Kama ilivyo kwa Watanzania wengi, mimi nami nimekuwa nikifuatilia Blog ya Bwana Michuzi na ni kweli kwamba blog hii ni moja wapo ya blogs mashuhuri hapa Tanzania. Hivyo sifa kwako bwana Michuzi.
Kama nilivyo dai hapo juu kwamba hii ni blog inayotizamwa na wengi (hapa tu ninapoandika tayari watazamaji ama watembeleaji wa hii blog tangu ianzishwe imefikia 5961931 na pengine makala yangu itakapo bandikwa ninaimani idadi ya watembeleaji itakuwa imefikia mbali.
Mada yangu kwa leo ni kujadili dhana ya “nguvu ya Hoja ama Hoja ya Nguvu” (vyovyote utakavyo iweka ni sawa tu) Sababu ya dhana hii ni kutokana na uchambuzi nilio ufanya kuhusiana na posts za watu na maoni mengi kufuatana na posts hizo (samahani mimi sio academician bali ni mkulima lakini pia wakulima nao wanafanyaga chambuzi eti).
Kabla sijaendelea ningelipenda kuweka wazi kwamba kama tunaheshimu uhuru wa watu basi kila kilicho postiwa kina haki yake (maana, kila aliye sema neno, basi ana haki kufanya hivyo bora asivunje sheria).
Kumbe hata mtu akisema utumbo ni Ruksa bora asitukane kama kutukana ni kuvunja sheria sivyo? Okay, pamoja na haki ya mtu yeyote ku post atakacho bila kutovunja sheria, ninalo swali pia: Je posts nyingi ambazo zimewekwa kwenye hii blog zinaangukia wapi? Kwenye “hoja ya nguvu” ama Nguvu ya hoja”?
Je mtu anapouliza swali (potelea mbali hata kama anatafuta mchumba kupitia hii blog) ni kwanini inakuwa ndio njia ya watu wengine kupepeta (wana haki though) badala ya kujibu swali ama kutoa msaada ama basi kujibu sawia na alichosema mtoa mada?
Nitasema kwa mifano nielewekwe zaidi. Jamaa mmoja alikuwa na research yake kuhusu Sirikali yetu ya muungano. Akauliza apewe msaada wa kupata data Fulani Fulani. Majibu yaliyo tolewa yalivuka mpaka kwanza wengine waka ulizia (question) uwezekano wa research ya jamaa / sijui swala la msingi la research yake / je ni PhD (Pile Head Deep (with trash)) / ama ni Masters (ubwana vs. utwana) n.k./ mara research (tafiti) hiyo haiwezekani na mitusi kidogo haikukosekana.
Sasa swali ni je majibu yote hayo yalilenga hoja ya nguvu ama nguvu ya hoja?
Je kuna uungwana hapa(lugha ya kistaarabu)?
Jamaa mwingine akazungumzia swala la tourism (utalii). Jamaa points alikuwa nazo. Majibu mengine pia yalikuwa mazuri. Lakini jamaa wengine hawakukosa mitusi kidogo kwa mtoa mada na zaidi basi jamaa alijitahidi kiingereza chake (ndipo alipata nafasi ya kujaribu masikini) akafyekwa bila huruma criticism kalikali (sijui critisisms kwa Kiswahili fasaha ni nini samahani). Nilikosa kuona nguvu ya hoja zaidi hoja za nguvu (za kimabavu) zilitembea.
Mtu mwingine akaomba msaada wa kupata mchumba - sina haja ya kueleza majibu aliyo pewa kwani kama wewe ni mtembezi ndani ya hii blog pengine uliona. Jamaa alipigwa mijaruba ya maneno hata kuchambuliwa vilivyo sema tu hakuweka picha kwani ingelikuwa balaa. Tuelewe kila mtu ana haki pia lakini je ni uungwana?
Ndio nia ya blog ya jamii kwa wana jamii kutwangwa mifundo (ngumi) na wakali kama wa jela? Mifano ni mingi lakini nina imani nimeelewekwa. Shida basi ni kwamba, ni kwanini hatuthamini kutoa hoja zenye nguvu na badala yake tunatoa hoja za kimabavu?
Pamoja na sababu kwamba blog hii tuiitayo ya “jamii” inatoa mafunzo / inapasha habari / inaburudisha / lakini sidhani kama ina nafasi ya kashfa / kejeli / kukatishana tama – ijapo kila mtu ana haki ya kusema neno ili mradi asivunje sheria.
