Houston wakiwa katika tizi
Bongo United wakiwa kambini kujifua
Kile kidumbwe dumbwe cha mpira wa miguu kati ya Bongo United fc(DC) na Houston Stars(Tx),wasi wasi na hofu kwa timu zote mbili wazidi kuongezeka.

Mpaka jana wachezaji watano wa Houston Stars wametinga Washington Dc,tayari kwa mpambano huo utakaochezwa kwenye viwanja 3928 Greencastle Rd,Fairland Md, leo Jumamosi.

Habari za uhakika toka kambi ya Houston ni kwamba kati ya hao wachezaji wa tano waliofika hapa jana, mmoja ni kiongozi kwenye kamati ya ufundi aliyeagizwa maalumu toka Bwagamoyo.

Msafara wa wachezaji wengine wa Houston Stars umeingia usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya kukodi, ikiwa na wachezaji ishirini, kocha, daktari, na viongozi wawili ambaye mmoja ameisha ingia Dc kwa matayarisho ya mwisho mwisho ya mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki Washington Metro Area na jirani zao bila kuwa sahau washabiki kutoka Houston.

Kwa habari tulizo dodosa kutoka Bongo United fc,wachezaji wote wapo fiti,tayari kwa mpambano hio jumamosi na wana ari kubwa ya ushindi

Kocha msaidizi na maalumu kwa mpambano huo wa kesho Yahaya Kheri amesema mechi itakua ngumu kwa sababu timu zote zinafahamiana kimchezo na zote zimefanya maandalizi ya mpambano huu wa kihistoria kwani ni mara ya kwanza kwa timu hizi kucheza kwenye ardhi ya Washington Metro Area.

Habari toka ndani Bongo United fc zinasema Yahaya Kheri amekabiziwa timu kwa mechi hii na Houston kwa sababu tu ni mtaamu wa ushindi kwani inasadikiwa timu inapokua chini yake ushindi ni lazima.

Hata hivyo uchunguzi wa ripota wa globu ya jamii umebaini kwamba mratibu mchezaji wa Bongo United, Luke, hatokuwepo uwanjani leo ila ataongoza jahazi kwa kutumia mawasiliano ya blackberry. Inasemekana kenda Atlanta kikazi na hatowahi mechi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Eti wameingia na ndege ya kukodi.Watu mna mikogo.Kazi zenyewe za $8 kwa saa afu mkodi ndege.Semeni mmepanda SouthWest nauli $5 pungufu unaongea

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2009

    jamani mbona hilo kabumbu msituni?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2009

    baada ya kazi ngumu ya box ni vizuri kufanya mazoezi kama wapiga box hawa wafanyavyo.
    natoa wito kwa wapiga box wenzangu tuwage tunafanya mazoezi. si kukalia kuosha wazee tu, kusafisha vyoo tuu halafu ukirudi apartment unakishia kupata coors au budright na kulala. mazoezi muhimu wapiga box wenzangu!!!
    BIG G
    Baltmore

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2009

    hamna chochote hapo. wote wachovu tu. wabongo kwa kujikung'utia maujiko tu hatujambo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...