HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI ZINASEMA KWAMBA KUNA MELI IMEKAMATWA BANDARINI DAR AMBAYO INASEMEKANA IMEBEBA MABOMU NA WATU WOTE WA HUMO MELINI WAMEKIMBIA NA KWAMBA HAKUNA SHUGHULI INAFANYIKA HAPO BANDARINI MPAKA SASA.
WAFANYAKAZI WA BANDARI IMEWALAZIMU KUAMBIWA WATOKE NJE YA BANDARI BAADA YA BOTI YENYE SPIDI KALI KUINGIA BANDARINI BILA IDHINI, KWA MUJIBU WA HABARI ZISIZOTHIBITISHWA BADO.
GLOBU YA JAMII INAFUATILIA KUTHIBITISHA HABARI HII NA ITAWAPASHA UKWELI WA MAMBO BAADAYE KIDOOOOOOOGO....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2009

    Duh!!! sasa naona tunaelekea kubaya....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2009

    Taarifa nilizonazo ni kuwa askari wa majini walikuwa wakifanya mazoezi na sio mabomu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2009

    Ni mazoezi hayo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2009

    Balozi wa naniii wewe kiboko sio mchezo unatupa vitu live poa sana . Naona mtandao wako wa habari ni mkubwa sana.Fuatilia uje utupe kilichotokea Nyumbani.Bahari zote mpya uwa napata kwako endeleza libeneke.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2009

    Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2009

    kaka michuzi mbona hii habari inatisha, hebu tuhabarishe aisee wengine tuko mbali na nyumbani na tuna ndugu wafanyakazi wa bandari

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2009

    Kweli nyie globu ya jamii,tunashukuru kwa habari.Hiyo imekuwaje lakini?tunasubiri more news.its me paulina.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2009

    Duh bongo inataka kuwa Baghdad! M/Mungu atusalim salama.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2009

    mbona umeondoa picha ya yule msichana wa kazi aliyetoroka kwa muajiri wake? tuambie kama mjadala umefungwa, manake tuko wengi tunaonyanyasa wafanyakazi wa ndani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2009

    SEMA HAKYANANI

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2009

    Dili ya mabomu mbona ni ya kila siku?Mabomu yaliyopasuka Mbagala tunajua mpaka siku yaliingizwa nchini na serikali inajua batch number na manufacturer.Siku Hosea akitoka usalama wa taifa hali itabadilika

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 08, 2009

    aya!!mengine sasa haya

    nini tena jamani hii nchi??ivi nchi zilizotuzunga na vita hatujifunzi au tunaona mzaha???

    ndo shida kuzungukwa na mijitu yenye misismamo ya kipepo na roho ya kumwaga damu

    ayo mambo ya sattelite za wazungu,na ivi wanajua nchi za pembe ya afrika sio salama kwa sasa na mambo ya ugaidi

    shindwa katika jina la Mungu muumbaji na mlinzi

    whoever is behind this should be killed!!na bado tutawashika tu

    ALUTA KONTINUA

    ReplyDelete
  13. duh kweli Bongo Security ZERO

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 08, 2009

    ...heeeeee...

    tunasubiri balozi

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 08, 2009

    WAMEKIMBIAJI?

    ilhali wako majini??

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 08, 2009

    Hii sasa kazi kweeli kweli

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 08, 2009

    Ohhh huko nyumbani kunarudika kweli mbona zahama za mabomu zimetuandama siku hizi....

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 08, 2009

    Mbona ni muda sasa umetoa hii taarifa na bado hujatupa update? Unatutisha michuzi hapa kazi zimelala tunasubiri taarifa zaidi. Maana mabomu tena ndugu inatisha. Mbagala penyewe ilikuwa hapatoshi itakuwa huko bandarini?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 08, 2009

    Nimepata taarifa kwamba ni emergency drill

    ReplyDelete
  20. hii hali inatisha, nadhani inahitajika uchunguzi wa kina juu ya hili swala pia hali ya ulinzi iimarishwe hasa maeneo makuu ya kuingilia nnchini

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 08, 2009

    BALAA HILO TENA JAMANI HATUTAKI BONGO YETU IWE NA MISUKOSUKO UFISADI UNATOSHA KABISA

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 08, 2009

    Unajua tatizo sio hayo mabomu, tatizo viongozi/jeshi/watu wa usalama wenyewe hatuwaamini, mfano mzuri ni wakati wa mabomu ya mbagala, taarifa zilizokuwa zinatolewa zote zilikuwa mbovu, mara ilikuwa mazoezi ya wanajeshi, mara ni vibomu vidogo vilivyobaki kwa hiyo vinamaliziwa, baada ya siku 4 yakaanza tena, mara ni vibomu vilivyosahaulika, sasa kwa mtaji huu tutawaaminije? lazima tutoke nduki kuzinusuru roho zetu

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 08, 2009

    Please kaka Michuzi endelea kutuhabarisha .....kasheshe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...