Nisingelipenda kurudi kwenye mifano lakini nigusie kidogo tu, kuna wenzetu waliweka mijadala humu. Nilitarajia mijadala ile (ama debates) ingelijadiliwa kwa nguvu za hoja lakini ilifikia kiwango kwamba hata mtu ana eleza (express) hisia kali dhidhi ya mtu mwingine hata asiye wahi kukutana naye. Je hizo ni nguvu za hoja ama hoja za nguvu ijapo kila mtu ana haki ya kusema neno ili mradi asivunje sheria?
Kuna hoja kadhaa zilizo husu wale wanaoitwa “wabeba mabox”, tena hoja nyingine zililenga watu specific na nyingine zilidhiriki kutaja hadharani kwamba Fulani oh! Wala hajapata makaratasi huko aliko / mara oh huyu ni kula kulala / na kadhalika. Nafikiri mnanielewa jamani (samahani kuulizia hivyo ). Lakini cha msingi ni je huu ni uungwana? Je hoja kama hizi zinajenga ama zinabomoa? Je ni hoja za nguvu ama ni nguvu za hoja?
Swali langu la mwisho ni kuwa, hivi kama tungeliamua kuwa na kile wanachokiita kwa kimombo : positive attitude badala ya negative attitude (kwa wale wajuzi wa Kiswahili sanifu nisaidieni jamani maana ya haya maneno) si posts mbalimbali humu zingelifundisha jamii? Maadam nib log ya “Jamii” kumbe pangelikuwa ni pahala pa jamii kujifunzia hata kutoa mada – wengine jamani ni mara ya kwanza kupata nafasi kama hii.
Sasa tukitwangwa mitofali ya mi critic inatujenga ama ina tududumiza? Huu ni utamaduni gain basi? Kumbuka lakini kila mmoja wetu ana haki ya kusema lolote ili mradi asivunje sheria ijapo swali ni Je huu ni uungwana? Kuna kitu kina itwa kusafisha nyumba (house cleaning). Kama sote tukiwekana sawa humu kweli blog hii ya jamii ingelitunufaisha sana kwa mengi bila kutukatisha tama wengine.
Mwisho, nina mshukuru Mungu kwa ajili ya Mheshimiwa Michuzi kwa kutupatia njia hii ya mawasiliano hata mkulima kama mimi nina weza kuandika kitu nikiwa huku madongo kuinama kikasomwa na kila mtu toka kila pembe sio tu za Tanzania bali za dunia (hapo kitambo hata kupata gazeti la uhuru ni shida sema uandike makala mle – thubutu) sema tu bahati mbaya nyumba bado (kwa mitazamo yangu) inahitaji kusafishwa ili iwe na hadidu rejea (modus operandi) zifaazo kwa manufaa ya jamii ambayo chombo hiki kimekabidhiwa kwao na sio ukandamizwaji.
Msinijibuni kwa hoja za kimabavu bali hoja zenye nguvu, na tuudumishe utamaduni mwema.Pleeeese! Michuzi kwa mara nyingine nikupe BIG kwa kwenda chini kihistoria kwamba umeweza kutukutanisha kwa namna hii. Hata kwenye "wikipedia" upo mzee. Pongezi
Mdau Mkulima July
-----------------------------------------
Mdau Mkulima July,
Huwa nasita sana kubandika 'magazeti' lakini nguvu ya hoja yako imenilazimu nibandike makala yako hii kwani imegusa sehemu nyeti ambayo hata mie hunikera sana, hasa pale uhuru wa kutoa mawazo unapotumika vibaya na baadhi ya wadau almaarufu kama 'waosha vinywa'.
kwa kweli inakatisha tamaa kuona jinsi Wabongo wasivyokuwa na zuri. Baadhi (ishukuriwe sio wote) hawana jema. Chochote kile ni kukosoa na kuchafua hali ya hewa. Na inaudhi zaidi pale Globu ya Jamii inapoandamwa baada ya kupiga chini maoni ya waosha vinywa. Hakika ningekuwa naruhusu kila kitu ingekuwa nongwa. Ujue hayo uyaonayo ni robo tu ya maoni ya kukatisha tamaa yanayokuja. Unajiuliza; hivi kuna ulazima gani kukatisha mwenzio tamaa?
Hata hivyo, yote maisha. Naunga mkono hoja zako zote na kuendelea kuwasihi wadau kuwa wavumilivu, kutoa maoni hata ya upinzani ila yasiyo na kashfa kwa wengine. Kumbuka usimfanyie kitu mtu ambacho wewe hutopenda kufanyiwa. Nakushukuru sana Mdau Mkulima July.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Mdau MbuliJune 17, 2009

