mitaa ya tegeta nyakati za jioni

mkuu wa kaya, hebu tusaidiane kidogo
picha hii inaonyesha hali halisi ilivyo katika maeneo ya wilaya yako ya tegeta, kituo cha mabasi kimevamiwa na wafanya biashara hasa wakati wa jioni hali inayopelekea kukosekana kwa sehemu za kupaki magari.
hali hii inasababisha magari kupaki barabarani hivyo kupelekea kuwa na msongomano na usumbufu katika hili,
soko hili lilihamishwa na kupelekwa maeneo ya tegeta kibaoni ambako pia kuna kituo kikubwa cha mabasi lakini hili lilikuwa kama nguvu ya soda kwani lilisimamiwa kwa muda na kisha kuachwa na hali imejirudia kama zamani, nani wa kulaumiwa hapa!....jiji,manispaa,serikali au wananchi???
mdau
Ael.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    Wananchi na MJumbe wa Nyumba Kumi KUmi, Huyu Mjumbe wa nyumba 10,10 yeye anakaa tu kusubiri mke na mume wagombane anajifanya kwenda kutatuwa tatuwa mambo kama hayo bwana na wananchi wako wa mtaani. Ya mke na Mume waachie waliowaozesha na wazee wao. Seif.
    WAKULAUMIWA.

    1. Mjumbe(wakazanie Alamshauri ya jiji)

    2. Almashauri ya Jiji la hapo.(kuweni makini na kazi yenu na wasimamieni sana wananchi na mjumbe wenu)

    3.Wananchi(Jukumu lenu la Usafi na Kupenda Vijiwe Vyenu ni muhimu ipo mikononi mwenu na Mjumbe wenu.)

    Seif.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2009

    Hii nchi yetu ni ya ajabu sana, wanapoona tunakaribia uchaguzi wowote kila kitu kinaaachwa holela,yaani hakuna sheria.tukimaliza tu na hao ccm wakishashinda huo ushindi wao wa kishindo ndio tunaanza kampeni kushafisha jiji! hasa biashara zinazofanyika kiholela.hebu angalia suala la machinga tumerudi wapi? nini kimebadilika? wanajaa katikati ya msimbazi st.Alimwinyi RD hata magari yanapita kwa taabu sana.Elekea manzese barabara mpya inayounganisha manzese na sinza(sweet corner) yote imekuwa maegesho ya malori ya nafaka hivyo kusababisha msongamano usio na lazima.suala la tegeta kuna madiwani,kuna mbunge,wenyeviti wa mitaa wote hao hawalioni? tunahitaji kutawaliwa kwa kufuta sheria tulizojipangia na si siasa kwenye kila kitu inakera sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2009

    Tatizo ni kuwa Polisi wa usalama barabarani wanapenda kuuza sura huku mijini hasa A. Hassan Mwinyi road ili waonekane watendaji kazi lakini barabara zisizo mijini hawazijali.

    Daladala zimekuwa zikivunja sheria hadi inakuwa kero kwa wasafiri wao kufika katika bara bara hizi imekuwa kitendawili.

    Mfano wa barabara ambazo hawafiki na nikero kwa daladala kusimama barabarani kupakia na kusababisha foleni ni:- Tegeta, Tandale kutokea Kinondoni, Mwanyanyamala etc.

    Tunaomba hawa polisi wafuatilie barabara hizi waache kuuza sura katika barabara ambazo wanajua Rais anapita tuu kwani huo ni unafiki kujidai unafanyakazi kumbe unataka tu kujionesha.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2009

    mie nilishajizoeza zangu saa 12 kamili niko mjini, na kuanzia saa 1:30 na 2 kila siku ndio natoka mjini ili niepukane na kadhaa hii. Kwakweli inabidi tu tukubali kwamba mawaziri wangekua wanakaa tegeta, boko, bunju, nakwambia barabara zingetengenezwa, wala kusingekua na foleni za kijingajinga ambazo tunasababishiwa na daladala. Viongozi wetu kila leo wanasafiri nje ya nchi, wanaona jinsi wenzetu mambo yao yalivyo mswano lkn wakirudi nyumbani wao ni wizi tu. angalia, hatuna ndege mpaka wakenya wanatupiga bao lakini wao wako hepi tu yaani wizi wizi wizi, aiseeeee. kila kitu tuko nyuma shauri ya watu kukosa uzalendo. watu wanakaa kutoa makosa ya maximo....

