Mkuu Nanihii
 
Ninaomba msaada kwenye tutaz.  Jana tulitembelewa hapa UA na Professor Bill Rabel wa Harvard Business School, ikawa na mimi nimepata nafasi ya kupresent makaratasi yangu ya research.

 Wakati wa break huyo Professor akanifuata tukaanza kupiga story, jamaa akaniomba nimtafutie Wanafunzi wake wa Kitanzania aliyowafundisha wakati anaanza kazi Mwaka 1967 akiwa Syracuse University, Jamaa bado anawakumbuka tena kwa majina, Ahmed Jumbe na Geofrey Mwoga. 

Kama kuna mtu anawafahamu hawa jamaa ninaomba awasiliane na mimi kupitia email yangu ili niwaunganishe na huyo Professor. Ameniachia mawasiliano yake, na pia tutakutana naye Yale University June 23rd.
Yeyote mwenye mawasiliano na hawa jamaa aniandikie email kupitia hii email hapa chini.
wpkuja@cba.ua.edu
Aksante kaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2009

    Huyu Ahmed Jumbe si ndiye yule mume wa Wema Sepetu. Mie sikujua kasoma Havard... kwikwikwi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2009

    Ustake ncheke, hahahahaha.

    I am sure utawapata tuu, blogu ya jamii hii bwana.

    Ila what is UA? University of atlanta ama?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2009

    Utawapata tu kwani swala la mawasiliano kwa sasa nje ya tanzania ni nafuu kuliko ndani ya Tanzania.Sijui nchi yetu anjiandaa vipi kutupoke ndani ya hii miaka mitatu ijayo wengi tunarudi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2009

    Majina kama hayo hapa kwetu unaweza kuwakuta wengi wakiwa na jina hilo hilo moja linalofanana.Lakini iwapo huyo Ahmed Jumbe ni mtu aliyesomea mambo ya Management Sciences na iwapo kipindi fulani huko nyuma aliwahi kufanya kazi jeshini kisha akastaafu na kufanya shughuli zake binafsi basi yupo mmoja niliyemfahamu ambaye kwa hivi sasa ni marehemu,na alipatwa na mauti mwezi Desemba 2008!Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi.Alifariki ghafla tu kwa ugonjwa wa moyo.Iwapo ndiyo huyo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2009

    haki ya mungu,wewe mtoa maoni wa kwanza u really make my day
    mbavu kidogo zinichomoke!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2009

    UA ni University of Alabama! Dogo hongera kwa kusoma shule nzuri.

    Unajua wabongo wengi huishia vishule vidogo vidogo visivyotambulika wakija huku ughaibuni. Na huwa wanalipa pesa sawa na hizi state university.So huwa najiuliza kwa nini wasingesoma kwenye shule nzuri?

    Eniwei, quality ya degree inatokana na shule inayotoa. Wabongo wengi utakuta wanasoma shule ndogo ndogo wakimaliza shule hata kuandika one sentence in english wanashindwa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 15, 2009

    Mhh na wee nae kwa kujifagilia eti nikiwa napresent research yangu....hakukuwa na ulazima tujue ulipresent mshamba wewe

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 15, 2009

    Sasa jamani wewe Anony wa 1:19 kuna tatizo gani mtu kueleza kwamba alikuwa anafanya presentation...kwani kama ni ujiko uko kwenye paper aliyoandika au kwenye presentation? Tuache ulimbukeni!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 15, 2009

    ni mhaya huyu!!

    hahahahaaaaa
    heeeee

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 15, 2009

    Kwanza nimjibu huyo ambaye hajui kwa nini wabongo wanasoma vyuo vidogo.
    1. Vyuo vikuwa huwa havina flexible schedule kwa hiyo kama wewe huna ada utalipaje hiyo ada? Vyuo vidogo unaweza kufanya kazi full time na shule full time.

    2. Vyuo vikubwa ni lazima usome zaidi ya miaka 4 wakati vyuo vidogo inategemea wewe mwenyewe.


    Nadhani hili ni swala la msingi kwa wale ambao wanataka kusoma US. Wengi huwa wanakuja kwenye vyuo vikubwa matokea yake hawamalizi shule kwa kushindwa kulipa ada na kuishia kubeba mabox.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 15, 2009

    huyu jamaa lazima atakuwa anatokea bukoba i mean.. ni muhaya kwa kabila.. sasa kulikuwa na ulazima gani wa kutuelezea habari yako kuwa ulikuwa unapresent research.. unakutana na prof kutoka Havard... unaongea naye.. kisha ndio inakuja sababu ya kuomba msaada... then hausishii hapo..unakuja na kusema utakutana nae.. Yale University.. siku si nyingi... then... tunasububiri tu utupe ratiba baada ya kukutana Yale Univer itakuwa MIT kabla ya kumalizia Princeton kama sio UCLA ha ha awabongo bwana..