    Mdau Mkulima Jully nikupongeze kwa mada yako safi na kuhoji JE HUU NI UUNGWANA? SI UUNGWANA HATA KIDOGO! Pongezi pia Bro Michuzi kwa kuikubali hiyo post ya Mdau Jully. Jambo la msingi ambalo wanajamii (waosha vinywa)wanasahau ni kwamba hapa ni mahali pa kuhabarishana na kuelimishana na si kutukanana. They ain't aware of what kind of people visit this blog. Wasifikiri ni wote wanaoingia (visit this blog)wana mawazo kama yao. Jambo moja nawasihi WANAJAMII kama maoni ni yako ni (criticize) bas lugha nzuri na maneno yenye busara yakitumika itakua jambo jema zaidi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2009

    BIG UP!!! Mkulima July.

    AHSANTE SANA KWA POST YAKO HII LAZIMA TUJIFUNZE.

    - Mikail Rikab

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2009

    Subawulful ya akhee
    Nimesoma kwa makini mawazo ya mkulima na pia yako wewe Misupu. Nakubaliana nanyi. Mie leo na mara nyingi nimeandia kusema kwamba blog hii yatembelewa na jamaa lukuki ambao wana nia ya kujifunza lugha Mimi binafsi NAWAAMBIAGA wote kwamba kujifunza lugha kwa vitabu tuu ni nusu ya ujuzi ni lazima kuitumia lugha barazani hadharani
    Tumrudie mkulima, naomba wajuzi wa lugha watueleze
    Kwanza matumizi ya maneno kama wanafanyaga au nawaambiaga hakika hiki si kiswahili safi, naomba jibu
    Pili ingawa mara nyingi twatumia neno MUUNGWANA si neno zuri sana kwani asili yake ilikuwa ni kuwatofauti baina ya mtumwa na mwarabu au mswahili asiyekuwa mtumwa,in English a slave and a free man, or a child of a slave woman and her master,Kwa hivyo dont call me muungwana I dont think you can call an African American Hullo freeman, unless his first name is Morgan
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2009

    Ndugu Mheshimiwa Balozi Michuzi,

    Nategemea umefika salama nyumbani na hujasahau zawadi kwa my wife wako, watoto, jamaa na majirani wote.

    Mimi binafsi huwa napenda sana kutoa maoni yanayohusu jamii na siasa. Nasikitisha kusema kuwa sio kweli kuwa unabana maoni kwa kuwa "yanachafua hali ya hewa". Maoni yangu mengi umeyachapisha lakini pia mengi umeyabana, hasa yanayohusu CCM, Serikali na Mwalimu Nyerere.

    Kuamua kuchapisha au la ni uamuzi wako kama mwenye hii Blogu ya Jamii, lakini sikubaliana nawe kuwa umebana maoni yangu kutokana na lugha yangu mbaya. Sio desturi yangu na inaenda kinyume na uhuru wa kutoa maoni bila ya kukashifu unayoitangaza.

