http://news.bbc.co.uk/2/shared/spl/hi/pop_ups/08
/africa_kenyan_aristocrat_sentenced/html/2.stm
 
Kwa hii link wadau wataweza kusoma kuhusu maoni ya baadhi ya wakenya kuhusu mzungu aliyeuwa Mkenya kwa mara ya pili eti kwenye shamba lake toka enzi za ukoloni la eka 50,000 (huku wakenya wengine hawana ardhi).

 Eti wakenya wengine wanasema ni haki kwa jamaa kufungwa miezi 8 tu.Inaingia akilini? Alafu hawa jamaa wameshindwa kutatua tatizo la ardhi kwao ambako kuna wakoloni kama huyu Lord De La Mare na familia yake walogawiwa ardhi ya eka 50,000 ya wamasai na makabila mengine kiubabe tu wakati wa mkoloni na mpaka leo wanaimiliki. 

Sasa viongozi wa Kenya wanaogopa ufisadi na mafisadi wa ardhi huko kwao na sasa eti wananyemelea ardhi ya Tanzania- eti land sharing kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Walie tu hatutaki hiyo land sharing! Wagangamare namafisadi wao kama sisi tunavyogangamara na mafisadi mwetu. 

Lakini kuna kitu kimoja tunafanana nchi zote mbili zina viongozi ambao wanatetea mafisadi. Eti jaji anasema afungwe miezi 8 kwa kuua bila kukusudia (tena kwa mara ya pili katika kipindi kifupi tu, zaidi kidogo ya mwaka.Mara ya kwanza alisevu bila adhabu) wakati mwizi wa kuku anafungwa miaka 5!
Michuzi naomba uiweke hii tuijadili kwenye blog yetu. 
 
Ni mimi, 
Anonymous

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2009

    WATANIZETU WA JADI NI WATUMWA WA FIKIRA,MZUNGU KWAO NI MUNGU MTOTO,NA HII KESI IMESIBITISHA HILO,KUHUSU ARDHI SERIKARI ISIFANYE KOSA,ARDHI YA TANZANIA NI YA WATANZANIA ASILIA BILA KUBAGUA RANGI WALA DINI,NA WAKENYA NI VIBARAKA WANATUMIWA NA UK,WAWEKE MSUKUMO WA SWALA LA ARDHI KATIKA JUMUYA ILI WAZUNGU WAPATE MWANYA KUPATA ARDHI KWA MANUFAA YAO,KITU AMBACHO WALIJARIBU KWA MIAKA MINGI KWA USHUJAA NA UPENDO WA BABA WATAIFA AKUFANYA KOSA SASA KIJA JK MSIMSLALITI NYERERE KWA KUBADILI SHERIA YA ARDHI,IN FEATURE DAMU ITAMWAGIKA TU KWA VITA VYA UKOMBOZI WA ARDHI,ZUMA AMESHA TANGAZA KUIGAWA ARDHI KWA WANANCHI WAKE,KENYA NA UGANDA WANGOMBEA KICHUGUU CHA MIGINGO SEMBUSE WAKIPATA DABAGA NYEE WAHUNGILAGE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2009

    Kenya ni moja ya nchi ambazo wananchi wake wanashida sana.Watanzania na wakenya hatuko sawa hata siku moja kwani hilo nitalikataa kabisaa.Kidogo tuna weza fanana na watu toka mombasa lakini wajaluo na wakikuyu ni mbwa.Ila waliwahi tutoka na kurudi hiloliko wazi.
    Watanzania tutaendelea kuchekwa mpaka lini?Kwa swala lakudai kuwa kuwe na ujirani mwema wakati wenzetu wanaendelea kwa kupitia rasilimali zetu.
    Je serikari ya Tanzania inajiaandaaje na wasomi wanao rudi toka ulaya,ndipo hapo utagundua kuwa tutaendelea kuwa nyuma,Hata wasomi wa hapo nyumbani wanaangaliwa tu.Halafu anakuja mtukuwekeza na wafanyakazi wake toka kenya eti hawana vibali kwa sababu wanaongea kiswahili.nanikasema kiswahili kibovu ni viza ya kufanya kazi Tanzania???.Serikali Ya Tanzania na Uhamiaji yake wote ni mabwabwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2009