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 15, 2009

    KAKA MICHU NAOMBA HUYO MTOA MAONI WA KWANZA ASHIRIKIANE NA DOGO WA USWAZI KUTUBURUDISHA.YANI KANIVUNJA MBAVU KWELI WE ACHA BIG UP KIJANA

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 15, 2009

    Ndiyo maana huwa nasema elimu ya Tanzania ni bora kuliko Marekani yaani huyu yuko kwenye chuo kikubwa na bado anaandika utumbo kama mwanakijiji.
    Hivi ndiyo ulivyotakiwa kuandika.

    "Professor Bill Rabel wa Harvard Business School anawatafute Ahmed Jumbe na Geofrey Mwoga, wanafunzi aliyowafundisha Syracuse University mwaka 1967. Yeyote aliye na taarifa ya ndugu hawa, tafadhali niandikie mimi kwa kutumia email hii wpkuja@cba.ua.edu au wanaweza kuwasiliana na Professor Rabel mojakwa moja katika email hii xxxxx@xxx.xx. Ahsante"

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 15, 2009

    Sikujua kwamba wahaya ni bado wasomi namna hii, ila kijana alikuwa anataka kuelza sababu ya yeye kukutana na mtu huyo, halafu amuwezi kushangaa huyo prof. alivyofurahi kukutana na mtu toka Tanzania na kutaka kujua hali za wanafunzi wake miaka yote hiyo iliyopita na vile vile siku hizi kuna kitu kinaitwa reunion sioni sababu za watu kukashifu mambo yote hayo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 15, 2009

    wewe anonymous wa 4:48 nimekukubali. jinsi ulivyomrekebisha na kupendekeza ni jinsi gani tangazo lake lilitakiwa liwe kwa kwakweli nimekukubali.halafu ukamalizia na ahsante. yaani nimecheka mpaka mbavu zinaniuma hapa. uko juu mwana!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 15, 2009

    hiii bhaghosha sikujuaga kama hili libulogu ni litamu kiasi hiki. hii ng'wanawane michuzi ninakupaga bigiapu

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 15, 2009

    reunion iko siko zote sema wewe ndio umeijua siku izi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 15, 2009

    ehehe big up wahaya, yaani kila msomi hapa mhaya kazi mnayo kweli kweli. sasa watu uwazi umewashinda nini? ndiyo maana tunauana na kuambukizana virusi kila kukucha sababu uwazi umetushinda, sa ye kusema alichokuwa akikifanya imewaumiza wapi? wabongo bwana, wakati ukikutana na mzungu ataanza kukuhadithia alivyokula na alivyolala mtachekelea mlivyokuwepo wajinga nyoo, big up wewe uliyeandika hivyo ndivyo unavyositahili kuandika, sisi tungejuaje huyo bil mmekutana wapi, je kama anadanganya?? wabongo elimikeni hizi ni zama za uwazi na ukweli. koku

    ReplyDelete
  19. Wabongo nongwa imezidi!.
    Kwa wewe uliesema ukisoma shule kubwa ndio education yako bora. FYI, Knowledge ni jinsi unavyoitumia na kuapply and it allll depends on the person, sio wapi umesoma. Na kuandika sentensi ya kiingereza haitegemei umesoma chuo kikubwa au kidogo!!!!!

    ReplyDelete
  20. Al MusomaMay 16, 2009

    We anonymous poster wa 3:53PM usimzulie mtu mambo. Moja, hawezi kuwa Mhaya kwa sababu hakuna Wahaya wanaume na pili kasema anakutana naye tena June 23 Yale University ili kama una taarifa umpe haraka kabla ya hapo...

    ReplyDelete
  21. Lugakingira RweyongezaMay 16, 2009

    Hivi UA ni University of America,campus ya Egypt au University of Alabama,University of Arizona,University of Arkansas,University of Alaska,University of Auckland,University of Alberta,University of Aberdeen,University of Adelaide? Mimi pia ni MUHAYA; hivyo nataka ku-kurepresent research yangu hapa Stanford University,California.
    Lugakingira Rweyongeza,PhD Candidate

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 16, 2009

    Mbona Alabama ni mashambani sana? Yaani Alabama ni sawa na Kigoma ya bongo.

    Noma kwelikweli.