    Pia, ukirudi nyuma kidogo, kuna dada wa watu umeacha maoni yaliyochafua hewa yampitie. Wadau walikuwa wanamkashifu kwa kuacha maoni kuwa walishalala nae japokuwa ana mume wa kizungu lakini maoni yalipenya. Kwa hivyo sielewi nini hasa maana ya " maoni yanayochafua hali ya hewa".

    Shukurani.
    Mdau, Tokyo, japan.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2009

    Mkulima!Kama kweli hiyo ndio kazi yako, Basi naona utakuwa Umekula Mbegu!(Joke!)
    Nadhani kuna wenye Hoja za Nguvu katika comments unazozizungumzia ndugu Mkulima.Lakini pia kuna wenye Nguvu za hoja.
    Wakati mwingine ni kutokana na upeo wetu sisi wasomaji kuchambua mambo.I mean Nguvu ya Hoja kwako, mimi naweza iona kama ni hoja ya Nguvu.It depend na maono yako.
    Kitu ambacho hatutaki humu ni MATUSI.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2009

    Ndugu Balozi michuzi,

    Naomba upitilie tena maoni ya baadhi ya wadau yaliyopenya na picha ya Mwamvita Makamba wa Vodacom Foundation, tarehe 04 June 2009 alopokuwa anawatembelea watoto wa SOS children's Village.

    Niambie kuwa maoni yao yamechafua hali ya hewa au la. Na kama yamechafua hali ya hewa, mbona yamechapishwa?

    Naona maoni yangu ya kwanza kuhusu hili swali umeshabana tayari. Muhimu kuwa yamekufikia wewe binafsi.

    Mdau, Tokyo, Japan

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2009

    mimi mtazamo wangu tatizo lipo kwa michuzi mwenyewe,nadhani ni yeye anaelewa kusudio la kupost hizo mada na uwezo wa kuachia maoni au kuyabana anao yeye.sasa inakuwaje maoni yasio na hoja tena yenye kashfa yanapita na yale yenye nguvu za hoja yanabaniwa.hadi naanza kuamini ndugu michuzi unabagua baadhi ya wachangiaji unawafahamu kabisa hivyo kuwapa uhuru wa chochote.umekuwa unapenda maoni chanya kwa ccm na serikali yake hata kama wanaotoa maoni hasi wana hoja.sipendi lugha za matusi au kashfa kwani si utamaduni wetu watanzania.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2009

    Kama ulivyosema hii ni blog ya `jamii' na sio blogi ya `wanafalsafa' au magwiji wa taaluma fulani. Hii ni blogi ya wanajamii na waaina tofauti ambao wanaobahatika kupitia hapa.
    Nieleweke wazi kuwa sikupingi mtoa hoja,ulichozungumza ni sawa kabisa, lakini lazima tukubali kuwa jamii inapokutanisha watu wengi, lazima akili, uoni na utambuzi utatofautiana, vinginevyo haitakuwa blogi ya jamii,itakuwa imewatenga wale wenye tabia ya `kuosha vinywa' kwao hiyo ni starehe!
    Kitu tunachowaomba hawa waosha vinywa waangalie athari za `hoja zao za nguvu' kwani nguvu wanayoitumia kama wengetumia `akili na busara' ingekuwa hoja ya nguvu na ya msaada kwa mwenye kutaka msaada!
    Mjue kuna watu wanamatatizo ya kikweli, wanaogopa kuyaweka hapa na wangeyaweka hapa wangepata ufumbuzi mzuri,kwani kwa vile ni blogi ya jamii,basi ujue wapo wanataaluma wazuri, watoa ushauri mzuri, lakini wanaogopa kuwekwa uchi, watakatishwa tamaa kabisa.
    Kwahiyo na mimi ombi langu ni kuwa ndio ni blogi ya jamii, pasipokuwepo watu wa namana yenu haitakamilika, lakini muangilie nani, ni nini na kwa wakati gani mnatakiwa mseme nini, hii ndio hekima, na hekima ni bure kabisa!
    M3

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2009

    Hii ni aina ya maoni tunayotakiwa kuyatoa humu ndani. Maana ni maoni ya kujenga na pia ya kuelimisha. Hongera sana kwa kazi nzuri Mkulima Ally.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2009

    Napingana na mto hoja na wote waliochangia. Vilevile sikubaliani na matusi kwenye maoni.
    NIna swali moja tu juu yenu.

