wananchi wakiangalia mtu anayesadikiwa kuwa ni kibaka katika mtaro maoeneo ya tabata leo asubuhi. hali yake ilikuwa mbaya wakati akiondolewa eneo la tukio baada ya kupigwa sana
wakiangalia alikoangukia baada ya kipigo
akiopolewa kutoka mtaroni
mtuhumiwa akiwa hoi baada ya kipigo. picha zote 
na mdau mike mlingwa wa jarida la BabKubwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. hao vibaka si tishio ni njaa tu.adhabu za namna hii wanastaili majambazi ambao hutumia silaha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2009

    Kama ni kweli huo kijana ni mwizi, naamini wa bongo wamechoka kwa kero zao.

    Fisadiz watusumbue na hao wanyonge wenzetu tena? Kazi ipo.

    ReplyDelete
  3. tunapaswa tuelimishane jamani dhidi huu unjama.nakumbuka siku moja tulipiga mtu anayesadikiwa kibaka maeneo ya mwananyamala baada ya kuzimia swali likaja nani kaibiwa kila mtu alililudi njuma.sasa wakati umefika kwa kila binadam to reason b4 u act,hawa vibaka ni wakuchapa makofi na kukabidhi kituoni,wanaostili kuchomwa moto ni wafwatao;
    zombe
    wezi wa epa
    mafisadi
    majambazi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2009

    Mwisho hatutaki Ona mapicha kama haya michuzi yanahuzunisha tunajua uchumi mkali ila sio kutoana madamu live mbele za watoto aaaaaaah

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2009

    Huo ndio utamu wa kujing'ata baada ya kuiba....Haya majamaa sijui hata tuyachukulie vipi... Sio sheria kuyaua / kuchukua sheria mkononi kwa kuua mtu kwani Vyombo vya sheria vipo vinaweza kuhukumu ila wamezidi....Wao wakikuibia hawakuonei huruma halafu bora waibe tuu wakuache nao wanajichukulia sheria wanaweza kukuua na silaha zao walizo nazo...Mfano pia ukiwapeleka Polisi hawakai muda wanarudi uraiani na kuendeleza libeneke la kuiba wewe uliempeleka unaonekana zoba au adui...Wkt mwingine naona bora tuu wananchi wawaadhibu ila wawasiaue....Ingewezekana Tanzania tungekuwa mwizi akikamatwa anakatwa mkono wake mmoja au vidole nahisi wangejifunza.......Wanatutesa sana hasa madada tunarudishwa square one na hawa vibaka....Hakika ambaye hajaibiwa nao huwaonea huruma sana lakini kama ulishawahi kulizwa na kukabwa nao huwaonei huruma......BIG UP WALIOMPIGA

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 16, 2009

    Kila mmoja anaambiwa anakula urefu wa kamba yake lkn hawa wasingekuwaga wanaiba then wanampa kipigo mtu au wanamuua mtu ingekuwa peace. Tatizo la hawa wanaiba then wanaua au wanamjeruhi mtu. Bora matapeli coz hawamuumizi mtu. Tunajua life ngumu kila mmoja anatafuta kwa ujanja wake,Kila mmoja anaiba ofisini kwake hakuna mtu asiye mwizi, mafisadi pia ni mfano wa WEZI!!!. Hawa wangeanzisha mfumo wa kuiba bila kuua au kujeruhi vibaya raia wangewaachia..Watafute mbinu nyingine. Kibaka yeyote kama anasoma blog hii waambie wenzako waanzishe mfumo mwingine wa kuiba hivyo mtakwisha mikononi mwa raia. Tumechoka nasi

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 16, 2009

    Salaa lah ala Nabii
    People may think this is not serious but mark my words.
    This is symptomatic, its an expression of bottled up frustrations,A CAGED ANIMALS REACTION. Today its vibaka tomorrow its going to be another excuse.. remember Kikuyu against Majaluo etc
    See the last picture? the man has stones in his hands but look closely at the brutal strength of sinews of his hand telling you what is in his heart
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 16, 2009

    Eti Jamani michizi! Wanavyofanyiwa hawa vibaka ni haki au !? Kwanini selikariisituruhusu siwananchi hasa sisi wenye uchungu na wezi, tukawashughurikia hawa mafisadi PAPA NA NYANGUMI,kwasababa wao ndo wanasababisha hawa vijana waibe! Si ndawaliochukua mali za nchi yetu? Hizi Billioni 133 kama walau tungewapa haww vijana wanaozurula kama mkopo ingetosha wangapi ata kwakuwapa laki 300,000 kilakijana.