    si afadhali huyo kafungwa,mbona Bro Dito aliuwa na akawa anapeta uraiani

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2009

    Nimeona kwenye TV juzi inauma sana nasie tanzania tufufue hizi kesi kama zipo. Africa bwana mahakama ukiona hivyo washalipwa PESA KIBAO. Dawa Yao kuwachapa na kuchoma mali zao tushachoka.

    Tizameni hii documentary youtube. sijui kama kweli au si kweli. part 1 tizameni mpaka ya mwisho. bofya chini. Africa addio youtube.

    http://www.youtube.com/watch?v=r5G2NDnfjj0

    ReplyDelete
  5. PETER NALITOLELAMay 16, 2009

    MICHUZI NAWAKILISHA HIKI KIOJA...!

    WEWE MANDIKAJI WA HII MADA NAONA NI MBUMBUMBU KWANZA SEHEMU KUBWA KAMA UNGETAKA UPATE MAONI YETU UNGEPUNGUZA MANENO YA ETI... ETI NYINGI SASA INAONEKANA UNATU CONVINCE TUKUBALIANE NA MAWAZO YAKO YA KIBAGUZI. HIYO ARIDHI WAZUNGU WAMEIPATA KWA KUFUATA SHERIA ZA KENYA ZA KIBEPARI SASA MBONA KUNA WAKENYA WENGI TU UGHAIBUNI WANAOWN ARIDHI HUONGEI PUMBA ZAKO. UNAONEKANA UNAKELEKA NA RANGI NYEUPE SI AJABU HATA ALBINO KWAKO NI SUMU. NENDA KATOE UMANDE ACHANA NA UMBEYA USIYO NA FAIDA, WEWE UKIPEWA HELA UTAZIKATAA? MIMI NASIKITIKA SANA WATU WASIYO KWENDA KUPATA ELIMU LAKINI WANAPOTEZA MUDA MWINGI KUTOA MAONI YA UMBEYA UMBEYA KWA KUSISITIZA ETI WAZUNGU NI MAFISADI PUNGUZA HIZO ETI WEWE ELEZEA UMBEYA WAKO BILA KUTUPA HIZO ETI ACHA SISI WASOMI WA MUZUMBE CHUO KIKUU CHA MULOGOLO TUZICHAMBUE KWA KINA, UNAANDIKA PUMBA MPAKA UNASHINDWA KUMWEKEA JINA LAKO KAKA MICHUZI? AIBU TUPU.....ETI..ETI..ETI!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 16, 2009

    Peter Nalitolela you are so ignorant it is unbelievable.Hujui kwamba familia ya Lord Delamare ililmilikishwa ardhi ya wamasi huko kenya kutoka enzi za ukoloni na serikali eti huru ikaubali umilikishwaji huo kama masharti ya uhuru? Hujui kwamba serikali ya UK ilikuwa na sera ya makusudi ya kuwapatia ardhi mamwinyi na maafisa wake jeshi waliopigana katika vita ya kwanza na ya pili ya dunia wa kiingereza katika makoloni yake kama Zimbabwe na Kenya? You are unveliveably primitive my friend! How do you think the the Delamares and other families ended up with 50,000 acres my friend in Kenya and Zimbabwe? Hujui kuna wanaharakati wa Kimasai na Kikiuyu wanaodai hiyo ardhi mpaka leo. Eti wazungu walijipatia ardhi kwa misingi ya kisheria za kibepari! Sema wakubwa wa Kenya walizikubali hizo taratibu za umiliki ardhi wakati wa uhuru na wakaendelea kuzitumia kujinufaisha wenyewe kuzitumia taratibu hizo hizo. Walijumuika na ufisadi na wazungu.Pesa kidogo iliyotolewa na serikali ya UK kama sehemu ya makubaliano ya uhuru wa Kenya kununua ardhi kutoka kwa masetla ili kuwapa wakenya waliokosa ardhi wkjati wa uhuru ilitumika kikabila na serikali ya Kenyatta iliwajali zaidi wakikuyu na kunua ardhi hata iliyo maeneo ya wakalenjini kuwapa wakikuyu japokuwa ilikwapuliwa kwa wenyeji wa kikalenjini na masetla wa kiingereza. do you really consider yourself informed on this issue? Ha ha ha ha ha!!!!!!! My poor imbecile! Why are you exposing your ignorance so freely and so pretensiously? Nyamaza kama hujui au huelewi badala ya kusema wenzako hawajui.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 16, 2009

