Marehemu Mama Mary Donata Watondoha


Tunapenda kutoa shukrani kwa wote walioshiriki kwenye msiba wa mama yetu mpendwa mama mary donata watondoha amefariki tarehe 29/05/2009 na kuzikwa tarehe 01/06/09 kwenye makaburi ya ukuta kinondoni.


Sisi watoto wa marehemu tunatoa shukrani kwa watu wote walioshiriki kwa hali na mali kuanzia kuumwa kwakwe mpaka kupatwa kwake na mauti na kukamilisha safari yake ya mwisho ni ngumu kuwataja majina moja moja kwa maana hiyo ningeomba kuwapa asante sana toka moyoni kwetu kwa wote walioshiriki nikiwataja wachache:

Madaktari wa Aghakhan hospital na Muhimbili Hospital,
Padri Tegete Paroko msaidizi wa parokia ya UKonga
na wanajumuiya wa parokia ya ukonga
wanajumuiya ya SEGO
CCM-mkoa wa dar

Na wengine wote ambao sikuweza kuwataja hapa ila mchango wao ndio tumeweza kufanikisha kila jambo.
Bwana ametoa na bwana ametwaa
Jina lake litukuzwe
Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie
Apumzike kwa Amani.
Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    R.I.P mama you sure will be missed, what a loss.
    Christine.

    ReplyDelete
  2. Mimi namkumbuka sana huyu mama Watondoha alikuwa Mwalimu wangu wa Sekondari, Mwenge, Singida katika miaka ya 70 na Mungu amependa kuchukua kiumbe chake. Mama ulale mahali pema peponi. Amen.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2009

    R.I.P Mama ni kweli we will miss you mama. Mungu wajalie heri watoto wake Eddy, Rose, John na Grace, twajua ni jinsi gani inaumiza twawaombea kwa mungu awape nguvu.

    ReplyDelete
  4. Mama ametutangulia na sote tu njia moja. Namkumbuka sana mama tangu mimi na Grace tukiwa wadogo sana Mtwara those days. Poleni sana Grace, Rose, Eddie na John. RIP mama. Always, Colle

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2009

    Pole sana Grace kwa kuondokewa na Mama.Mungu akupe nguvu. RIP mama.
    Athy.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2009

    Kwa kweli ni pigo kubwa sana, lakini hatuna jinsi mungu aliumba na mungu ametwaa. Tunachoomba mwenyezi mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu na naamini kwa matendo yake aliyoyaonyesha akiwa duniani naamini atafika peponi tu. Mama seif.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2009

    Kwa kweli ni pigo kubwa mno katika familia, kwa upendo aliounyesha, kwa ushauri na mengine mengi, lakini tutafanyaje kwani mungu ndiye aliumba na mungu ndiye ametwaa cha msingi ni kumuombea kwa mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Na naamini kwa matendo yake mema aliyoyaonyesha akiwa duniani ndiyo yatakayomfikisha peponi. Khadija

    ReplyDelete
  8. H.M.J.MassoudJune 05, 2009

    R.I.P Mama Watondoha, nakukumbuka kwa busara zako na uongozi uliotukuka pale wizara ya Elimu na Utamaduni tulipofanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu. Mola akuweke mahali pema peponi- Amen

    ReplyDelete
  9. Duh! ni huzuni kuondokewa na mama Watondoha.

    Pole sana kwa familia yote.Naamini nipindi kigumu,lakini kwa uweza wa Mungu azidi kuwafariji na kuwatia nguvu.

    Tulimpenda mama yetu,na Mungu wetu kampenda zaidi.Mwenyezi Mungu iaweke roho ya mama yetu mahala pema peponi.Amina

    ReplyDelete
  10. I will surely miss you auntie...may the Almighty rest your soul in eternal peace.... pole sana Rose, Grace, John na Eddie...May God comfort you during this tough time....
    Irene

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2009

    Huyu Mama alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam enzi za Mwinyi? RIP

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2009

    mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina nimeona jina nakumbuka mama watondoa alikuwa mkuu wa wilaya ya mtwara 1987 tuliishi mtaa mmoja shangani alaf akaamishiwa kuwa mkuu wa mkoa wa lindi. pole sana grace nakumbuka we used to play together me you and ratifa. poleni sana katika wakati huu mgumu wa majonzi ya kumpoteza mama.

    khadija.m

    ReplyDelete
  13. Poleni sana akina Grace na Joshu kwa msiba mzito, pamoja na sisi akina Kalembo wote. Tumempoteza mama hakuna mfano wake, Mungu amweke mahali pema peponi. Amen

    Luitfrid Peter Nnally Nyaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...