Tafsiri Isiyo Rasmi ya Makala ya John Mashaka
Na US Blogger
Baada ya kusoma makala ya John Mashaka na maombi ya wadau kutaka makala iwe imeandikwa kwa lugha ya kwanza ya taifa, yaani Kiswahili, nimeona nijaribu kuandika ‘tafsiri isiyo rasmi’ juu ya yale yaliyoandikwa na John Mashaka ili wenzetu waliolalamika nao waweze kunufaika. Ninaamini kwamba tafsiri yangu itakuwa na kasoro za hapa na pale kutokana na ukweli kwamba lugha ya Kiswahili bado ni changa kulinganisha na Kingereza pamoja na uwezo wangu wa kutafsiri ambao bado unahitaji kuboreshwa. Kasoro za kiasilia zitakuwepo kwa hiyo ninawasihi wasomaji waangalie zaidi ‘maana kwa upana’ badala ya ‘tafsiri ya neno moja moja’.
Kuporomoka kwa uchumi, isafishe watumishi wa umma walio wavivu na wasio watendaji? Mdahalo:
Mwanzoni mwa majadiliano yetu kuhusiana na mgogoro wa kiuchumi, wasomaji wetu wengi walipinga ukweli kwamba nchi yetu, Tanzania ingeathirika kiuchumi.
Kama kawaida, waandishi walipakwa kama watu wasiofahamu hali halisi ya nchi kwa kuwa Tanzania ilikuwa na kinga dhidi ya migogoro, kwa kuwa haipo ndani ya mfumo wa fedha wa ulimwengu.Wengine walidai kwamba mgogoro ulikuwa ni wa mataifa ya magharibi na kukataa uweli ulio wazi wa utandawazi.
Leo hii bila ya mashaka yoyote, sote tunaona jinsi mgogoro wa kiuchumi unavyotuathiri na kuikamua Tanzania.
Pamoja na kwamba fumbuzi mbalimbali zililetwa ikiwemo kushusha viwango vya riba mwanzoni mwa mgogoro, leo hii Tanzania bado ni miongozi mwa nchi zenye viwango vikubwa vya riba.
Watumishi wetu wa umma wakiwemo wabunge inaonesha wako kwenye mfadhaiko na hawajui la kufanya juu ya mgogoro. Sekta ya utalii imeadhirika, uzalishaji viwandani umekaribia kufa, sekta ya kilimo ipo katika ‘sakaratul mauti’ ikihitaji msaada kutokana na kuanguka kwa soko la bidhaa.
Sekta ya huduma inapunguza wafanyakazi kwa kiwango cha kutisha na hapohapo inajaribu kujipanga. Na pale ambapo uchumi mkubwa kama ule wa Jimbo la California wanapoanza kutoa ‘hati ya kudaiwa’ kwa wadai wake badala ya kulipa madeni yaliyofikia wakati wa kulipwa, kwa yule aliye makini ataanza kunusa harufu ya matatizo katika upatikanaji wa misaada ya nje. Uporomokaji wa sekta nyingine tunabaki kusema Mungu tusaidie.
Tanzania imebarikiwa na Bunge la wasomi wenye shahada za PhD ambalo tulitegemea lingechukua maamuzi ya haraka kupitia midahalo yenye hoja nzito na fikra ili kuokoa uchumi kutokana na kuzama zaidi. Tulitegemea wabunge wetu walio wasomi wangekuja na mikakati ya kudhibiti ama kuepusha hali hii.
Bunge lililobobea kwa wasomi tulitegemea japo wangepitisha ‘miswada ya dharura’ kuharamisha mtindo wa ‘kukopesha kiwindaji’ ama ‘kibaguzi’ ama taratibu nyingine za utoaji wa mikopo kwa umma.Juu ya yote wangelazimisha mabenki ya kibiashara yapunguze viwango vya riba ikiwa kama ufumbuzi wa muda mfupi .