    Msomi wewe Peter Nalitolela? Wewe? Hujui hata basic facts za migogoro tunaiona leo Kenya. Unadhani Wakikuyu wanozozana na Wakalenjini katika maeneo ya ya Kikalenjini waliingiaje na kwa nini kuna ugomvi? Kwa kifupi ardhi iliyokwapuliwa na masetla wa kiingereza ilinunuliwa kutoka kwao kutumia hela iliyotolewa na serikali ya wingereza ili kuwapa ardhi wakenya aliokoseshwa ardhi na masetla.Kenyata akawapa kipa umbele nduguze wakikuyu na kuwapa ardhi mapaka maeneo ya wakalenjini,Maeneo ya ukikuyu wakubwa wakapata mapande makubwa makubwa tu. Na malodi wakubwa wa kizungu waliomilikishwa na wakoloni wakaachiwa tu waendelee.Chuki ya wakalaenjini na wakikuyu huko Kenya chimbuko lakr ni nini hasa unadhani? Wewe msomi wa Mzumbe wewe? Mbona unakidhalilisha na kukitukanisha chuo?
    Hoja ya msingi iliyoanzisha mjadala huu ni kwamba Kenya bdiyo champions wa land sharing katika East African Community wakati wao kwao wana ufisadi (wa wazungu na wakubwa wa kiafrika)mkubwa wa ardhi ambao ni sababu moja kuu ya chuki za kikabila na vurugu za kisiasa huko Kenya. Sasa badala ya kupambana na ufisadi huo kwao wanaangaza ardhi ya TZ eti kwa hoja ya sharing of means of productio katika community. Si wakiipata wataendeleza ufisadi huo huo au watataka kutatua tataizo ya waliolkosa ardhi kenya kwa kuwahamishia TZ? Wewe si msomi hata kidogo Nalitolela, labda fisadi wa Kikenya.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 17, 2009

    Ndiyooo! msomi wa muzumbe, CHOO kidogo cha Mulogolo, mpe panadoli zake huyoo mumbeya eti, eti, eti, Eti nini? unalazimisha kuungwa mguu hapa?
    at least leo musomi wa muzumbe Pumba zako zina mantiki! Umeonyesha kuwa wewe some times YES some times NO!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2009

    Wewe unayemwambia mwenzako ameongea pumba na umesoma chuo kikuu na yeye hajasoma, hutendi haki kabisaa, kwanza jambo ambalo unasema (anataka kukushauri umchukie mzungu) hizo ni fikra zako finyo, hakuna mtu anayeweza kumshauri mtu mzima na akili zake amchukie mzungu, muhindi, mwarabu, mjaluo au mtanzania, wewe unajishuku tu na kwakusema hilo naamini kabisa hujasoma mpaka chuo kikuu point blank...na hii ni blog ya jamii watu wooote wanaweza kuleta hoja na kuidiscuss watakavyo uwe msomi wa chuo kikuu, darasa la saba au form six, kwahiyo tulizo jazba na jaribu kuelewa hoja...Na hii hoja ni muhimu sana ktk jamii kuwa inakuwaje Ardhi wapewe wengine na kuna wazaliwa hawana hata kimfereji cha kufulia nguo??? Hii ndo point ya kudiscuss na sio mambo ya rangi, sura au tabak...thank you very much..Asante Michuzi kwa kutuwekea hoja nzuri....Tuzidi kupendana...... :-0

