Balozi wetu Ujerumani Mh.AhmadaNgemera akiwa na wafanyabiashara waliohudhuria warsha iliyoandaliwa na chama cha urafiki wa ujerumani na bongo akiwaelekeza fursa kibao za uwekezaji na biashara za bongo
Balozi Ngemera akibadilishanamawazo na baadhi ya wafanyabiashara
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh Ahmada Ngemera amewahakikishia wafanyabiashara wa Ujerumani wanaotaka kuwekeza Tanzania, kuwa mazingira ya kuwekeza nchini humo ni mazuri na ya kuvutia.

Alisema hayo katika kongamano la uchumi mini ambalo liliandaliwa na chama cha urafiki wa watanzania na wajerumani na kuudhuriwa na wafanyabiashara na wawekezaji wa kijerumani kutoka katika jimbo la Munich ambalo ndiyo tajiri kabisa nchini Ujerumani.

Balozi Ngemera amesema pamoja na kuyumba kwa uchumi wa dunia, lakini bade uchumi na mazingira ya tanzania ni ya kuvutia kwa wawekezaji wa nie kuwekeza.
Aidha alisema serikali imedhamiria kwa dhati kupambana na rushwa ambayo ilianza kupigwa vita toka enzi zu mwalimu Nyerere.
Hata hivyo alikiri kuwa kasi ya kuchukua hatua si kubwa kama ilivyo katika nchi zu Ulaya, akitolea mfano wa kashfa ya rushwa iliyolikumba kampuni moja kubwa la magari la hapa Ujerumani, ambapo serikali ilichukua hatua zu haraka.
Lakini Balozi Ngemera amesema, serikali inajitahidi kuongeza kasi hiyo ya kupambana na ufisadi.
Pia alizungumzia suala la ardhi ambapo alisema ni suala nyeti lakini lisiwatishe wawekezaji kwani tanzania ina Sera mujarab katika suala zima la ardhi.
Hata hivyo alisema haiwezekani muwekezaji akapewa ardhi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula, lakini yeye akatumia kwa kilimo cha mazao mfano ya kutoa mafuta.

Akizungumzia juu ya mchango wa sekta ya wafanyabishara wadogowadogo hususan wanawake, Balozi Ngemera alisema wawekezaji katika eng hilo wanakaribishwa ambao watavisaidia vikundi via kinamama.
Wakati hub hub Balozi huyo wa Tanzania nchini Ujerumani ameanza utaratibu maalum wa kuwatembelea na kukutana nah watanzania wanaoishi katika majimbo ya hapa Ujerumani.

Ujerumani ni moja kati ya nchi kubwa Barani Ulaya ambapo imekuwa vigumu kwa watanzania kukusanyika sehemu moja kutoka shemu mbalimbali.
Watanzania kadhaa wametoa pongezi kwa hatua hiyo ya BALOZI Ngemera ya kuwa karibu na watanzania na kusema anatekeleza kivitendo tabia ya Rais Jakaya Kikwete ambaye anasifika kwa kuwa karibu na wananchi wa chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2009

    huyo mwenye liheleni nani tena au kazamia?
    halafu anaonekana kabisa anatumia sigara kubwa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2009

    Mh!! muandishi alikuwa anasinzia ama? mbona amekosea maneno mengi, jamani tuwe tunajaribu kurudia tunayoandika na kusahihisha makosa madogo tuliyofanya kabla ya kutuma ujumbe ama habari itakayosomwa na wengine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2009

    Naona mambo ya vipurikwenye sikio.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2009

    huyu balozi anaonekana ni mtu makini sana, na ni msikivu kwa watu na kuchambua mambo, yuko kama askari lakini anaonekana is nice guy!!

    keep it up mjumbe wa serikali.

    mdau canada.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2009

    ee jama ee kiereni na bendera ya bongo vinaenda???
    Mdau

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2009

    Mashalah, jamani kijana huyo mrefu mweupe ni nani, jamani kijana mzuri mbaka naumia moyo, hebu nipeni jina lake na anaishi ujerumani, naweza hata kumfuata ikiwezekana, jamani vijana kama hawa mbona ngumu kuwapata wako wapi jamani na wasaka .

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2009

    Maashallah my butt, Chagga looks

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2009

    huyo balozi alivyokuwa na sura nzito kama mimi mwekezaji siwezi wekeza najua nitazulumiwa tu .Mheshimiwa balozi tabasamu kidogo uvutie wawekezaji

    ReplyDelete
  9. Huyu Mshikaji wa nne kulia(picha ya kwanza) kama sijasoma naye Azania basi itakuwa Umbwe.Jina limenitoka.Anyway,Big up bro.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 18, 2009

    Hawa wanasiasa wanadanganya sana watu hivi kweli tanzania kuna mazingira mazuri kweli ya kuwekeza?? tanzania hamna utawala wa haki na sheria .Mnangaika tu safisheni kwanza nchi wawekezaji watakuja wenyewe sio kutafutwa nchi imejaa rushwa kama nini , hamna demokrasia .

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 18, 2009

    kwa yule ananniulizia mimi kijana mrefu nionekanae hapo kwenye picha napenda kumwambia nashukuru kwa kuvutiwa nami. niandie kwa email yangu tukae2009@hotmail.com. nitafurahi kusikia toka kwako.
    ahsante

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 19, 2009

    utawaweza vijana wa kibongo wakiwa nje ya TZ, wengine hata nywele wanasuka yaani wana kasumba na kuiga tamaduni zisizokubalika kwenye jamii yetu mpaka wanakera.
    Im not trying to be judgemental, lakini niambieni kweli mtu mwenye kihereni utamwamini hata kufanya nae biashara ya maana? to me anawakilisha wasanii, either musicians au wacheza sinema period!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 22, 2009

    HUYO NI BABA YAKO MWENYE HERENI,WACHAGA HAMVAI HERENI NINI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...