    Nawalaumu sana MAFISADI ila kiama kinakuja kwao, tukitoka kwa vibaka wadogo ni zamu yao nawao kuingia mtaloni

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 16, 2009

    Watanzania wenzangu tuache unafiki eti tuna amani na uoendo kwa nini tunajichukulia sheria mkononi, mbona wezi wakubwa kama wa EPA, Richmond nk, tunawapigia makofi na kuwapongeza na kuandamana na kuwapa misifa!! Jamani shime shime si ajabu alikwapua mkufu usiozidi tsh 10,000, tuache hizo, walau tuvilalamikie vyombo vya dola kama vinawaachia watu kama hao

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 16, 2009

    COME ON MR MICHUZI UNATUFANYA TUOGOPE KURUDI NYUMBANI HII TENA NINI JAMANI??
    WATANZANIA NINI BAYA YA KUUWANA KWA MKATE JAMANI EEH!!

    MMENIHARIBIA WEEKEND YANGU BYEE!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 16, 2009

    hii tabia ya kupiga wezi na kuwaponda ponda kama nyoka imechangia sana kupunguza watarii nchini tanzania sio safa kabisa,

    kunawazungu waliibiwa basi wana nchi walienda kuwapondaponda wale wezi kama nyoka wale wazungu wa watu wakaogopa na kuanza kulia tena wanaomba wawaruhusu waendezao wana nchi wanawaambia wakae mpaka polisi waje kwani wao ni mashahidi walilia sana

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 16, 2009

    uwongo umekuwa too much. CCM waache kutuhadithia tamthilia za kusadikika eti "Maisha bora kwa kila Kila Mtanzania inawezekana" hadithi za eti Wanyama wote walishiriki kuchimba kisima isipokuwa Sungura alikataa... hatutaki sisi sio watoto. pia fulana, vipeperushi, bendela, n.k. na kututhamini kila october baada ya miaka mitano, hatutaki. sijui huduma za afya, barabara, zimefanya hivi hatutaki. tumejenga barabara nyingi na shule hata wapinzani nao wanazitumia, hatutaki. sijui eti tangia uhuru sisiemu imeleta maendeleo makubwa, amani na mshikamano, hatutaki.... huo ujinga wooote wakae na familia zoa ndio wawe wanaueleza. ukiangalia hilo mob linalomchomoa msela tunduni lime-loose hope kutokana na ugumu maisha, ingekuwa kweli hizo tamthilia za CCM basi hao jamaa wasingekuwa na hasira kiasi hicho cha kujichukulia sheria mkononi. sio ombi ila ni wajibu wa serikali kurudisha JKT vijana wanohangaika mitaani huku hawaijui kesho wachukuliwe wakapate mafunzo waende huko wakazalishe then wapewe mitaji wayatumie mafunzo yao walikomboe taifa... hapo ndipo tutashinda na kupunguza hilo wimbi la vibaka... vilevile serikali iache uongo iboreshe huuduma vijijini ili kupunguzo ongezeko la wanaokimbilia mijini na wawe na mjadala wa kitaifa katika kutatua matatizo ya nchi yetu, sio wanakuja kichamachama kila kitu kichamachama. sijue eti mkiwakamata msichukue hatua mkononi muwapeleke polisi hilo si suluhisho ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.. Wadau mpo hapo?

    Lumbo
    Arusha

    ReplyDelete
  13. Yap! Hii ndo dawa! piga hao wezi na vibaka, tumewachoka!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 16, 2009

    Du! sidhani kama huu ni ubin-ada-m yaani sijui kuna haki za binadamu kweli hell no! juzi kati mwingine kaokolewa leo tena huyu..kwanini inatia uchungu mambo ya sheria mkononi mapaka lini?..lakini wezi/vibaka na nyie hamkomi tu?
    Mdau
    H-Town.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 16, 2009

    hawa jamaa kama watakuwa wanapata mkong'oto wa staili hii wanapokamatwa laivu wakiiba wataacha kunyemelea mali za watu na kupiga watu roba za mbao.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 16, 2009

    Haki za binadamu ziko wapi?
    Huyu mtu bado ni mtuhumiwa na anapigwa kiasi cha kufa, je ikija kubainika kwamba hakuiba waliompiga wataomba msaada?
    Mtuhumiwa anapelekwa kwenye vyombo vya sheria lakini haya yakubundana hata haijajulikana kosa labda huko huko TZ kwenu. nchi zinazojali haki za binadamu basi hata waliompiga kibaka wanachukuliwa hatua.

