MILLVINA DEAN 1912-2009
Millvina Dean afariki dunia, huyu ni mhanga wa wa mwisho kufariki kati ya wahanga waliosalimika katika ajali ya Meli ya Titanic iliyotokea mnamo 15 April 1912.
Mdau Kipatimu Kilwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2009

    Inamaana alikua na umri wa miezi minne au less ajali ilipotokea.?
    sidhani kama ana kumbukumbu yeyote kuhusiana na tukio.

    ReplyDelete
  2. wewe hapo juu 100:0am huyu kipind hicho alikuwa infant kwa kifupi naye alidithiwa na jamaa zake lakini madam kwenye tukio aliopolewa ndio chanzo cha kusema hivyo ungana na hiyo link upate maelezo sahihi kaka ni hayo tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2009

    Mkuu wa Wilaya ya Nanihii..... Huyo Bibi ni Manusura (aliyenusurika). Wahanga ni wale wanaojitolea muhanga. Hata kule Mbagala watu walikuwa wanasema wahanga wa Mabomu lakini tunasahihishwa kuwa wale ni manusura. Sijui kipi ni kipi! kwa wengine kiswahili tumejifunzia shule. ni lugha ya pili.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2009

    yanatuhusu nini???

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2009

    mie napenda tuu kusema ya kuwa, nashukuru tuna MICHUZI BLOG ambayo inarusha habari za maana na za uhakika za dunia nzima. sio kama ile ya ZE UTAMU ambayo ilikuwa ikiwa zalilisha wananchi, pamoja na kwamba baadhi ya habari walizokuwa wakitoa za SERIKALINI ni za kweli, ikiwamo na barua za siri za ndani ya serikali mnakumbuka ile barua ya waziri Lawrence Masha. Ambayo ni wazi hawa walikuwa na uhusiano wa karibu na watu wa ndani ya serikali, kwani wangepataje habari na barua kama zile? mambo mengine ni ya upuuzi tu ambayo hatuna haja ya kuyajua kwani yalikuwa hayaleti manufaa yeyote katika jamii yetu, mafano mwezi April walitoa habari za jamaa wa UK aitwaye KASSIM KALLING alipokuwa arrested kwa kufanya dodgy businesses, na kuwa ni mlea watoto tu hana kazi, pamoja na story ya MAILANIE BATIHO BUZWILILI aka PITCHI, kwa kumponza rafikiye na udokozi wa marks and spencer, wakati alijifungua alikuwa akienda woodgreen na kupata shoppingi ya nguvu bila kulipa, na kwamba familia yao wana mkosi kwani waume zao wote walikuwa na biashara nzuri na mapesa, ila punde baada ya kuoa kwenye familia hii wanaume wao wote hawana kazi ya maana na wamedidimia kipesa, hata huyu wa hapa B.O.T pia mumewe ni hivyo hivyo ilieleza ZEUTAMU. sasa jamani YOTE HAYA NA MENGINEYO HAYAHUSU KUJENGA UCHUMI WETU. Natumaini kuwa watawapata wamiliki wa blog ile. NA WOTE MNAOTARAJIA KUFUNGUA BLOG, JAMANI OMBENI MPEWE SOMO NA MICHUZI, SIO MNAJIFUNGULIA TUU, KWA NIA YA UPUUZI. MICHUZI NI PROFFESSIONAL JOURNALIST, ANAYEHESHIMIKA, KAMA MNAVYOONA HABARI ANAZOLETA NA PICHA NI ZA UHAKIKA NA ZINA-COVER DUNIA NZIMA. naomba muombe awape mawaidha na hata KUWAPA TRAINING, MAANA NAJUA WAZI UWEZO HUU ANAO.
    KEEP UP THE GOOD WORK, MICHUZI.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2009

    Alikuwa na wiki Tisa tu tangu azaliwe wakati ajali inatokea. Baba yake alifariki katika ajali hiyo. Wakati ule waingereza walikuwa na ile busara ya ''lady's first''. wakati abiria wa meli walipokuwa wakiokolewa na kuingizwa kwenye zile boat za kuokolea maisha ''lifeboats'', kapteni wa meli aliamrisha kuwa wanawake na watoto ndio waanze kuingia kwenye boats zile za kuokolea maisha. hapo ndipo haswa huyu bibi wakati huo akiwa kichanga wa wiki 9 tu alipopata nafasi yeye na mama yake kuingia kwenye boat. boti zilikuwa hazitoshi kwa hiyo zilipoisha basi wale waliokuwa wamebaki wooote walikufa na maji akiwemo baba mzazi wa huyu bibi. ukumbuke wengi wa waliokufa ni wanaume sababu ya ile ''ladies n' children first''.
    Ukisoma story ya hiyo ajali ni ndefu na inasisimua sana. Inasemeka waingereza wakati huo walikuwa ni watu waastarabu sana pengine kuliko wote. sasa mle melini kuliwa na wamarekani pia wao hawakuwa wastaarabu. wakati wa kugombania kuingia kwenye lifeboats kapteni wa meli alikuwa akisisitiza ''be british be british boys!!!'' waingereza kwa ustaarabu wao walipanga foreni kama kawaida yao, lakini wamarekani hawakutaka makunyanzi wao na hawakuwa na muda wa kupanga foreni wao walifight na kuingia kwenye boats kwa wingi, inasadikiwa kuwa hiyo ndio sababu ya waingereza kufa wengi zaidi kuliko wamareka katika ajali ile!! huyo bibi alikuja kusimuliwa tu akiwa na miaka 9!! lakini alipata kuwa mtu maarufu UK na alikuwa kivutio hata cha watalii na watu ambao huwa hawaamini kama kweli kitu titanic iliwahi kuwepo au ni stories tu.
    Nenda wikipedia utapata simulizi nzuri sana yani full mkanda wa titanic accident chanzo na mauzauza yote. inavutia na kusisimua kwa kweli.
    Macmuga