Benki Kuu za nchi mbalimbali duniani zimejaribu kadri ya uwezo wao kupunguza viwangi vya riba kama hatua muhimu kudhibiti mporomoko wa uchumi.Benki kuu ya Uingereza imepunguza riba na kuweka rekodi ya kihistoria kwa kuwa na riba amabayo ni karibu asilimia sifuri. Hazina ya Marekani imeshusha riba hadi asilimia 1. Kwa upande mwingine, wakopaji wa Tanzania wanalazimika kulipa riba ya kama asilimia 30 na baadhi ya watunga sera na wataalamu wetu wa maswala ya uchumi na fedha wameamua kutochukua hatua kwa malengo ya kukidhi ‘usahihi wa kisiasa’ badala ya kupigia debe kushusha kwa riba ili iwe chachu ya kukua kwa harakati za uchumi nchini.
Haiingii akili kuona taifa changa lenye uchumi dhaifu kuwa na viwango vikubwa vya riba. Haileti maana kiuchumi kumfanya muuza mboga alipe riba ya asilimia 20. Taratibu za namna hii katika hali ngumu ya kiuchumi hutafsiriwa kama ‘ukopeshaji uwindaji’ ama ‘ukopeshaji wa kibaguzi’.
Vilevile ninatafsiri kwamba benki nyingi za Tanzania zina malengo ya kuhudumia wale walio na uwezo wa kiuchumi, mashirika makubwa na wateja walio mamilionea wanaofaidika kutokana na viwango vya chini vya riba ukilinganisha na wananchi wa kawaida. Katika nchi zilizoendelea kiuchumi, wakopaji wenye uwezo mdogo wa kurudisha mikopo, kwa nadra sana hutozwa asilimia 20 na watunga sera huangalia ama huchunguza chanzo cha riba za kiwango hicho.
Ninakubaliana na Dr. Hildebrand Shayo kwa mtazamo wake kwamba nafisi (matumizi kuzidi mapato) ya bajeti itaongezeka katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka wa bajeti wa 2010/11 na hii itakuwa na athari kubwa juu ya mfumuko wa bei, viwango vya riba n.k.
Kwa kweli itatokea, na wingu jeusi linaloelea juu ya vichwa vyetu linatisha. Baadhi ya wabunge wetu watalazimika kutambua hali halisi badala ya kuamini kwamba umma hautafahamu kwamba wao hawana faida.Wananchi lazima tuamke na tudai kutoka kwa wabunge wetu rekodi ya kazi walizozifanya kwa kulinganisha na ahadi zao kwa wapiga kura kabla hatujawafikiria kuwapa nafasi za kuwa wagombea ili watetee maslahi yetu; hapa ni maslahi ya kiuchumi na kijamii.
Pamoja na kwamba hawa wasomi wana shahada za udaktari wa filosofia, bado wana ‘ulemavu wa kitaaluma’ na hawana fikra juu ya nini kifanyike ili kudhibiti huu mgogoro wa kiuchumi, wana wajibu wa kufafanua na kuwaelezea wapiga kura wao kwa uwazi na kinagaubaga jinsi ambavyo ridhaa ya miaka 5 waliopewa ilivyotumika kuboresha majimbo yao kabla hawakupewa tena ridhaa na wapiga kura kuendelea kuongoza.
Mkakati wao wa kutofanya lolote unaoumiza nchi na usiendelezwe,mfano ni Tarime ambapo wananchi wasio na hatia wanakufa kwa sababu chanzo chao cha maji safi kimechafuliwa na kampuni ya uchimbaji madini na Bunge limekuwa bubu juu ya hilo.
Tanzania ni nchi pekee ambayo mwanasiasa anaweza kutojali wapiga kura wake, kuwarudia na kuwatuhumu wapinzani wake, kupinda ukweli, kuwahonga na kuchaguliwa pamoja na kutofanya lolote.Sehemu nyingine duniani wenzao huchaguliwa kutokana na utendaji wao wakiwa kama watumishi wa umma. Wale waliozongwa na kashfa na rushwa, huwa wanajing’atua ama huamua kutogombea tena nafasi zao.Watanzania wengi wanatakiwa kudai uwajibikaji wa kiuchumi na kijamii kutoka kwa viongozi.
Ndani ya huu mgogoro wa kiuchumi, tusishangae kuona baadhi yao wakipanga mikakati ya kurudiwa kwa EPA (EPA number 2) ambayo itawakikishia fedha za bure za umma kwa miaka mitano pamoja na viti vya kusinzilia huko Dodoma.Kama itakuwa hivyo, Tanzania kwa hakika itaingia katika janga la kiuchumi kama la Iceland.
