MAVUMBI AKIWA STUDIO
MAVUMBI NA ALI KIBA WALIPOKUWA STUDIO WAKIREKODI "JISOGEZE"

SEEWEAR STYLE & GAMILY PRODUCTION WANAYO FURAHA KUWALETEA MSANII MPYA WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA "BONGO FLAVA" MAVUMBI. MSANII HUYO ALIONEKANA KWA MARA YA KWANZA KATIKA SHOW YA ALI KIBA ILIYOFANYIKA NAPOLI, APRIL 25, MWAKA HUU.
MSANII MAVUMBI ANAWALETEA WAPENZI WA BONGO FLAVA SINGLE INAYOITWA "JISOGEZE" AMBAYO IMETENGENEZWA KATIKA STUDIO YA NAPOLI ITALY.
KATIKA SINGLE HIYO,MAVUMBI AMEMSHIRIKISHA MSANII ALI KIBA.KWA MUJIBU WA MANAGEMENT YA MSANII MAVUMBI SINGLE HIYO ITAANZA KUSIKIKA KATIKA REDIO STATION ZA EUROPE NA TANZANIA,NA ITAFUATIWA NA VIDEO CLIP AMBAYO IPO KATIKA MATAYARISHO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2009

    mbona studio haina kelele absorbers? namna hiyo nyimbo hazitoki utamu sana, zinakuwa na unwanted foreign noises. kila kitu ni hatua, pole pole tutasogea

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2009

    Studio wasiwasi hiyo, hapa bongo tuna studio babu kubwa zaidi ya hiyo,Njoo mwenyewe ujionee,Mdau Jiji la maraha Dar es salaam.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2009

    Studio Marekani...agggg acheni utani

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2009

    Studie Majuu makubw ahahahhahahah nyumbani kwa mtu ana ka mixer na ka mic anadanganya watu studio ili?Anaubavu kuingia studio Ughaibuni???Ali Kiba rudi nyumba urekodi wanakudhalilisha sasa chumbani kwa mtu mnaita studio yote hiyo uonekane umerekodi ughaibuni????????????????

    krs
    Pitt,USA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2009

    MAMAAAA???CHINGA KACHOKA KUBEBA MABOX KAAMUA KUWA MWANAMUZIKI????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2009

    Ili mradi waseme CD hii ilirekodiwa marekani. MhhHHHHHHH

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    Watanzani mliotoa maoni yuu yangu,acheni wivu, acheni kuongea negative.sijui studio nini,sijui mbaya,bla bla bla. kwanini msiwe positive? mpeni basi nyie studio ambayo mnaona inafaa na bomba. be positive,jiangalieni wenyewe,nyie mnafanya nini katika maswaala ya muziki?je,mna studio bomba zaidi ya hiyo?muiteni basi kwenye hizo studio zenu alipie kurecord.

    Guys, be positive on other's citizens achievements. Wivu muache.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...