Makamu wa Rais  Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran Mhe. Parvis Davoodi wakipungia mikono wananchi walipowasili kwenye  viwanja vya Karimjee Dar leo. Makamu wa Rais wa Iran yupo Nchini kwa ziara ya siku mbili ya kiserikali.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh. Parvis Dawoodi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mh. Muhammad Seif Khatib mara baada ya kuwasili Dar Jumapili usiku
Makamu wa Rais   Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimtambulisha kwa Makamu wa kwanza wa  Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran Mhe. Parvis Davoodi , Mwenyekiti wa Chama cha TLP Agostin Mrema katika mapokezi ya Kiongozi  huyo  kwenye  viwanja vya  Karimjee Dar
JK akimkaribisha makamu wa kwanza wa Rais Jamhuri ya kiislam ya Iran Bw.Parviz Davoodi mara tu baada ya kuwasili ikulu jijini Dar kwa mazungumzo katika ziara yake nchini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    Mbona mheshimiwa mrema kama uso umebabuka!!au macho yangu jamani

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    mrema ngoma ngumu inabidi alegeze misimamo na nakujiletaleta kwa wazee wanchi otherwise atakufa akiwa mpinzani na njaa tupu. hiyo ndio bongo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2009

    kuna kitu nilisikia kuhusu mrema ngoja ntafute ukweli kwanza ntauleta siku moja,halafu ni kwa nini mrema kwenye issue kama hizi anakuwa na mkuu wa kaya mara nyingi sana akitambulishwa(nimeshuhudia matukio mengi sana ya aina hii)bado najiuliza pia kwa nini yeye tu
    katika kambi ya upinzani?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2009

    Hapo!

    Mkuu ataambiwa ".. Pamoja na mengine kuna moja la muhimu tumepata taarifa kwamba Tanzania imeanza kuiga sera za Apartheid. Kwamba kuna mbunge na mfanyabiashara maarufu ambaye ni raia wenu mwenye asili ya kwetu anabaguliwa, ananyanyaswa na kusingiziwa shutuma nzito nzito na mzawa wa hapa. Taarifa hizi zimetustua na kutusikitisha sana. Je mmechukua hatua gani?"

    Mkuu atajiumauma "..Ni kwamba mawaziri wangu Mama Sofia Simba na Mheshimiwa Mkuchika tayari wameshatoa rasmi msimamo wa serikali juu ya sakata hili. Vyombo vya dola navyo vimeshaingilia kati suala hili. Sasa hivi tunapozungumza Bwana Hosea na kikosi chake cha TAKUKURU na DPP wetu Bwana Feleshi wamo katika mchakato wa kulifikisha suala hili mahakamani..Therefore be rest assured that we have given this issue a serious consideration!.."

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...