Freddy Macha kafanya maonyesho na kuongoza semina mbalimbali za sanaa za maonyesho na fasihi miaka mingi. Hapa anaonekana akitongoa shairi lake maarufu linalokejeli urasimu katika tamasha la muziki na ushairi (“Soul to Soul”) mjini Copenhagen, Denmark, 1985. picha na mdau Jørn Stjerneklar.
Kitabu cha hadithi fupi fupi : “Mpe Maneno Yake” kilichochapishwa mwaka 2006 na E & D Limited Dar es Salaam kitakuwa moja ya mada husika za semina zake Freddy Macha hususan katika fani ya uandishi na maisha ughaibuni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2009

    Freddy Macha ni mfano wa kuigwa katika maendeleo ya "fani" ya wana-habari na wana-mziki kwa sisi watanzania.

    Shairi la mwaka 1985 mpaka hii leo lipo katika "kumbu kumbu" mbali mbali maeneo ya utamaduni Denmark.

    Kuna umuhimu mkubwa wa kuzindua "vita" ya kupigana na maelimisho ya usomaji na sanaa zingine za utamaduni zisimezwe na maendeleo ya kuiga nchi zilizoendelea ambazo zimefika ukutani na hazina mwelekeo wa uzinduzi wa "utamaduni" wao uliyopotea kabisa.

    Watanzania turudi katika misingi yetu ya utamaduni wa jadi na usomaji wa vitabu,habari za kila siku vijijini na miji mikubwa.

    mickey@mail-online.dk
    Denmark

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2009

    toka miaka yote iyo uko kwa watu??
    nini asa wee mpemba au!!

    ni ayo tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2009

    Kitabu cha Mpe maneno yake ni kipimo tosha cha kuwafahamu watanzania, ama wabongo, na nafikiri ni chaguo zuri sana kwa sisi sote ambao hatuna uwezo wa kuweka kumbukumbu za masaa matatu yaliyopita.
    naamini ni mfano mzuri kwa kila mtunzi, awe wa vitabu ama mashairi, kalamu na karatasi ndiyo silaha.
    lakini je, sisi watanzania ni wakweli kwa kiasi gani ili kuweza kuandika bila kutia porojo?
    nimesoma kitabu ni kizuri lakini kwa mara ya kwanza kiliunzwa kwa bei ya chini sana ili hali kina thamani kubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...