Wadau wa Arusha wa blog ya jamii wanakupa pongezi Mzee wa Nainhii kwa kuijulisha jumuia ya Watanzania duniani kote (kasoro Unchina) kuhusu habari za Bongo na kwa kukuunga mkono Mzee kidevu Mpumilwa naye ameanzisha website yake kama invyoonekana hapo katika sherehe za uzinduzi. Libeneke hilo linakwenda kwa jina la
Pichani ni Dr. Nyamajeje Weggoro akizindua libeneke hilo akiwa kama mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zilizofanyika hoteli ya Golden Rose. Danford Mpumilwa (akiwa na tai ya nanihii) anaangalia huku mdau aliyeitengeneza Da' Anna Donald amekaa.
Wengine katika picha toka shoto ni Novatus Makunga, Said Abdallah, Gerald Munisi, Sombyo Mwakatobe, Savo Mung'ong'o, Mohamed Mpagama, Dr. Moses Ligonile, Suk Chat na Charles Panyika.
----------------------------------------------
GLOBU YA JAMII INAPENDA KUTOA PONGEZI SANA KWA MZEE KIDEVU MPUMILWA KWA UAMUZI WA KUANZISHA LIBENEKE AMBALO SINA SHAKA LITATOA HABARI NA TASWIRA ZA A-TAUN AMBAZO KWA UMUHIMU WA KIPANDE HICHO CHA NCHI, ZINAHITAJIKA KILA SIKU.
NINA UHAKIKA KWA UZOEFU ULIONAO WA UANDISHI ULIOTUKUKA PAMOJA NA UBUNIFU NA KUCHEZA NA LUGHA, ZA KIMATUMBI NA KIINGLISHI, WADAU WAKO TUTABURUDIKA VILIVYO.
KARIBU KUNDINI MZEE KIDEVU
-MICHUZI


hiyo website mbona imekaa kikampeni zaidi? na rangi zake zimekaa ki CCM zaidi. Mr. Mpumilwa hongera kwa kufinga website.
ReplyDeleteUshauri: ni vyema ukaweka bayana kama website ni ya kutangaza biashara? fundraising? kampeni za ubunge/kisiasa? au kujijengea umaarufu na network ya marafiki.
I do not get, I just do not get, I swear I do not get it! I have seen a number of time Wabongos launch their products with fun fair when those products are still in crude stage!
ReplyDeletePeople launch their website and then advertise them to the mass but when you go visit them site what you find is either under construction or coming soon.... messages. why rush???
see like Danford's site, he launched the site but he does not have anything on the home page, nothing! not even a "welcome" message.
Please some one please tell me why we so love to do half backed stuff and shamelessly ask the masses to go take a look ....
Hawa watu wote kwenye uzinduzi wa website?Kweli kazi ipo
ReplyDeleteMaoni: Kwanza kabisa hakuna haja ya kuweka tovuti ambayo haijakamilika, ungesubiri kidogo mpaka uimalizie and then uitundike mtandaoni. Pili badilisha neno under contructions kuwa Under Construction. Tatu Tatu nimesoma kidogo lakini sijaona hii tovuti inahusu nini (seriously)...elezea kwa kifupi sababu watu wengi huwa hawapendi kusoma maelezo marefu Nne kwenye contacts rekebisha pale kwenye Resident phone number. Tano, weka rangi ya background iwe tofauti na main page, ili isionekane kama karatasi la kijani lenye maandishi meusi Sita, umejitahidi kazi nzuri
ReplyDeleteHi ni nini jamani? Nilitaka kusema ni UPUMBAVU MTUPU, lakini nikajirudi isije ikaonekana kama ni tusi...