    Halafu wala sio chuo bab kubwa. Kipo kwenye the top 20,000

    Ha ha haaaa

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 16, 2009

    Wewe ananymous wa May 15th 4.48pm usiwe na njia moja ya uelewa wa jambo. Hili Tangazo linaweza kuandikwa na walimbukeni kama wewe kwa njia nyingi zaidi ya mia moja. Huyu jamaa kuandika kwa kifupi kukutana na huyo Prof inajibu maswali ambayo watu wangeuliza wamekutana wapi na wakifanya nini. Haya hayakuwa mashindano ya kuandika insha hakukuwa. Mnapoteza muda kuchambua swala dogo ambalo halina maana yoyote. kwa sababu za Privacy anakuwa kama bridge ili kama kutakuwepo na wasiowangwana wasiweze kutumia fursa hiyo kutoa upupu wao.
    Basi bwana umesema na wewe umesikika kwenye Blog, lakini mimi nimeona huyu jamaa kaandika ujumbe mfupi wa Kingwana sana.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 16, 2009

    Mjomba kama kweli sio Muhaya, basi lazima awe MUHA!wa Ujiji.Maana huko ndio machimbuko ya malimbukeni.

    ReplyDelete
  25. Mie naona kama hakuna mtu anaye wafahamu hao jamaa tunyamaze make Wabongo tumeziki kuwa -ve.
    Huyo dogo tulisoma naye Minaki, dogo alikuwa mtu simple sana, sio mtu wa kupenda makuu. Halafu pia alikuwa smart sana. Ila kwa sababu Wabongo tumebarikiwa kwa kusema na kuuana ndo maana tunaongea sana.Kama unataka kujua UA ni ipi kati ya utumbo huo hapo juu ingia kwenye email address aliyokupa www.cba.ua.edu ili upate tofauti unayotaka. Ninaomba tu atumegee kipande cha research yake kwenye Blog ya Jamii kidogo tu. Michuzi mwambie dogo atupatie angalau kipande kidogo cha research kwenye Blog ili mijitu mingine ifunge Midomo yao.
    Jay, Toronto

    ReplyDelete
  26. Badala ya kumsaidia kwa kumpa taarifa wengine mumeona mumshambulie huyu Kuja.

    Huwezi kuzuka tu na kusema fulani na fulani ni 'wanted', inabidi utoe maelezo kidogo hasa ukizingatia kwamba yeye anawatafuta wahusika kwa niaba ya mtu mwingine.

    Bila ya shaka wapo wanaomtania tu and some humour is understandable lakini kuna na wale waliodhamiria hasa kumkejeli bila ya msingi wowote, hawa wanasikitisha.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 16, 2009

    Inasikitisha sana ukiona mwanafunzi wa chuo tena wa level yako alafu hawezi ku-communicate to the public. Ukweli ni kwamba umechemka we kaka wa UA.Ujumbe wangu kwako na kwa wanaokufagilia, LEARN TO COMMUNICATE TO THE PUBLIC your notice is full of non-sense.Tumia elimu yako kijana jifunze kutoa public notice bila kuweka all the stories around you. Sasa shule yako inakusaidia nini?? bado unafanana na mtoto wa primary!

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 16, 2009

    Swali kwa mdau wa UK May 16, 2009 6:23 AM. ujumbe mfupi wa Kingwana sana ndiyo nini? Halafu wewe unamwambia mwenzako limbukeni nadhani wewe ndiye limbukeni.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 16, 2009

    ...na wewe Lugakingira Rweyongeza,PhD Candidate
    Siyo "ku-kurepresent research" ungeandika "ku-present research".. kwa manufaa ya wengi humu kuna tofauti kubwa kati ya represent na present unakuwa kama Mwanakijiji.

    Kifimbo Cheza

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 16, 2009

    Jay,
    "ingia kwenye email address aliyokupa www.cba.ua.edu". www.cba.ua.edu siyo email address. Yeye ametuka email address na wewe unatakiwa utueleze hiyo www.cba.ua.edu ni nini.

    Kifimbo Cheza

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 16, 2009

    una-present research? research ya u-ngwini nayo research.halafu wabeba box mnasoma vikozi vya ajabuajabu mnaanza kutamba mmesoma.mwenye Ph.D ya sayansi (maths,engineeering,computer science etc) yeye asemeje? kumbukeni hata maprofesa wanatofautiana, prof. kwenye fani ya sayansi huwezi kumlinganisha na prof. wa performing arts.washamba wa Bukoba msisumbue watu.Nshomile kwa kujitangaza hata la maana hakuna!

    ReplyDelete
  32. Fellow Bloggers

    With Great respect, I acknowledge your criticisms. I salute your autonomous views and proof reading elucidations. But,how can imperfect man make anything perfect. No matter how deep one is educated, learning from each other is infinite. I was enormously aware of the people I was facing and it comes precisely to my expectations.

    I sincerely appreciate the rejoinder dispatched by right handed ladies and gentlemen across the planet. Through your emails I have helped the Harvard Elite to locate two of his best students from Africa who he calls African cream of the crop of the 19th Century.