Hawa viongozi wanaoamini kwamba watakuwa madarakani milele na pengine kuwarithisha watoto wao, lazima wawajibishwe kupitia katika sanduku la kura, na wakati wa kufanya hivyo ni sasa kwa kuangalia kwa umakini kabisa sifa na uwezo wao, hii ni fursa bora zaidi katika kuwasafisha katika hili wimbi zito la kiuchumi.

Duuh kuna watu mna muda kweli. Watu sio kwamba hawajui kiingereza bali wanataka kuua kasumba za kudhania kuwa lugha ya kiingereza ni bora kiswahili.
ReplyDeleteTatizo watanzania kuongea kingereza wanaona ni maendeleo. Au kuandika kingereza wanaona ni maendeleo.Ndio maana tunaona watu wanatumia bombastic words ili kuonyesha hayo maendeleo. Tunapenda kudharau lugha yetu.
Tujifunze toka kwa wenzetu Wachina, Wajapani, Wajerumani na mataifa mengineyo mengi ambayo yanazipa kipaumbele lugha zao.
Nakumbuka nilishawahi kusikia stori kuwa Waziri Mkuu wa Pakistani alienda kutembea Uingereza. Aliporudi Pakistani akaulizwa na waandishi wa habari je anadhani ni kitu gani amekiona Uingereza ambacho anadhani ni siri kubwa ya maendeleao ya nchi hiyo. Waziri Mkuu akajibu kuwa ni kuongeza kingereza. Akasema Uingereza hara mtoto wa miaka mitano anaongea kingereza :)
Enewei,Waafrika bado tuna safari ndefu sana. Tatizo kubwa tulilo nalo ni la kisaikolojia. Hatutaweza kupiga hatua kama tusipolitatua hili tatizo.
Tipu Tip
Asante sana US BLOGGER. Kila siku huwa nasoma makala za mashaka halaf nikisoma comments za watu ndio nachoka kabisa.
ReplyDeleteMakala zake siku zote huwa ni za kawaida sana tu, na kwa tafsiri hii wenye akili mtaona na kuelewa kwamba huwa zinakuwa mbwembwe za kimombo ndio zinamfanya yohana kuwa na wafuasi wengi kwenye dini yake lakini ukiangalia kwa undani zaidi, hakuna lolote linalosemwa ambalo halijasemwa kabla yake.
Asante sana kwa tafsiri.. Manaake dhamira yako nimeipata vilivyo. Na hii ni kuwashtua tu wale wasiokuwa wanaelewa huyu jamaa ni nani.
TAFSIRI YAKO NI POTEFU WALA HAITAFSIRI SAWASAWA ARTICLE YA MASHAKA NA PIA HII JUU YA RIBA ILIYOPUNGUZWA NCHI ZA MAGHARIBI WATU WAJUWE WAZI NI RIBA KATI YA BENKI KUU NA MABENKI, NI KWAMBA BENKI ZIKIENDA KUKOPA BENKI KUU WATALIPA RIBA YA 0.5% NA SI RIBA KATI YA MABENKI NA WATU, NI HIARI YA MABENKI KUPUNGUZA RIBA ZAO HAWALAZIMISHWI KUPUNGUZA NA BENKI KUU, KWANI BENKI NI BIASHARA WANAPANGA RIBA KUTOKANA NA GHARAMA ZA UENDESHAJI KWANI WAO PIA PESA SI ZAO WANATAKIWA KULIPA WENYE PESA NA GHARAMA ZINGINE, PAMOJA NA RIBA KATI YA BANK OF ENGLAND NA MABENKI KUSHUKA NI BADO RIBA KATI YA WATEJA NA MABENKI IPO PALEPALE NI KUBWA PIA KAMA ILIVYO HUKO BONGO.
