka mbele zaidi. kwa hivyo hongera kwa kuwa na shule pia.
    nikifika tanzania nitakutafuta,au naweza pia kukutembelea geneva nikiwa ktk symposium tofautitofauti kama nikijaliwa.
    hamna ugonvi hapa wala nini.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 23, 2009

    kama una PhD basi hakuna anayemzidi mwenzake. hongera sana ulifanya la maana sana coz PhD ni shughuli pevu nadhani unafahamu hongera shule muhimu hasa wakati huu ambao kila mtu ana masters au anatafuta masters. zamani watu walidhani anaesoma PhD ni mwalimu wa chuo kikuu tu. siku hizi ni tofauti. mashirika makubwa yanataka PhD hasa upande wa research nk. haya nikutakie siku njema.

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 26, 2009

    OOoopss!!! PhD! PhD!!! Permanent head Damage. So what???? Msituboe hapa. Hata mimi nina Most Permanent head Damage MPhD

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...