    ReplyDelete
  17. Wasomaji wa hii blog naomba nieleweshwe. Hivi kitendo cha kuwahukumu vibaka na kuwapiga, kuwachoma moto na kuwaua ni ustaarabu kweli? Haionyeshi kuwa na nyie mnaemtendea hivyo na nyie hamko tofauti na yeye, Kwamba nyie nyote ni vibaka ila tu yeye hakuwa mwangalifu ndiyo maana kakamatwa. Hivi unaielezaje tabia za watanzania wengi tena huko uswazi ambako mambo hayo ndiyo hutokea sana ikitokea ajali ya gari lazima watapora mali ya majeruhi. Utafiti nilioufanya unaonyesha kuwa mambo hayo yako huko uswazi kwenye maeneo ya manzese, tabata, ukonga, sinza , vingunguti na kunakofanaa na maeneo hayo. Kibaka akikamatwa Masaki sana sana atafungwa kamba au pingu na kupewa lift na victim wake hadi kituo cha polisi.

    Kama wewe siyo muuaji kwa nini uue? Ninachotaka kusema ni kuwa kibaka na nyie mnayempa kibano wote mnatakiwa mshtakiwe kwa sababu na nyie mnavunja sheria ya nchi. Two wrongs never make it right.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 16, 2009

    Michuzi acha kupoteza habari. Huyu ni menzi wa Liverpool alikuwa anataka kujiua tulikuwa tunamuokoa.

    Man U oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  19. EBWANA HIYO KALI Naitwa James Lubus wa Tumaini University Iringa kampasi nipo kwenye faculty of law kwahiyo na maoni yangu mimi yanahusiana na Position under the law. Kutoka na principles of nature justice audi alteram parte kuwa mtu yeyete yule haruhusiwi kuhukumiwa bila yeye mwenyewe kutoa mawazo juu ya kesi ilivyokuwa kujitetea. Hivi karibuni wananchi wengi sana wamekuwa wanachukuria sheria mkononi na hii ni ukiukaji wa haki za binadamu uliokithiri,. Kinachotakiwa ni kumchukua huyo jamma na kumpeleka kwenye vyom,bo vya sheria ambacho ni Mahakama hapo ndio atasikilizwa na yeye ataongea. Katika katiba hamna kifungu chochote kile kinachoonesha kuwa mtu akiiba basi apigwe mawe. Kifungu namba 13(1) cha katiba kinaonesha usawa mbele ya sheria.
    kwa maoni zaidi unaweza kuyapata katika wwwmwanasherialubus.blogspot.com

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 16, 2009

    Sad in deed.Tanzanians need to stop this.shame on us .usimuhukumu mwenzio.if vibaka wanapigwa.what about wazinzi,wabakaji,mafirauni the list goes on and on.so kama mnapiga vibaka anzeni kuwashughulikia wazinzi maana ukimwi unatumaliza

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 16, 2009

    khaa jamani huyu mwingine tena maskini,yaani wabongo mna roho ngumu ninyi hii picha ya mwisho inaonyesha mtu kafa lakini kuna mtu kashika jiwe,sasa sijui anataka kuuwa maiti hapo,mambo kama haya ndio yananifanya niendelee kubeba boksi licha ya kuwa nina phd,utu hamna bongo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 16, 2009

    Michuzi,
    These are disturbing pictures and indeed no one is supposed to cheer .
    On a peaceful country, which takes pride in rule of law, this is very disappointing indeed.
    Please, refrain from showing of these incidences (this is a second one in a week) without a kind of warning attached.
    I am sure you are aware that unlike ze utamu, we watch our blog ya jamii with our young families.
    Cheers
    John

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 16, 2009

    Watanzania tuwe macho kwani 'mob justice' yaweza kuwa 'mob injustice'. Watu hawa walishindwa nini kumkamata mtu huyo na kumpeleka mbele ya vyombo vya sheria wakiwa na ushahidi na akapata hukumu ipasayo. Angekuwa kaka yako, ungejisikiaje hata kama ni kibaka? Yaweza kuwa kasakiziwa au kama waitavyo waswahili, kakuniwa nazi, kachomekewa wizi :) Mlahabwa

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 16, 2009

    kwanini watanzania tunakuwa na unyama kiasi hiki?mambo ya kupigwa watu kiasi hiki tumeshasahau kuona kwa miaka mingi sasa,m/mungu subuhanahu wataala amesema mwizi akatwe mkono sisi hatufuati sheria na ndio maana nchi inazidi kunakamika kwa matatizo na maradhi.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 16, 2009