ReplyDeleteTUNGEPENDA TUWE NA WABUNGE WENYE PESA ZAO NA WANAOTOA HUDUMA BURE KWA WANANCHI BILA MALIPO YEYOTE. BWANA MASHAKA NATAKA UNIHAKIKISHIE KWAMBA UNA UWEZO WA KUWATUMIKIA WANANCHI BILA HATA KUWANYONYA KWA HAKI JASHO LAO.MAAMUZI BORA YANATEGEMEA MAADILI BINAFSI YA KUTOSHAWISHIKA KURIDHIA MIKATABA YENYE NIA YA KUWANONYWA WENYE NCHI. HIVYO BASI KURIDHIKA KIMAISHA NA KUTOKUWA NA TAMAA YEYOTE YAANI HATA CHEMBE YA KUJILIMBIKIZIA MALI ISIVYO HALALI NI NDIYO SIFA KUBWA YA VIONGOZI WATARAJIWA WATAKAYO IKOMBOA TANZANIA NA WATANZANIA
ReplyDeleteTANGAZO RASMI. HUYU US-BLOGGER ANAJIKOMBA KWA NABII MTAKATIFU YOHANA MASHAKA, JINIASI WETU NA RAIS MTARAJIWA 2015. US BLOGGER ANATAKA MASHAKA AKICHUKUA UONGOZI 2015 NAYE APEWE WIZARA NA YEYE.ANATAKA KUMFURAHISHA SHAKESPEAR ILI NAYE AONEKANE WAMO. RAIS MASHAKA, HAWA NI WATU AMBAO NI LAZIMA UWAOGOPE KAMA NYOKA, KWA SABABU WANAKUJA KUKUANGUSHA. DAKTARI SHAYO ANATOSHA KUWA NAIBU KAMANDA MKUU. MIMI NINAOMBA KAZI MOJA TU, KUWA DEREVA WAKO KUENDESHA YALE MABENZI YA IKULU TU, SAWA MKUU SIKU ZOTE TUPO WAFUASI TUNAKUTETEA HADI MWISHO KWA HIYO USIWE NA WASIWASI.ENDELEZA KUIHAMASISHA UMMA WA KITANZANIA, ASANTE SANA RAIS MTARAJIWA 2015
ReplyDeleteninachoweza kusema ni kwamba, mashaka na shayo ni DHAABU adimu kwa Tanzania, siyo wivu, ukweli lazima tuuite ukweli nimemaliza
ReplyDeletehivi US blogger, mbona umepoteza maana ya kila kitu mashaka alichokiandika? kinachonishangaza ni kwamba US blogger hatumjui. Huyu mtu ni jini na ningemuomba mashaka akaye mbali naye kabisa
ReplyDeleteKwako mdau uliyetafsiri atiko ya Mashaka kwa lugha ya kiswahili.
ReplyDeleteKwanza nakupongeza sana kwa kuuona umuhimu wa kuitafsiri kwani wadau wengi wangependa sana kuisoma kwa lugha hiyo kama lugha yao wanayoielewa vizuri.
Nina imnai kubwa kwamba hata mwandishi anashindwa kuandika katika lugha hiyo kwa mantiki kwambahana maneno mazuri ya kiswahili bali ana maneno ya kiingereza ambayo ndiyo amesomea fani hiyo ya uchumi.
Nakanusha kabisa kwa lugha ya kiswahili ni CHANGA.Aidha labda sijakuelewa una maana gani unaposema lugha ya kiswahili ni changa? Je ni changa kwa wewe au kwa kwa Mashaka ambaye hataki kuitumia lugha hiyo?Katika hilo kwa kweli umenoboa sana licha ya kwamba umefanya jambo jema la kutafsiri atiko hiyo katika lugha hiyo.Kuna wachumi wengi nchini kwetu ambao wanatoa mihadhara kwa lugha ya kiswahili kila wakati,lakini ninyi kukanyaga ughaibuni tu imekuwa nongwa kuibeza lugha yenu,Je utakumbuka hata lugha ya kabila lako?Hapa Minnesota University tuna idara ya kiswahili watu wanakisoma kiswahili kwa bidii, nimekuwa ujerumani vyuo vikuu fulani vinafundisha kiswahili wewe leo unatuambia ni lugha changa eti haiwezi kutafsiriwa kwa ufasaha.Mbona kiingereza chenyewe cha kunakirisha tu sijaona maneno yenu wenyewe ambayo mumeyaumba.Kiswahili kinakua na kuongezeka maneno mageni mengi.
hata hivyo nakupongeza kwa kazi nzuri uliyoifanya ili wengi washriki kikamilifu kuisoma na kuelewa nini mwenzetu huyo anasema juu ya uchumi nchini kwetu.
