Mkuu Nanihii
Ninaomba msaada kwenye tutaz. Jana tulitembelewa hapa UA na Professor Bill Rabel wa Harvard Business School, ikawa na mimi nimepata nafasi ya kupresent makaratasi yangu ya research.
Wakati wa break huyo Professor akanifuata tukaanza kupiga story, jamaa akaniomba nimtafutie Wanafunzi wake wa Kitanzania aliyowafundisha wakati anaanza kazi Mwaka 1967 akiwa Syracuse University, Jamaa bado anawakumbuka tena kwa majina, Ahmed Jumbe na Geofrey Mwoga.
Kama kuna mtu anawafahamu hawa jamaa ninaomba awasiliane na mimi kupitia email yangu ili niwaunganishe na huyo Professor. Ameniachia mawasiliano yake, na pia tutakutana naye Yale University June 23rd.
Yeyote mwenye mawasiliano na hawa jamaa aniandikie email kupitia hii email hapa chini.
wpkuja@cba.ua.edu
Aksante kaka
Huyu Ahmed Jumbe si ndiye yule mume wa Wema Sepetu. Mie sikujua kasoma Havard... kwikwikwi!
ReplyDeleteUstake ncheke, hahahahaha.
ReplyDeleteI am sure utawapata tuu, blogu ya jamii hii bwana.
Ila what is UA? University of atlanta ama?
Utawapata tu kwani swala la mawasiliano kwa sasa nje ya tanzania ni nafuu kuliko ndani ya Tanzania.Sijui nchi yetu anjiandaa vipi kutupoke ndani ya hii miaka mitatu ijayo wengi tunarudi.
ReplyDeleteMajina kama hayo hapa kwetu unaweza kuwakuta wengi wakiwa na jina hilo hilo moja linalofanana.Lakini iwapo huyo Ahmed Jumbe ni mtu aliyesomea mambo ya Management Sciences na iwapo kipindi fulani huko nyuma aliwahi kufanya kazi jeshini kisha akastaafu na kufanya shughuli zake binafsi basi yupo mmoja niliyemfahamu ambaye kwa hivi sasa ni marehemu,na alipatwa na mauti mwezi Desemba 2008!Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi.Alifariki ghafla tu kwa ugonjwa wa moyo.Iwapo ndiyo huyo!
ReplyDeletehaki ya mungu,wewe mtoa maoni wa kwanza u really make my day
ReplyDeletembavu kidogo zinichomoke!!!!!!!!!!!!!
UA ni University of Alabama! Dogo hongera kwa kusoma shule nzuri.
ReplyDeleteUnajua wabongo wengi huishia vishule vidogo vidogo visivyotambulika wakija huku ughaibuni. Na huwa wanalipa pesa sawa na hizi state university.So huwa najiuliza kwa nini wasingesoma kwenye shule nzuri?
Eniwei, quality ya degree inatokana na shule inayotoa. Wabongo wengi utakuta wanasoma shule ndogo ndogo wakimaliza shule hata kuandika one sentence in english wanashindwa.
Mhh na wee nae kwa kujifagilia eti nikiwa napresent research yangu....hakukuwa na ulazima tujue ulipresent mshamba wewe
ReplyDeleteSasa jamani wewe Anony wa 1:19 kuna tatizo gani mtu kueleza kwamba alikuwa anafanya presentation...kwani kama ni ujiko uko kwenye paper aliyoandika au kwenye presentation? Tuache ulimbukeni!!
ReplyDeleteni mhaya huyu!!
ReplyDeletehahahahaaaaa
heeeee
Kwanza nimjibu huyo ambaye hajui kwa nini wabongo wanasoma vyuo vidogo.
ReplyDelete1. Vyuo vikuwa huwa havina flexible schedule kwa hiyo kama wewe huna ada utalipaje hiyo ada? Vyuo vidogo unaweza kufanya kazi full time na shule full time.
2. Vyuo vikubwa ni lazima usome zaidi ya miaka 4 wakati vyuo vidogo inategemea wewe mwenyewe.
Nadhani hili ni swala la msingi kwa wale ambao wanataka kusoma US. Wengi huwa wanakuja kwenye vyuo vikubwa matokea yake hawamalizi shule kwa kushindwa kulipa ada na kuishia kubeba mabox.
huyu jamaa lazima atakuwa anatokea bukoba i mean.. ni muhaya kwa kabila.. sasa kulikuwa na ulazima gani wa kutuelezea habari yako kuwa ulikuwa unapresent research.. unakutana na prof kutoka Havard... unaongea naye.. kisha ndio inakuja sababu ya kuomba msaada... then hausishii hapo..unakuja na kusema utakutana nae.. Yale University.. siku si nyingi... then... tunasububiri tu utupe ratiba baada ya kukutana Yale Univer itakuwa MIT kabla ya kumalizia Princeton kama sio UCLA ha ha awabongo bwana..
