Na Mwantanga Ame--Zanzibar leo,
JUHUDI za uokoaji wa Meli ya MV. Fatihi, iliyozama katika Bandari ya Zanzibar zimefanikiwa kuiondosha kutoka sehemu ilipozama na kuisogeza mbele kidogo.
Hatua hiyo inaleta matumaini ya kuwepo uwezekano wa kurahisisha juhudi za kuibirura ili kuwatafuta maiti waliosalia kwenye meli hiyo.
Meli hiyo ilizama mwishoni mwa wiki iliyopita katika Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati na kusababisha watu sita kufariki na wengine 33 kunusurika.
Kazi ya uokoaji inayowashirikisha Vikosi vya Jeshi la Ulinzi , Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM) na wataalamu mbali mbali jana iliingia siku ya tano huku juhudi zikiendelea.
Usogezwaji wa meli hiyo ulifanywa kwa kutumia ‘tagi’ ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) iliyowasili rasmi kusaidia juhudi hizo za uokoaji kushirikiana na ya Shirika la Bandari Zanzibar.
Hata hivyo, ‘tagi’ hiyo ya TPA ilipata hitilafu na kushindwa kuifunua meli hiyo, pale jenereta lake lilipogoma kuwaka kwa muda. Hatimaye ilipowaka kazi iliendelea vyema, na baada ya mafanikio hayo ya kuisogeza kidogo bidhaa kadhaa zilizokuwemo kwenye ajali hiyo zilishuhudiwa zimetawanyika na kuelea baharini huku kukiwa na harufu kali ya kuhanakiza katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Bandari Zanzibar, Abdi Omar Maalim, alisema kwa kiasi fulani zoezi hilo limeweza kufanikiwa .Alisema kazi hiyo inafanywa kwa vile bado upo wasiwasi kwamba wapo watu zaidi wanaweza kupatikana kwenye meli hiyo.
Alisema iwapo itashindikana kuenuliwa itabururwa kwa kutumia ‘tagi’ na kuwekwa mbali na eneo la bandari.
Alieleza kwamba hivi sasa baada ya juhudi za siku nne jana kuna dalili kubwa ya kuwepo mafanikio ya kazi za uokoaji kukamilika.
Awali jana Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi akiwemo mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), David Mwanyange, walitembelea Bandari hiyo na kuzungumza na Kamati ya Maafa ya Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema, alisema tukio la kuzama meli hiyo ni la kusikitisha na litoe fundisho kwa Viongozi wa Shirika hilo kuandaa mazingira bora ya kunusuru majanga kama hayo.
Nae Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamnyange, aliwataka askari katika kikosi cha uokozi cha JWTZ, chenye wapiganaji 30 kufanya kazi vizuri kwa kuwa ni sehemu ya jukumu lao.
Alisema Askari hapashwi kutumika katika vita pekee na ndio maana jeshi hilo likaitwa ni la wananchi wa tanzania na sehemu ya uokozi katika majanga ni kazi zao.
Hadi tunakwenda mitamboni vikosi vya uokoaji viliendelea na juhudi hizo kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanikiwa haraka iwezekanavyo.
Jan SMZ imesema mmiliki wa meli atalipa gharama zote za uokoaji, jee ataweza? jee meli ilikuwa na bima ya kinga kama hiyo, jee familia za waliokufa na mali zao kupotes nao watafidiwa vipi na nani? wataalam wa sheria na mambo ya usafirishani tafadhalini toeni mawazo yenu
ReplyDeletendiyo maana kila siku tunasema acheni kushindana na majeshi ya rwanda na uganda ktk ufundi wa kuharibu maisha na mali.
ReplyDeletejeshi letu liwezeshwe kuwa mahiri na wajuzi ktk masuala ya ufundi, utafiti, kuzalisha mali, na shughuli za UOKOAJI.
nilishangaa wanajeshi wetu walivyopelekwa Comoro mmoja wao alizama na hakukuwepo mtu yeyote wa kumuokoa.
waasi wa Wacomoro wangetulia timing tukiwa bado baharini basi tungepoteza kikosi kizima.