Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mkuyuni ,Tarafa ya Mkuyuni , Wilayani Morogoro  wakiangalia mchezo baina timu ya Manchester United  dhidi ya timu ya Wigan zote za nchini Ungereza katika mfululizo wa ligi ya nchi hiyo uliofanyika juzi jioni ambapo matokeo yalikuwa ni kwa Man Utd kushinda mabao 2-1. wanafunzi hao na watu wengine  walilazimika kulipa kiingilio cha sh: 300  kuangalia mpambano huo. Picha na mdau wa mji kasoro bahari John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2009

    Duh Jamani mbona mnapenda kutuongopea hapahapa tupo macho au mie ndio nimeshindwa kuelewa.

    1. Game siilikuwa jana? sio juzi. hii picha ya Alhamisi imewekwa hapa.

    2. Je ni wanatizama hapo moja kwa moja au? sababu kama umemanisha moja kwa moja kwa Tanzania itabidi iwe saa Tano usiku. nikitizama kwenye Tundu za Nyumba hiyo au Jengo hilo naona mwanga wa Juwa kumaanisha kwamba Kweupe si Usiku.

    Michuzi tufahamishe vizuri tunaomba.

    John Nditi unatuzamisha majini hivihivi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2009

    Michu hapo mdau kaku-jazz, mbona gemu la Mani Yuu na Wigan lilipigwa night kali? Hapo naona kama jua linawaka kwenye hako kadirisha vile, au ilikuwa recorded, feedback puliiiz!

    Mzalendo 101

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2009

    Wanalipaje sh: 300 wakati unaweza kuona bure kwenye matundu ya ukumbi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2009

    PPV in the dust

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2009

    raha sana bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...