Hii imetokea leo asubuhi kwenye jengo linalojengwa hapa karibu na ofisi za UNICEF.waliopigwa short ni wawili ila mmoja hali yake ni mbaya. Picha siyo nzuri kwa vile zimepigwa kutoka juu kutumia simu ya mkononi.

kuna kijana mmoja ambaye jina lake halijapatikana amepigwa shoti ya umeme mnamo saa tatu kasoro dakika kenda. Watu kibao wamemzunguka bila ya kujalikama wanamnyima kuvuta hewa.Mara ikaja ambulance ya makontrakta kuja mchukua.
Latest modo ya ambyulensi (aina ya baluni mayai) ambayo baada ya kumbeba majeruhi hiyoo inageuza na kuwahi hospitali.
Mdau wa Dar


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. MUNGU MWEMA MWENYE UWEZAYE YOTE TUSAIDIE SISI WAAFRICA MPAKA LINI MAMBO HAYA NJAA,MAGONJWA,UFISADI,SHOTI ZA UMEME,NO AMBULANCE NK NI MATATIZO YA KAWAIDA KWENYE JAMII ZETU,TUSAIDIE MUNGU WASAIDIE NA HAO WALIOPIGWA SHOTI YA UMEME WAPONE WAWEZE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU NA KUWAPA UGALI WATOTO WAO,NINAOMBA HAYO KATIKA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU,AMEN

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2009

    michuzi,hicho kichwa cha habari'mdau ala shoti ya umeme' sio kizuru hapo kumbuka ni maisha ya binadamu yanayohusika

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2009

    MADE IN CHINA NDIO HIZO HATHARI ZAKE. MASHAKA JOHN HUKO WAPI, MWAGA NONDOZ HAPO. NAJUA UMEFURAHI HADI OFISINI KKWENU KARIAKOO. TETETETETETETETETETET

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2009

    SASA NDANI YA HIYO AMBULENSI YA BALUNI MAYAI WANAMPA DRIPU TOKA KWENYE REJETA YA HILO BALUNI? JAMANI HATA WAPALESTINA WANATUSHINDA WANAWEZA KUNUNUA AMBULENSI KIBAO! HUKU BADO HAWANA NCHI INAYOELEWEKA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2009

    HUO UMEME KATIKA ENEO AMBALO NDIYO KWANZA LINAANZA KUSAFISHWA KWA UJENZI, UMETOKA WAPI? AU KULIKUWA NA WIZI WA UMEME UKIFANYIKA? TANESCO WATOE MAELEZO KAMA WANATAARIFA HII.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2009

    kwa wale waliukuwepo ughaibuni hilo neno kenda ni tisa ni kiswahili fasaha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...