    KWA NINI TANZANIA KAMA NCHI HATUENDELEI?

    Jibu lake kwa mtazamoa wangu mimi ni kwasababu tunaunga mkono kila hoja inayotolewa. hakuna wa kupinga hakuna wa kutoa critisism japo kidogo. ndo maana wabunge huenda bungeni kulala. sababu hoja zao zitapita tu.

    MI nadhani mtu bila kutupiwa mitofali kidogo hautakuwa ngangari. so michuzi ruhusu matofali ila yasiwe na matusi

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 17, 2009

    ukiona hivyo huyo mkulima (jina) kapigwa Dongo, ndio maana anamind,
    Hii ni blog ya jamii!!
    Dr. Kamugisha Moscow!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 17, 2009

    Mdau wa 4:26pm na 4:39pm nina wapongeza kwa kumade my day today!!way to go timu!!!!!!!!!

    Mshauri mkuu
    University of cuba.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 18, 2009

    Kuna wakati mchafuko wa hewa Ndugu Michuzi unausababisha wewe mwenyewe , kwa kubania comments za wadau hususani zile zinazolenga chama tawala i mean CCM au serikali . mimi binafsi si chini ya mara nne umenishanibania comments zangu ambazo nina hakika zimegusa mahala pake(moja wapo yah: kikao cha bungekinachoendelea ) ambayo niliituma siku sita zilizopita , na nina amini asilimia 100 sikuwahi kutumia neno hata moja matusi lakini kwa utashi wako ukazibania sababu ziligusa penyewe . sikulazimishi uwe unazitoa hiyo ni hiyari yako . lakini kama wewe mwenyewe ulivyoita blog hii kuwa ni ya jamii basi uwe unawapa wadau nafasi ya kutoa hoja zao. pengine hazitowafurahisha wengi lakini kutakuwa na wachache watakao zikubali. kuna wakati wadau wengi tunaamini pengine wewe si mwanajamii yetu ni mtu wa system (na hiyo ndio inavyoonyesha ) upo nasi ukitung'ong'a visogo.
    Pili - nitakuwa mwizi wa fadhila kama sijakushukuru pia kwa mchango wako mkubwa unaotupa walio mbali na nyumbani kwa kutupatia habari zinazohusu maswala mbalimbali yanayohusu Jamii , siasa, michezo na burudani.kwa hilo asante sana Ndugu Michu mtoto wa Aggrey a.k.a brother man wa Jugnu Mehu. Plz hii usiibanie .
    Nawakilisha Mdau Zee la Bandari Leicester UK.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 18, 2009

    Blog ya jamiii Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!! mwenye kuona na aone na mwenye kusikia na asikie!
    Michuzu no 1!!! no body can stop michuzi!!!!!!

    Mama mingoi!!!!!!!!


    ila jamani matusi amna wala kununiana hiyo aimo, au sio jamani!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 18, 2009

    ..blah, blah, blah, blaah...

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 18, 2009

    anony wa JUne !7, 4:26 kula tano kabisa. Huyu michuzi na huyo mkulima hawaelewi kuwa tofauti ndizo zinatufanya tuwe binadamu. Na tofauti hizo siyo urefu weusi au rangi. Ni nmana ya kutumia ubongo wetu. Kama watu wote tungekuwa tunafikiri sawa sawa basi ingebidi awepo mtu mmoja tu. Kwako mkulima ukileta mda ya uchumba humu tegemea madongo na majibu ya aina unayopenda.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 18, 2009

    hii ni blogu ya jamii...sio kukalilishana nini tujibu

    kwako chawezekana na upupu/kuchafua hewa ila kwa mwingine ni point na inahamasisha

    sasa km wewe michuzi na uyu aloandika gazeti hilo mwataka tufanye hii blogu kitabu fulani-mtukremishe?semeni mana itatushinda

    blogu ina maana kuelimisha jamii ILA PIA kuchangamsha wana-blogu

    mshaanza mambo yenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...