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2009

    Jamani si mlisema wananchi hawana ajira hivyo waruusiwe wajiajiri.Jiji wakiwaondosha nyie wanaharakati mwasema haki za binadamu zimevunjwa na mnakuja juu kama moto wa kifuu.Wakati mwingine nikiangalia maisha yetu wabongo nakosa majibu kila kitu kinaenda shagala bagala kwa visingizio vya kipuuzi tu,acha tuendelee hivyo hivyo mpaka tutapoona umuhimu wa kufuata kanuni na sheria zilizopo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2009

    NANIHII!, Mkuu wa wilaya hii ndiyo wa kulaumiwa!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2009

    Hahahahaha ISSA MICHUZI ndio wa kulalamikiwa Issa Michuzi kuwa na haki za wanyonge anza kuhoji watu wa Uswazi sio mara Kylyn mara TID nenda ndani ndani bwana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2009

    Jamani, tatizo hapa sio wafanyabiashara. Wabongo tunaangalia puani na ndio maana hatutaweza kufika mbali. tatizo ni serikali na wakala wake wa mipango miji. suluhisho si kuwafukuza wafanyabiashara, bali ni kupanga jinsi ya kuboresha hiyo barabara wakati na wafanyabiashara wakiendelea kupata ajira na kutoa hiyo huduma ambayo inawafanya wang'ang'anie HAPO!! tena HAPO HAPO!!!! (kuna kitu hapo)

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2009

    Hii picha inaonesha moja ya uozo uliopo ndani ya Serikali ya Tanzania.

    1: Ndani ya Serikali ya Tanzania pamoja na ofisi zake hakuna mtu ata mmoja ambaye anayeipenda nchi hii, Kuanzia Rais mpaka raia wa kawaida wote wana mawazo ya kuweza kujipatia utajiri na hakuna mtu mwenye kujari na kujiuliza je kizazi kijacho kitafanyaje?.

    2: Kutokana na kwamba hakuna mtu anaye weza kujari kuhusu nchi au kizazi kijacho cha Tanzania ndio maana mapato na matumizi ya Serikali na ofisi zake hazina muelekeo ktk kuleta maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla, hapo ndio utakapo kuja kuona hakuna barabara zikijengwa na ata zikijengwa basi hazina uimara wa kudumu.

    3: Kutokana na kipengere cha (2) ndio maana nchi haina maendeleo yoyote miaka yote hii, watu wapo tayari wafanye sherehe za uhuru na kupoteza mabilioni ya Pesa na kuzidisha umasikini badala ya kufanya sherehe ndogo na kuongeza nguvu za kuleta maendeleo. Kutokana na ili nchi ya Tanzania inakuwa kama Congo Drc ambapo mwenye nguvu uvuna na kwenda zake na kumpisha mwingine...

    4: Ni aibu kwa Rais wa nchi, mawaziri, Wabunge, Wasomi, Wanasiasa na raia wa Tanzania kushindwa kuwa na uchungu wa nchi hii na kuiacha ikiteketea na kuzidi kuwa masikini. Viongozi hawa hawa ndio wale wale wanao kuwa na maekalu, magari, pesa za wizi na kusomesha watoto wao nje za nchi, n.k

    5: Tanzania ni nchi tajiri yenye kuweza na kuwa na maendeleo makubwa sana, Ni sisi wenyewe kujiwekea mipangilio katika maisha yetu ya kila siku, kuheshimu sheria, kuhacha wizi, na kuwa wakweli ktk kuendesha maisha yetu.