    Kweli hii niya watanzania kuokua na imani na mfumo wa wa sheria na haki. Wameamua kuchukua madaraka na sheria mikononi mwao na kumuadhibu huyu kijana bila utaratibu unaopaswa kufwatwa.Kuna crisis of confidence with au legal and enforcement system. Lakini bado hatua za naman hii hazileti haki wala kufwata sheria maana kwa fitna tu naweza kwa mfano nikamzomea michuzi mtaani "mwizi, mwizi, mwizi" na kuanza kumrushia mawe na wengine wakaniunga mkono kwa fimbo, ngumi, mateke na hata moto bila kujua ukweli wa jambo au tukio. Alafu kuna mafisadi ambao tuna taarifa ambazao zilizo rasmi zaidi, za kimaandishi, za uhakika zaidi, zenye msingi wa utafiti na uchunguzi wa kina, za Controller na Accountant General na hata Serious Fraud Office ya Uingereza lakini hakuna hata mtu anathubutu kusema mwizi mbali na kuokota hata kokoto na kumrushia fisadi. Kwa hiyo hapa anaadhibiwa mnyonge tu (iwe kweli kaiba au hajaiba) na mwenye nguvu haguswi hata kama ushahidi wa kiutafiti, kisomi, mzito na unaozidi kuongezeka upo!!!!!!!!!! Kwa hiyo naungana na mdau Anony May 16, 2009 8:58 PM anaesema "mob injustice". Zaidi ya hapo nauliza je kuongezeka kwa matukio kama haya siyo dalili tu ya wananchi kukosa imani na mfumo wa haki na sheria lakini vile vile kuendelea kumomonyoka kwa amani na utulivu nchini mwetu? Alafu hawa wote wanopiga mawe, fimbo, mateke na ngumi vibaka je wao kweli wote ni safi kabisa? Je kuna mazingira ambayo na wao, laiti wangebambwa, na mtu akapiga yowe la "mwizi" na wao wangeadhibiwa vivyo hivyo kama wao wanavyowaadhibu wengine? Je katika matukio kama haya kuna wangapi wanayatumia kama fursa ya kulipiza visasi au kukomoana kwa sababu tofauti kabisa na za tukio lenyewe? Sijui; lakini Mungu atunusuru na kutusamehe makosa yetu.Sidhani kama matukio kama haya ni dalili au ishara ya jamii inayoelekea kuzuri.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 16, 2009

    Annoy uliesema wakatwe mkono wewe ndo unajua,asipigwe wala kupelekwa polisi ni mkono mmoja tu anaachiwa inakuwa nembo ya vibaka.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 17, 2009

    Street Justice ndio hivyo?!!!!! Kama ni kibaka tu kipigo hicho sio chema. Majambazi wenye kutumia silaha na wanaishi kwenye majumba mazuri sana tu ndio wapigwe hivyo lakini kibaka anayetafuta kula mchana, that is too much. I am sorry

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 17, 2009

    Mmmh CCM wakiondoka madarakani wanaingia viongozi wengine ambao wanawambia wananchi wengine wawapige wengine manati. Zitto upo? Sawa mzee wako mdomo..!

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 17, 2009

    LUMBO WA ARUSHA UMENENA
    SERIKALI SERIKALI SERIKALI

    PAMOJA NA UONGOZI USIO NA MIPANGO ENDELEVU, PAMOJA NA WALE WOTE WANAOIBA MALI YA NCHI....NI WANAIBIA WANYONGE.


    MATOKEO YAKE...WEZI, VIBAKA, WANAOJISHUGHULISHA NA BIASHARA ZA NGONO WENGI WAO SIO KWAMBA WAMEPENDA KUFANYA HIVYO..WANAFIKA SEHEMU HAWANA JINSI...WANAKUWA WAMEKATA TAMAA

    SERIKALI INGEKUWA NA MIPANGO ENDELEVU YA KUWAINUA WANANCHI ILI WAWEZE KUJIKIMU, TOKA YULE ALIYE KIJIJINI KWA ALIYE MJINI...KWA IDADI YA HELA MLIZOIBA TOKA MIAKA 47 ILIYOPITA....HALI INAYOONEKANA SASA ISINGEKUWA KATIKA KIWANGO HICHO.

    HIVI VILIO VYA WANAOHANGAIKA, IKO SIKU VITAWAMALIZA WAZIMA WANAJIONA.

    HIYO PICHA HAIPENDEZI KABISA..INASIKITISHA.