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2009

    Tatizo sio kukumbuka ni Rekodi zao wanaweka Pengine alikuwa mtoto Mzazi wake aliokoka naye wanaandika mwanangu jina fulani wa fulani inawekwa kwenye kitabu. MV bukoba sijui kama waliandikisha majina ya watoto? michuzi itabidi uchunguze. na mbona hatukumbuki siku za MV bukoba au Train zile?. Jumbe.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2009

    and why is this relevant to us then ?
    At least ingekuwa MV Bukoba ingekuwa more relevant.
    Hope there is any records of that at all !

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2009

    Kweli British zamani walikuwa watu waliosoma na wastaarabu. Ila sio sasahivi sio British tena watoto wak iengereza wamekuwa wabishi hawasomi bora hata nchi yetu unaweza kusema mbele itakuwa na maendeleo British ndio basi tena wasubiri Vita, tuone watu watavyorudi kwao Tanzania. Titanic ndio nini? Kanumba mungu akipenda subiri Miaka mitatu ukiwa hai Toa Filamu ya MV Bukoba. Ili tujue tukio na siri zengine. au fanyeni Documentary ya Mv Bukoba. Seif.

    ReplyDelete
  10. Baba UbayaJune 01, 2009

    huyu kikongwe juzi juzi tu alipigiwa harambee na wahusika wa ile sinema ya Titanic ili kusaidia kulipa deni la nyumba ya kuhudumia wakongwe.mungu mkubwa,hadaiwi na mtu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 01, 2009

    Anony 12:29
    Ni Professional sio Proffessinal

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 01, 2009

    huyo bibi alikuwa na miaka 20 au chini kidogo meli ilipozama,ukitazama sinema yake ndio utaelewa alikuwa msichana wa familia ya kitajiri,sasa atakuwa ana miaka 100 na zaidi,watu msionge tu kama hamjui ana umuhimu gani huyo ni shujaa kwa wakati huo

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 02, 2009

    Anon waTarehe June 01, 2009 8:12 PM

    WEWE NDIO USIONGEE KAMA HUJUI KILICHO ANDIKWA HAPO, UNAYESEMA WEWE MWENGINE KABISA AMBAYE NDIO WAMEFANYA MOVIE YA STORI YAKE. HUYU BIBI KAZALIWA FEB 1912.

    HAWEZI KUWA NA UMRI WA MIAKA 20 WAKATI HUO, HUYU ALIKUWA KATIKA WALIOOKOKA WACHANGA.

    AJALI ILITOKEA APRIL 15 hapo ukisoma kwahiyo alikuwa na Miezi tu MIWILI.

    Jamani ya MV BUKOBA TUWEKEENI PIC.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 02, 2009

    Anony 12:29.
    Hongera kwa mawazo yako finyu. Ulichoandika hakina mtiririko naona ulikimbia uchambuaji wa vitabu kama vile Shida, Ngoswe na vinginevyo. Issue yako ni irrelevant na Titanic na Ujumbe uliofikisha ni kuisifia hiyo blog kwamba may be ina watu wa serikali.
    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 02, 2009

    anoni wa 8:12 u,esoma hadi darasa la ngapi??? ni mashaka nawewe inawezekana kabisa kuwa ulikimbia umande wewe!! si kawaida!!! unajua kusoma lakini?? kama unajua kusoma basi hebu chukua muda kidogo upitie hiyo linki uliyopewa na michuzi chini yz picha!!! usituletee mambo ya sinema hapa!!! yani unawa kisinemasinema tu!!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 02, 2009

    je mnajua kwamba ajali ya meli ya TITANIC ilikuwa planned itokee na freemasons?.Kama ujui soma kitabu kinaitwa 'the secret terrorist'

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 02, 2009

    weee annon 3.10am koma tena uishie apo wee hater kazi kumpenda-penda MASHAKA tu,anahusiana nini na ili dubwana??nyambafu

    na wee 8.59am secret terrorist gani,freemasons ndo nini??usilete paukwa pakawa apa

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 03, 2009

    anoni wa 1:41 PM si ungekubali yaishe tu?? we huoni jinsi ulivyochemka pale juu?? ulikurupuka tu ukarukia ishu hata bila kuijua!! wenzio wanaongea reality wewe unaleta za kisinemasinema!!! ndo maana wamekuuliza umesoma lakini?? umefikia darasa la nagapi!! manake bro michuzi amekupa linki pale chini kuifuatilia hutaki ukabakia kuchemka na sinema zako!! wakati watu wanasoma vitabu na majarida kujua uhalisia wa dunia wewe unajitanua kwenye sofa ukiangalia sinema halafu unakuja ku-argue kwa kutumia ulichokiona kwenye sinema!!!
    halafu hata michuzi mwenyewe ulimfanya hajui ameposti nini??
    acha wakushambulie wanakuelimisha na kukupanua mawazo.
    ni hayo tu!
    ahsante
    Juma Ndachao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...