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 17, 2009

    jamani hili swala la huyu mzungu wa watu si jepesi hata kidogo. mzungu huyu amemeliki shamba hilo kwa zaidi ya miaka 50 kama ilivyoelezwa hapo juu. Mzungu huyu ni raia wa kenya hivyo upande wangu ninaona kuwa ana haki zote za kuwa na hiyo ardhi kama alifuata sheria za nchi. Kama huyu mzungu anamiliki hilo shamba au ardhi na kulifanyia kazi ambazo zinanufaisha nchi na raia wake kwanini asiendelee kulimiliki. Sometimes sisi waafrika huwa hatutaki kukubali hata tunapokosea "and its sad" baadhi ya mila zetu mara nyingi huwa zinazingatia vyitu visivyo na msingi "thats why we normally do'nt want to face the reality". Kuna mifano mingi sana barani Africa na hata hapa kwetu TZ. Miaka ya nyuma tulikuwa na ndugu wengi wa kizungu ambao walikuwa wanajishirikisha sana na kilimo cha large scale kama vile kule Arusha ,iringa ,Tanga nakungineko. Wazungu hao pamoja na uchache wao walikuwa wakilima mazao mengi sana kiasi cha kuweza kutosheleza mahitaji ya nchi na surplus kuuzwa ng'ambo na kutuingizia fedha nyingi sana za kigeni zaidi ya hapo kutoa ajili nyingi sana kwa ndugu wengi. Thats why miaka hiyo uchumi wa Tz ulikuwa karibu sawa na nchi kama Singapore na kadhalika ambazo sasa zimetuacha mbali sana. Miaka ya 60's Tanzania ilikuwa the 2nd or 3rd largest Exporter wa Vitunguu vilivyokuwa vikiingia au kupelekwa USA. Pia enzi hizo ninakumbuka nikiwa mtoto Kila siku Nduli airport iringa saa nne asubuhi kulikuwa na ndege( Airplane) iliyokuwa ikija kubeba maua na vegetables kupelewa Dar ili yapelekwe kwenye masoko ya ulaya. barabara za iringa ambazo hazina lami zilikuwa zikimwagiwa maji kila wiki kupunguza vumbi. Mabwana afya walikuwa wakipita kila nyumba kumwagia dawa za mbu kwenye makaro au septic tanks, ilikuwa marufuku kutupa taka nje , unakifanya hivyo unachukuliwa hatua inayostahili. Mara baada ya ndugu zetu wazugu kuanza kuondoka basi tukaanza kurudi ktk tabia zetu ambazo baadhi yake badala ya kujenga nchi zinabomoa nchi. Ndugu zetu Zimbabwe miaka ya nyuma walikuwa hawajui njaa kwani wakulima wa kizungu walikuwa wakitumia ardhi inavyotakiwa na kufanya wazalishe mazao mengi kupita kiasi. Mara baada ya ndugu zetu wa Zimbabwe kudai warudishiwe ardhi na hatimaye kurudishiwa Nchi ikaanza kukumbwa na balaa la njaa. Ka hiyo kutokana na hoja hizo mimi ninaona kuwa hakuna sababu ya kuwanyanganya hawa ndugu zetu wa kizungu ardhi especially kama matumizi ya ardhi hiyo/hizo yanafaidisha wananchi na serikali yake. We are all one people no matter our skin pigments. Kalenga Boy.