ReplyDeleteSasa na wewe mheshimiwa wetu wasije wakakutumbukiza kusifu vitu ambavyo bado havijawa tayari. Tafadhali wasitumie hii glob YETU ya jamii kutangaza vitu visivyo na msingi.
sasa huu ndio mwanzo gani,maana site inasema 'WEBSITE UNDER CONTRUCTION' hiyo 'contruction ndio nini?itabidi nishuke bongo niwape tution kidogo ya lugha ya mama
ReplyDeletewhy launching a site which is under construction? halafu rangi zenyewe zimekaa kichama na kifisadi.ovyoooo!that is for your party members only.wengine tunaona kinyaa kwenye hizo rangi.crazy design!!!!
ReplyDeleteMheshimiwa Mpumilwa mbunge mtarajiwa wa Njombe Magharibi hongera veyaa. Make sure hio blog is active my friend.
ReplyDeleteBongo kazi zipo kweli???? Website nayo unaita watu kuifungua....teheteheteh....Mbona wengine tungekaa mwaka mzima home tukisherekea kuanzishwa kwa site za watu....please people be serious....vitu vingine ni sooooooo damn funny.....
ReplyDeleteNa wewe kaka yetu kabla hujatangaza hebu pitia basi uone unaendorse nini????? Usije ukawa wale kina mcCain ...I Iprove the message wakati hujaisoma hiyo msg na wala hujui inasema nini......Site under construction watu wanafungua why rush
Rangi, rangi, rangi, designer unaonekana haujui kabisa kuhusu rangi, rangi kali sana na zinaumiza macho...badilisha rangi ya bacground na maandishi, unaweza ata tumia green iliyo fifia ili isije umiza watu macho................ webmaster kuna mengi ya kujifunza la sivyo hii ni haibu.................
ReplyDeleteMsi-sakame sana huyu mzee wa watu, yeye anataka kuanzisha website kama ya Oboma kwa kampeni za Njombe 2010, lakini hebu angalieni website ya designer wake, nayo ni yale yale under construction. http://www.annawebdesign.com/ Hawa ma-designer uchwara ndio wanatuharibia kazi tunaonekana Tz hatujui web designing.
ReplyDeleteDuh NIMECHEKA SANA!!! Jamani duniani wawili wawili Jamaa wa kulia anafanana na TX MOSHI WILLIAM... Duuuh...Charles Panyika nakosea???
ReplyDeleteDu! jamani kwa kweli usomi na hadhi uliyonayo Danford haviendani na hii website ulofungua, kwanza haijakamilika - ungesubiri uikamilishe ndio ututangazie, RANGI ni mbaya mbaya kuliko labda kama unajiandaa na kugombea ubunge wa Njombe 2010 - na ndio tafsiri za hizi rangi na ujumbe wako uliojaa CCM na TANU nyingi mno.Onana na wataalamu wa website waliobobea wakusaidie.
ReplyDeleteWebsite hata keywords haina, search engine zitakupata vipi usipoweka keywords kwenye code??
ReplyDeleteWeb designer ameharibu kazi ya huyu mzee.But also he could wait get a proper website before calling people to innagurate it.
ReplyDeleteudesign uliotukuka
ReplyDeletekidumu zaidi....!
wembe ni ule ule.. ushindi.....,
wembe ni ule ule.. ushindi.....,
2010 wembe ni ule ule.. ushindi.....,
tanu haaa...,tanu yajenga nchi...!
afande midako
mzee? life experience in public relation, marketing, advertising.. lakini mbona umeshindwa ku-apply kwenye website yako!!!!! mh!!
ReplyDeleteWatanzania wengi hapa kwenye maoni wanaonyesha wivu tu na kutokutaka maendeleo ya huyu mtu ingawa mimi simjui. yeye kaamua kuanzisha blog yake,kujitangaza mwenyewe.nimeingia kwenye website yake na nimesoma mambo kibao tu,profile yake,nk.kasema wazi kua anataka kujitanganza na kushare maisha yake na mambo mbalimbali na watu wengine.kwa hiyo ni uamuzi wa kila mtu,uisome blog yake au usiisome.na nyie mnaokandia, hizo website zenu bomba ziko wapi?????!!!Pendeni maendeleo ya watanzania wenzenu.mmejaa wivu na dharau zisizo na maana. there are no constructive ideas.
ReplyDelete