    ReplyDelete
  30. HAPO KWENYE PICHA KUMEJAA MIJIZI MITUPU.NAOMBA TUACHE UJANJA WA MACHO KUONEKANA UNAGHALIMU MAISHA YA WATU.KUNA BAADHI YA WATU WAPENDA SIFA KUKIWA NA WATU WENGI WANAOMJUA NDIO ANAJIFANYA ACTIVE,NI VYEMA KUJUA KILICHOIBIWA KABLA UJAINUA MKONO WAKO KAMA NDO UNAHASIRA SANA NA VIBAKA,MARA NYINGINE MTU ANAITIWA MWIZI KUTOKANA NA SABABU NYINGINE NA KWA VILE AMECHOKA KIMAISHA BASI KILA MTU ANAAMINI.naomba mzushi michuzi unipostie maoni yangu

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 17, 2009

    Mi nazani watu walio nje na ambao hajaibiwa wasichangie hii mada.

    Hawa watu lazima tuwamalize, kwani wao wakitupa wanatumaliza. Umeona juzi Karikaoo walivyopiga na Polisi? Mi naimani, mmoja wao angefanya kosa raia wangemkamata, wangemmaliza.

    Au kwa mfano hao wanaua Albino, mbona wao wanajichukulia sheria MKONONi au mbona hawafuati haki za binadamu? au Mkuki kwa nguruwe, kwa kibaki ni MCHUNGU?

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 17, 2009

    Jamani! jamani!This brutal, Kwanza huyu anaonekana ni kijana mdogo sana. Ameiba kipi kikubwa kupigwa namna hii. Labda alikuwa na njaa, hajala siku kadha, alikuwa hana njia ila kuiba. Watu kupiga binadamu mwingine namna hii sio haki, Tumekuwa kama wanyama. kweli inasikitisha. Imeniharibia siku yangu nzima.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 18, 2009

    Hii Ilikuwa Ubungo karibu na Mabibo hostel na si Tabata mimi niliona. Ila huu ni unyama mkubwa. Jana kuna kijana kapigwa Shekilango kumbe sio mwizi. Kasingiziwa tuu.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 18, 2009

    Hii sheria ya jamii ni kali kuzidi ile ya dini.

    Kama mnataka kuuwa uweni mafisadi.

    ReplyDelete
  35. GodfatherMay 18, 2009

    Nimeibiwa sana Bongo. Dawa ya wezi vibaka, ni PIGA/UWA! Shauri zao! Tuwapunguzie kazi polisi. Hao vibaka warudi vijijini wakalime kama maisha ya mjini yamewashinda!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 18, 2009

    kila siku napinga sheria ya kufukuza watoto shule eti kwa sababu ya utundu au ukorofi.

    Wanaofukuzwa shule baadaye huwa wanawaibia wenye kubaki shule.

    Kwa nini tuchague nani awe mzuri nani mbaya mbeleni.

    Kufukuza shule ni adhabu kubwa saana kwa kosa la jeuri/kiburi/ukorofi na pia ni kupoteza nguvu kazi endelevu. Bora mjenge jela za watoto ambazo pia zina shule kama USA.

    Na nyinyi walimu kazi yenu ni kufundisha elimu siyo tabia, hiyo ni kazi ya wazazi na viongozi wa dini.

    mjeuri afukuzwa shule japo kafaulu mitihani, je aliyefeli mtihani mtamfanya nini?

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 20, 2009

    http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/8059298.stm Mimi nadhani jamii yetu inazidi kupotea na kukosa amani utulivu na nidhamu.Kama vyombo vyetu vya usalama vyenyewe vinaweza kuleta vurugu, kivunja sheria na kukosa nidhamu kama story iliyo kwenye link hapo juu noi chombo gani kitalinda usalama. Na hii si ripoti ya kwanza ya askari jeshi kupiga askari polisi. Aidha kuna kesi Arusha ya polisis kuua raia kwa kizingizio ya walikuwa majambazi, mbali ya kesi ya Zombe. Na raia wenyewe wanachukua sheria mkononi kama Michuzi alivyoytuonyesha huko tegeta na maeneo ya Drive-In (Ubalozi wa Marekani) hivi karibuni. Alafu kuna waancahri na wananihii huko musoma na kila kwemye uchaguzi mdogo kuna vurugu na watu kupigwa.Alafu tena waalimu walipiga mawe viongozi wao wa Chama cha Waaalimu mwaka jana, na wastaafu wa EAC vivyo hivyo, na Rais wetu msafara wake huko Mbeya mwaka jana yakawa hayo hayo. Mzee wetu Mwinyi tena, maskini, hivi karibuni yamemsibu....... Mbona vurugu kibao tena za aibu hata heshima na uvumilivu hakuna tena.Hivi serikali inayaonaje haya matukio na inafanya nini? Bado Tanzania kisiwa cha amani na utulivu? Jamani tusibweteke hakuna amani hakuna utulivu hakuna kuheshimu sheria. Serikali inafanya nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...