    ReplyDelete
  11. Mdau, UmanganiMay 17, 2009

    Akhaaa! Ubaguzi wenu, ukabila wenu na roho mbaya zenu huko huko!! Msituletee sisi! Yetu ya kuzibiti mafisadi papa na mafisadi nyanguma yanatushinda, ndo mtuletee na upuuzi wenu, tutaweza wapi?
    Baada ya hili mtatuletea ya museveni na kichuguu! Nyie gombaneni sisi tufaidi, maana mking'oa reli ya kwenda ug, watapitishia mizigo kwetu, watu wale bingo bongo!
    Bongo mswano sana!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 17, 2009

    Mheshimiwa anonymous May 17, 2009 7:33 AM. mengi usemayo inawezekana yana ukweli. Lakini naomba ujibu hoja:
    1. kina Delamare wamemiliki ardhi Kenya zaidi hata ya miaka 50 nchini Kenya.Ni miongoni mwa familia za kwanza za kisetla Kenya. Lakini ardhi ilikuwa na wenyewe kabla ya hapo na kama ilivyosemwa ilikuwa ikitumika na wamasai ambao hawakupata compensation wala hawakusema hawataki kuendelea kuimiliki kulisha ng'ombe wao.Ukaja mfumowa kikoloni uiyowapa free hold wazungu kadhaa na kwa kupokonya makibila mengi tu wakiwemo wasamburu na wakalenjini. hata kama mzungu ni very productive, je basi ana haki ya kujikwapulia tu ardhi? Kuna wakenya mpaka leo wanalilia ardhi hiyo. Akitokea jamaa very productive kuliko wewe basi achukue cha kwako au mkeo?
    2) Kama kuna maelewano na si ubabe katika kumiliki ardhi haina tabu, lakini basi tukae as equals tukubaliane. Siyo wewe kwa vile mbabe ukwapue na uweke mfumo wa kumiliki ardhi na unishinikize nikubali mfumo huo.Hili halina uzungu au unhindi au unini, ni swala la fairness.Ila kihistoria ndivyo wazungu walivyoingia Kenya na Zimbabwe na kwingineko- waliingia kibabe.
    3) Sawa we have a lot to learn about so many things including agriculture.Lakini yote haihalalishi ubabe.haihalalishi kupokonya ardhi ya wazalendo kuweka land tenurre system inayokufaisha wewe alafu kuijustify kwamaba anaeimiliki yulo productive.
    4)If we are all the same ni vema basi that we treat each other the same katika yote. isikumbukwe we are all the same wakati wa kutetea watu fulani, nyakati fulani tu.
    5) Alafu kama wakenya wenye tatizo la land deprivation na waliowamiliksha wachache wakubwa ardhi haiwezi kuwa solution kumezea mate ardhi ya Tanzania.Kwa nini umiliki mkubwa wa ardhi uendane na historia ya madaraka ya kisiasa- the biggest land owners in Kenya ni wale waliowahi kushika madarka na wenye political influence- kama kina Delamare au Lord Cholmondley, kina Kenyatta, kina Moi wnamilikishwa ardhi sawa na wilaya au zaidi.Siyo ufisadi huu. Alafu matatizo ya ardhi yakiwakumba wansema land sharing iwepo EAC ambako sasa wataendeleza ufisadi huo huo au kutatua taizo lao la kuwakosesha ardhi walio wengi huko Kenya kwa kutumia ardhi ya TZ.Tell me why should this rubish be right, why do you find it attractive? Mnaona matatizo yaliopo Kenya kiasi cha makan=bila kuuana na bado mnatetea utaratibu huu?
    5) Mengine ya bwana afya hayo na vumbi na nini wala hayahusiani na hoja ya hapa, japo kuwa ni kweli na yana umuhimu wake wa pekee.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 17, 2009

    Nataka kuuliza mtu wa rangi, kabila,dini hastahili kumiliki kitu kwa mujibu wa sheria za nchi? au kutolewa hukumu ?------------------------------------------------------Answer ?????