Ubaki na amani ya Bwana.
bado naendelea kuamini kuwa, ni bahati mbaya walio na access na internet na kuchangia hapa, wana upeo mdogo wa kufikiri, na baada ya kuchangia mada iliyombele hapo huishia kupondana ambayo haisadii.
ReplyDeletewengi ni watu walio frustrate na kukosa cha kufanya huku tuishiko ughaibuni.
Siku zote tafasiri yoyote huwa haibebi ujumbe uleule aliokusudia mtoa mada. hata hivyo kwa content za mashaka, ujumbe upo wazi kwa wananchi kuamka na kutumia kalamu zenu kuleta mabadiriko kwani uwezo upo mikononi mwenu. ujumbe mwepesi lakini wenye maana sana ,kuliko kuishia kulaumu viongozi mliowachagua wenyewe.
MUNGU MBARIKI, MASHAKA, SHAYO ,NA US BLOGGER NA WOTE WANAOITAKIA MEMA TANZANIA.
NINI MAANA YA BOMBASTIC WORDS, HAMNA KITU KINAITWA BOMBASTIC WORDS!!!!! UMETOWA WAPI HII.
ReplyDeleteNyie mnaojidai kwamba hamuelewi kiinglishi cha Mashaka mnajua dawa ni nini? Inabidi mvute Bangi , kunywa Mbege ay Gongo la nguvu matokeo yake mambo yatatiririka kama mto wami. Unajua ukilewa unakuwa na concentration nzuri sana. Unajuwa walezi ni dereva wazuri sana kwa hiyo chiinglishi cha mashaka hakitakuwa kigumu sana
ReplyDeleteShukurani kwa jitihada yako ya kutafsiri makala ya Mashaka ili wadau wengi tuweze kuelewa mantiki yake.
ReplyDeleteKuna kitu ambacho mwandishi bado hajakijibu. Sehemu kubwa ya makala yake inaungumzia serikali au wabunge wafanye jitihada za kuunusuru uchumi. Je ni jitihada zipi zinafaa kwa mazingira ya Tanzania? Hilo mwandishi amelikwepa.
Tumeona nchi zilizoendelea serikali zao zimeweza kutoa fedha za ruzuku kusaidia sekta zilizoathirika. Je hapa Tanzania hilo linawezekana. Kabla ya matatizo haya ya kiuchumi serikali (kwa ukosefu wa fedha) imekuwa ikitenga bajeti ndogo kwa sekta muhimu kama kilimo, afya na elimu. Je kama kabla ya mtikisiko wa kiuchumi hali ilikuwa hiyo, mwandishi anataka kutuambia kwamba serikali hiyo hiyo itaweza kusaidia sekta zake wakati huu?
Serikali inaweza kukopa nje ili kusaidia uchumi wake. Je huko watakakoenda kukopa wao vipaombele ni vipi, kusaidia uchumi wa Tanzania au kwao ambako uchumi umeathirika?
Sekta ya utalii inategemea sana hali ya uchumi wa mataifa mengine. Kama mataifa hayo hali ni mbaya ni wazi kuwa watalii wachache ndio watakuja Tanzania hata kama tukitanga vivutio vyetu kila kona ya dunia.
Do, ama kweli sasa mdahalo unakomaa. Ila ninapenda kuwapeni ukweli, kama alivyosema mdau mmoja hapo juu, John Mashaka na Dr Shayo ni dhamana kwa Taifa la Tanzania. Ninafikiri walio wengi wanalielewa hilo.
ReplyDeleteTatizo hawa vinaja wako nje ya Tanzania, na ingekuwa bora wakarudi nyumbani wakajichanganya na watanzania wenzao na halafu tujue ni kitu gani kitaendelea.
Ila nitajaribu kumuandikia mkuu wa TBC Tido Mhando ili aandae mdahalao ambao utawakutanisha Dr Shayo na Bwana Mashaka angalau viongozi wetu na wabunge wetu waweze kupta nafasi ya kuwasikia msimamo wao kuhusu ni njia gani bora ya kuisaidia Tanzania.