ReplyDeleteKAKA MICHU NAOMBA HUYO MTOA MAONI WA KWANZA ASHIRIKIANE NA DOGO WA USWAZI KUTUBURUDISHA.YANI KANIVUNJA MBAVU KWELI WE ACHA BIG UP KIJANA
ReplyDeleteNdiyo maana huwa nasema elimu ya Tanzania ni bora kuliko Marekani yaani huyu yuko kwenye chuo kikubwa na bado anaandika utumbo kama mwanakijiji.
ReplyDeleteHivi ndiyo ulivyotakiwa kuandika.
"Professor Bill Rabel wa Harvard Business School anawatafute Ahmed Jumbe na Geofrey Mwoga, wanafunzi aliyowafundisha Syracuse University mwaka 1967. Yeyote aliye na taarifa ya ndugu hawa, tafadhali niandikie mimi kwa kutumia email hii wpkuja@cba.ua.edu au wanaweza kuwasiliana na Professor Rabel mojakwa moja katika email hii xxxxx@xxx.xx. Ahsante"
Sikujua kwamba wahaya ni bado wasomi namna hii, ila kijana alikuwa anataka kuelza sababu ya yeye kukutana na mtu huyo, halafu amuwezi kushangaa huyo prof. alivyofurahi kukutana na mtu toka Tanzania na kutaka kujua hali za wanafunzi wake miaka yote hiyo iliyopita na vile vile siku hizi kuna kitu kinaitwa reunion sioni sababu za watu kukashifu mambo yote hayo.
ReplyDeletewewe anonymous wa 4:48 nimekukubali. jinsi ulivyomrekebisha na kupendekeza ni jinsi gani tangazo lake lilitakiwa liwe kwa kwakweli nimekukubali.halafu ukamalizia na ahsante. yaani nimecheka mpaka mbavu zinaniuma hapa. uko juu mwana!!
ReplyDeletehiii bhaghosha sikujuaga kama hili libulogu ni litamu kiasi hiki. hii ng'wanawane michuzi ninakupaga bigiapu
ReplyDeletereunion iko siko zote sema wewe ndio umeijua siku izi.
ReplyDeleteehehe big up wahaya, yaani kila msomi hapa mhaya kazi mnayo kweli kweli. sasa watu uwazi umewashinda nini? ndiyo maana tunauana na kuambukizana virusi kila kukucha sababu uwazi umetushinda, sa ye kusema alichokuwa akikifanya imewaumiza wapi? wabongo bwana, wakati ukikutana na mzungu ataanza kukuhadithia alivyokula na alivyolala mtachekelea mlivyokuwepo wajinga nyoo, big up wewe uliyeandika hivyo ndivyo unavyositahili kuandika, sisi tungejuaje huyo bil mmekutana wapi, je kama anadanganya?? wabongo elimikeni hizi ni zama za uwazi na ukweli. koku
ReplyDeleteWabongo nongwa imezidi!.
ReplyDeleteKwa wewe uliesema ukisoma shule kubwa ndio education yako bora. FYI, Knowledge ni jinsi unavyoitumia na kuapply and it allll depends on the person, sio wapi umesoma. Na kuandika sentensi ya kiingereza haitegemei umesoma chuo kikubwa au kidogo!!!!!
We anonymous poster wa 3:53PM usimzulie mtu mambo. Moja, hawezi kuwa Mhaya kwa sababu hakuna Wahaya wanaume na pili kasema anakutana naye tena June 23 Yale University ili kama una taarifa umpe haraka kabla ya hapo...
ReplyDeleteHivi UA ni University of America,campus ya Egypt au University of Alabama,University of Arizona,University of Arkansas,University of Alaska,University of Auckland,University of Alberta,University of Aberdeen,University of Adelaide? Mimi pia ni MUHAYA; hivyo nataka ku-kurepresent research yangu hapa Stanford University,California.
ReplyDeleteLugakingira Rweyongeza,PhD Candidate
Mbona Alabama ni mashambani sana? Yaani Alabama ni sawa na Kigoma ya bongo.
ReplyDeleteNoma kwelikweli.