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 17, 2009

    WATANZANIA NI MAJITU MAPUMBAVU KUPITA KIASI.
    TANZANIA WAZALENDO HAWANA HAKI HATA KIDOGO WANAVUNJIWA MAJUMBA USIKU WA MANANE LEO MNACHEKA KENYA.

    AU MKOLONI MPAKA RANGI IWE NYEUPE ACHENI UPUMBAVU KINA MZEE MWINYI WANA MAHEKA YA ARDHI NA MZEE SUMAYA NA WENGINE NA WATANZANIA WALALA HOI MASIKINI HATA HATI MILIKI HADI LEO HAWANA.

    HII INANIKUMBUSHA HADITHI YA BIBI KIZEE KAJIFUNIKA MBELE NYUMA YUKO UCHI NDIO WATANZANIA MLIVYO.

    MWALIMU BABA WA TAIFA ALISEMA UKABURU HAUNA RANGI KUNA WEUSI MAKABURU TENA NI HATARI KULIKO HAO WEUPE MAANA RANGI YAO YA WEUSI NDIO WANAJIFICHA.

    CHUKULIA WATANZANIA MAISHA WANAYOISHI MASIKINI TAABANI WAKATI VIONGOZI WANAIBA MABILION YA PESA HALAFU MNAJIITA WATANZANIA KWA KIPENGELE CHA RANGI.

    CHANGAMKENI WATANZANIA NA MUWEZE KUTOFAUTISHA BAINA YA MCHANA NA USIKU.

    LEO KIBAKA WATANZANIA TENA KAIBA CHUNGWA ROHO INATOLEWA YOTE KUTOKANA NA SHERIA KUTOFANYA KAZI INAVYOSTAHILI BADO MNAJISIFU.

    ReplyDelete
  15. Mdau, umanganiMay 17, 2009

    We 1:59 ni mkenya ama? toa hoja au changia mada kwa ustaarabu, watanzania hatuna tabia ya kutukanana na kuwa na roho mbaya. Usituite wapumbavu tafadhali!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 17, 2009

    HIVI MNAJUWA KWAMBA ASILIMIA 60 YA ARDHI YA KENYA INAMILIKIWA NA FAMILIA AMBAZO ZIMEWAHI AU ZIPO SERIKALINI?

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 18, 2009

    Heee!!! huu ni unyonyaji na ubepari, utamilikaje ardhi yote kubwa hiyo kwa faida yako na manufaa yako binafsi, bila kujali wenzako watakaa wapi, kwa kuwa wewe umemiliki, na umeikalia kwa manufaa yako binafsi pekee yako, ndio, Raisi wa wa awamu ya kwanza, akaunda AZIMIO LA ARUSHA, ili kuleta mapinduzi ya serikali, kutoak kwenye umiliki wa serikali ya kikoloni na serikali ya kujitawala wenyewe, ili kila mtu afaidike na nchi yake pasipo ubepari, wala unyonyaji,

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 18, 2009

    Anon wa may 17-1:59, umeongea mambo ya maana kupita kiasi..YAANI NINGEKUONA NINGEKUKUMBATIA NA KUKUPA FREE LUNCH..KWELI WATANZANIA TUCHANGAMKE NA TUAMKE USINGIZINI TUMELALA KWA MUDA MREFU SANA SIJUI NI COMMA AU PARALYZE AU NI NINI J'MANI?????? MAFISADI WALIO IBA BILLIONS OF CASH HAWASUMBULIWI HUYU MZUNGU KWA KUWA RANGU YAKE NI NYEUPEEEE NDO TUNACHONGA MIDOMO KA NJIWA!! JAMANI UJAMAA HUFANYI KAZI, UZALENDO UMEDATA, NA UJUMUIA UMELALA KA MENDE....WAKE UP AND SMELL THE COFFEE TANZANIANS...WAKE UP!!!! TUWAADHIBU MAFISADI KTK JAMII THEN TUWAFUATE WAZUNGU LAKINI KABLA YA KUWAADHIBU WALIO IBA BILLIONS OF CASH, TUSIONGEE TURUDI KULALA USINGIZI MUNONO HIVYO HIVYOOOOOOO MPAKA MWISHO WA DUNIA...GOOD NIGHT TANZANIANS.. :-}