Unajua nikuambieni ukweli, kama Tanzania hatutakuwa tayari kuwapa na kuwatumia vinaja kama hawa na wengineo, basi mataifa yenye "AKILI" yatawachukua.
Si mnakumbuka prof. Lipumba alipokuwa Uganda? Mnaelewa ni kwa kiasi gani alimsaidia Rais Museven?
Huu ni mfano mmoja tu na iko mifano mingi
John mashaka, Dr hayo msikate tamaa, tupo nyuma yenu na tunawaunga mkono
Serikali ya kitanzania itakuwa ni serikali ya kipumbavu ikizidi kuwakumbatia mafiaadi na ma TX feki wakati Marekani na uingereza inafaidi rasilimali zetu Kama Mashaka na Shayo. Ni lazima tupige kelele warudishwe. Hawa vijana ni mali hasa kale katoto Mashaka. Mithupu mtumie JK ujumbe wetu bwana
ReplyDeleteMashaka na shayo msikate tamaa wapinzani wenu wanajua wazi kabisa uwezo wenu, na lengo kuu la US- blogger ilikuwa ni kupotosha wadau lakini umma umemshtukia tayari. Blogger man hacha wivu mashaka na shayo ni vijana wenye hadhi zao wewe hatukujui
ReplyDeleteUnayedai Mr. Blogger amepotosha kwenye riba unatakiwa usome tena atiko ya nabii.
ReplyDeleteAlichofanya nabii ni kuonesha riba ya benki kuu ya Uingereza na Marekani lakini hakuonesha riba ya BOT kwa benki za nyumbani. Hapo nabii hakutenda haki na kazi ya Blogger ilikuwa ni 'kutafsiri' na sio 'kurekebisha'kwa hiyo mpotoshaji sio Blogger.
Upotoshaji mwingine wa nabii upo pale aliposema Tanzania ni nchi pekee amabayo mbunge anaweza kuchaguliwa bila ya rekodi ya utendani. Huo ni uzushi wa nabii kwa sababu kuna nchi nyingi tu amabazo hilo lipo.
Mashaka na Shayo ni watu wa kawaida tu. Msifikiri kuandika makala humu kwa michuzi ndiyo wanaakili sana. Wapeleke makala zao kenye ''Journal'' zinazoeleweka tuone. Hapa kwenye blogg ya michuzi nani ana-review hicho kilichoandikwa zaidi ya watu wengi kushangilia kiingereza tu.
ReplyDeleteWapeleke makala zao The Economistsna kwingineko kwenye kwenye viwango vya kuchapisha makala.
Yaani kuto makala kwa michuzi humu basi mmeshawapa nafasi ya kuongoza nchi??
Ebo!!!!!!!!!!
Shukrani zukufikie mdau wa Tarehe Sun Jul 12, 02:37:00 PM. Umegonga msumari sawa sawa. Hilo ndio la kujadiliwa na mwandishi sio lawama na blah blah.
ReplyDeleteTATIZO YA GLOBU HII WATU HAWAPENDI TOPIC MUHIMU ZINAZOGUSA JAMII NA KUJARIBU KUCHANGIA HOJA KWA KUWEZA KUELIMISHANA.WATU WANATUMIA GLOBU HII KAMA KILEVI,NASEMA KILEVI NI KWAMBA MTU ANAKUJA HAPA AKIWA NA STRESS ZAKE KWAHIO ANAJARIBU KUFURAHISHA NAFSI YAKE KWA KUONGEA PUMBA.JARIBUNI KUBADIRIKA WATANZANIA HAMUEZI KUWA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU MILELE.
ReplyDeletemdau mzawa.
huyu US blogger kusema kweli ni jinamizi linalomuonea wivu mtakatifu yohana mashaka.mashaka na shayo ni malighafi za tanzania ambazo us blogger anajaribu kuharibu. huyu mtu inabidi afungiwe. sisi wafuasi na washabiki wa mashaka tupo kidete hadi ulingoni, yaanu kure ikuru 2015 tutkuwa tunapiga debe kidedea
ReplyDelete