    6: Tunahitaji raia wenye mawazo mema, elimu kwa wote, uongozi ulio safi na mipangilio mirefu iliyo kwenda shule, Raia wote kuhacha na kutopenda rushwa, kuheshimu sheria na kuwa na uchungu wa nchi yetu Tanzania kwa pamoja.

    Nilikuwa nje Ya Tanzania kwa muda, nikarudi nyumbani kidogo haya ndio niliyo yaona:

    a: Kila sehemu niliyo kwenda ni rushwa, Kuanzia Uwanja wa ndege, polisi, mawakili, Viongozi, wanasiasa, raia, n.k

    b: Kutokana na hali ngumu ya Maisha umalaya umeongezeka na kurudisha nyuma maendeleo. Ukimwi umeongezeka.

    c: Hakuna kilicho endelea, kila kitu kile kile kama nilipo acha zamani.

    d: Idadi kubwa haina kazi wala elimu - Hiki ndicho kinacho niogopesha, kizazi hiki kisicho kuwa na kazi kitakwenda wapi na kufanya nini??? Wachache ni matajiri sana na hakuna ukweli wa utajiri wao, gap ya masikini na matajiri ni kubwa sana na ina ogopesha!!!

    e: Kila kitu kinachofanyika ni kama hakuna mawazo yaliyo kwenda shule, kuanzia serikali, n.k. Ukiangalia utadhani nchi haina Uongozi.

    f: zaidi ya 80% ya viongozi, wanasiasa, wafanyakazi wa serikali na binafsi wanapokea na kutoa rushwa, kuibia serikali, nchi au waajiri wao, n.k Hakuna mtu mwenye uchungu wa nchi na kwa jinsi inavyo onekana wanaweza kuuza nchi au kufanya chochote kibaya, kupindua nchi kutokana na pesa, kujitafutia utajiri, madaraka, n.k

    g: Wachina wameleta vitu feki kila kona, hakuna anae onekana akifanya lolote sio serikali wala ofisi za Serikali, hii inaonesha wame ridhishwa na hali halisi, sio kwamba hawajui bali wamefumba macho kwakuwa wanapata 10%
    Unaweza uka feki kila kitu, chochote unachotaka...inatia uchungu na uruma sana, uwezi kujua kipi cha kweli kipi feki.

    Nilibaki kusikia uchungu sana, nilishindwa jinsi ya kuishi, kwakuwa nilizoea kupata mahitaji yangu muhimu na haki zangu bila ya kutoa rushwa, niligandisha kila kona kwakuwa sikutoa rushwa!!!

    Jamii yenye mafanikio ni ile inayo fundishwa toka ikiwa changa nini maana ya maendeleo kwa ujumla, madhara ya rushwa, umuhimu wa amani, kuipenda nchi, n.k cha kushangaza sikuona Tangazo lolote eidha ktk radio, tv, au magazeti ikizungumzia yoyote kati ya haya kwa kipindi chote cha mapumziko yangu.

    Hapa nilipo, kila siku ni lazima nione moja ya Tangazo yakielimisha jamii, hapo ndipo jamii inapokuwa na upendo wa nchi na kuweza kuleta maendeleo.

    Nina amini Tanzania ni nchi tajiri, ila hatuna uongozi na raia wenye kuweza au kuwa na mawazo ya maendeleo. Lakini sitokata tamaa, ipo siku nitakuja kuona maendeleo.

    Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2009

    Matatizo yaliyopo ni madogomadogo tena basi yanarekebishika kirahisi ila kwa kuwa tumezoea mpaka tutafute wawekezaji ... sijui. Ukizingatia mkuu wa nanihii hii naye anapiga misele kwenda sambamba na ya Vasco da Gama basi inakuwa tabu tupu.
    1. Ukipeleka soko tegeta kibaoni unataka nani afunge safari kununua ndizi mbili kote huko? Halmashauri zingechangamkia kuboresha maeneo ambayo watu wameyachagua kwa njia zisizo rasmi na kutengeneza visoko mshenzi kisha wakalamba ushuru wa kishkaji badala ya kupoteza nguvu kupigana kufukuzana baada ya uchaguzi.
    2. Suala la magari yasiyozingatia sheria jibu lake wanalo askari wa trafiki. Sheria tayari zipo, wao wafuatilie tu utekelezaji. Eti trafiki anapokuta magari yamefanyiana usenene badala ya kuwalima jamaa anaanza kuhangaika kuwakwamua. Wot foo? Walimwe hao watu tuone watalipa hizo ishirini ishirini mara ngapi kabla hawajatia adabu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2009

    HUWEZI AMINI LAKINI UKIFIKIRI UNAKUWA UNAUMIA ZAIDI KWA NINI TANZANIA INAKUWA NCHI KAMA HAINA WATU WASIOFIKIRI AU HAWAKWENDA SHULE,MIMI PAMOJA NNA ELIMU YANGU NDOGO NINAJUA KUWA MIPANGO MIBAYA NA RUSHWA ILIYOKIDHIRI NA UFINYU WA KUANGALIA WENZETU NCHI NYINGINE WANAFANYAJE AU MIPANGO YAO BARABARA IPOJE.NA KWAMBIA TEGETA,UBUNGO NA TABATA ISINGELIKUWAWPO FOLENI,MUHIMU NI KUWA KUWE NA BARABARA KUTOKA TEGETA KUTOKEA MBEZI YA MOROGORO ROAD ITAKAYOKWENDA KUUNGANA NA PUGU MPAKA KUUNGANA NA KILWA ROAD MPAKA KONGOWE HARAFU KUUNGANA NA KIGAMBONI KUSINGELIKUWA NA HIZI FOLENI.NAAMINI HIVYO KWA KUWA MTU WA TEGETA AU BAGAMOYO ANAYETOKEA MOROGORO,KIBAHA,NK LAZIMA AJE UBUNGO VILE VILE KWA MTU ANAYETOKEA AIRPORT ,MTWARA,KILWA,KILWA ROAD,NK ANAENDA TEGETA LAZIMA APITIE UBUNGO JE FOLENI ZITAKWISHA .AFADHALI TEGETA FOLENI NJIA YA UBUNGO SIKU HIZI SI JIONI AU ASUBUHI INAANZIA KIMARA ,TANZANIA INAHITAJI KUBADILIKA VIONGOZI WAKUBALI MAWAZO YA WATU WENGINE SIO WAO WANAFIKIRIA WATATAJIRIKA NAMNA GANI????

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 08, 2009

    Tumeshazoea,tunataka tuwahi twende wapi?? Acha foleni hizo ziwepokwani sisi wengine twaweza kujiajiri kwa kupua,biashara ndogo ndogo,utalii(vijiwe).Eti barabara ziongezwe! Hizo zilizopo zenyewe zinatushinda kuzidhiti,gari zikienda kasi tunaweka matuta eti kuzuia ajali ebu chukueni takwimu muone kama kweli ajali zimepungua na hasara gani tunapata kwa kufanya hivyo.Jamani kazi bado ipo kama kweli tunataka kuondosha haya matatizo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 08, 2009

    Jamani huyu aliyeandika hii taarifa naye namshangaa, hicho kituo kikubwa cha mabasi hapo tegeta kibaoni kiko wapi?! Unapajua vizuri tegeta?!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 08, 2009

    Hiyo tisa, temblea njia ya kwenda Gongolamboto, FOLENI YAKE ilikuwa inashindana na njiaya Mbagala, ingawaje Mbagala siku hizi wanapeta.
    Jioni ukienda njia ya Gongolamboto ujue utakaa foleni ya zaidi ya masaa mawili??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...