Halafu wala sio chuo bab kubwa. Kipo kwenye the top 20,000
Ha ha haaaa
Wewe ananymous wa May 15th 4.48pm usiwe na njia moja ya uelewa wa jambo. Hili Tangazo linaweza kuandikwa na walimbukeni kama wewe kwa njia nyingi zaidi ya mia moja. Huyu jamaa kuandika kwa kifupi kukutana na huyo Prof inajibu maswali ambayo watu wangeuliza wamekutana wapi na wakifanya nini. Haya hayakuwa mashindano ya kuandika insha hakukuwa. Mnapoteza muda kuchambua swala dogo ambalo halina maana yoyote. kwa sababu za Privacy anakuwa kama bridge ili kama kutakuwepo na wasiowangwana wasiweze kutumia fursa hiyo kutoa upupu wao.
ReplyDeleteBasi bwana umesema na wewe umesikika kwenye Blog, lakini mimi nimeona huyu jamaa kaandika ujumbe mfupi wa Kingwana sana.
Mdau UK
Mjomba kama kweli sio Muhaya, basi lazima awe MUHA!wa Ujiji.Maana huko ndio machimbuko ya malimbukeni.
ReplyDeleteMie naona kama hakuna mtu anaye wafahamu hao jamaa tunyamaze make Wabongo tumeziki kuwa -ve.
ReplyDeleteHuyo dogo tulisoma naye Minaki, dogo alikuwa mtu simple sana, sio mtu wa kupenda makuu. Halafu pia alikuwa smart sana. Ila kwa sababu Wabongo tumebarikiwa kwa kusema na kuuana ndo maana tunaongea sana.Kama unataka kujua UA ni ipi kati ya utumbo huo hapo juu ingia kwenye email address aliyokupa www.cba.ua.edu ili upate tofauti unayotaka. Ninaomba tu atumegee kipande cha research yake kwenye Blog ya Jamii kidogo tu. Michuzi mwambie dogo atupatie angalau kipande kidogo cha research kwenye Blog ili mijitu mingine ifunge Midomo yao.
Jay, Toronto
Badala ya kumsaidia kwa kumpa taarifa wengine mumeona mumshambulie huyu Kuja.
ReplyDeleteHuwezi kuzuka tu na kusema fulani na fulani ni 'wanted', inabidi utoe maelezo kidogo hasa ukizingatia kwamba yeye anawatafuta wahusika kwa niaba ya mtu mwingine.
Bila ya shaka wapo wanaomtania tu and some humour is understandable lakini kuna na wale waliodhamiria hasa kumkejeli bila ya msingi wowote, hawa wanasikitisha.
Inasikitisha sana ukiona mwanafunzi wa chuo tena wa level yako alafu hawezi ku-communicate to the public. Ukweli ni kwamba umechemka we kaka wa UA.Ujumbe wangu kwako na kwa wanaokufagilia, LEARN TO COMMUNICATE TO THE PUBLIC your notice is full of non-sense.Tumia elimu yako kijana jifunze kutoa public notice bila kuweka all the stories around you. Sasa shule yako inakusaidia nini?? bado unafanana na mtoto wa primary!
ReplyDeleteSwali kwa mdau wa UK May 16, 2009 6:23 AM. ujumbe mfupi wa Kingwana sana ndiyo nini? Halafu wewe unamwambia mwenzako limbukeni nadhani wewe ndiye limbukeni.
ReplyDelete...na wewe Lugakingira Rweyongeza,PhD Candidate
ReplyDeleteSiyo "ku-kurepresent research" ungeandika "ku-present research".. kwa manufaa ya wengi humu kuna tofauti kubwa kati ya represent na present unakuwa kama Mwanakijiji.
Kifimbo Cheza
Jay,
ReplyDelete"ingia kwenye email address aliyokupa www.cba.ua.edu". www.cba.ua.edu siyo email address. Yeye ametuka email address na wewe unatakiwa utueleze hiyo www.cba.ua.edu ni nini.
Kifimbo Cheza
una-present research? research ya u-ngwini nayo research.halafu wabeba box mnasoma vikozi vya ajabuajabu mnaanza kutamba mmesoma.mwenye Ph.D ya sayansi (maths,engineeering,computer science etc) yeye asemeje? kumbukeni hata maprofesa wanatofautiana, prof. kwenye fani ya sayansi huwezi kumlinganisha na prof. wa performing arts.washamba wa Bukoba msisumbue watu.Nshomile kwa kujitangaza hata la maana hakuna!
ReplyDeleteFellow Bloggers
ReplyDeleteWith Great respect, I acknowledge your criticisms. I salute your autonomous views and proof reading elucidations. But,how can imperfect man make anything perfect. No matter how deep one is educated, learning from each other is infinite. I was enormously aware of the people I was facing and it comes precisely to my expectations.