    I would like to express my compassionate condolence to the family and survivors of late Ahmed Jumbe. Prof Rabel and I have received this horrific news with great sadness. May the Lord lend the survivors with new heart to overcome the grief.

    Fellow bloggers, I find it hard to answer some of your queries, why all these sicknesses, frustrations and personal attacks from people with great love and unity like us, Tanzanians. I have been dubbed all kinds of names, from Bukoba, Kigoma and everywhere else in the country. But with all these negativities, my feelings are intact because I was born in Tanzania, I could be either tribe, and proud of who I am, but not even close to suggestions vomited above. A true Tanzanian is identified by the colors of our “national flag” not from the tribe he/she comes from. One simple case I would like to articulate to my fellow citizens, lift your hearts and start thinking positively, these brainless counter riposte will never shove us to the Promised Land. They are impediments to solutions of divine intervention. We need clear-minded younger generation with self-esteem to lead the nation forward as opposed to these kitchen sink attitudes.

    Thanks – Lets continue blogging
    Kuja

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 17, 2009

    wape wape ee vidonge vyao, wakitema wakimeza ni shauri yao.
    English hiyo mwanangu ka ya Mashaka. Hivi nyie nlishoma shule moja au. Kweli wengine wamezidi utumbo humu ndani, wape vidonge vyao kaka.
    List inaongezeka, Mashaka Dr Shayo na Kuja tunawaunganisha pamoja watrudi bongo watuokoe na mafisadi.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 17, 2009

    I second you 4:48 wow!

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 17, 2009

    university of alabama ni chuo kikubwa? huyo mtu anajiandikia tu hajui anachosema ingekua Tuskegee University ningekusikiliza nani wabongo wengi tu wamesoma tuskegee

    kwanza wewe umesoma wapi? unayo hata AA kweli?

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 17, 2009

    Watu muache ukabila wenye chuki binafsi. Watu muwe mnajibu kutokana na kitu ulichoulizwa. Watanzania mna mambo ya ajabu sana. Mtu akijitambulisha basi ni muhaya. Kuna watanzania wana ukabila kama Wakenya. Watu wengine kujifanya mnajua mamuma msioyajua. Mtu mmoja akitaja mhaya, basi mnakuwa bendera fuata upepo. Kama huna maoni kuchangia kaa kimya. Halafu wachaga kujifanya mnajua sana. Acheni kuchi kwa wahaya. Na wanachukia wahaya ni wanawake ambao waliolewa na wahaya, baada ya kuachika kwa wanaume wao kutokana na tabia mbaya zenu. Basi mkawaona wanaume wa ki-haya hatutaki kuwasikia kwa sababu ya tamaa zenu za kupenda hela. Nakaa na wanawake wakichaga tabia mbaya kama konokono. Wanapenda kukaa na ndugu wa wanamke. Lakini kwa mwanamme hawapendi kabisa. Kwenda huko wanawake wa kichaga hakuna lolote roho mbaya na uchoyo. Wanawake wa kichaga wanapenda kumbana wanamme kwa mali ambayo amemkuta nayo. Wako kama wamarekani weusi. Kila mtu anajua tabia za wanawake wakichaka. Sasa wewe kama uliolewa na mme wa kihaya ukashindwa jinsi ya kumbana, ndo maana una chuki. Na muache chuki na ukabila. Nyerere alipinga sana ukabila.

    ReplyDelete
  37. Good for you kuja WP!These people need to grow up and stop being nasty,its bad and it doesn't help anybody!Great response.

    ReplyDelete
  38. Rugaimukamu Ishengoma RwegoshoraMay 18, 2009

    Aisee Mzee Lugakingira, nimefurahi sana ulipofikia hapo.Pigana sana kwenye level yako.Hiyo shule ya California niliipenda sana. Nami niko hapo Massachusetts Institute of Technology(MIT),nikifanya PhD yangu ya Computer Engineering.On my vacation in December,I will pay a visit to Stanford University.Labda naweza kupata faculty position baada ya shule yangu.I will probably see you.Kuna kijana rafiki yangu hapo,anaitwa Rwebangira Kaishozi anafanya PhD ya Computer Information Systems.Ukimuona,msalimie sana.
    Rugaimukamu Ishengoma Rwegoshora

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 18, 2009

    Ukilinganisha Tuskegee na University of Alabama ni sawa na kulinganisha Mwananyamala na Muhimbili. Zote ni hosipitali lakini inapokuja kwenye kiwango cha wagonjwa watakaotibiwa an vifaa vya kuwatibu, tunaongea lugha nyingine.....endelea kutafuta shule nyingine ulinganishe
    lakini sio Tuskegee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...