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 18, 2009

    i never understood the kenyans,never will and i dont want too either!!

    yani wananiacha hoi...wee hii ndo unaona kiroja?sasa mmeona ile ya kisiwa cha migori sijui,lile bunge la kenyans wavokuwa watukana (uganda) kwa tamshi la gwiji M7

    hahahahahhaaaaa..raha sana!!

    ReplyDelete
  20. mbona hivo ndugu zangu? hii ni blog ya kuelimisha jamii sio malumbano na matusi please! kama ulifika cuo kikuu au lah! its not our interest, toa maoni kama huna nyamaza, thats better. Osman

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 18, 2009

    Muhimu kabisa ubaguzi wa rang kusema au dini au ukabila usiathiri analysis. Muhimu vile vile tusiogope kusema kwa kuogopa tutasemwa ni wabaguzi.
    Ukweli huyu jamaa kauwa tena kwa mara ya pili kwa bunduki shambani kwake na kapewa jela miezi nane. Mwizi wa kuku anafungwa miaka 5.
    Hakuna hata anaesema anyang'anywe leseni ya kumiliki bunduki.
    Ukweli vile vile anamiliki ekari 50,000 zilizokwapuliwa kutoka kwa wamasai enzi ya mkoloni.
    Ukweli Kenya shabiki mkubwa wa land sharing katika EAC.
    Ukweli ardhi inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na cha kutish na watawala na wanawamilikisha ndugu zao kikabila katika maeneo ambayo kiasili ni ya makabila mengine (hili la kumilikisha nje la eneo la asili kikabila linatisha kwa sababu Kenya ina ukabila sana, ingekuwa haina ukabila isengetisha na isengekuwa chanzo cha vita na mauaji kama tulivyoona hivi karibuni).

    Swali sasa: ni salama kuwa na land sharing na nchi kama hiyo ambayo ina taka land sharing na nchi jirani huku matatizo yake ya land yatokanayo na ufisadi inayafumbia macho? si tutakuwa tunajiongezea matatizo zaidi tu, zaidi na tuliyo nayo?

    Hapa TZ kama kuna ufisadi wa aina yoyote hakuna sababu ya kumuonea mtu aibu awe mzungu, burushi, mhindi au muafrika mweusi na katika miaka ya karibuniye ujasiri umeonyeshawa mpaka ngazi ya bunge. Tuendelee na uzi huo huo tuanike ufisadi wa Kiwira Coal Mine, Dowans, Richmond, Meremeta EPA na kadhalika bila woga kama tulivyokwisha anza.

    Ni muhimu tuwe macho na wale ambao watasingizia eti wanaonewa kwa sababu eti wao wana asili ya kiasia au wao ni wamasai au wao dini fulani au kabila lipi au rangi nzuri au upuuzi mwingine, wakati facts ziko wazi kuhusu ufisadi wao.Tusizibwe mdomo hata siku moja na upuuzi wa aina hii.

    Hakika safari bado ni ndefu lakini mwanzo ni mzuri na hakuna muda wa kuvuta pumzi. Ifikapo uchaguzi jamani tusijali chama au rangi au dini ya mgombea, wala rupia tutakazo shawishiwa nazo; tujali kwamba je mtu tunaemchagua kweli anapinga rushwa na ufisadi na tukisema huyo anayachukia hayo kweli inaaminika na kuingia akilini kwamba ni kweli?

    Hakuna anaechonga eti kwa sabau ni mzungu. Lazima tuseme kwa vyovyote vile mzungu, burushi, mhindi ana mabati kichwani, anajua sana sindimba au kakaaje tuseme tu kwa ujasiri!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...