I sincerely appreciate the rejoinder dispatched by right handed ladies and gentlemen across the planet. Through your emails I have helped the Harvard Elite to locate two of his best students from Africa who he calls African cream of the crop of the 19th Century.
I would like to express my compassionate condolence to the family and survivors of late Ahmed Jumbe. Prof Rabel and I have received this horrific news with great sadness. May the Lord lend the survivors with new heart to overcome the grief.
Fellow bloggers, I find it hard to answer some of your queries, why all these sicknesses, frustrations and personal attacks from people with great love and unity like us, Tanzanians. I have been dubbed all kinds of names, from Bukoba, Kigoma and everywhere else in the country. But with all these negativities, my feelings are intact because I was born in Tanzania, I could be either tribe, and proud of who I am, but not even close to suggestions vomited above. A true Tanzanian is identified by the colors of our “national flag” not from the tribe he/she comes from. One simple case I would like to articulate to my fellow citizens, lift your hearts and start thinking positively, these brainless counter riposte will never shove us to the Promised Land. They are impediments to solutions of divine intervention. We need clear-minded younger generation with self-esteem to lead the nation forward as opposed to these kitchen sink attitudes.
Thanks – Lets continue blogging
Kuja
wape wape ee vidonge vyao, wakitema wakimeza ni shauri yao.
ReplyDeleteEnglish hiyo mwanangu ka ya Mashaka. Hivi nyie nlishoma shule moja au. Kweli wengine wamezidi utumbo humu ndani, wape vidonge vyao kaka.
List inaongezeka, Mashaka Dr Shayo na Kuja tunawaunganisha pamoja watrudi bongo watuokoe na mafisadi.
I second you 4:48 wow!
ReplyDeleteuniversity of alabama ni chuo kikubwa? huyo mtu anajiandikia tu hajui anachosema ingekua Tuskegee University ningekusikiliza nani wabongo wengi tu wamesoma tuskegee
ReplyDeletekwanza wewe umesoma wapi? unayo hata AA kweli?
Watu muache ukabila wenye chuki binafsi. Watu muwe mnajibu kutokana na kitu ulichoulizwa. Watanzania mna mambo ya ajabu sana. Mtu akijitambulisha basi ni muhaya. Kuna watanzania wana ukabila kama Wakenya. Watu wengine kujifanya mnajua mamuma msioyajua. Mtu mmoja akitaja mhaya, basi mnakuwa bendera fuata upepo. Kama huna maoni kuchangia kaa kimya. Halafu wachaga kujifanya mnajua sana. Acheni kuchi kwa wahaya. Na wanachukia wahaya ni wanawake ambao waliolewa na wahaya, baada ya kuachika kwa wanaume wao kutokana na tabia mbaya zenu. Basi mkawaona wanaume wa ki-haya hatutaki kuwasikia kwa sababu ya tamaa zenu za kupenda hela. Nakaa na wanawake wakichaga tabia mbaya kama konokono. Wanapenda kukaa na ndugu wa wanamke. Lakini kwa mwanamme hawapendi kabisa. Kwenda huko wanawake wa kichaga hakuna lolote roho mbaya na uchoyo. Wanawake wa kichaga wanapenda kumbana wanamme kwa mali ambayo amemkuta nayo. Wako kama wamarekani weusi. Kila mtu anajua tabia za wanawake wakichaka. Sasa wewe kama uliolewa na mme wa kihaya ukashindwa jinsi ya kumbana, ndo maana una chuki. Na muache chuki na ukabila. Nyerere alipinga sana ukabila.
ReplyDeleteGood for you kuja WP!These people need to grow up and stop being nasty,its bad and it doesn't help anybody!Great response.
ReplyDeleteAisee Mzee Lugakingira, nimefurahi sana ulipofikia hapo.Pigana sana kwenye level yako.Hiyo shule ya California niliipenda sana. Nami niko hapo Massachusetts Institute of Technology(MIT),nikifanya PhD yangu ya Computer Engineering.On my vacation in December,I will pay a visit to Stanford University.Labda naweza kupata faculty position baada ya shule yangu.I will probably see you.Kuna kijana rafiki yangu hapo,anaitwa Rwebangira Kaishozi anafanya PhD ya Computer Information Systems.Ukimuona,msalimie sana.
ReplyDeleteRugaimukamu Ishengoma Rwegoshora
Ukilinganisha Tuskegee na University of Alabama ni sawa na kulinganisha Mwananyamala na Muhimbili. Zote ni hosipitali lakini inapokuja kwenye kiwango cha wagonjwa watakaotibiwa an vifaa vya kuwatibu, tunaongea lugha nyingine.....endelea kutafuta shule nyingine ulinganishe
ReplyDeletelakini sio Tuskegee